Ubaguzi, Uchawi na Ushirikina kikwazo cha maendeleo baadhi ya vijiji Tanzania

mocoservices

Member
Feb 24, 2023
45
144
Habari yako mwana jukwaa.

Naandika uzi huu nikiwa Katikati ya Tanzania (kanda ya kati). Nimeishi hapa kwa miezi 4 sasa, kwa hiyo ninacho andika nina kifahamu vizuri kwa kushuhudia kwa macho yangu.

Naishi kwenye mkoa wa 3 toka mwisho kwa umasikini nchini hapa, mkoa ambao elimu iko chini sana na mwamko wa elimu bado uko chini sana.

Kuna vitu vinafanyika vinashangaza sana. Mosi, ni wananchi hawa mapenzi (ngono) inapewa kipaumbele sana. Nimekuwa nikishuhudia watu wanaenda kwa waganga ili kupata mwanaume au mwanamke, nao kwa ni kawaida tu kuongelea kwamba "akikataa namwendea kwa mganga." Hii hali si kwa watu wazima tu bali hata wanafunzi, mtoto wa kike anamwendea mwalimu wake kwa mganga ili awe naye, na baadhi ya wazazi wanasaidia mabinti zao kufanikisha hayo, hasa wanawake.

Pili, mtu mgeni (hasa watumishi wa serikali) akiwa anajituma katika shughuli mbalimbali za uchumi hugeuka kuwa adui wao. Atafanyiwa vitimbwi vyote, kwa makusudi kabisa hawatanunua bidhaa yako hata kama ni nzuri. Yaani wapo tayari wanunue dagaa wenye mchanga kuliko kununua wasio na mchanga kutoka kwa mtumishi.

Wakiona bado unakomaa, basi mbinu za giza hutumika, bidhaa zitaharibika bila sababu, watanyagia hela (kuvuta kichawi) na wataenda mbali hata kukuroga wewe binafsi. Usiku utakuwa wa shida sana, utaona paka wenye sura za watu, vyakula vitachacha sana. Na kama umepanga na unaishi na mwenye nyumba atakuletea figisu, ukiwa na fridge utaambiwa "hilo fridge lako linakula sana umeme" ili hali yeye pia analo aina ileile na analitumia.

Tatu, mashamba huku hayalimwi bila dawa. Kipindi cha kuandaa mashamba mwezi wa 9, 10 na 11 basi utashuhudia wananchi hawa wakialika waganga kuzindika mashamba yao. Wao wanasema usipozindika shamba hupati kitu hata ukilima kwa utalaamu mkubwa. Pili wakima mazao yakikomaa mganga anarudi kuzindika mazao.

Nne na mwisho, mabaya na kesi zinazotokea wanatamani iwe ni mtumishi amepata. Kwa mfano ikitokea mwanafunzi amepata ujauzito wao wanatamani mwalimu ndiye awe hatiani, na kama kuna namna fulani mwalimu alikuwa na ukaribu na mwanafunzi watakuandama sana.

Mwezi uliopita tu yametokea matukio mawili ya ujauzito kwa wanafunzi lakini wananchi wakawa wanashinikiza kuwa haiwezekani kuwa walimu hawahusiki. Lakini ukweli ni kwamba vijana wao ndo wamesababisha na ikibainika ni vijana wao wamefanya hivyo wanamaliza kifamilia, sasa itokee ni mtumishi ni umeisha aisee.

Kwa kuhitimisha, naomba serikali iangalie mambo haya kwa jicho la tatu. Najua UCHAWI ni imani na kuthibitishwa ni kazi sana. Lakini serikali inawajibu mkuu wa kulinda watumishi wake. Watumishi wengi wanaishi mjini na kufanya kazi vijijini si kwamba wanapenda kufanya hivyo bali wanalazimishwa na mazingira.

Fikiria sehemu ambayo hudumu za kijamii ni za shida (hakuna maji mathalani) mtumishi anatakiwa apambane na ushirikina na uchawi pamoja na ubaguzi. Hapo ndipo wengi wanaamua kukimbilia mijini au familia zao ziishi mjini na wao wapange mageto karibu na mazingira ya kazi na kurudi kwenye familia zao siku za mwisho wa wiki na kufanya watumishi hawa kuisha kwa gharama kubwa sana. Watumishi hawa hawana furaha kabisa, wengi wanawaza kuhama tu iwapo wakipata nafasi.

Naomba serikali ipange mkakati wa kusaidia maalumu (kwenye project yangu chuo niliandika kuhusu Unjust Distribution of Teacher in Tanzania) baadhi ya vitu nilivyobainisha ni kuwa baadhi ya maeneo si kwamba hayapata watumishi walimu mathalani ila walimu wanakimbia maeneo hayo kulingana na mambo kadha wa kadha ikiwemo uchawi na ushirikina.

Nilipendekeza kuwa kwepo na "scheme" maalumu ya kupeleka vijana huko kwa kujitolea huku serikali ikiweka makazi mazuri shuleni na mishahara mizuri inatakayo wavutia kwenda huko, na iwe ni mkataba, kwa mfano miaka 3 na baada ya hapo warusiwe kuhama na waende wengine.

Pia nitoe rai kwa wananchi wa sehemu kama hizo, maendeleo huja kutokana na mwingiliano wa watu, watu wapya huleta mawazo mapya na uzoefu mpya, acheni ushirikina na kuroga watu wanaokuja kwenye vijijini vyenu, si kwamba mnakomoa watu hao bali mnafanya Watoto wenu wasipate elimu nzuri, na matatibabu yanakuwa duni. Acheni mara moja.
 
Usimwache mwanamke mchawi kuishi...

Vita vyetu sio vya damu na nyama ni vita ya kiroho...

Haya ni maneno ya Biblia...
 
Back
Top Bottom