Mwanahalisi imesalimu amri Kwa Zitto: Umbeya hauwezi kuzaa Ukweli

jifunze kuandika kwanza ndio uchangie
Nafikiri mtoa mada hamjamwelewa vizuri, kwangu mimi naona kama labda anaendelea na maelezo, zijaona point hata moja maelezo yake yanarudia jina zito mara kibao. Msimtukane jamani mwwelewesheni.
Anayeponda gazeti la mwanahalisi nafiki atakuwa ni mmoja wa wale wanaotamba mitaani kwamba walinyweshwa maji ya bendera ja rangi fulani hivyo hawawezi kubadirika.
 
Kuanzia mwezi December 2010 hadi mwezi wa march 2011 kulikua na vita kali ya maneno ya kimbea ya gazeti la Mwanahalisi kwa Mbunge Mzalendo Zitto Zuberi Kabwe! Mwanahalisi ilitoa kashifa nyingi kuwa Zitto anatumiwa na Usalama wa Taifa kuihujumu CDM,Mwanahalisi bila aibu na Mwandishi wake Kebenea ilishadadia mambo mengi juu ya Zitto kuwa anatumiwa na Mafisadi! Mwanahalisi ikafika mbali zaidi na kusema Zitto anaihama CDM,bila kujua au kutumiwa kwa fitina Gazeti la Tanzania Daima gazeti la Chadema nalo lili ingia mkumbo na kuanza umbea juu ya Zitto! Ndugu yangu Godbless Lema nae bila kuelewa siasa za majungu au alitumiwa nae aka anzisha umbea na ugomvi na Zitto! Watu wenye Ubongo wa Kuku hapa JF nao wakaingia mkenge na kuanza chuki na matusi mazito kwa Zitto! Lakini Zitto alitoa jibu moja tu "CDM nimetoka nayo mbali sana siwezi kuihujumu" leo hii Kazi inayofanyika na Mwanasiasa huyu kijana imeonesha ni mtu anaejua kujenga hoja na kuanzisha hoja bila jaziba papala kama wanasiasa wengine kama Lissu ambao hujenga hoja kwa jaziba na papara nyingi! Wengine walitabiri kuwa Zitto atafunikwa na akina Mnyika,Sugu na wengine kwa kujenga hoja! Lakini Zitto ni Mshare mrefu haufichiki kabisa! Zitto amekua mtu wa kutulia na kujenga hoja ambayo mara nyingi inakaa kwenye akili za Watanzania! Hapa JF miezi iliyopita kulikua na Ushabiki wa kumsifia sana Dr fulani(Phd ya Ekaristi Takatifu kutoka Rome) lakini Zitto hakutishika na hilo amekua mwanasiasa makini mda wote! Wenye macho na akili wanaona sasa kazi anayo fanya Zitto Bungeni Kujenga CDM!
My Take: Tusikimbilie kumchukia mtu kwa Umbeya wa Mtu mwingine bila kupima ukweli halisi,Mwanahalisi imejivua nguo peupe kwa Umbea juu ya Zitto!
umetumwa!!!!!!!!!!!
 
Bila shaka wewe unaUbongo wa Kuku! Ulikuwa unataka kuandika kitu gani?

Mmh Mchungaji,
Unatakiwa kuwafundisha kondoo wako mambo ya neema, sasa kondoo akianza kudonoa mchanga tu tayari cells zote za ubongo wa kuku zinakuwa induced kwa kondoo......aaahaha ahahaha aha...tteeh..teeeh.
 
Vyombo vya habari ni nguzo muhimu sana katika ustawi wa jamii yoyote ile iliyostaarabika.Kuna baadhi ya vyombo vya habari vinatumika vibaya,pia nimegundua waandishi makini Tanzania hii ni wachache sana.

Gazeti linaandika andika tu,kulingana na upepo...ushabiki tu! Vigazeti vingine ni vya kupuuza,vinajadili watu baadala ya Issues. Raia Mwema inaonekana kuwa na waandishi wazuri sana
 
Vyombo vya habari ni nguzo muhimu sana katika ustawi wa jamii yoyote ile iliyostaarabika.Kuna baadhi ya vyombo vya habari vinatumika vibaya,pia nimegundua waandishi makini Tanzania hii ni wachache sana.

Gazeti linaandika andika tu,kulingana na upepo...ushabiki tu! Vigazeti vingine ni vya kupuuza,vinajadili watu baadala ya Issues. Raia Mwema inaonekana kuwa na waandishi wazuri sana

Unaweza kuongea maneno haya mbele ya Komu?
 
Vyombo vya habari ni nguzo muhimu sana katika ustawi wa jamii yoyote ile iliyostaarabika.Kuna baadhi ya vyombo vya habari vinatumika vibaya,pia nimegundua waandishi makini Tanzania hii ni wachache sana.Gazeti linaandika andika tu,kulingana na upepo...ushabiki tu! Vigazeti vingine ni vya kupuuza,vinajadili watu baadala ya Issues. Raia Mwema inaonekana kuwa na waandishi wazuri sana
Gazeti baya pale linapoandika usiyopenda! Cha kujiuliza je hizo habari zina ukweli? Alafu nashangaa sana huu usemi wa kujadili issues na si watu! Uadilifu ni muhimu sana na unapoandikwa mwenendo wa kiongozi ingawa anatajwa sana lakini issues ndio zinafanya atajwe na wakati mwingine ni muendelezo tu wa uchafu wake.nafikiri itakuwa tatizo kama unaandikwa uongo.mfano kuandikwa sana habari za ndoa ya Dr slaa haikuwa tatizo maana ni kweli maadili yanaanzia ndani lakini tatizo letu ilikuwa ni jinsi ilivyokuwa inaandikwa kwa kupotosha.kama kuna habari ya uongo iliandikwa mwanahalisi wekeni hapa otherwise chuki binafsi tu,mangapi yaliogopwa kuandikwa yakaanikwa kule jamani? Mnajua mchango wa gazeti hili kwenye hili vuguvugu la mabadiliko?
 
Mwanahalisi ni zaidi ya gazeti hapa Tanzania. Kwa kiasi kikubwa naweza kusema limemsaidia sana Zi kurudi kwenye mstari. Binafsi ni miongoni mwa vijana nilio poteza imani na Zi ila naona taratibu narudisha imani. Ngoja nione kama hatanitonesha tena kidogo changu. Akijaribu tu..... Maisha.
 
I still believe Zitto is much better than most of CHADEMA leaders....
Of course ndugu,unadhani uwezo unalingana kwa watu? Unadhani hata vichwa wanaweza peke yao? Mfano hata mm naona Mnyika is much better then? Haya kila mtu ataje wake ambae ni much better! Upupu mtupu kutaka kuharibu chama kwa sifa za kijinga
 
huwa nawaza kama Nyerere angekuwa analewa sifa enzi hizo sijui ingekuwaje! Naamini Zitto hawezi kurudi alipotoka,mwacheni alitumikie taifa jamani.
 
Ni kweli ZITTO alikuwa anatumika ila baada ya wazee kuweka kikao na kumsema,ZITTO alibadilika,hongera ZITTO kwa kubadilika sasa tunasonga mbele.VIVA CHADEMA.
 
Yaani unajiona umeshaingia ktk ubongo wa Zitto Kabwe na kujua hata atakayofanya kesho na keshokutwa.
Huu sio Ubongo wa Kuku, tena kifaranga?

Mimi naona jamaa umemuonea wewe ndio una ubongo wa kuku, kwanini nasema hivi, ni kwa sababu kuku hana uwezo wa kukumbuka ya leo ,kesho wala kesho kutwa, kwahiyo wewe kumfananisha huyo jamaa na kuku nimeona wewe ndiyo kuku. samahani kwa hilo.
 
RATED: CRAP, No citation, supporting evidence or even quotations. Mkurya mjinga namba 2 ni wewe baada ya Werema na Nyambari. Akili ya nanii...
 
Marwa timka urudi ulikotoka,huna tofauti na kengere ya baiskeli...unatufundisha sisi kuhusu Zito ama unaomba tukufundishe kuhusu Zito?mabaya aliyoyafanya Zito hakuna mtu yeyote tunayemhtaji wa kumsemea na kuyakanusha zaidi ya yeye mwenyewe neno kwa neno,kituo kwa kituo,japo kidooogo kwa sasa kama vile anarudi kwenye uhai...John kauze pipi
 
Mtoa mada amekalia chuki dhidi ya viongozi wa CDM. Huwezi kumsifia zitto na kuwaponda viongozi wengine kama Lissu, Lema na Mnyika na hii yote ni kutaka kuwagombanisha. Ukweli ni kwamba Zitto alipotea na tushukuru mwanahalisi wamesaidia kumrudisha kwenye mstari.
 
Back
Top Bottom