John Marwa
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 275
- 28
Kuanzia mwezi December 2010 hadi mwezi wa march 2011 kulikua na vita kali ya maneno ya kimbea ya gazeti la Mwanahalisi kwa Mbunge Mzalendo Zitto Zuberi Kabwe! Mwanahalisi ilitoa kashifa nyingi kuwa Zitto anatumiwa na Usalama wa Taifa kuihujumu CDM,Mwanahalisi bila aibu na Mwandishi wake Kebenea ilishadadia mambo mengi juu ya Zitto kuwa anatumiwa na Mafisadi! Mwanahalisi ikafika mbali zaidi na kusema Zitto anaihama CDM,bila kujua au kutumiwa kwa fitina Gazeti la Tanzania Daima gazeti la Chadema nalo lili ingia mkumbo na kuanza umbea juu ya Zitto! Ndugu yangu Godbless Lema nae bila kuelewa siasa za majungu au alitumiwa nae aka anzisha umbea na ugomvi na Zitto! Watu wenye Ubongo wa Kuku hapa JF nao wakaingia mkenge na kuanza chuki na matusi mazito kwa Zitto! Lakini Zitto alitoa jibu moja tu "CDM nimetoka nayo mbali sana siwezi kuihujumu" leo hii Kazi inayofanyika na Mwanasiasa huyu kijana imeonesha ni mtu anaejua kujenga hoja na kuanzisha hoja bila jaziba papala kama wanasiasa wengine kama Lissu ambao hujenga hoja kwa jaziba na papara nyingi! Wengine walitabiri kuwa Zitto atafunikwa na akina Mnyika,Sugu na wengine kwa kujenga hoja! Lakini Zitto ni Mshare mrefu haufichiki kabisa! Zitto amekua mtu wa kutulia na kujenga hoja ambayo mara nyingi inakaa kwenye akili za Watanzania! Hapa JF miezi iliyopita kulikua na Ushabiki wa kumsifia sana Dr fulani lakini Zitto hakutishika na hilo amekua mwanasiasa makini mda wote! Wenye macho na akili wanaona sasa kazi anayo fanya Zitto Bungeni Kujenga CDM!
My Take: Tusikimbilie kumchukia mtu kwa Umbeya wa Mtu mwingine bila kupima ukweli halisi,Mwanahalisi imejivua nguo peupe kwa Umbea juu ya Zitto!
My Take: Tusikimbilie kumchukia mtu kwa Umbeya wa Mtu mwingine bila kupima ukweli halisi,Mwanahalisi imejivua nguo peupe kwa Umbea juu ya Zitto!