Mwanangu hataki kuongea nami, nafanyaje?

Mwanangu hataki kuongea nami, nafanyaje?

Usipompenda mtu aliyekuzaa na kukunyonyesha utampenda nani tena?
Potelea mbali hata nikiitwa mtoto wa mama kisa nampenda mama haina shida
Mi naona niko vice versa.......Mama sina bond naye kabisa......
 
Morning. Naombeni ushauri wenu kidogo wakuu..

Mimi ni kijana first born kwenye familia ya watoto 5. Wanaonifuata ni vijana walio juu ya miaka 18 mmoja wa kiume anaenifuata na wa kike. Huyu wa kiume anaishi Tanga na wa kike yupo kwa wazazi, mimi niko Northland.

Tuna wazazi wote wawili vijana kiasi (Hawajafika 50). Juzi nilikuwa namtafuta kwa simu my mom nikawa simpati ikabidi nimtext dingii "Ukiwa karibu na mama nipige nataka niongee nae maana simu yake hapokei" (ana mtindo wa kuacha simu jikon au chumbani).Dingii hata hakunipigia!

Baadae akanipigia akaanza kunilalamikia sana, anasema kuwa kwanini kila mkipiga simu hamuongei na mimi? Mnaongea na mama yenu tu! Kwani mimi niliwakosea nini? Au mimi sina umuhimu kwenu? Niliduwaa!!

Mimi nikajitetea kuwa kuna vitu nilikuwa nataka nimwambie mama kuhusu mimi.. akashika hapo hapo tena kwa kusema..kwa hiyo kuna vitu mpo tayari kumshirikisha mama yako mimi haupo tayari? Nikasema kuwa sikuona umuhimu wa kukuambia wewe jambo dogo kama hili ila ikifika muda nitakuambia. Aliongea sana kwanini tunamfanyia vile. Akakata simu!

Maneno ya dingii yaliniumiza kiasi yakafanya nimuonee huruma maana alikuwa anazungumza ukweli, huwa siongei nae kitu zaidi ya salamu then naongea na mama mpaka basi.Nakumbuka kipindi fulani nilikuwa naongea na rafiki yake dingii akaniambia eti mimi ni mtoto wa mama nampenda mama yangu tu nikamjibu ndio mimi ni mtoto wa mama sababunimezaliwa na mama alafu watoto wa kiume huwa tunapenda wazazi wa kike.

Hilo likapita nikachukulia poa ila hili la sasa ni serious.Mwanzo nilijua kuwa ni mimi tu ndio huwa naongea na mama pekee kumbe hata huyu jamaa wa Tanga huwa haongei na baba kabisa anaongea na mama tu. Baba analalamika pia kuwa hataki kuongea nae.

Chanzo cha tatizo:

Japo baba sio mzee ila ni kijana mwenye misimamo ya kizee. Ni ile aina ya wazazi wanaoona kuwa mtoto inatakiwa amuogope baba. Kubwa zaidi huwa ni mtu mkimya mno (ndio katuambukiza watoto ukimya hasa mimi na dogo). Huwa tukiwa ndani ni shikamoo tu ndio zinatembea tu no stori maana hakuna wa kumsemesha mwenzie..Nitaongea stori gani na baba wakati namuogopa, ni mkimya na mimi mkimya, ni mkali? Napiga kimya tu.

Ukiangalia kwa makini utajua ni malezi aliyotujengea ndio yamefanya tushindwe kuongea nae (Japo mimi nimeishi nae nyumba moja kwa miaka 4 tu) sasa wanae wamekuwa vijana anaona wanamtenga watoto wote wanampenda mama so anajisikia vibaya na upweke hakuna kibaya kama kukataliwa na familia yako mwenyewe.

Pia mimi na huyu dogo wa Tanga hatunaga stori kabisa huwa tunajuliana hali tu kwa simu. Kama tukiwa home pamoja tunakuwa kimya tu maana hakuna cha kuongea wote tuna asili ya ukimya. Ni salamu tu hata tukiwa tunaenda sehemu pamoja huwa tupo kimya no stori. Maana family conversation it wasn't applied to our family. Labda mama awe pamoja na sisi ndio tunaongea mno. Mimi nikiwa home nashinda zangu jikoni na mama stori tu mwanzo mwisho maana ndio kiumbe niliyemzoea zaidi duniani.

Ila kwa yule wa kike yeye tunaongea vizuri sana laafu yeye hana asili ya ukimya! Hata baba yake anaongea nae mno kuliko sisi.

Wakuu ambao ni wazazi tujifunze kuongea na wanetu vizuri yasije yakawakuta haya mambo. Ishi na watoto zenu kama marafiki. Wazazi wa kike wana win mioyo ya watoto ajili wao ni watu waelewa na wapole kwa watoto wao.

Msaada:
Nataka nijizoeshe kuwa naongea na father kila wiki hata kama sina shida nimpigie. Sasa naombeni mnishauri jinsi ya kuanza kupiga nae stori, stori gani niwe naongea nae? Mimi sio muongeaji mzuri.

Thanks
~Vers
MH aisee inauma ukweli alilokwambia Dingi,hata Mimi watoto wangu uwa wanakuwa mbali nami nadhani wananiogopa,kwani Mimi ndio natakiwa kuwanyoosha kitabia na uwa ninakuwa na muda WA kuwachekesha kidogo,yaan vimatani vya hapa na pale na wakifanya kosa nakuwa mkali Sana kwani Mama Yao vingine anakuwa kama haoni,na wakati sipo uwa wananikumbuka sana,Ila watoto badilikeni bila Sisi wazazi WA kiume msinge kuwa hapo mlipo,nawe badilika kwa kuwa litakutokea na litakuumiza jifunze kuongea na mdingi wako.shauriana nae mambo ya muhimu na ya kifamilia Zaid Sisi tunapenda watoto wenye misimamo na ajili za kimaendeleo Zaid,pia mkumbuke kwa zawadi zote tunaridhika tu
 
Wazazi wengi wa kiume ni wakali sana. Tofauti na wazazi wa kike.
Mama unaweza mpigia hata mkapiga umbea lakini baba ni ngumu.
Hata mimi inanitokea.
 
Nimependa maneno yako nitajitahidi kuyafanyia kazi
 
Sina hakika kama unanielewa.

Nimekuelewa!

Tatizo ulilolitoa hapo ni kwamba,although nyie ni watu wazima ila bado baba wana authorities over you!

Na hilo ni tatizo,maana italeta confusion ambapo mtu mzima anatakiwa awe na autonomy bila kua impeded na authority,shida hao wababa zenu wana authority still ndio maana hamna friendship genuinely!
 
Hii wazazi wakali inabaki inawakost wakizeeka maana wanakosa wa kuwafariji.. upendo wote upo kwa mama baba anajiona mpweke
Wazazi wengi wa kiume ni wakali sana. Tofauti na wazazi wa kike.
Mama unaweza mpigia hata mkapiga umbea lakini baba ni ngumu.
Hata mimi inanitokea.
 
Vice versa mkuu me naongea sana na mzee kuliko mama
Hili jambo hata mimi nilikuwa sina story na father nilianza kupiga nae story kidogo nilivyomaliza A'level.

Ilikuwa hata nikipiga simu ni salamu ya shikamoo kwisha ila nikatafuta mbinu mwenyewe kama kuulizia shughuli zake zinaenda vipi. Kuulizia ndugu na kumpa salamu na habari ya ndugu niliyoongea nao.

Japo huwa tunazungumza sana hadi leo ila likija kwa mama hapo naweza hadi kumaliza bundle.
 
Hongera je ulianza vipi? Sidhani kama nishawahi kuongea na mzee zaidi ya dk 2. Ni simu tu ya shida basi. Wazazi wa kizazi kipya tubadirike kwakweli
Watu tunatofautiana, mtoto wangu wa kiume yupo karibu nami hata inakera, wakitofautiana na GF lazima aniambie nimshauri hapo ataridhika, akiudhiwa na mtu atanipigia nami nampa moyo na kumkanseli.
Kwa upande wako, jitahidi kujua interest ya baba yako! Kama anapenda mpira anzia hapo na kama anapenda dini mwanze kwa kumweleza kuwa unapenda kuwa Padre au Imamu
 
Story yako nikama yangu ..mzee ana lalamika kweli simu shirikishi kwenye mambo yangu adi apelekewe habari na mom .....ila uki angalia mzee aingiliki kabla ya kuongea lazima uji tafakari kwanza duh..
 
Watu tunatofautiana, mtoto wangu wa kiume yupo karibu nami hata inakera, wakitofautiana na GF lazima aniambie nimshauri hapo ataridhika, akiudhiwa na mtu atanipigia nami nampa moyo na kumkanseli.
Kwa upande wako, jitahidi kujua interest ya baba yako! Kama anapenda mpira anzia hapo na kama anapenda dini mwanze kwa kumweleza kuwa unapenda kuwa Padre au Imamu
nitalifanyia kazi kiukweli nampenda baba angu mkubwa ni mtu muongeaji sana yaani hua naongea nae sana nikiwa kwake...nataman angekua ndio baba
 
Back
Top Bottom