Getrude Mollel
JF-Expert Member
- Apr 26, 2022
- 259
- 353
Huwa nafuatilia sana, kusoma na kufuatilia mijadala na hoja nyingi zitolewazo na vijana wa vyama mbalimbali vya siasa nchini.
Nimeona shida kubwa sana kwa vijana wetu ambao wengi wanaonekana dhahiri wanatamani kuwa na madaraka au nafasi kubwa ndani ya serikali. Shida iliyopo ni kwamba vijana wengi ni wachovu bado kwenye uwezo wa kujenga hoja.
Ukisoma Tweets au maandiko yao kwenye mitandao ya kijamii unakutana na mtu anashauri serikali katika hali ambayo hudhani mtu kama yeye anaweza kuandika jambo zito kwa wepesi kiachi hicho.
Unakuta kijana anaishauri TRA kupunguza VAT au kodi kwenye bidhaa nchini. Lakini kwenye hoja yake hiyo hakuna 'case study', kuonesha kwanza utashi juu ya jambo analoshauri, pia kuonesha kwamba amefuatilia kwa kina juu ya jambo hilo kabla ya kutoa ushauri. Hajui kwamba TRA inaendeshwa kwa sheria na kanuni ambazo ndio chanzo cha maamuzi mbalimbali ya mamlaka hiyo.
Kuna kijana mwingine wa chama fulani sitomtaja, yeye aliwahi kuishauri serikali inunue mafuta kutoka Urusi kwani i bei rahisi na yataweza kupunguza sana bei ya mafuta nchini na kuwapunguzia Watanzania ugumu wa maisha.
Ushauri wake ni mzuri kwa asiyefahamu kama yeye, ila ni ushauri mbovu na umemvua nguo mbele ya kadamnasi pia umemweka dhahiri uwezo wake wa kuelewa na kudadavua mambo. Fikira, katika hali kama ya sasa ambapo mataifa mengi makubwa yamejitenga kufanya biashara na Urusi, halafu anatokea mtu kutoka nchi masikini kama ya kwetu, nchi inayotegemea misaada na mikopo kujiendesha, anashauri eti sisi, tukafanye biashara na Urusi, anataka kuiweka wapi nchi yetu katika medani ya Kisiasa?
Ushauri wa kijana huyu umeonesha namna gani kijana huyu hana ufahamu na masuala ya uhusiano wa kimataifa, pia imeonesha namna gani hana 'rational thinking'.
Vijana wengi wanaona kuandika matusi na kukosa viongozi mtandaoni na kuwa na sauti kubwa ni mtaji wa kuwa mwanasiasa mzuri. Hapana, mtaji mkubwa wa kuwa mwanasiasa bora, sio bora mwanasiasa ni kusoma sana vitabu. Tazama mtu kama Zitto Kabwe, ni moja ya mifano ya watu ambao wana uwezo mkubwa sana wa kujenga hoja. Uwezo huu unatokana na mapenzi yao ya kusoma vitabu na kupenda kufuatilia mambo ya kidunia.
Ushauri wangu kwa vijana wenye ndogo kubwa kwenye tasnia ya siasa, mnawajibu wa kukuza na kuongeza maarifa yenu kila uchwao kwa kusoma vitabu.