Kwanini ni lazima nioe Mwanamke wa Kaskazini?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
Habari za Leo.

Kwangu ni lazima kuoa Mwanamke wa Kaskazini au jamii zinazokaribiana Mila, desturi, falsafa na mitizamo kama ya Wanawake WA Kaskazini. Kuoa Mwanamke wa Kaskazini kwangu Sio Optional, bali ni lazima. Hii itabaki kuwa hivyo ilivyo.

Sio kila mtu atakayetaka kujua sababu ya Mimi kuwa na uamuzi huo, kwani ni uamuzi binafsi unaohusu Maisha yangu mwenyewe lakini ninauhakika wapo watakaotaka kujua sababu ya Mimi kuwa na Uamuzi huo.

Wanawake WA Kaskazini ni Wanawake wote wenye tabia halisi za Mwanamke wa shoka bila kujali amezaliwa Iringa, Kigoma, mtwara, Morogoro, Mwanza, Moshi, Musoma .n.k.

Zifuatazo ni sababu za Kwa nini Taikon lazima Aoe Mwanamke wa Kaskazini;

1. Wanapenda Mali.
Kwa jamii zingine huona Jambo Hilo katika mtazamo Hasi lakini Kwa wanaume Strong tunachukulia Jambo hilo kama Motivation.
Mwanamke lazima apende Mali, ili kuzalisha Vijana wachapakazi na sio vijana wavivu na wazembe wazembe.

Ili mwanaume uheshimike Mali ni moja ya vigezo vya kumfanya mwanaume aonekane yupo serious na Maisha. Fanya kazi Kwa bidii na juhudi yenye Akili.
Ukiona eneo hilo limekushinda Hama tafuta sehemu nyingine, sio unakaa sehemu moja kama Mwanamke.
Wanawake WA Kaskazini kumwambia unaenda kutafuta Maisha nchi za mbali yeye haoni shida, au kumwambia muondoke wote muhame mwende Mikoa ya mbali kwao sio tatizo ili mradi umwambie kuna mchongo wa kutafuta Maisha.

Hii ni tofauti na Baadhi ya Wanawake WA jamii zingine, ukiwambia mhame mwende mbali watawaza sijui wazazi sijui ndugu kwamba watakuwa mbali na nyumbani.

Kupenda Mali kunazalisha Vijana wawe wachapakazi na Risk taker,

2. Wanakiu ya Maendeleo Kwa Watoto wao.
Wanawake WA Kaskazini hata umtelekezee mtoto hapo ninakuhakikishia lazima atasoma kivyovyote vile bila kutegemea Pesa yako.
Wanawake WA Kaskazini wengi wao ndio wazalishaji hasa WA hizi kazi ndogondogo Kam umachinga WA nguo, kuuza mitumba, kulima vibarua kwenye mashamba, n.k.
Vijana wengi wa Kaskazini wamesomeshwa na Mama zao.
Wababa wanasimamia shoo kubwakubwa kama ujenzi wa nyumba, ununuzi wa viwanja na utanuzi wa Ngome na miradi.

Sasa ni Mwanaume gani Strong ambaye hatataka kuoa Mwanamke wa Kaskazini ikiwa anauhakika hata asipokuwepo Watoto wake wataishi vizuri, sidhani kama kuna mwanaume wa hivyo.

3. Hawapendi wanaume Cheaters.
Ukitaka uonje joto la Jiwe basi OA Mwanamke wa Kaskazini alafu mfanyie mambo ya kiduwanzi, mcheat mara Kwa mara uone nini kitatokea.
Utawahadithia wenzako na utakuwa fundisho Kwa wengine. Kwanza lazima utoke ndani ya nyumba kivyovyote iwe Kwa Amani au Kwa Shari.
Wale wanaume Werevu wakishaona wametosheka na kukinaiwa na Wake zao huwaachia Nyumba(Mji) na kuendelea na Maisha mengine. Lakini hawapeani Talaka. Hiyo mbinu inatumiwa na wanaume wajanja.

Lakini wale wanaume wajinga hugangamala hapohapo na ndipo ubaya wa Wanawake WA Kaskazini utakapoonekana. Hakuna rangi ambayo hautaacha kuiona.

4. Huwezi kuwatapeli Mali Kama mlichuma Wote.
Kwanza hakuna kazi ngumu kama kumtoa Mwanamke wa Kaskazini ndani ya nyumba hasa kama mmejenga wote. Ni ngumu Sana. Kesi hiyo itasimamiwa vilivyo na atapata uungwaji mkono na Ndugu zake Kwa namna yoyote Ile.
Hii inamaanisha unapooa Mwanamke wa Kaskazini lazima ujue mlango wa kutokea endapo ikitokea mkiachana. Kwani wengi wao wana-backup ya Kufa mtu Kutokana na umoja waliokuwa nao.
Hivyo kama Mwanaume kwenu ukoo wenu hauna umoja kila MTU kivyake inaweza kukugharimu.

Hii inahamasisha Vijana kuunganisha nguvu na Ndugu zao. Sio kijana ukishaoa tuu unakata mawasiliano na Ndugu zako unashindwa hata kuwainua, ninakuhakikishia inaweza ikakusumbua Huko Mbele.

5. Ni Wakali na hawadekezi Watoto.
Labda ninashindwa kueleza Jambo hili vizuri. Lakini Wamama wa Kaskazini ni Wakali Kwa Watoto kuliko Wababa. Wanaume ni Wakali linapokuja suala la utafutaji na mipaka ya Ardhi lakini kwenye malezi wamama wameshindikana.

6. Ni washamba Kwa Mambo ya Kijingajinga yasiyoingiza Pesa.
Wanawake WA Kaskazini ni washamba Kwa mambo yasiyo na tija, mfano sijui udaku wa masupastaa, sijui kukata mauno au kucheza, sijui kuunganisha madanga, Kwa kweli Kwa hayo mambo NI washamba, wengi hawajui na hawafuatilii hivyo vitu.

Wao wanachojua ni Mambo ya Pesa, sijui Vikoba, Michezo, Brac, kuuza Kwa kukopeshana, ujenzi, usomeshaji wa watoto, biashara n.k. hayo ndio mambo Yao.

7. Wengi Hawana Umalaya.
Umalaya ni tabia mara nyingi inayochangiwa na Mwanamke kuwa tegemezi, utegemezi unaleta tamaa alafu Pesa hauna.
Utachunguza mwenyewe Wanawake wenye Tabia za kimalaya wengi wanatoka jamii tegemezi ambazo wao kila Pesa wanamtegemea mwanaume.
Pesa ya Kodi mwanaume,
Pesa ya chakula mwanaume,
Pesa ya kusomeshea mtoto mwanaume,
Pesa ya mavazi mwanaume
Pesa ya kila kitu mwanaume alafu kazi huna Mwanamke ataachaje kuwa Malaya.
Wanawake wengi WA Kaskazini na jamii zinazofanana NAO ni wachakarikaji, wanajua Pesa inavyotafutwa Kwa kazi ndogondogo na biashara za Kati.
Mwanaume akitafutwa ni kwaajili ya kufanya Maisha.
Weka niweke.

8. Hawana unyenyekevu Kwa Wanaume wapumbavu.
Wanawake WA Kaskazini wamefundishwa kujitambua, Haki zao. Mheshimu atakuheshimu, mpende atakupenda, mshirkishe atakushirikisha. Hawana mambo ya unafiki.
Wanawake WA Kaskazini kwenye hii nchi ndio wanaoongoza Kwa kuhonga Vijana waaminifu. Yaani ukitaka kwenda naye Sawa basi Mpe Haki zake naye akupe Haki zako.

Tabia hiyo inachukuliwa na wanaume dhaifu kama ujeuri, kiburi na kutokuwa na heshima. Jambo ambalo sio Sahihi.
Mwanamke wa Kaskazini na jamii zinazofanana nayo hawezi kukuheshimu kama Mume wake ikiwa kuna mambo unapuyanga, yaani ufanye uhuni na umalaya wa kujirudiarudia alafu utegemee heshima. Hizo ni dharau kubwa.

Sisi kama Kaka zao na Baba zao tumewafundisha wasivumilie hiyo Hali endapo ikijitokeza Kwa kujirudiarudia mara Kwa mara. Ndio maana tunawafanya wajitegemee kiuchumi zaidi ili wasinyanyasike na kunyanyaswa na wanaume wendawazimu.

Hakuna mwenye Haki ya kufanya uhalifu au uovu Kwa Mwenzake iwe Mwanamke au Mwanaume. Mimi kuwa mume wa Fulani sio kigezo cha kumpiga au kumrudia Usiku WA manane nikiwa nimelewa, hiyo hauvumiliki, na ninachowapendea Wanawake WA Kaskazini hawatakukopesha watakujibu Kwa nguvu zote.
Aidha muachane au ubadilike. Na mkiachana mtasomana kwenye mgawanyo wa Mali na kuhudumia Watoto.

Kama ni MTU mwenye Tabia za umungu mtu sikushauri ukaoe Kaskazini, kama ni Mwanaume usiyependa HAKI basi Kaskazini sio sehemu sahihi kwako.
Mnaweeza Anza vizuri hasa kama unamali au unavikazi kazi vyenye kipato lakini ninakuhakikishia Baada ya miaka 20 picha litaanza kugeuka, hapo Watoto wamekua ni muda wa kujibu mapigo.

Wanawake WA Kaskazini wengi huonekana ni Feminist Kutokana na Ile Hali wanayokabiliana na uonevu na unyanyasaji wa baadhi ya wanaume wajingawajinga.

Unapomuoa Mkeo elewa kuwa huyo ni Msaidizi wako, mnasaidizana majukumu ya kimaisha na sio mmoja kumfanya mtumwa mwingine. Mwanaume asiwe mtumwa wa Mwanamke, pia Mwanamke asiwe mtumwa wa Mwanaume. Wote muwe kitu kimoja. Mnapokabiliana na mambo yenu yawekeni bayana mjue mnayatatuaje,

Ugumu unatoka wapi?
Wengi hujikuta katika ubinafsi ndio maana migogoro haiishi.
Mfano Mwanamke anazalisha laki tano kwa mwezi, mwanaume naye laki tano.
Hiyo Pesa Kwa nini msiiweke pamoja kisha muipangie matumizi pamoja?
Au mmoja anapokea laki tatu mwingine laki Saba. Mnaona shida gani kuunganisha hizo Pesa.
Kama ni kusaidia nyumbani si msaidie, mnaona shida gani?
Semeni Kila mwezi elfu 50 itaenda familia ya MKE, elfu 50 itaenda familia ya Mme. Jumla ni laki moja itatengwa Kwa Pesa ya Wazazi.

Sasa mkishaanza kuleta mambo ya mzazi wangu, mzazi wangu sijui kanisomesha sijui kanizaa, kwani Nani hakuzaliwa? Kwani Nani hakusomeshwa, sijui Mimi nimekuoa nimekutolea Mahari hiyo Mahari ndio nimemalizana na kwenu, hivi wewe ni Kichwa? Mahari ya milioni mbili au hata milioni 10 ndio umemalizana uliambiwa hiyo ni Ng'ombe?

Alafu kuna mizazi mingine kama imelogwa, ati kisa limesomesha basi linataka mtoto wake amhudumie yeye kuliko familia yake, umelogwa wewe mzazi, kama unataka kumpangia matumizi mwanao au Binti yako ungemuoa au kuolewa naye, pumbavu.

Watu wamejaa ubinafsi Sana!

Ngoja nipumzike!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Hata mimi wanawake wa kaskazini nawakubali sana hawaendekezi mapenzi na upuuzi ni pesa kwanza, jitu linatoka huko na ubabe wake linataka limuonee mtoto wa watu kisa yeye ni mwanaume, mimi mwanaume hata awe ametoka sijui kanda ya barafu kama halijielewi halitapata hata theluthi ya heshima yangu na hakuna kitu atanifanya ni either abadilike au kila mtu ashike hamsini zake
kwani wewe sio wa kaskazini?? ulivo mkorofi hivo 😂
 
Hata mimi wanawake wa kaskazini nawakubali sana hawaendekezi mapenzi na upuuzi ni pesa kwanza, jitu linatoka huko na ubabe wake linataka limuonee mtoto wa watu kisa yeye ni mwanaume, mimi mwanaume hata awe ametoka sijui kanda ya barafu kama halijielewi halitapata hata theluthi ya heshima yangu na hakuna kitu atanifanya ni either abadilike au kila mtu ashike hamsini zake
Nime'subscribe...
Nitarudi tena Mdogo wangu..
 
🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧🔧
 
Habari za Leo.

Kwangu ni lazima kuoa Mwanamke wa Kaskazini au jamii zinazokaribiana Mila, desturi, falsafa na mitizamo kama ya Wanawake WA Kaskazini. Kuoa Mwanamke wa Kaskazini kwangu Sio Optional, bali ni lazima. Hii itabaki kuwa hivyo ilivyo.

Sio kila mtu atakayetaka kujua sababu ya Mimi kuwa na uamuzi huo, kwani ni uamuzi binafsi unaohusu Maisha yangu mwenyewe lakini ninauhakika wapo watakaotaka kujua sababu ya Mimi kuwa na Uamuzi huo.

Wanawake WA Kaskazini ni Wanawake wote wenye tabia halisi za Mwanamke wa shoka bila kujali amezaliwa Iringa, Kigoma, mtwara, Morogoro, Mwanza, Moshi, Musoma .n.k.

Zifuatazo ni sababu za Kwa nini Taikon lazima Aoe Mwanamke wa Kaskazini;

1. Wanapenda Mali.
Kwa jamii zingine huona Jambo Hilo katika mtazamo Hasi lakini Kwa wanaume Strong tunachukulia Jambo hilo kama Motivation.
Mwanamke lazima apende Mali, ili kuzalisha Vijana wachapakazi na sio vijana wavivu na wazembe wazembe.

Ili mwanaume uheshimike Mali ni moja ya vigezo vya kumfanya mwanaume aonekane yupo serious na Maisha. Fanya kazi Kwa bidii na juhudi yenye Akili.
Ukiona eneo hilo limekushinda Hama tafuta sehemu nyingine, sio unakaa sehemu moja kama Mwanamke.
Wanawake WA Kaskazini kumwambia unaenda kutafuta Maisha nchi za mbali yeye haoni shida, au kumwambia muondoke wote muhame mwende Mikoa ya mbali kwao sio tatizo ili mradi umwambie kuna mchongo wa kutafuta Maisha.

Hii ni tofauti na Baadhi ya Wanawake WA jamii zingine, ukiwambia mhame mwende mbali watawaza sijui wazazi sijui ndugu kwamba watakuwa mbali na nyumbani.

Kupenda Mali kunazalisha Vijana wawe wachapakazi na Risk taker,

2. Wanakiu ya Maendeleo Kwa Watoto wao.
Wanawake WA Kaskazini hata umtelekezee mtoto hapo ninakuhakikishia lazima atasoma kivyovyote vile bila kutegemea Pesa yako.
Wanawake WA Kaskazini wengi wao ndio wazalishaji hasa WA hizi kazi ndogondogo Kam umachinga WA nguo, kuuza mitumba, kulima vibarua kwenye mashamba, n.k.
Vijana wengi wa Kaskazini wamesomeshwa na Mama zao.
Wababa wanasimamia shoo kubwakubwa kama ujenzi wa nyumba, ununuzi wa viwanja na utanuzi wa Ngome na miradi.

Sasa ni Mwanaume gani Strong ambaye hatataka kuoa Mwanamke wa Kaskazini ikiwa anauhakika hata asipokuwepo Watoto wake wataishi vizuri, sidhani kama kuna mwanaume wa hivyo.

3. Hawapendi wanaume Cheaters.
Ukitaka uonje joto la Jiwe basi OA Mwanamke wa Kaskazini alafu mfanyie mambo ya kiduwanzi, mcheat mara Kwa mara uone nini kitatokea.
Utawahadithia wenzako na utakuwa fundisho Kwa wengine. Kwanza lazima utoke ndani ya nyumba kivyovyote iwe Kwa Amani au Kwa Shari.
Wale wanaume Werevu wakishaona wametosheka na kukinaiwa na Wake zao huwaachia Nyumba(Mji) na kuendelea na Maisha mengine. Lakini hawapeani Talaka. Hiyo mbinu inatumiwa na wanaume wajanja.

Lakini wale wanaume wajinga hugangamala hapohapo na ndipo ubaya wa Wanawake WA Kaskazini utakapoonekana. Hakuna rangi ambayo hautaacha kuiona.

4. Huwezi kuwatapeli Mali Kama mlichuma Wote.
Kwanza hakuna kazi ngumu kama kumtoa Mwanamke wa Kaskazini ndani ya nyumba hasa kama mmejenga wote. Ni ngumu Sana. Kesi hiyo itasimamiwa vilivyo na atapata uungwaji mkono na Ndugu zake Kwa namna yoyote Ile.
Hii inamaanisha unapooa Mwanamke wa Kaskazini lazima ujue mlango wa kutokea endapo ikitokea mkiachana. Kwani wengi wao wana-backup ya Kufa mtu Kutokana na umoja waliokuwa nao.
Hivyo kama Mwanaume kwenu ukoo wenu hauna umoja kila MTU kivyake inaweza kukugharimu.

Hii inahamasisha Vijana kuunganisha nguvu na Ndugu zao. Sio kijana ukishaoa tuu unakata mawasiliano na Ndugu zako unashindwa hata kuwainua, ninakuhakikishia inaweza ikakusumbua Huko Mbele.

5. Ni Wakali na hawadekezi Watoto.
Labda ninashindwa kueleza Jambo hili vizuri. Lakini Wamama wa Kaskazini ni Wakali Kwa Watoto kuliko Wababa. Wanaume ni Wakali linapokuja suala la utafutaji na mipaka ya Ardhi lakini kwenye malezi wamama wameshindikana.

6. Ni washamba Kwa Mambo ya Kijingajinga yasiyoingiza Pesa.
Wanawake WA Kaskazini ni washamba Kwa mambo yasiyo na tija, mfano sijui udaku wa masupastaa, sijui kukata mauno au kucheza, sijui kuunganisha madanga, Kwa kweli Kwa hayo mambo NI washamba, wengi hawajui na hawafuatilii hivyo vitu.

Wao wanachojua ni Mambo ya Pesa, sijui Vikoba, Michezo, Brac, kuuza Kwa kukopeshana, ujenzi, usomeshaji wa watoto, biashara n.k. hayo ndio mambo Yao.

7. Wengi Hawana Umalaya.
Umalaya ni tabia mara nyingi inayochangiwa na Mwanamke kuwa tegemezi, utegemezi unaleta tamaa alafu Pesa hauna.
Utachunguza mwenyewe Wanawake wenye Tabia za kimalaya wengi wanatoka jamii tegemezi ambazo wao kila Pesa wanamtegemea mwanaume.
Pesa ya Kodi mwanaume,
Pesa ya chakula mwanaume,
Pesa ya kusomeshea mtoto mwanaume,
Pesa ya mavazi mwanaume
Pesa ya kila kitu mwanaume alafu kazi huna Mwanamke ataachaje kuwa Malaya.
Wanawake wengi WA Kaskazini na jamii zinazofanana NAO ni wachakarikaji, wanajua Pesa inavyotafutwa Kwa kazi ndogondogo na biashara za Kati.
Mwanaume akitafutwa ni kwaajili ya kufanya Maisha.
Weka niweke.

8. Hawana unyenyekevu Kwa Wanaume wapumbavu.
Wanawake WA Kaskazini wamefundishwa kujitambua, Haki zao. Mheshimu atakuheshimu, mpende atakupenda, mshirkishe atakushirikisha. Hawana mambo ya unafiki.
Wanawake WA Kaskazini kwenye hii nchi ndio wanaoongoza Kwa kuhonga Vijana waaminifu. Yaani ukitaka kwenda naye Sawa basi Mpe Haki zake naye akupe Haki zako.

Tabia hiyo inachukuliwa na wanaume dhaifu kama ujeuri, kiburi na kutokuwa na heshima. Jambo ambalo sio Sahihi.
Mwanamke wa Kaskazini na jamii zinazofanana nayo hawezi kukuheshimu kama Mume wake ikiwa kuna mambo unapuyanga, yaani ufanye uhuni na umalaya wa kujirudiarudia alafu utegemee heshima. Hizo ni dharau kubwa.

Sisi kama Kaka zao na Baba zao tumewafundisha wasivumilie hiyo Hali endapo ikijitokeza Kwa kujirudiarudia mara Kwa mara. Ndio maana tunawafanya wajitegemee kiuchumi zaidi ili wasinyanyasike na kunyanyaswa na wanaume wendawazimu.

Hakuna mwenye Haki ya kufanya uhalifu au uovu Kwa Mwenzake iwe Mwanamke au Mwanaume. Mimi kuwa mume wa Fulani sio kigezo cha kumpiga au kumrudia Usiku WA manane nikiwa nimelewa, hiyo hauvumiliki, na ninachowapendea Wanawake WA Kaskazini hawatakukopesha watakujibu Kwa nguvu zote.
Aidha muachane au ubadilike. Na mkiachana mtasomana kwenye mgawanyo wa Mali na kuhudumia Watoto.

Kama ni MTU mwenye Tabia za umungu mtu sikushauri ukaoe Kaskazini, kama ni Mwanaume usiyependa HAKI basi Kaskazini sio sehemu sahihi kwako.
Mnaweeza Anza vizuri hasa kama unamali au unavikazi kazi vyenye kipato lakini ninakuhakikishia Baada ya miaka 20 picha litaanza kugeuka, hapo Watoto wamekua ni muda wa kujibu mapigo.

Wanawake WA Kaskazini wengi huonekana ni Feminist Kutokana na Ile Hali wanayokabiliana na uonevu na unyanyasaji wa baadhi ya wanaume wajingawajinga.

Unapomuoa Mkeo elewa kuwa huyo ni Msaidizi wako, mnasaidizana majukumu ya kimaisha na sio mmoja kumfanya mtumwa mwingine. Mwanaume asiwe mtumwa wa Mwanamke, pia Mwanamke asiwe mtumwa wa Mwanaume. Wote muwe kitu kimoja. Mnapokabiliana na mambo yenu yawekeni bayana mjue mnayatatuaje,

Ugumu unatoka wapi?
Wengi hujikuta katika ubinafsi ndio maana migogoro haiishi.
Mfano Mwanamke anazalisha laki tano kwa mwezi, mwanaume naye laki tano.
Hiyo Pesa Kwa nini msiiweke pamoja kisha muipangie matumizi pamoja?
Au mmoja anapokea laki tatu mwingine laki Saba. Mnaona shida gani kuunganisha hizo Pesa.
Kama ni kusaidia nyumbani si msaidie, mnaona shida gani?
Semeni Kila mwezi elfu 50 itaenda familia ya MKE, elfu 50 itaenda familia ya Mme. Jumla ni laki moja itatengwa Kwa Pesa ya Wazazi.

Sasa mkishaanza kuleta mambo ya mzazi wangu, mzazi wangu sijui kanisomesha sijui kanizaa, kwani Nani hakuzaliwa? Kwani Nani hakusomeshwa, sijui Mimi nimekuoa nimekutolea Mahari hiyo Mahari ndio nimemalizana na kwenu, hivi wewe ni Kichwa? Mahari ya milioni mbili au hata milioni 10 ndio umemalizana uliambiwa hiyo ni Ng'ombe?

Alafu kuna mizazi mingine kama imelogwa, ati kisa limesomesha basi linataka mtoto wake amhudumie yeye kuliko familia yake, umelogwa wewe mzazi, kama unataka kumpangia matumizi mwanao au Binti yako ungemuoa au kuolewa naye, pumbavu.

Watu wamejaa ubinafsi Sana!

Ngoja nipumzike!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
True IGWE IGWE IGWE IGWE IGWE IGWE IGWE IGWE UMEONGEA POINT NA JARIBU KUWAAMBIA NA HAWATAKAGI KUSIKIA UKWELI . LEO UMESEMWA
 
Nadhani huu uzi mleta uzi kauleta baada ya kusoma uzi fulani hapa JF ambao umeongelea wanawake wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha kwa tabia zao za kikauzu, kuendekeza utafutaji wa pesa uliopitiliza, kutokuwa romantic kwa wanaume zao etc.

Sijui wewe mleta uzi una asili ya wapi ila kwa watu ambao wameoa huko au wameishi huko au wale wenyeji wa huko then yale mambo yaliyosemwa ni dhahiri kuwa yapo na yanatendeka.

Kimsingi sio chuki au kuwachafua ila ni kuzungumza bayana tabia ambazo zinaharibu taswira yao kwa ujumla. Si kweli kwa wanawake wa Kilimanjaro au huko Arusha wote wapo hiyo ila majority wanahizo haiba.

Hizo tabia zinazolalamikiwa hata Kenya zimeonekana sana kwenye jamii za wanawake wa huko na ukisiliza wanaume wa kule malalamiko yao unaweza kudhania wanaongelea wanawake wa maeneo hayo.

Mimi nimefanikiwa kuishi hayo maeneo kwa muda mrefu zaidi ya miaka kumi nikiwa mkazi. Nikwambie tu wanachosema raia hapa ni kweli kwa asilimia kubwa. Kama kuna mtu anatetea basi ni kwa kutaka kuonekana shujaa au mtetezi wa wanawake ila tukisimama kwenye haki hawa wadada wa pande hizo wanazingua tena sana.

Kutafuta pesa ni kitu muhimu ila sasa kisikupe ukichaa ukawa kama mwehu katika kuzitafuta na ndio maana wengi wao huwa hawafanikiwi wanaishia kuwa wapambanaji tu ila hela wanaisikia tu hawaimiliki hadi uzee unawakuta.

Wanaume wengi wa pande zile huwa wakiona mwanamke amezidisha fujo na sifa wanaondoka bila taarifa na ndio maana ukienda kule katika kaya 10 basi 9 ni mama na watoto wake tu baba hata sijui yupo wapi ila yupo ameikimbia familia sababu mwanamke anampelekesha race as if meneja wa kampuni.

Wanaume katika maisha katika kitu tunahusudu ni familia yenye utulivu ambayo itapatikana ukiwa na mwanamke ambaye anakuwa ni zaidi ya rafiki yako sio mtu ambaye anakupangia namna ya kuwa mwanaume wa aina gani. Hili jambo ndilo limewashinda wadada wa huko, ile image ya kutaka mwanaume wa mafanikio huwa inawaandama sana.

So sijajua kama wewe mleta uzi unawaongelea katika muktadha upi, kwamba unawafahamu vema ile deep au umeandika uzi wako kama tu namna ya kusawazisha maoni maana raia katika ule uzi mwingine wamewapondea sana na jambo ambalo ni kweli.
 
Nimezaliwa Huko
Nimekulia Huko
80% ya Ndugu ni Watu wa Huko.
 
Back
Top Bottom