Mwanakijiji, huu ni UDINI pia...

Status
Not open for further replies.
Labda nisahihishwe. Pengo si mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania. Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania ndiye mwenye dhamana kwa hili. Why Pengo Mwanakijiji?
 
The Boss usemayo ni kweli lakini angalia upande wa pili wao huwa wanakimbilia wapi.............angalia roles za viongozi wa Kikristo na zile za viongozi wa waislamu, utagundua kwanini Mwanakijiji kasema vile
Kweli kabisa, hii ni kwa sababu watawala hawajali kabisa kuuzima moshi hivo ni bora kuomba msaada pahala pengine ili mambo yawe sawia.
 
Mimi nadhani kuwa kauli ya Kardinali Pengo ina nguvu sana kwenye jambo hili
'
Lakini kauli yake ni muhimu sana kwa Wakristu Wakatoliki,unadhani akisema walipize hawatamsikiliza?
'
Anaweza kutoa kauli ya kuwataka wawe watulivu na msimamo wa kanisa juu ya kadhia hii
'
Itasaidia!
 
Haiwezekani viongozi wa kikristo waendelee kuawa halafu akina Pengo wamekaa kimya wakiendelea kuwachekea viongozi wa serikali. Kama kuna mtu anadhani wakristo wataendelea kukaa kimya ni mjinga. Ni swala la muda tu hili jambo litakuwa halidhibitiki tena na ndipo tutakapoamini kwamba serikali hii ni dhaifu kwa maana ya neno lenyewe. Wakristo hawezi kuwageuzi wauaji hawa mashavu kwa sababu sasa mashavu yote mawili yameshapigwa. Viongozi wetu wapo busy kutuma salamu za rambirambi na kutoa vitisho motomoto.
 
Mkuu unasema "kukimbilia kwa kiongozi wa dini kuomba muongozo kwa matatizo ya kitaifa ndiyo udini wenyewe" na wakati matatizo hayo unayaita "uzembe wa kisiasa wa wanasiasa",na pia ukasema "serikali hii ni dhaifu",halafu hapo hapo unamlaumu Mwanakijiji kwa kumtaka Pengo atoe msimamo na kuitaka serikali hiyo dhaifu ifuatilie hao magaidi?

Sidhani kama mwanakijiji alimchukulia Pengo kama kiongozi wa nchi(wewe unasema "wa kitaifa"),tambua pia Pengo ni kiongozi wa kitaifa wa kanisa la katoliki na hivyo ana haki ya kutoa misimamo ya kitaifa inayohusiana na kanisa analoliongoza,ie mauwaji ya mapadri huko Zanzibar.

Sasa hapa nashindwa kuelewa,mara unasema serikali ni dhaifu,halafu hapohapo ukitaka isimamie issue za kitaifa kwa weledi,sasa hapa unasema wanaonewa waislam ama ni serikali imekosewa?Kuendelea kuwaita magaidi wahuni hakutamaliza tatizo.

Unaposema Pengo hawezi kuplay role ya kitaifa unashindwa kutofautisha mtizamo wa kanisa vs ule wa serikali.Kama ni issue iliyowagusa wakatoliki wa nchi nzima,basi issue hiyo ikiongelewa na kiongozi wa katoliki ngazi ya juu/taifa,hakuna shida.
 
Naona watu tumeichoka hii fursa tunayoipata ktk hizi nyuzi mbalimbali hapa jf. Jamani amani hii ndio inatupa mda wa kujadili hapa jf, ndg zangu waTZ tuache mbwembwe udugu tulionao wa utanzania ni mkubwa huu. Mwnzenu bado napenda kuwaona kina mzee mwanakijiji, the boss, utantambua nk ktk jf wakinielimisha, sasa cjui nyny hamuitaki fursa hii.
 

You are really.............. THE BOSS
 
The Boss ........I feel you!........kinachonisikitisha kutoka serikalini ni kuwa wamekuwa kimya sana....hawakemei/hawalaani hivi vitendo...na hawachukui hatua....they are too Soft!!....and trust me it will cost us big time.........kwani wananchi wanaanza kukosa imani.....na wengie wameshakosa imani na serikali (e.g. Mwanakijiji)....and one is asking why should he/she trust the Government.....kwa sababu pale serikali inapotarajiwa kuchukua hatua imekuwa KIMYAAA......

Serikali inabidi ichukue hatua kali ili walau irudishe imani kwa baadhi ya wananchi ambao ni potential kwenye amani ya Taifa letu........
 
Last edited by a moderator:
Yafaa kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi kwa wapenda amani Tanzania...Watanzania tunachonganishwa, bahati mbaya sana hili jambo wengi wetu wanalichukulia kijujuu tu kuwa litakuwa linauhusiano na mambo ya imani...mtazamo wangu ni kuwa huu ni mpango mahususi ulio ratibiwa kwa minajili ya kutuvuruga watanzania...hope vyombo vya usalama vitafanikiwa kuwatia mbaroni magaidi wote waliohusika...
 
Huyu mzee mwanakijiji nilmdharau zamani cuz ni mdini na hana nidhamu ya kuitumikia kalamu nashindwa kumvunjia heshima bt ni mbumbumbu wa mawazo
 
Naona hapa TB uliamua kumpandisha msalabani Mwanakijiji wa watu ili tu kuchagiza mjadala na kusawazisha hoja yake ndio maana ukaifungulia sred kabisa.

Ila kama watz kama jamii inayokomaa na kukua kwa maana ya kupitia changamoto mbalimbali za kiwakati na mazingira ya ndani na nje, ni lazima ifike wakati tuache kuenenda kwa mazoea tu.
Kwamba vitu vilivyokuwa jana basi ndio vitakuwa na kesho.
Siku za sasa hazituruhusu kuenenda namna hyo tena na hivyo ni sahihi kabisa kwa Viongozi wetu wa kidini (mf Pengo kama Mwanakijiji alivyomchagua) kuanza kupata aina mpya ya mashinikizo kutoka kwa "wazalendo" wetu,
ni mda sasa tunahitaji mbinu mpya kuelekea uvumbuzi wa matatizo yetu "mapya" au hata kama sio mapya basi yanakuja kwa njia mpya.....

Hvyo naona mshtuko wako mkuu TB umekuja kutokana kwamba ulitarajia muitikio wa kimazoea wa "kama kawaida ya desturi zetu watz", kitu ambacho hakipo saiv, kilichopo saiv ni tatizo jipya hvyo tuamke kutoka kwenye usingizi wa mazoea, vitu vinabarika akili zichemke na ziende mbio manabii waonyeshe unabii wao, waonyeshe uheshimiwa wao na utukufu wa madhabahu ambapo wanashinda kila siku.....
Hivyo ni haki kulilia uongozi wa kiroho maana wa kisheria ndo umetufikisha hapa.....
So Pengo atafanya nini hyo sio juu yetu ila afanye kitu sasa jamii ikubali unabii wake na utume wake!

Mwanakijiji yupo sahihi ukimuangalia kwa upande huo.
 
The Boss, tatizo ni kwamba hao viongozi wa upande wa pili wanatoa instructions ambazo zimekuwa zikiwagharimu Wakristo. We as Christians we want our leaders to do the same

Sawa wao wamefunzwa hivyo lakini wakristo hawajafunzwa hivyo. Nitamshangaa sana Pengo akitoa tamko kama linavyodhaniwa. Anachotakiwa ni kugeuza shavu la pili
 
Watanzania tumeshajichanganya na tunAingiza siasa na dini pamoja. Tukubaliane wanaotoa matamko ya kitaifa ni viongozi wa kisiasa na wa kidini huwa wanashauri ili kudumisha amani. Yaliyotokea Zanzibar si ya kufumbiwa macho lakini nani wa kulaumiwa? Ni serikali peke yake ndio yapaswa kumaliza uhasama. Kama Pengo anatakiwa atoe tamko basi ni kuikaripia serikali dhaifu na wala si kulaumu asichokijua.
 
Watanzania tumeshajichanganya na tunAingiza siasa na dini pamoja. Tukubaliane wanaotoa matamko ya kitaifa ni viongozi wa kisiasa na wa kidini huwa wanashauri ili kudumisha amani. Yaliyotokea Zanzibar si ya kufumbiwa macho lakini nani wa kulaumiwa? Ni serikali peke yake ndio yapaswa kumaliza uhasama. Kama Pengo anatakiwa atoe tamko basi ni kuikaripia serikali dhaifu na wala si kulaumu asichokijua.
 
Nashangaa wengi humu wameshatuhumu kuwa huyo mchungaji wa kondoo kauliwa na Waislaam. Muuwaji anaweza kuwa wa dini yeyote ile, hata mchungaji mwenzie anaweza kumuuwa.

Isitoshe, kuna sababu za mtu kuuwa na au kuuliwa. Madudu mengi tuliyoyasikia duniani kwa hawa wachungaji hususan yale ya kuharibu watoto wadogo yanaweza yakapelekea mzazi mwenye hasira kuuwa.

Huyo anaejiita Mzee Mwanakijiji anaweza pia kuwa ndiye muuwaji na anakuja humu kwa shutuma na hamaki na kujifanya imemuuma sana ili kupoteza watu maboya.

Hili tukio inatakikana lifanyiwe uchunguzi wa kina na bila kutazamwa kwa mtazamo wa dini, linaweza linaweza kuwa ni mtego wa panya kuingiza walliokuwemo na wasiokuwemo.

Suspicion yangu kubwa iko katika mambo matatu:

  • Moja ni biashara ya utalii na mahasimu wa Zanzibar wa hiyo biashara.
  • Mbili ni "inside job" ya wenyewe kwa wenyewe huko kanisani.
  • Tatu ni "revenge" ya uharibifu m'baya wa aina fulani.
 
Hicho ndo Pengo alichokuwa anasema kila mara
sasa Mwanakijiji anataka ajiuzulu au atoe kauli nyingine kali
kwangu mimi huu ni UDINI wa waziwazi.....
Huhitaji kauli ya kiongozi wako wa dini,kama unajua nini maana ya utaifa
kwenye tatizo la kitaifa

Mkuu,Mwanakijiji hajasema Pengo atoe kauli kali,yenye kulipa kisasi,wala yenye kubomoa,yeye anamtaka Pengo atoe kauli tu kama kiongozi na amekwenda mbali zaidi kwa kuifananisha kauli/ujumbe huo kama (prophetic message).
Kauli hiyo(prophetic message) haiwezi kuwa kali,daima ni kauli yenye kutoa dira chanya,muelekeo thabiti,yenye kutuliza na kuweka sawa mambo kwa mustakhabari wa amani ya nchi,hasa ukizingatia kwamba wakristo na wengine wote wapenda haki wapo katika wakati mgumu kufuatia tukio hilo bila kujali lengo lake.
My take: Hoja ni nzuri na kukosoana na kuhujiana ndio nyenzo katika ujenzi wa jamii huru.
Tuendelee kujadili hoja na tusije tumbukia ktk personal attacks.
 

Hii ndio point ya Mwanakijiji,rejea mfano wa "prophetic message".
Ujumbe huo hauwezi kuwa mkali kama mtoa mada anavyodai.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…