Mwanamke akiweza kumiliki vitu hivi ni ngumu ndoa Kudumu

nashukuru mzima

JF-Expert Member
Jul 11, 2017
1,014
1,896
Habari za jioni, tunashukuru Mungu kwa uzima aliotupa.

Katika ulimwengu huu tunaoishi katika dunia ya utandawazi ambayo imeonekana imejitosheleza katika kila sekta, ila kuna taasisi moja kubwa sana ambayo ni Nndoa, taasisi hii inaundwa na mwanamke na mwanaume matokeo ya muda mrefu hadi mfupi uzalisha kiumbe (mtoto).

Ila Tukirudi katika jamii ya sasa imeonekana ndoa nyingi sana zinazofungwa hazidumu kwa muda mrefu sana na hakuna sababu za msingi kwa kuwa kila mtu anajaribu kutoa sababu kwa mitazamo wake anaona ni sahihi maana hadi muda huu hakuna utafiti wa moja kwa moja uliofanyika na ukaleta majibu ya moja kwa moja sababu ya ndoa kuvunjika.

Katika hhapisho hili nitaweka mambo matatu ambayo kama mwanamke akipata ni ngumu sana ndoa yake kudumu kwa muda mrefu.

Jambo la kwanza Elimu
Hili jambo la kwanza inapotokea mwanamke akapata elimu na akashindwa kuitumia basi ni ngumu sana kudumu katika ndoa yake. Elimu ni jambo la msingi sana katika dunia ya sasa pasipo kuzingatia misingi ya kijinsia kama ilivyokuwa inafanyika awali ambapo mwanaume ndio alikuwa anapewa kipaumbele katika hili.

Ila kwa sasa tuna wasomi wengi sana ambayo ni jinsia ya kike lakini inapotokea mahusiano ya ndoa yanahusishwa katika msingi ya Elimu ni ngumu sana kwa jinsia ya kike kuweza kuisimamia, hali ya Kufahamu kila kitu, hali ya kujiona kipekee, hali ya kutaka kuthaminiwa, imewafanya wanawake waweke hali hii katika ndoa zao na kupelekea ndoa nyingi kuvunjika kwa ndoa.

Jambo la pili Cheo/Wadhifa
Mara nyingi inapotokea mwanamke anapopata nafasi katika eneo la kazi au cheo chochote katika masuala ya kisiasa inatokea ugumu sana kuweza kutofautisha majukumu yanayotokea kati ya anapokuwa katika eneo la kutekeleza majukumu ya cheo chake na anapokuwa katika majukumu ya ndoa yake.

Na inapotokea inabainika na kichwa cha familia ambaye ni mwanaume, basi unatokea mtafaruku na hali ya kujiona anajitosheleza katika kila kitu ndipo uonekana hapo. Hivyo husababisha mtafaruku na ndoa kushindwa kudumu.

Jambo la tatu Pesa
Kwa maisha ya sasa kuna umuhimu mkubwa sana wa wanandoa kumiliki pesa na kuwa na uchumi wa uhakika, ila kwa mwanamke hali inakuwa tofauti sana inapotokea ana kipato kikubwa kuliko mumewe.

Ni wanawake wachache wanaweza kuendeleza heshima pindi wanapokuwa vizuri kiuchumi. Mwanamke analomiliki pesa ya kutosha katika kila kitu hali ya kujihisi anajitosheleza inajitokeza na anadhani anaweza kuishi katika hali yoyote ile pasipo na mwanaume yeyote yule, hivyo upelekea kushindwa kumuheshimu mume wake.

Hitimisho

Siyo muafaka ya kuwa wanawake wakiwa na hivi vitu hawadumu kwa ndoa, ila kwa asilimia kubwa inakuwa hivi.

Niwatakie majukumu mema ya kazi kesho.
 
Kataa ndoa nao wapo logic kabisa. Maana ulimwengu wa Sasa unawafavour wanawake Elimu ajira na vyeo vipo kwao. Wanaume wengi wakiwaoa watu wa namna hiyo wanapata mateso maana mwanamke atataka Yeye ndo awe kichwa Cha familia. Hili kuondokana na hii Kadhia Kampeni ya kataa ndoa iendelee itasaidia vizazi vijavyo kufaidia na Kampeni maana ndoa itaheshimika kutokana na kuwa adimu. Sasa hivi ndoa inachezewa sababu sio kitu adimu.

KATAA NDOA, NDOA NI UTUMWA
 
Ongezea haya
Mwanamke akifanikiwa kumiliki Matako makubwa na sura ya mvuto kwa mujibu wa wanaomtongoza basi hapo suala la ndoa hua gumu sana kwake kudumu, maana anaamini kwa uzuri wake hawezi kubabaishwa na mwanaume mmoja ktk ndoa.

Hivyo basi ndoa ya namna hii ya mwanamke slayqn tegemea ugomvi usioisha, masimango, kufananishwa kwa mume wake na wanaume nje ya ndoa huko mitaani, kutolewa mifano ya kiuchumi na wanaume wengine, majigambo, uvivu&uzembe wa kazi, tamaa mbaya, mwisho wa yote tegemea uaminifu ktk ndoa kuwa mdogo sana, la mwisho ni kusalitiwa.

Mwanaume Kataa ndoa za michongo, pesa ni bora kulko ndoa za mchongo, tumia muda wako kujijenga ktk ujana wako kutafuta pesa sana ili hapo baadae uache urithi mzuri kama utafanikiwa kupata watoto.

Ni aibu kwa kijana kukimbilia ndoa na kuacha mambo ya msingi.

Kataa ndoa za michongo, kataa kunyanyasika, kataa kupelekeshwa, kataa umasikini, kataa magonjwa ya akili, afya yako ni bora kuliko hiyo ndoa ya kipuuzi.

Ingia kwenye ndoa ukiwa umetimiza ndoto zako na ndoa iwe last wish na isiwe sehemu ya ndoto zako, muoe mwanamke ambaye ametimiza ndoto zake angalau 50% na %zilizobaki msaidie kuzitimiza kwa kumdunga mimba akuzalie majembe ya kuja kuurithi ufalme wako ulioujenga kwa muda mrefu.

Ukweli mchungu.
 
Maana nyepesi kulinda ndoa basi mwanamke asisome, wala asijishughulishe na cheo chochote.

Haki yao ipo wapi?
Unajua mada haujaielewa.

Ninaongelea vitu vitatu ambavyo kama mwanamke atakuwa navyo ni ngumu sana kudumu katika ndoa kwa asilimia kubwa.

Ushindi mkubwa inategemea sasa na yeye kuweza kutofautisha hivi vitu vitatu na ndoa ,hapa ni wengi sana wanashindwa hili
 
Kataa ndoa nao wapo logic kabisa. Maana ulimwengu wa Sasa unawafavour wanawake Elimu ajira na vyeo vipo kwao. Wanaume wengi wakiwaoa watu wa namna hiyo wanapata mateso maana mwanamke atataka Yeye ndo awe kichwa Cha familia. Hili kuondokana na hii Kadhia Kampeni ya kataa ndoa iendelee itasaidia vizazi vijavyo kufaidia na Kampeni maana ndoa itaheshimika kutokana na kuwa adimu. Sasa hivi ndoa inachezewa sababu sio kitu adimu.

KATAA NDOA, NDOA NI UTUMWA
Unajua Logic ya Haki sawa.
Kwa asilimia kubwa inampa favour mwanamke na anashindwa kuitumia hiyo nafasi na kufanya mambo kinyume.
 
1.Jichunguze wapi mahusiano yako na Mungu hayako sawa.

2.Chunguza ni tabia gani mbaya ambazo umeshindwa kuziacha

✓Mambo hayo mawili yatakufanya ukose amani muda mwingi kwa sababu roho yako itakuwa na hofu kama kuna mashaka.

✓Mambo hayo yatampa kibali shetani cha kukunyanyasa kwa magonjwa na mikosi mbalimbali ilimradi tu aindoe roho yako.

Habari njema ni kwamba Yesu anakupenda na bado anakusubiri umgeukie.

Kutana na nguvu ya maombi yenye matokeo ambayo itakufanya uimarike mwenyewe na umjue Mungu kibinafsi.
Kubali kumpokea Yesu leo ...hatima njema ya maisha yako, ipo mikononi mwa Mungu.

Nitafute nikulekeze cha kufanya
0627648493 WhatsApp/Calls
 
Taliban wanataka kuimarisha taasisi ndoa na jamii yao ndo maana wameanza maswala dhidi ya wanawake🤣🤣
 
Taliban wanataka kuimarisha taasisi ndoa na jamii yao ndo maana wameanza maswala dhidi ya wanawake
Ila Tayari Tuko katika Jamii yenye Utandawazi.

Ni ngumu kurudi nyuma kama Kulipoonekana mwanamke ana nafasi ndogo sana katika jamii na wala haturudi nyuma katika Hilo.

Hivyo mwanamke mwenye Hela,Cheo,Elimu yeye mwenyewe ndo mwenye Maamuzi ya kuamua kudumu kwa ndoa yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom