Mwanamke 'kumhonga' Mwanamme . . . | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke 'kumhonga' Mwanamme . . .

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kongosho, Jul 27, 2012.

 1. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Naomba kupata mawazo yenu
  imekaaje kwa mwanamke 'kumhonga' mwanamme?

  Nadhani nimeishi kwenye jamii amabayo mwanamme ndio 'breadwinner' na ndio inaonekana halali hata yeye kumhonga mwanamke na si kinyume chake.

  Labda nitoe mfano
  Mdada ana kipato kuliko mpenzi wake (ikimbukwe si mme)
  Na kuna vitu ambavyo anataka kumpa ili waende sambamba
  vinaweza kuwa vitu vidogo vidogo kama mavazi n.k na aina hizo za huduma.

  Je hii imekaaje? Inakubalika machoni pa walaji?
  Na kama wewe ni mkaka mwanamke akikupa vitu hivyo utajisiakiaje?
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Kwanza definition ya kuhonga nadhani ni ngumu sana.

  Ila mtazamo wangu, 'kuhonga' as you put it, ama kumnunulia mwenza shati, soksi hata suit na simu haihitaji uwe umemzidi kipato. Kuna watu wana a 'giving heart'. Na haijalishi kama ni kitu cha tshs 500 ama kupika maandazi matamu na kumpelekea mpenzio. Kama unampenda mtu automatikale ukiona hata shati zuri unalipatia picha lilivyomkaa na unaamua kumnunulia.

  Mie nahonga sana kama hiyo ndo definition ya kuhonga aisee. Huna kakako kimeo kimeo hivi yuko pending?
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Mi naona kuna tofauti pale mwanamme anapokuwa ana kipato kuliko mwanamke
  Hapo mwanamke hata akimpa ataoneka anampa zawadi tu sababu kapenda na mwanamme kaamua kuchukua tu.

  Lakini pale mwanamke anapokuwa na kipato kuliko mwanamme, lazima utasikia 'huyu dada kiazi kweli, anamhonga mwanamme. Yaani anamnunulia kila kitu hadi pichu'

  Watu huwa hatuisemi kama ' a giving heart' rather mwanamke anaonekana 'mjinga au kipofu wa mapenzi'

   
 4. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  sasa hiyo sio kuhonga...leo hii hata kama mwanaume anaingiza hela zaidi ya mwanamke bado mwanamke anaweza kumnunulia vitu mwanaume sasa utaita hiyo kuhonga? utakataa? nadhani life ya siku hizi ni both ways, mnaweza kwenda dinner mwanamke akalipia bill..sa hapo tumehongwa? sidhani, kuna wanawake wengine they want to feel wana contribute kwenye rship na mi napenda wanawake wa namna hii.. ila kuna ile mianamke mingine hata kama ina hela vipi mradi yuko na mwanaume basi hatatoa hata senti tano..
   
 5. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  ni kitu kizuri sana kupewa zawadi (kuhongwa inaleta connotations za mtu kuhitaji kitu toka kwako in return) na mpenzi wako wa kike na haijalishi kama anakuzidi au unamzidi kipato; i hate the one-way traffic kind of relationship ambapo mwanaume ndiye anayeonekana anatoa hiki na kile kwa mwanamke kila wakati
   
 6. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,431
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mwanaume ahongwi analelewa
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  mtotowamjini na cartura, umeona Smile alivyosema?

  Mwanamme analelewa sio kuhongwa.
  Na nimeona mara nyingi sana mwanamke anakuwa criticized kwa kumpa vitu mwanamme hasa anapomzidi kipato.
  Utasikia kazi 'kulea wanamme tu'

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,631
  Likes Received: 1,389
  Trophy Points: 280
  Haswaaaaa! kama mimi nahisi nalelewa kupita kiasi and i like it
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Hiyo si kuhonga
  Mie sioni tatizo kama mnapendana kwa nini kila siku kusubiri kupewa zawadi?
  Ukipita shop ukiona shati inamfaa Boifie ama mpenze mpelekee
  Kama amekwama sehemu kumsaidia pia sio kuhonga
   
 10. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,188
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Hiyo mbona mzuka tu bana!
   
 11. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ni mfumo tu wa maisha anaoishi mwanamke na mwanamme hasa wapenzi, na hapoo huwa wanapeana zawadi zio kwamba wanahongana, mimi kwa upande wangu huwa natoa zaidi kwa mwanamke kuliko yeye anavyonipa lakini huwa nafurahia sana ninapopokea zawadi zake
   
 12. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #12
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Kwanza kama hampo kwenye ndoa,kupeana hela sio lazima,huu ni msimamo wangu.Kuhusu mwanamke kumpa hela mwanaume(silipendi neno kuhonga,tafsiri yake haimaanishi ulichokisema)hakuna ubaya wowote.Wala halinipi shida kabisa,ndo maana mwanamke mwenye hela na asiekua nazo kwangu wote hawana tofauti na ni WANAWAKE tu!
   
 13. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kuna shida gani kumuhonga unayempenda ukianza kuangalia kila kitu kwa jicho la pembeni u will never enjoy mapenzi badale yake ni kuishi kwa kuviziana.
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Imekaa sawa na mwanaume kumhonga mwanamke, malengo ni yale yale njia tofauti tu
   
 15. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #15
  Jul 27, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  hapo labda Smile anazungumzia vile visharobaro vinavyowekwa ndani na ma-sugarmumy ambayo ni phenomenon tofauti kabisa ukilinganisha na ile ya wapenzi kupeana zawadi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. O

  Old Moshi Senior Member

  #16
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  unajua neno kuhonga halisound vizuri.. Tatizo kubwa la jamii yetu; mwanamke akimfanyia kitu mwanaume itaitwa kuhonga. cha msingi ni kudecide mapenzi yenu mnayaendesha kama nyie mnavotaka au kama jamii inavotaka.
   
 17. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #17
  Jul 27, 2012
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,877
  Likes Received: 1,046
  Trophy Points: 280
  HAINA SHIDA!! Kutokukubali zawadi kutoka kwa mwanamke ni inferiority complex!! ongoka utoke huko!!
   
 18. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #18
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Kongosho sijui maisha kwanii yako bias kwa mwanamke. skiliza mwanaume aitoa inaonekana ama kutoa kwa ulazima lkn mwanamke inaonekana kama analinunua penzi umeona eeh! Ila ukweli binafsi nilipopenda hata pesa ya gesti nilitoa pale ambapo mwenzangu alitindikiwa na pia kwakua nilikuwa napenda apendeze basi hata pamba nilimnunulia za woolworth sikuweza lkn za manzese nilimudu.

  ila sasa kuna wale ambao wananunua penzi kabisa wazwazi hili nimelishuhudia pale jimama linapomlea kijana hali akijua no future ni just kula raha tu. mimi hii huwa si admit kabisa mara nyingi hawa huwa wanatoa hela mpaka milion wa kijana sasa najiuliza what next?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #19
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  pamt, nadhani wewe umenielewa kabisa.

  Nimefikia kuandika haya baada ya kuona rafiki yangu akipata changamoto toka kwa kila mtu anayemzunguka.
  Kisa ana mahisiano na kaka anayemzidi sana kipato, so kuna vitu inabidi ampe ili waende sambamba.

  Kuna raha gani ya kutoka na mwanamme wewe mwanamke umemzidi sana na hali waweza mpiga tafu mkawa karibu sawa?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #20
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Ndo najitahidi kuongoka hapa.

   
Loading...