Ukichunguza sana, "mungu" na "mzungu", etymologically speaking, zina mzizi mmoja.
Mungu ni mtu tu, specifically mzungu.
Katuletea habari za dini tukaziamini na kumvika ukuu.
Ndo maana mpaka leo ramani inaonyesha ulaya iko juu na Afrika iko chini, ingawa dunia haina juu wala chini.
Mental slavery.
Nimeuliza hapa.
Kama mungu ana uwezo wote na ujuzi wote na upendo wote, kwa nini hakuumba ulimwengu ambao mabaya, magonjwa, mauaji etc haviwezekani?
Kwa nini hakuumba ulimwengu wa hivyo?
Ina maana alikuwa hawezi? Kama hawezi, je ni kweli anaweza yote?
Ina maana aliweza lakini hakutaka tu? Kama aliweza ila hakutaka tu, je ana upendo wote?
Ukiofikiria sana hili suala utaona hii habari ya mungu, at least in the context of Judeo-Christian/Islamic/Personal god, ni uzushi mtupu.
It does not satisfy a very simple and human test of logical consistency.
Kama mungu angekuwa anakaa miongoni mwetu,
EMT, ningepetition kumpeleka ICC akashtakiwe kwa mauaji ya halaiki.
Maana anaweza kuzuia mabaya yote lakini hazuii, kwa nini?
Kwa nini tutake kumpeleka Uhuru Kenyatta, mtu asiye na uwezo wote wala upendo wote, ICC, lakini mungu mwenye uwezo wote na upendo wote asishitakiwe?
Of course, hawezi kushitakika kwa sababu hathibitishiki kuwepo, ni hadithi tu.