Mwanamke 'kumhonga' Mwanamme . . .

hapa pagumu sana.
Umuhimu wa kuwa na mwenza mnae fanana kidogo status zenu ndio hapo una onekana lasivyo kila siku utajiona mnyonge sana.

Hapo kwa hayo mazingira mwanaume lazima nijione mnyonge sana hata kama si nyanyaswi.
Ndio nilikua namwambia Kongosho. Kuna wanaume wengi ambao hawapo comfortable na haya mambo.
 
Last edited by a moderator:
Sioni tatizo mapenzi ni kusaidiana where necessary,mmoja akiwa down economicaly mwenzie akimboost hakuna ubaya as long as mapenzi ya kweli yapo! Lakini pia haipendezi mmoja ndo awe anatoa daily huku mwingine awe wa kupokea tu hiyo ni tabia ya kupe!
 
unajua kuna wakati unaweza zifuma hela ukataka kwenda sehemu nzuri, sasa umwache huyu mwenza ili asijisikie vibaya?

Na ukienda vakesheni peke yako wakati ulitaka enda na mwenzio ina maana gani?

Ndio nilikua namwambia Kongosho. Kuna wanaume wengi ambao hawapo comfortable na haya mambo.
 
Last edited by a moderator:
Kama wote mna mutual interests and kipato pia sioni ubaya. Ila tatizo linakuja pale baadhi ya wanawake wanahonga vijana wa dogo alimaarufu kama MARIO ili tu wawapate kimapenzi. Unakuta mwanamke anamgharimia kila kitu, good time mjina, nguo, usafiri and the like na kijana anatamba kabisa nina bibi or jimama!!!! Ili kujadili hili kwa upana inabidi tuona aina ya mahusiano kama ni ya kidhati au ni ya kimaslahi zaidi. Na hii ndiyo mitindo iliyopo mjini siku hizi kuna sugar mummies kama huko awali ilivyokuwa sugar daddies!!!! Sodoma and Gomora.
 
Sioni tatizo mapenzi ni kusaidiana where necessary,mmoja akiwa down economicaly mwenzie akimboost hakuna ubaya as long as mapenzi ya kweli yapo! Lakini pia haipendezi mmoja ndo awe anatoa daily huku mwingine awe wa kupokea tu hiyo ni tabia ya kupe!
ni sawa kama wote mnajiweza, ingawa kwa hali tofauti, na mnapendana kwa dhati, ila ikionekana mara kwa mara kua uwezo wa mdada unamzidia sana mwanaume inakua soo. Mapenzi yanachanua vizuri kati ya watu wenye background zilizo fanana fanana. tena bora hata wanawake, ni wepesi ku-move out of their comfort zone kuliko wanaume
Mfano :
Kwako wewe kusafiri nje ya nchi kila baada ya miezi sita ni jambo la kawaida sana kufatana na kazi zako, pia kufatana na pato lako. Kwangu mimi sina uwezo huo. hapo inabidi wewe ukubali kua grounded ili tuwe pamoja ukiwa leave, au mimi nikubali kulipiwa hizo safari za nje kila baada ya miezi sita. Hapa itakua rahisi zaidi kwako kupunguza safari zako kuliko kwa mwanaume kukubali kulipiwa nauli kama mtoto mdogo. In the inverse situation (mwanaume kua na uwezo kuliko mpenzi wake) mwanamke tena atakua shap kukubali kulipiwa nauli kuliko mwanaume kubadili utaratibu wake wa leave.

We do appreciate a thoughtful gift from time to time ila acha wanawake wahongwe na walelewe, haipendezi kwa mwanaume.
 
hivi kumpa mwanamme gari kwa nini ni shida hivyo?? Naona hata wanamme wenyewe hawataki, why?

Mbona anapewa K tena labda kavu? Gari kitu gani hadi iwe shida sana mwanamke kumpa mwanamme?

Inawezekana bajeti ya gari kwa bi dada ni kitu kidogo kama kilo ya sukari.

Yaani 'gari' lol

nilitegemea kitu anachopewa mwanamme na mwanamke kisiwe kigezo sana bali 'sincerity' ya kutoa kitu hicho iwe sindano ya kushonea au mkapa tower
 
unajua kuna wakati unaweza zifuma hela ukataka kwenda sehemu nzuri, sasa umwache huyu mwenza ili asijisikie vibaya?

Na ukienda vakesheni peke yako wakati ulitaka enda na mwenzio ina maana gani?
Hapo sasa you have joined my position: Mkiwa na pato tofauti sana, ni bora mwanaume akubali ku-step down. Bila hivo ataonekana analelewa na it would be hard to tell if he is in love with the lady or with the financial comfort she provides (just like mabuzi wanajiuliza hivo linapokuja suala la kutambua mapenzi toka kwa vitotoz vyao). Hata mkipendana vipi, kama tofauti ya pato ni kubwa basi mchanga umesha ingia...
 
kwa hiyo hakuna penzi la kweli kati ya watu wenye vipato tofauti sana?

Kweli mapenzi magumu sana.

Penzi linaweza kuwepo (na mara nyingi nadhani lipo) ila itakua vigumu sana kutofautisha kati ya penzi la dhati, na tamaa ya finncial comfort. Hilo ni moja. La pili ni mazowea. wanaume wengi wamezowea kuhong, na si kuhongwa. kwao ni kama wanafanyiwa kua wanawake ndani ya couple. Ukisoma women are from venus and men from mars utaona kua wanaume wengi wanajitambua kuffatana na pato lao. Sasa ikiwa mwanamke umemzidi pato wanapoteza confidence kidogo. bora hata ndani ya ndoa sababu mara nyingi decision ya affectation of revenues zinachukuliwa pamoja hivo mwanaume anajihisi yupo "in charge" kwa kiasi fulani. but just a girlfriend? sijui kwa kweli... ngoja kwanza tuwaskilize homeboyz wanasemaje...
 
Taz, si kwamba sikupati unachosema, nakupata but sielewi kwa nini kwa hata wanamme wenyewe hamko 'comfortable' mwanamke kuwazidi kipato.
 
Last edited by a moderator:
Taz, si kwamba sikupati unachosema, nakupata but sielewi kwa nini kwa hata wanamme wenyewe hamko 'comfortable' mwanamke kuwazidi kipato.
Mi sijasema sipo comfortable na mwanamke kunizidi kipato, nimesema sipo comfortable na mwanamke anae tumia pesa nyingi kunipa zawadi, bila mimi kua na uwezo wa kumpa zawadi zinazo lingana na zake kithamani. Sababu mimi nipo comfortable zaidi ku-provide. call it mfumo dume, or machismo but that's just the way it is.
Kama ana pesa zake na anazitumia huko huko, ila akiwa na mimi sihisi tofauti hilo kua mzigo sina shida mbona?
 
hivi kumpa mwanamme gari kwa nini ni shida hivyo?? Naona hata wanamme wenyewe hawataki, why?

Mbona anapewa K tena labda kavu? Gari kitu gani hadi iwe shida sana mwanamke kumpa mwanamme?

Inawezekana bajeti ya gari kwa bi dada ni kitu kidogo kama kilo ya sukari.

Yaani 'gari' lol

nilitegemea kitu anachopewa mwanamme na mwanamke kisiwe kigezo sana bali 'sincerity' ya kutoa kitu hicho iwe sindano ya kushonea au mkapa tower
hahahahahahahaha
hapo kwenye gari labda mke wangu!
 
ata baba yetu adamu alihadaiwa na kuhongwa ka tunda na mama yetu! enzi zileee za bustanini
 
Hiyo si kuhonga
Mie sioni tatizo kama mnapendana kwa nini kila siku kusubiri kupewa zawadi?
Ukipita shop ukiona shati inamfaa Boifie ama mpenze mpelekee
Kama amekwama sehemu kumsaidia pia sio kuhonga

Sitaki wanawake wote duniani, nakutaka wewe tu! Wapi unapatikana ati?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom