Mwanangu hataki kuongea nami, nafanyaje?

Mwanangu hataki kuongea nami, nafanyaje?

Baba zetu wa ki Africa wengi huzaa watoto na kukimbia majukumu unakuta mzazi amekupeleka shule anakuacha kama gerezani, unasoma kwa majuto na kusononeka simu mara moja kwa mwaka anakujengea hostile ukipata kaposition hata ka INTERN anaanza oooh hupigi simu, lakini mama zetu wapo na sisi mwanzo mwisho.
 
Jitahidi, ila kosa ni la Baba na Mama yako! Wakati watoto wanakuwa Baba anajidai ki Dume, kupiga watoto na kuwa mkoloni anaweka distance na wa Toto mwisho wa Siku anakuwa mpweke! Tengeneza urafiki naye ila hauna kosa ni tabia ambayo ni jukumu la Mzazi kuweka I Karibu na watoto wake
Sikia vitoto vya mama vinawaza (softy life) mwishoe vinalelewa na vimama wengine wanakua mashoga... ....... nashukuru sana Baba angu kua mkali kwa malezi yangu haya maisha ya Tz yangenishinda hayana huruma am a hursler bcz of you, thank you Dad............Baba angu hataki nonsense zenu mpigie husimpigie niwewe tu ila I call him oftenly kwa ushauri wamaisha hacheki namtoto hovyo I love your character Dad thankx
 
Morning. Naombeni ushauri wenu kidogo wakuu..

Mimi ni kijana first born kwenye familia ya watoto 5. Wanaonifuata ni vijana walio juu ya miaka 18 mmoja wa kiume anaenifuata na wa kike. Huyu wa kiume anaishi Tanga na wa kike yupo kwa wazazi, mimi niko Northland.

Tuna wazazi wote wawili vijana kiasi (Hawajafika 50). Juzi nilikuwa namtafuta kwa simu my mom nikawa simpati ikabidi nimtext dingii "Ukiwa karibu na mama nipige nataka niongee nae maana simu yake hapokei" (ana mtindo wa kuacha simu jikon au chumbani).Dingii hata hakunipigia!

Baadae akanipigia akaanza kunilalamikia sana, anasema kuwa kwanini kila mkipiga simu hamuongei na mimi? Mnaongea na mama yenu tu! Kwani mimi niliwakosea nini? Au mimi sina umuhimu kwenu? Niliduwaa!!

Mimi nikajitetea kuwa kuna vitu nilikuwa nataka nimwambie mama kuhusu mimi.. akashika hapo hapo tena kwa kusema..kwa hiyo kuna vitu mpo tayari kumshirikisha mama yako mimi haupo tayari? Nikasema kuwa sikuona umuhimu wa kukuambia wewe jambo dogo kama hili ila ikifika muda nitakuambia. Aliongea sana kwanini tunamfanyia vile. Akakata simu!

Maneno ya dingii yaliniumiza kiasi yakafanya nimuonee huruma maana alikuwa anazungumza ukweli, huwa siongei nae kitu zaidi ya salamu then naongea na mama mpaka basi.Nakumbuka kipindi fulani nilikuwa naongea na rafiki yake dingii akaniambia eti mimi ni mtoto wa mama nampenda mama yangu tu nikamjibu ndio mimi ni mtoto wa mama sababunimezaliwa na mama alafu watoto wa kiume huwa tunapenda wazazi wa kike.

Hilo likapita nikachukulia poa ila hili la sasa ni serious.Mwanzo nilijua kuwa ni mimi tu ndio huwa naongea na mama pekee kumbe hata huyu jamaa wa Tanga huwa haongei na baba kabisa anaongea na mama tu. Baba analalamika pia kuwa hataki kuongea nae.

Chanzo cha tatizo:

Japo baba sio mzee ila ni kijana mwenye misimamo ya kizee. Ni ile aina ya wazazi wanaoona kuwa mtoto inatakiwa amuogope baba. Kubwa zaidi huwa ni mtu mkimya mno (ndio katuambukiza watoto ukimya hasa mimi na dogo). Huwa tukiwa ndani ni shikamoo tu ndio zinatembea tu no stori maana hakuna wa kumsemesha mwenzie..Nitaongea stori gani na baba wakati namuogopa, ni mkimya na mimi mkimya, ni mkali? Napiga kimya tu.

Ukiangalia kwa makini utajua ni malezi aliyotujengea ndio yamefanya tushindwe kuongea nae (Japo mimi nimeishi nae nyumba moja kwa miaka 4 tu) sasa wanae wamekuwa vijana anaona wanamtenga watoto wote wanampenda mama so anajisikia vibaya na upweke hakuna kibaya kama kukataliwa na familia yako mwenyewe.

Pia mimi na huyu dogo wa Tanga hatunaga stori kabisa huwa tunajuliana hali tu kwa simu. Kama tukiwa home pamoja tunakuwa kimya tu maana hakuna cha kuongea wote tuna asili ya ukimya. Ni salamu tu hata tukiwa tunaenda sehemu pamoja huwa tupo kimya no stori. Maana family conversation it wasn't applied to our family. Labda mama awe pamoja na sisi ndio tunaongea mno. Mimi nikiwa home nashinda zangu jikoni na mama stori tu mwanzo mwisho maana ndio kiumbe niliyemzoea zaidi duniani.

Ila kwa yule wa kike yeye tunaongea vizuri sana laafu yeye hana asili ya ukimya! Hata baba yake anaongea nae mno kuliko sisi.

Wakuu ambao ni wazazi tujifunze kuongea na wanetu vizuri yasije yakawakuta haya mambo. Ishi na watoto zenu kama marafiki. Wazazi wa kike wana win mioyo ya watoto ajili wao ni watu waelewa na wapole kwa watoto wao.

Msaada:
Nataka nijizoeshe kuwa naongea na father kila wiki hata kama sina shida nimpigie. Sasa naombeni mnishauri jinsi ya kuanza kupiga nae stori, stori gani niwe naongea nae? Mimi sio muongeaji mzuri.

Thanks
~Vers
hongera sana mkuu maana wewe inaongea hata na mama yako. Mimi ipo hivi siku nimeongea na Mother mda mrefu kwenue simu basi ni dakika chini ya kumi, kwa mzee huwa chini ya dkk 5. kiufupi mimi huwa si muongeaji sana naana kuna kipindi mpka kuna demu fulani aliniambia asiponitafuta huwa simtafuti ikabid nimwambie nizoee hivo hivo maana mm sinagana story kwa sana.
 
  • Bora wew zinafika 5 Mimi sana sana dkka2 ni salam unaendeleaje,umepata kazi kwisha
 
Pamoja na hayo ni muhimu kutengeneza mahusiano kati yenu,
Wakati ule hukuweza ila sasa unaweza, zingatia wewe ni kijana wa kwanza kwa familia (Vunja tabia ya ukimya/Woga).
Anza taratibu kumfahamu mzee wako, omba ushauri kwake wa mawazo na nambo mengine atafunguka tu.
Ahsante sana kiongozi. Japo hatuongei sana ila hunishirikisha kimawazo kwa vitu anavyotaka kufanya. Kama mm nipo laziama akitaka kufanya kitu cha maendeleo lazima niwe shahidi na saini iwepo. Basi tu yale mazungumzo ya indeep ndio hakuna...ana nitreat right kama mwanae wa kwanza and i appreciate. Ila nitaufanyia kazi ushauri wako
 
Baba zetu wa ki Africa wengi huzaa watoto na kukimbia majukumu unakuta mzazi amekupeleka shule anakuacha kama gerezani, unasoma kwa majuto na kusononeka simu mara moja kwa mwaka anakujengea hostile ukipata kaposition hata ka INTERN anaanza oooh hupigi simu, lakini mama zetu wapo na sisi mwanzo mwisho.
Mama ndio binaadamu pekee ambae atakua nawe muda wote karibu hakuna cha baba wala nani... Mama anamchango mkubwa kimawazo kwangu ndio maana mm simfichi kitu hata kidogo
 
Pamoja na hayo ni muhimu kutengeneza mahusiano kati yenu,
Wakati ule hukuweza ila sasa unaweza, zingatia wewe ni kijana wa kwanza kwa familia (Vunja tabia ya ukimya/Woga).
Anza taratibu kumfahamu mzee wako, omba ushauri kwake wa mawazo na nambo mengine atafunguka tu.

This is wrong

Unamuangushia jukumu huyu mtoto wakati kosa sio lake to begin with!

Huyu mtoto mnampa mzigo ambao baba ndio angetakiwa atafute watoto wake afanye amendments!

Huyu mtoto mnamtwisha mzigo wa mawazo ambao astahili kabisa!

Huyo baba afanye heavy lifting hapa aache upumbavu
 
hongera sana mkuu maana wewe inaongea hata na mama yako. Mimi ipo hivi siku nimeongea na Mother mda mrefu kwenue simu basi ni dakika chini ya kumi, kwa mzee huwa chini ya dkk 5. kiufupi mimi huwa si muongeaji sana naana kuna kipindi mpka kuna demu fulani aliniambia asiponitafuta huwa simtafuti ikabid nimwambie nizoee hivo hivo maana mm sinagana story kwa sana.
Hata mm niko hvo ila kwa mama hua niko wide open yaani tunaongea mpaka basi.. hata kama kuna mtu nampenda lazima nimwambie mama nione atasemaje
 
Kwa baba
Yaani labda nimwambie mama msalimie baba ukute yupo! Ananiambia huyu hapa msalimie! Ila kumpigia huwa sikumbuki kabisaa mimi
Makubwa..pole sana.
Mimi najua kwenu wadada zinakua zinaiva sana na wababa kuliko mama..kwa mfano sisi tu nashindwa kuongea na baba ila wadogo zetu wa kike wanampelekesha wanavyoweza na anawadekeza. Ila sie wanaume ndio hatuko huko.

Je chanzo cha hayo yote ni nini..?
 
Pamoja na makosa yake,mzazi hatupwi,hatengwi wala kisemwa
"Jinyenyekeze tu mbele ya Dingi otherwise mtamuua mapema kwa mawazo"
 
Si kweli, Mi na mshua tulikua kam wachina but ilikua no story zaidi ya maswali na majibu. Ila kipindi namuuguza alitokea kuwa bonge la Best angu mpaka story za kupiga na rafiki zake au wangu tukawa tunazikung'oli fresh tuu.

Ila kuna kitu hawa wazee sijui huwa ni nini, unaweza kuta hana story na wanae ila vijana rika la wanae smtimez wengine wadogo anapiga nao story mpaka unaona wivu.
Nakubaliana nawe mkuu.
Marafiki zangu wanaogea vizuri na baba hadi hua wananiambia mbona baba yako ana stori sana ila nyie hamuongei nae?? Yaani hua nabaki kuwaangalia tu wanavyoongea mm hata sichangii.
Tena kwa baba ana experience ya vitu vingi maana ni mtu aliyeizunguka sana Tz yote,Kwa madiba na Bara Asia huko
 
Pamoja na makosa yake,mzazi hatupwi,hatengwi wala kisemwa
"Jinyenyekeze tu mbele ya Dingi otherwise mtamuua mapema kwa mawazo"
Hatujamtenga ila ndio vile hatuna stori sana
 
This is wrong

Unamuangushia jukumu huyu mtoto wakati kosa sio lake to begin with!

Huyu mtoto mnampa mzigo ambao baba ndio angetakiwa atafute watoto wake afanye amendments!

Huyu mtoto mnamtwisha mzigo wa mawazo ambao astahili kabisa!

Huyo baba afanye heavy lifting hapa aache upumbavu
Wanasema mzazi hakosei...so tujishushe tu maisha yasonge. Mimi niko tayari kufanya kila njia uhusiano uwepo
 
This is wrong

Unamuangushia jukumu huyu mtoto wakati kosa sio lake to begin with!

Huyu mtoto mnampa mzigo ambao baba ndio angetakiwa atafute watoto wake afanye amendments!

Huyu mtoto mnamtwisha mzigo wa mawazo ambao astahili kabisa!

Huyo baba afanye heavy lifting hapa aache upumbavu

Mahusiano mazuri na wazazi wote wawili na ndugu zake kwa ujumla ni muhimu.
 
Ahsante sana kiongozi. Japo hatuongei sana ila hunishirikisha kimawazo kwa vitu anavyotaka kufanya. Kama mm nipo laziama akitaka kufanya kitu cha maendeleo lazima niwe shahidi na saini iwepo. Basi tu yale mazungumzo ya indeep ndio hakuna...ana nitreat right kama mwanae wa kwanza and i appreciate. Ila nitaufanyia kazi ushauri wako
Vizuri Bro,
Nakutakia Heri.
 
Back
Top Bottom