huyo sio mpenzi wake ni mwanamke kamtongoza tu, je mnaunga mkono ukitongozwa tu uanze kupiga mizinga??
Nitamtafuta mwenyewe kwakweli maana nina shida naye haswaaaa.
Kwakweli inabidi waunde umoja maana wametuchosha kila siku lawama hizi hizi, wanaume na nyie mmezidi ubahiri khaaaah!! Kwani mkitoa mnakufa?
Wanataka wapewe wao.....hivi wanaume wa siku hizi mmekuaje....?.....kwa nini hamtaki kutoa hela......?.........ua bila kumwagiliwa mnadhani litapendezaje......?......
Mie nashindwa hata kuwashangaa kwakweli!! Huu ubahiri gani sasa na kukalamika tuuuu kama gari bovu, mwanamke gharama jamani hebu toeni tu msisubiri hadi tuwaombe, khaaaaaah!!
Shida iko wapi? Lengo la kumtongoza ni nini?? Atoe tu.
Poa, ukihitaji contacts zake nistue!
kwahio wewe kuombaomba huoni shida?
Sio kuomba omba, bali kuomba, shida iko wapi wakati unauhitaji?? Mbona nyie hamuonagi shida kutuomba omba?
Hizi kesi zimekuwa nyingi sana. Kuna wenzio kibao humu utawaona tu. Undeni umoja wenu wa wapigwa mizinga/vibomu halafu mjue mtasonga vipi kwa pamoja.
Sawa babu, thanx alot, ila nawe usiwe unapotea hivyo.
uhitaji gani unatongozwa leo hata hamjakubaliana ushaanza mizinga?? dont get it twisted....mada ya hapa sio kumuomba mpenzi wako, hilo linakubalika, anacholalamika mtoa mada ni wewe kutongozwa tu ushaanza mizinga hata ahakijaeleweka ushaanza kutangaza njaa!!
uhitaji gani unatongozwa leo hata hamjakubaliana ushaanza mizinga?? dont get it twisted....mada ya hapa sio kumuomba mpenzi wako, hilo linakubalika, anacholalamika mtoa mada ni wewe kutongozwa tu ushaanza mizinga hata ahakijaeleweka ushaanza kutangaza njaa!!
Mbona nipo tena sana? Tatizo lako hutaki kumtafuta/kumsalimia babu.
Kwani kakulazimisha? Kama huwezi kucheleza muziki wake kwa nini usiwaachie wanaouweza?
Kujiliza liza sasa....Wanakeraaaaaa!! Uchoyo tu usiokuwa na msingi