Mwanangu hataki kuongea nami, nafanyaje?

Huyu jamaa

1. Hana demu/ na hataki hawezi kuwa nae
2. Anakaa jikoni na kupika na mama yake wakati mzee yupo siiting room
3. Hashabikii mpira
4. Havuti sigara wala bangi
5. Meneno yake “...mpaka basi yani..”

Nahisi una umama umama wa kutosha

Mimi ni mkali sana kwa dogo inapokuja kwenye misimamo ya kimaisha, ila ni marafiki sana, na tunacheza (PS) na kuongea mengi, ila kwa namna mama yake alivyo bila mimi tungekuwa na toto kama mtoa mada
Umejuaje sina demu mkuu? Au ndio kuvamia mtu usie mjua...
 
Ckuwahi kuishi na baba! Mama angu alikuwa mkimya sana.... Muda wote ananisikiliza mimi tu nakucheka, kutabasamu ..nampa stori zooote za siku nzima! Namwimbia! Aisee nilikuwa mapepe! Mungu amrehemu
Pole kwa kufiwa na mama.. hope Mungu kamweka sehem salama
 
Kumbe wenye hii ishu tuko wengi, nilijua niko peke yangu.

Yani nilijaribu hadi kuwa naenda ofisini kwa mzee kujenga mazoea ila haikufua dafu kabisa.
 
Mi sipatani na wote na hawaongei nami.
achana upimbi yaani hupatani na wazazi wako...wewe ndio zile mada za mahusiano naona ulikuwa tayari kukosana na wazazi wako kisa mke?
 
Kumbe wenye hii ishu tuko wengi, nilijua niko peke yangu.

Yani nilijaribu hadi kuwa naenda ofisini kwa mzee kujenga mazoea ila haikufua dafu kabisa.
Hahahaaa Daaah pole sana mkuu
 
Baba yangu ni mkimya sana na mama yangu ni mcheshi sana na hii karithisha watoto wake wote hakuna mtu mkimya kwetu.

Ukimya wa baba haujamfanya aishi maisha ya upweke kwa wanae, tunamuelewa na tunaishi nae vile alivyo, ni mtu anayefurahi sana mtoto wake akimfata na kumwambia jambo au kumuomba ushauri hata kama wa kijinga yeye atajali na atasaidia.

Baba alikua mtu wa pili (kumtoa my bro) kumwambia kua "i am a lesbian" aliniangalia na kutabasamu kisha akasema "jembe langu fanya kile kinachokupa furaha as long as huumizi mtu".

Nirudi kwa mtoa mada, ushajua baba yako ni mkimya basi anza mazoea ya kumshirikisha katika vitu vyako na kumtaka shauri mbali mbali, sahau yaliyopita nyuma jenga sasa ushakua mtu mzima ambapo soon utakua na family yako na wewe utakua unaangaliwa.
kwamba wewe ni lesbian?
 
Hili suala binafsi linaniathiri mpaka leo. Baba yangu alitulea kiukali ukali....yaani ile kumuogopa sana. Akiwa sebuleni sisi tunatafuta pa kutokea.

Hata nikimpigia simu nikiwa mbali naye enzi hizo za u teenager anadhani nina shida ya pesa...hakuna ile socialization. Unapiga simu, yeye anakuambia useme shida yako as if it is always about the money.

Nimefika chuo, tatizo bado lile lile, ktk maisha yangu ya undergraduate sikumbuki ni lini nilipokea simu ya baba walau hata akunijulia hali, au naendelea vipi na masomo. Yeye akikupa ada anaona amemaliza.

Leo hii ktk utu uzima mzee amekuwa akinilalamikia kuwa simpigii simu. Yaani ninaweza kukaa hata miezi mitatu nisiwasiliane na baba na wala nisishtuke kabisa....why? Ni kwa sababu hatuna bond, hatuna uhusiano wa kirafiki kabisa. Na hata nikiwasiliana naye ni salamu tu, then basi.

Tatizo hili lipo kwa watoto wa kiume kwenye familia yetu. Hatuna ukaribu kabisa na baba. Hatukulelewa kwa urafiki na mzee.
 
Morning. Naombeni ushauri wenu kidogo wakuu..

Mimi ni kijana first born kwenye familia ya watoto 5. Wanaonifuata ni vijana walio juu ya miaka 18 mmoja wa kiume anaenifuata na wa kike. Huyu wa kiume anaishi Tanga na wa kike yupo kwa wazazi, mimi niko Northland.

Tuna wazazi wote wawili vijana kiasi (Hawajafika 50). Juzi nilikuwa namtafuta kwa simu my mom nikawa simpati ikabidi nimtext dingii "Ukiwa karibu na mama nipige nataka niongee nae maana simu yake hapokei" (ana mtindo wa kuacha simu jikon au chumbani).Dingii hata hakunipigia!

Baadae akanipigia akaanza kunilalamikia sana, anasema kuwa kwanini kila mkipiga simu hamuongei na mimi? Mnaongea na mama yenu tu! Kwani mimi niliwakosea nini? Au mimi sina umuhimu kwenu? Niliduwaa!!

Mimi nikajitetea kuwa kuna vitu nilikuwa nataka nimwambie mama kuhusu mimi.. akashika hapo hapo tena kwa kusema..kwa hiyo kuna vitu mpo tayari kumshirikisha mama yako mimi haupo tayari? Nikasema kuwa sikuona umuhimu wa kukuambia wewe jambo dogo kama hili ila ikifika muda nitakuambia. Aliongea sana kwanini tunamfanyia vile. Akakata simu!

Maneno ya dingii yaliniumiza kiasi yakafanya nimuonee huruma maana alikuwa anazungumza ukweli, huwa siongei nae kitu zaidi ya salamu then naongea na mama mpaka basi.Nakumbuka kipindi fulani nilikuwa naongea na rafiki yake dingii akaniambia eti mimi ni mtoto wa mama nampenda mama yangu tu nikamjibu ndio mimi ni mtoto wa mama sababunimezaliwa na mama alafu watoto wa kiume huwa tunapenda wazazi wa kike.

Hilo likapita nikachukulia poa ila hili la sasa ni serious.Mwanzo nilijua kuwa ni mimi tu ndio huwa naongea na mama pekee kumbe hata huyu jamaa wa Tanga huwa haongei na baba kabisa anaongea na mama tu. Baba analalamika pia kuwa hataki kuongea nae.

Chanzo cha tatizo:

Japo baba sio mzee ila ni kijana mwenye misimamo ya kizee. Ni ile aina ya wazazi wanaoona kuwa mtoto inatakiwa amuogope baba. Kubwa zaidi huwa ni mtu mkimya mno (ndio katuambukiza watoto ukimya hasa mimi na dogo). Huwa tukiwa ndani ni shikamoo tu ndio zinatembea tu no stori maana hakuna wa kumsemesha mwenzie..Nitaongea stori gani na baba wakati namuogopa, ni mkimya na mimi mkimya, ni mkali? Napiga kimya tu.

Ukiangalia kwa makini utajua ni malezi aliyotujengea ndio yamefanya tushindwe kuongea nae (Japo mimi nimeishi nae nyumba moja kwa miaka 4 tu) sasa wanae wamekuwa vijana anaona wanamtenga watoto wote wanampenda mama so anajisikia vibaya na upweke hakuna kibaya kama kukataliwa na familia yako mwenyewe.

Pia mimi na huyu dogo wa Tanga hatunaga stori kabisa huwa tunajuliana hali tu kwa simu. Kama tukiwa home pamoja tunakuwa kimya tu maana hakuna cha kuongea wote tuna asili ya ukimya. Ni salamu tu hata tukiwa tunaenda sehemu pamoja huwa tupo kimya no stori. Maana family conversation it wasn't applied to our family. Labda mama awe pamoja na sisi ndio tunaongea mno. Mimi nikiwa home nashinda zangu jikoni na mama stori tu mwanzo mwisho maana ndio kiumbe niliyemzoea zaidi duniani.

Ila kwa yule wa kike yeye tunaongea vizuri sana laafu yeye hana asili ya ukimya! Hata baba yake anaongea nae mno kuliko sisi.

Wakuu ambao ni wazazi tujifunze kuongea na wanetu vizuri yasije yakawakuta haya mambo. Ishi na watoto zenu kama marafiki. Wazazi wa kike wana win mioyo ya watoto ajili wao ni watu waelewa na wapole kwa watoto wao.

Msaada:
Nataka nijizoeshe kuwa naongea na father kila wiki hata kama sina shida nimpigie. Sasa naombeni mnishauri jinsi ya kuanza kupiga nae stori, stori gani niwe naongea nae? Mimi sio muongeaji mzuri.

Thanks
~Vers
Mkuu kwani wewe ni Kati ya wadogo ZANGU?
Yaani hili bandiko linahusu familia yangu kabisa. Baba tumeishi nae nyumba moja lakini hajawahi kuwa rafiki wala hakuwa akijihusisha sana na mambo yetu ya malezi, masomo wala chochote. Kila mtu huwa anampigia mama sim labda mama akosekane ndio anapigiwa yeye. Hatumchukii baba yetu ila kiufupi hatunaga kitu cha kuongea nae
 
Wababa kuna kitu cha kujifunza hapa🤔🤔🤔
 
Mkuu kwani wewe ni Kati ya wadogo ZANGU?
Yaani hili bandiko linahusu familia yangu kabisa. Baba tumeishi nae nyumba moja lakini hajawahi kuwa rafiki wala hakuwa akijihusisha sana na mambo yetu ya malezi, masomo wala chochote. Kila mtu huwa anampigia mama sim labda mama akosekane ndio anapigiwa yeye. Hatumchukii baba yetu ila kiufupi hatunaga kitu cha kuongea nae
Bahati mbaya mimi ndio first born...
Wazazi wa kiume wa kiafrika shida sana..mama angu ndio kila kitu kwa motivación na ushauri japo hayupo vzuri kipesa.. mzee anakuambia tu kua nitakusomesha ila ukitaka soma ukitaka acha. Japo sio mzee ila dah noma.
Yaani hakuna urafiki kabisa ila alikosea sana kutufanya tuwe tunamuogopa sasa ukaribu hamna na wanawe wamekua watu wazima ambao angebadirishana nae mawazo. Nimemuhusisha mama swala hili akasema tujitahidi kua tunaongea nae ila avumilie dawa imuingie ndio alichokipanda
 
Duh aiseee pole sana. Kwetu tumewazoea wazazi wote wawili,wana ukali sawa hawana upole,wala ukimya.
 
Pole sana. Ila nyie wakike ndio hua mnaukaribu zaidi na wazazi wa kiume. Sijui yeye kafeli wapi
 
Duh aiseee pole sana. Kwetu tumewazoea wazazi wote wawili,wana ukali sawa hawana upole,wala ukimya.
Hongeraa mm natamani sana nikiona watu wanavyopiga stori na baba zao. Kama nikiwa na baba mkubwa hua sitak hata kukaa nae mbali..maongezi mpaka basi
 
Kwa sasa its too late hivyo usirudie makosa kwa mwanao ajae.

Familia nyingi wababa wanadhan malezi ni pesa pekee. Yeye busy kutafuta pesa kuliko kufatilia maendeleo ya wanae. Wababa wa aina hii asilimia kubwa wakifiwa na wake zao huwa wanawahi kuoa tena hapo ndipo watoto wanaanza kuteseka vya kutosha chini ya utawala wa mama wa kambo
Hongeraa mm natamani sana nikiona watu wanavyopiga stori na baba zao. Kama nikiwa na baba mkubwa hua sitak hata kukaa nae mbali..maongezi mpaka basi
 
Hongeraa mm natamani sana nikiona watu wanavyopiga stori na baba zao. Kama nikiwa na baba mkubwa hua sitak hata kukaa nae mbali..maongezi mpaka basi
Msingi wa kuwa karibu hujengwa utotoni....jitahidi sana hili lisijirudie kwa watoto wako
 
Morning. Naombeni ushauri wenu kidogo wakuu..

Mimi ni kijana first born kwenye familia ya watoto 5. Wanaonifuata ni vijana walio juu ya miaka 18 mmoja wa kiume anaenifuata na wa kike. Huyu wa kiume anaishi Tanga na wa kike yupo kwa wazazi, mimi niko Northland.

Tuna wazazi wote wawili vijana kiasi (Hawajafika 50). Juzi nilikuwa namtafuta kwa simu my mom nikawa simpati ikabidi nimtext dingii "Ukiwa karibu na mama nipige nataka niongee nae maana simu yake hapokei" (ana mtindo wa kuacha simu jikon au chumbani).Dingii hata hakunipigia!

Baadae akanipigia akaanza kunilalamikia sana, anasema kuwa kwanini kila mkipiga simu hamuongei na mimi? Mnaongea na mama yenu tu! Kwani mimi niliwakosea nini? Au mimi sina umuhimu kwenu? Niliduwaa!!

Mimi nikajitetea kuwa kuna vitu nilikuwa nataka nimwambie mama kuhusu mimi.. akashika hapo hapo tena kwa kusema..kwa hiyo kuna vitu mpo tayari kumshirikisha mama yako mimi haupo tayari? Nikasema kuwa sikuona umuhimu wa kukuambia wewe jambo dogo kama hili ila ikifika muda nitakuambia. Aliongea sana kwanini tunamfanyia vile. Akakata simu!

Maneno ya dingii yaliniumiza kiasi yakafanya nimuonee huruma maana alikuwa anazungumza ukweli, huwa siongei nae kitu zaidi ya salamu then naongea na mama mpaka basi.Nakumbuka kipindi fulani nilikuwa naongea na rafiki yake dingii akaniambia eti mimi ni mtoto wa mama nampenda mama yangu tu nikamjibu ndio mimi ni mtoto wa mama sababunimezaliwa na mama alafu watoto wa kiume huwa tunapenda wazazi wa kike.

Hilo likapita nikachukulia poa ila hili la sasa ni serious.Mwanzo nilijua kuwa ni mimi tu ndio huwa naongea na mama pekee kumbe hata huyu jamaa wa Tanga huwa haongei na baba kabisa anaongea na mama tu. Baba analalamika pia kuwa hataki kuongea nae.

Chanzo cha tatizo:

Japo baba sio mzee ila ni kijana mwenye misimamo ya kizee. Ni ile aina ya wazazi wanaoona kuwa mtoto inatakiwa amuogope baba. Kubwa zaidi huwa ni mtu mkimya mno (ndio katuambukiza watoto ukimya hasa mimi na dogo). Huwa tukiwa ndani ni shikamoo tu ndio zinatembea tu no stori maana hakuna wa kumsemesha mwenzie..Nitaongea stori gani na baba wakati namuogopa, ni mkimya na mimi mkimya, ni mkali? Napiga kimya tu.

Ukiangalia kwa makini utajua ni malezi aliyotujengea ndio yamefanya tushindwe kuongea nae (Japo mimi nimeishi nae nyumba moja kwa miaka 4 tu) sasa wanae wamekuwa vijana anaona wanamtenga watoto wote wanampenda mama so anajisikia vibaya na upweke hakuna kibaya kama kukataliwa na familia yako mwenyewe.

Pia mimi na huyu dogo wa Tanga hatunaga stori kabisa huwa tunajuliana hali tu kwa simu. Kama tukiwa home pamoja tunakuwa kimya tu maana hakuna cha kuongea wote tuna asili ya ukimya. Ni salamu tu hata tukiwa tunaenda sehemu pamoja huwa tupo kimya no stori. Maana family conversation it wasn't applied to our family. Labda mama awe pamoja na sisi ndio tunaongea mno. Mimi nikiwa home nashinda zangu jikoni na mama stori tu mwanzo mwisho maana ndio kiumbe niliyemzoea zaidi duniani.

Ila kwa yule wa kike yeye tunaongea vizuri sana laafu yeye hana asili ya ukimya! Hata baba yake anaongea nae mno kuliko sisi.

Wakuu ambao ni wazazi tujifunze kuongea na wanetu vizuri yasije yakawakuta haya mambo. Ishi na watoto zenu kama marafiki. Wazazi wa kike wana win mioyo ya watoto ajili wao ni watu waelewa na wapole kwa watoto wao.

Msaada:
Nataka nijizoeshe kuwa naongea na father kila wiki hata kama sina shida nimpigie. Sasa naombeni mnishauri jinsi ya kuanza kupiga nae stori, stori gani niwe naongea nae? Mimi sio muongeaji mzuri.

Thanks
~Vers
Haya ndio maisha au tabia za wazazi wengi wa kitanzania
Wanaona ukali sana au kuogopwa na watoto ndio malezi
Wanasahau kuwa hiyo mbegu ndio inakuwa kadri miaka inavyosonga mbele,wàtoto wakiwa wakubwa wengi wanakuwa hawana ukaribu na mzazi,watakuwa karibu na mzazi ambaye hakuonyesha ukali sana kwao
 
Back
Top Bottom