Unafiki wa CCM kukubaliana na hoja za wakati ule za Zitto Kabwe kuhusu watoto wenye mimba kurudi shule inafikirisha sana

seedfarm

Senior Member
Feb 9, 2020
190
1,000
Wanabodi, Wabunge wa CCM walimtukana Zitto Kabwe wakati wa hayati JPM kuhusu hoja ya Zitto kuwa watoto Tanzania waliopata mimba hawapewi nafasi ya kusoma shule za kawaida

Wabunge wa CCM Wengine walitishia kumuua zito Kabwe kwa kosa kuwa anawasaliti

Wabunge wote wa CCM wakati wa JPM hawakutaka watoto wa kike waliopata mimba warudi shule kusoma kwa nafasi ya pili

Wabunge wa CCM Waliunga mkono ile hotuba ya JPM hayati kuwa Katika serikali yake hakuna mtoto aliyepata mimba kurudi shule kusoma, Lakini watoto wao wabunge na mawaziri Wakipata mimba wanaenda kusoma Kenya na uganda

Wabunge wa CCM walitukana kuwa hawa watoto ni wazazi, wananyonyesha, wapumbavu na hawana akili, Leo wamegeuka wanaunga mkono hoja ya Rais Samia na Zitto Kabwe kuwa watoto waliopata mimba wana haki ya kurudi shule kama watoto wengine

Zitto aliweka msimamo lazima watoto wa kike warudi shule na akaandika barua Benki ya dunia kuwa Serikali ya Tanzania inapokea pesa lakini hawatekelezi kitu

Kama Taifa tutaendelea na Vituko hivi vya CCM mpaka lini kwa kuwa na watu vigeugeu?

Watu wazima halafu wabunge wanakuwa vigeugeu kila wakati mara korona hakuna mara korona ipo, Mara chanjo hazifai mara chanjo ni nzuri

Hoja zote za wapinzani Bungeni wakati huo ndio sasa wana CCM wanashangilia, Walipinga hoja za upinzani huku wakimwimbia hayati JPM kila nyimbo ya ufalme, Leo wanakubaliana na hoja za mtu waliyesema msaliti

Mambo ya CCM yanasikitisha sana

Ni dhahiri wabunge wa CCM hawana uwezo wa kujenga hoja bungeni

Wabunge wa upinzani ndio wenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja na kuisaidia nchi, Hoja hizi waliziongea sana akina Zitto, Msigwa na wenzao lakini wabunge wa CCM walizikataa halafu Leo wanaunga mkono wakati wa Rais Samia

1.Hoja zao nyingi wapinzani kama elimu ya usawa kwa mtoto wa kike na kumpa fursa ya kusoma bila kumtenga kwani ana umri mdogo apatapo mimba Leo ndio hoja kuu ya CCM

2. Kuwa uchumi unaporomoka
3. Korona ipo, Chanjo muhimu
4. Serikali inakopa pesa nyingi kwa siri
5. Vyombo vya habari vinabanwa Leo Polepole analia kuandikwa na Raia mwema
6. Wamachingwa wanadanganywa na serikali kuna siku watatakiwa kufanya biashara kwa kufuata sheria, Leo Machinga wanatimuliwa
7. Umeme wa maji hauaminiki, Leo ccm wanaongelea tena Gas
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
21,532
2,000
Walisema akirudi tu pale Uwanja wa Ndege apigwe risasi Na yeye hakuogopa akarudi hakuna Mtu aliyesogea.
 

Airfryer

Senior Member
Sep 17, 2021
148
500
Walisema akirudi tu pale Uwanja wa Ndege apigwe risasi Na yeye hakuogopa akarudi hakuna Mtu aliyesogea.
CCM Bwana, kuna wenye chama chao

Akina Humprey na Bashiru walipata nafasi kwa bahati mbaya tu, ndani ya CCM hawa hawajulikani kabisa

Wenye chama Chao wamerudi wanajua kucheza dansi na Kwaito
 

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
15,273
2,000
Hivi muda wa kuwajadili Wabunge wa CCM na Spika yao mbovu huwa mnaupata wapi wenzangu?
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
11,815
2,000
2962938_IMG-20180405-WA0006 (1).jpg
 

Peramiho yetu

JF-Expert Member
May 25, 2018
3,278
2,000
Ukisha kuwa mwana CCM tu matako yana nafasi kubwa katika kufikiri kuliko ubongo

Mle kuna ma Dr maprof masters zimejaa lakn kusimamia kweli wameshindwa

Prof palamagamba Kabudi alimuita Magufuli MUNGU mbele ya kamera na Wala hakuonesha kujutia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom