Lakini mm sidhani kama kutafuta pesa ndio kunafanya mzazi asiwe na urafiki na watoto. Kwa baba ni yeye pekee kwenye familia yao ndio mkimya na mkali (wa maneno sio kupiga) kwa watoto. Ndugu zake wote wako very friendly kwa wanao namm nimelelewa na kaka yake (RIp) alikua very friend kwetu.Kwa sasa its too late hivyo usirudie makosa kwa mwanao ajae.
Familia nyingi wababa wanadhan malezi ni pesa pekee. Yeye busy kutafuta pesa kuliko kufatilia maendeleo ya wanae. Wababa wa aina hii asilimia kubwa wakifiwa na wake zao huwa wanawahi kuoa tena hapo ndipo watoto wanaanza kuteseka vya kutosha chini ya utawala wa mama wa kambo
mwambie baba ako aache ufala.Morning. Naombeni ushauri wenu kidogo wakuu..
Mimi ni kijana first born kwenye familia ya watoto 5. Wanaonifuata ni vijana walio juu ya miaka 18 mmoja wa kiume anaenifuata na wa kike. Huyu wa kiume anaishi Tanga na wa kike yupo kwa wazazi, mimi niko Northland.
Tuna wazazi wote wawili vijana kiasi (Hawajafika 50). Juzi nilikuwa namtafuta kwa simu my mom nikawa simpati ikabidi nimtext dingii "Ukiwa karibu na mama nipige nataka niongee nae maana simu yake hapokei" (ana mtindo wa kuacha simu jikon au chumbani).Dingii hata hakunipigia!
Baadae akanipigia akaanza kunilalamikia sana, anasema kuwa kwanini kila mkipiga simu hamuongei na mimi? Mnaongea na mama yenu tu! Kwani mimi niliwakosea nini? Au mimi sina umuhimu kwenu? Niliduwaa!!
Mimi nikajitetea kuwa kuna vitu nilikuwa nataka nimwambie mama kuhusu mimi.. akashika hapo hapo tena kwa kusema..kwa hiyo kuna vitu mpo tayari kumshirikisha mama yako mimi haupo tayari? Nikasema kuwa sikuona umuhimu wa kukuambia wewe jambo dogo kama hili ila ikifika muda nitakuambia. Aliongea sana kwanini tunamfanyia vile. Akakata simu!
Maneno ya dingii yaliniumiza kiasi yakafanya nimuonee huruma maana alikuwa anazungumza ukweli, huwa siongei nae kitu zaidi ya salamu then naongea na mama mpaka basi.Nakumbuka kipindi fulani nilikuwa naongea na rafiki yake dingii akaniambia eti mimi ni mtoto wa mama nampenda mama yangu tu nikamjibu ndio mimi ni mtoto wa mama sababunimezaliwa na mama alafu watoto wa kiume huwa tunapenda wazazi wa kike.
Hilo likapita nikachukulia poa ila hili la sasa ni serious.Mwanzo nilijua kuwa ni mimi tu ndio huwa naongea na mama pekee kumbe hata huyu jamaa wa Tanga huwa haongei na baba kabisa anaongea na mama tu. Baba analalamika pia kuwa hataki kuongea nae.
Chanzo cha tatizo:
Japo baba sio mzee ila ni kijana mwenye misimamo ya kizee. Ni ile aina ya wazazi wanaoona kuwa mtoto inatakiwa amuogope baba. Kubwa zaidi huwa ni mtu mkimya mno (ndio katuambukiza watoto ukimya hasa mimi na dogo). Huwa tukiwa ndani ni shikamoo tu ndio zinatembea tu no stori maana hakuna wa kumsemesha mwenzie..Nitaongea stori gani na baba wakati namuogopa, ni mkimya na mimi mkimya, ni mkali? Napiga kimya tu.
Ukiangalia kwa makini utajua ni malezi aliyotujengea ndio yamefanya tushindwe kuongea nae (Japo mimi nimeishi nae nyumba moja kwa miaka 4 tu) sasa wanae wamekuwa vijana anaona wanamtenga watoto wote wanampenda mama so anajisikia vibaya na upweke hakuna kibaya kama kukataliwa na familia yako mwenyewe.
Pia mimi na huyu dogo wa Tanga hatunaga stori kabisa huwa tunajuliana hali tu kwa simu. Kama tukiwa home pamoja tunakuwa kimya tu maana hakuna cha kuongea wote tuna asili ya ukimya. Ni salamu tu hata tukiwa tunaenda sehemu pamoja huwa tupo kimya no stori. Maana family conversation it wasn't applied to our family. Labda mama awe pamoja na sisi ndio tunaongea mno. Mimi nikiwa home nashinda zangu jikoni na mama stori tu mwanzo mwisho maana ndio kiumbe niliyemzoea zaidi duniani.
Ila kwa yule wa kike yeye tunaongea vizuri sana laafu yeye hana asili ya ukimya! Hata baba yake anaongea nae mno kuliko sisi.
Wakuu ambao ni wazazi tujifunze kuongea na wanetu vizuri yasije yakawakuta haya mambo. Ishi na watoto zenu kama marafiki. Wazazi wa kike wana win mioyo ya watoto ajili wao ni watu waelewa na wapole kwa watoto wao.
Msaada:
Nataka nijizoeshe kuwa naongea na father kila wiki hata kama sina shida nimpigie. Sasa naombeni mnishauri jinsi ya kuanza kupiga nae stori, stori gani niwe naongea nae? Mimi sio muongeaji mzuri.
Thanks
~Vers
akiitwa dingi kwani anabanduka uume?Title mwanangu hataki kuongea na mimi nifanyeje.
So ukishashauriwa utaenda kumpa ushauri mzee wako?
Kwanini umuite baba yako dingi? Sisi kumheshimu mzee wako inaanzia na wewe unavyomwasilisha kwetu, kama unamuwasilisha kama dingi na hujisikii kumuita baba mbele yetu pengine unataka tukuone mhuni sana basi kuna tatizo mahali.
ongeleeni ata biashara ya kuuza podaMzee hapendi mpira mm sipendi mpira.. hapo ndio nakosa cha kujadiliana
Mimi mzee wangu sitaki hata anipigie. Huyu mzee naamini kabisa alirogwa. Kuna siku hivi karibuni alimpa mwanachuo mwenzangu jirani yake tulio chuo kimoja eti aniulize mishe za chuo,malipo,n.k Yule jamaa nilimwambia kwanza anipe namba za mzee wake ili huyo mzee naye aniulize masuala ya mwanae[emoji23] Jamaa tuligombana hadi sasa kaniblock,yani nikijua kuna mtu anafahamiana na mzee kwa ukaribu anakuwa adui yangu. Mara ya mwisho kumpigia alinambia yuko anajiandikisha daftari la mpiga kura. Mara nyingine alikuwa kwenye kelele,mara nyingine alikuwa kwenye kikao. Mara zote hizo anadai atapiga baadae na hafanyi hivo. In short ni hivi,anataka kujua taarifa zangu lakini hataki kuongea na mimi
Anakua kama wewe.akiitwa dingi kwani anabanduka uume?
Mwandiko wa kitoto sana huu.Kua uyaone bwana.Kama ni mtu mzima basi una walakin sehemuMtaongea mara kwa mara then stori zitaisha,mtaongea hewa?
Baba hana touch na watoto!
Urafiki haulazimishwi!
Hiyo mnajenga artificial relationship!
Baba alichemka kuwalea wanawe,haya ndio matokeo yake na akubali kuyaishi!
Utajenga nae mastori na urafiki wa kinafiki hata ufanyeje urafiki utakua wa kinafiki,mtaendelea kufanya maigizo matupu!
Baba aache kulalamika!
Yeye ndio aanze kuwatafuta na kuwaongelesha,otherwise atajiju!
Makosa ni yake,arekebishe yeye,watoto hawana makosa kabisa!
Ni upumbavu jitu zima lilifanya makosa wakati wa kulea,lilivyp hovyo zaidi linageuzia makosa kwa hao watoto,badala lijirekebishe lenyewe!
Akiendelea kujifanya hamnazo,atakua mpweke forever!
Mi sipatani na wote na hawaongei nami.
Hongeraa. Shida inakuja mdingi hata ukimuuliza unapewa yale majibu mafupi mafupi...nimefanya ushauri huu wikii hii ila wapi naona mzee hafunguki japo kidogo Tuliongea kama dk 3Nimelelewa mazingira kama hayo lakin huniambii kitu kuhus mzee wangu.Nampenda na namchek pindi nipatapo nafasi japo sio kila mara.
Nilikua na tabia kama yako ya kumchek mama mara kwa mara ila nikaja kugundua kuwa mzee hajiskii vizur kuwa simpigii nikaamua kubalance mambo.Nikapunguza simu kwa mama pia.
Halaf wote nikawa nawapigia kwa pamoja .Nikimmkubuka mama basi naanza kwanza kumpigia baba naongea nae sana mambo maisha yake na shugul zake na maisha kwa ujumla.Nampa na mm mipango yangu kisha namuuliza kuhusu ya kwake.Ipi mipya na ya zaman utekelezaji wake umefika wap.Wap anakwama nakadhalika.Kwakua haya ni mambo mapya kila siku so huwa sikosi cha kuongea nae kila nikimcheki.
Nikimaliza nampigia mama.Hata kama wako pamoja kila mtu huwa nampigia kwenye cm yake.Niaacha kabisaa yale mambo ya kuwasiliana nao kwa kificho kiasi kwamba wote wanakua wanajua kama nimewasiliana na mmoja wapo.
Ushauri.
Ukijiskia kuongea na mama yako, anza kumche mdingi then bonga na maza.Balance mambo.Yule ni baba yako tu huwez kosa cha kuongea nae
Hii sio kweli mfano mimi ni Copy kabisa na Faza ila hatuna mazoea ya kuongea lakini mama hata lisaa nabonga nae kwa phone kwanza nikiwa naongea nae huwezi kujua kama naongea na mama mana ni rafiki angu mkubwa sana ambae sijui naweza mficha nini,Ukiona huna mahusiano ya karibu na baba yako tambua siku ya kutengenezwa kwako mama yako alikuwa hajalala na huyo unayemwita baba.
acha ufala dogoAnakua kama wewe.
Sawa kubwa la mashogaacha ufala dogo