Mwelekeo wa Maridhiano Ukitimiza Mwaka Mmoja

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Mazungumzo ya maridhiano kati ya CCM na CHADEMA yalipokewa vizuri na wapenda demokrasia nchini kwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan aliamua kuwasikiliza Chadema waliosusia na kuona haja ya vyama hivyo kukaa meza moja kuzungumza.

Rais Samia kwa mara ya kwanza, alikutana na Mbowe Machi 4, 2022, Ikulu ya Dares Salaam saa chache baada ya Mbowe kuachiwa huru kutoka gerezani alikokaa kwa takriban miezi minane kwa tuhuma za ugaidi. Kikao chao kilifungua milango ya vikao vingine baina ya viongozi wa vyama hivyo vilivyoendelea kwa nyakati tofauti kuyasaka maridhiano ya kisiasa.

Mei 2022, kamati ya watu 10 kutoka Chadema iliundwa, kadhalika idadi kama hivo kutoka CM na zilikutana Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma kuanza mazungumzo hayo. Hatua hiyo ilichukuliwa kama ukurasa mpya na chanya kwa siasa za Tanzania. Hata hivyo, mwaka mmoja baadaye, vyama hivyo vimeonyesha hali ya kutoaminiana ambapo viongozi wake wamejitokeza hadharani kuunyooshea kidole upande wa pili, kwamba haufuati yale wanayokubaliana kwenye vikao vyao.

Hali hivo inawaibua wachambuzi wa siasa ambao wanaeleza kwamba mwisho wa maridhiano baina ya vyama hivyo unaweza usifikiwe kwa kuwa kila upande unasukuma ajenda zake, hivyo wameshauri maridhiano kuhusisha wadau wengine na kujengwa Kitaasisi.

Kilio cha CCM
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana alisema wakati wa ziara yake ya kumarisha chama, kwamba haridhishwi na namna mazungumzo yao yanavyoendelea kutokana na upande wa Chadema kutokuzingatia misingi ya kuingia katika makubaliano hayo. Kinana alisema wakati wanaingia kwenye mazungumzo hayo na Chadema, walikubaliana kufanya siasa za kistaarabu, kujenga hoja na kujibiwa kwa hoja, jambo alilosema wenzao wameliacha na kuanza kutukana viongozi majukwaani.

"Saa hizi mambo vote wameweka kando, wameanza kutukana viongozi, hawajengi hoja tena, badala yake wanajenga vihoja na keieli. Nawasihi waheshimu misingi ya mazungumzo yanayoendelea," alisema.

Hata hivyo, mwanasiasa huyo anawasihi Watanzania kwa ujumla kupokea utaratibu wa maridhiano yanayoendelea kwa mikono miwili kwa kupenda kudumisha amani na ustawi na maendeleo ya Taifa.

"Nawasihi Watanzania, tuimarishe umoja na mshikamano, tupokee kwa mikono miwili utaratibu huu wa maridhiano ambao Rais ameuridhia kwa kupenda kuleta amani, umoja na amani katika nchi yetu. Tusiutumie vibaya, usifikiri kwa kutukana na kuonyesha kejeli na dharau hoja yako itakubalika kwa haraka, hoja yako itatupiliwa mbali, toa hoja yako kistaarabu itakubalika zaidi," alisema Kinana.

Kinana alisema Chadema ilipeleka mezani hoja zao 15 na nyingi zimefanyiwa kazi, ikiwemo kufuta kesi za viongozi na wanachama wao, isipokuwa zimebaki kesi mbili pekee ambazo ni ngumu kwa kuwa ni za jinai.

Kauli ya Chadema
Katibu Mkuu wa Chadema anasema chama chake kiliwasilisha hoja 11 kwenve mazungumzo yao na CCM, hata hivyo hakukuwa na hoja inayosema viongozi wao watumie lugha ya staha kwenve mikutano yao.
Mnyika anasema umma unapaswa kuelewa msingi wa mazungumzo hayo haukizuii chama hicho kutekeleza wajibu wake wa kisiasa kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi, hivyo wataendelea kutekeleza wajibu wao wa kuikosoa Serikali.

"Kitu ambacho ni muhimu Kinana akitolee kauli, ni kwa nini hadi sasa muswada wa sheria wa kukwamua mchakato wa Katiba mpya na muswada wa sheria wa marekebisho ya Katiba kuwezesha uchaguzi huru na haki haijapelekwa bungeni ili kutengeneza ukurasa mpya," anasema.

Alimtaka Kinana anapozungumzia kuhusu maridhiano baina ya vyama hivyo, basi aueleze pia umma kwa nini miswada hiyo haijapelekwa bungeni licha ya CCM kukubali hoja va Chadema ya kupata Katiba mpya.

Maoni ya wadau
wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema maridhiano hayo hayana tija kwa Taifa kwa kuwa yanahusisha kundi dogo la watu walio ndani ya vyama hivyo, badala yake yangehusisha pia wadau wengine.

Michambuzi wa masuala. ya siasa, Dk Onesemo Kyauke anasema haoni kama maridhiano hayo yana umuhimu kwa kuwa yamejikita katika masuala ya haki, isipokuwa hitaji la mchakato wa upatikanaji Katiba mpya.

Maridhiano ya CCM na Chadema kuhusu Katiba mpya hayana manufaa kwa Taifa, bali mchakato huu ulitakiwa kuanza sasa ukihusisha wadau wote, siyo chama cha siasa kimoja pekee.

"Binafsi sioni manufaa yoyote kwa sababu hizo haki wanazopewa Chadema zipo kikatiba, kama ambavyo vyama vingine vya siasa vina haki ya kufanya mikutano ya hadhara," anasema Dk Kyauke.

Dk Kyauke, ambaye pia ni mwanasheria, anasema suala linalotakiwa ni kufuata sheria na mikutano va hadhara ipo kisheria na siyo hisani ya mtu. Anasema hata mikutano ya hadhara ilipozuiwa mwaka 2016 ilikuwa ni tamko la kisiasa na si sheria. Anasema Chadema na vyama vingine kufanya mikutano ya hadhara si hisani, bali ipo kisheria.
Hata hivyo, Dk Kyauke alisema kuna lugha katika mikutano ya hadhara haziwezi kuepukika, hasa kukiwa mijadala mahususi wenye masilahi mapana kwa Taifa.

Dk Kyauke ambaye ni mtaalamu wa sheria, anasema kinachotakiwa ni Serikali na vyama vya siasa vyote kuheshimu utaratibu wa kufanya shughuli za kisiasa, ikiwemo mikutano ya hadhara kwa kutotukana watu au kukashifu.

"Sioni kama maridhiano vana manufaa sana kwa sababu Katiba ni suala la kitaifa. Maridhiano haya sioni hatima yake kwa sababu yamejikita kwenye haki zaidi na vitu wanavyovihitaji vipo katika sheria," anasema Dk Kyauke.
Kwa upande wake, mchambuzi wa siasa, Buberwa Kaiza anasema maridhiano hayawezi kufanyika kupitia Chadema peke yake bila kuhusisha wadau wengine vikiwemo vyama vya siasa, asasi za kiraia zilizopata misukosuko katika awamu iliyopita

"Chadema ingekuwa na ujasiri wa kutosha ingewatafuta wadau wengine, wakiwemo waliokumbwa na kadhia va kupoteza fedha zao za kigeni au mali zao kufilisiwa wakawa kitu kimoja katika maridhiano ambayo yangekamilika. Wadau wakiwa wengi na masuala yenu yanapewa uzito, lakini kinyume na hapo majadiliano yatakuwa ya kawaida yanayolenga siasa kwa siku hiyo.

"Sitashangaa kuna maridhiano haya yakaishia hapa kwa sababu kila upande ulikuwa unatafuta nafasi ambazo zimepatikana na zinatafuta namna ya kuzitumia.

Naweza kusema tusahau suala la maridhiano kama yale yaliyozungumzwa na Rais Samia na Chadema, hayapo tena," anasema Kaiza.

Akiwa na mtazamo tofauti, mtaalamu wa masuala ya siasa, Dk Richard Munda anasema yanayoendelea katika mchakato huo, ni chachu ya watu kufikiria na kuienga maridhiano katika mantiki na msingi mzuri, badala ya kutukuza watu.

Dk Mbunda, ambaye ni mhadhiri wa siasa na jamii katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), anasema maridhiano yakiwa katika msingi mzuri havatajali kumsema hata aliyeanzisha mchakato huo au kuzungumza pale panapoonekana kuna upungufu ili marekebisho yafanyike.

"Maridhiano havawezi kukifunga chama cha siasa kukisema chama tawala kwa sababu wapo kwenye mchakato, hayatakuwa maridhiano tena," anasema.

Dk Munda anasema maridhiano yanatakiwa kuwa kitaasisi ili kulenga mambo yatakayojenga na kukuza utaasisi, akitolea mfano sheria zinazotengeneza uwanja sawa wa ushindani kisiasa. Pia alitolea mfano Ofisi ya Msajili wa Vyama vva Siasa akisema inatakiwa kulinda masilahi ya vyama vyote.

"Lakini katika shughuli za kisiasa hazitakiwa kuguswa na maridhiano, kwa mfano kama maridhiano hayatakiwi kumsema mpinzani wako kisiasa haya si maridhiano. Kwa sababu yanaondoa uhuru wa kufanya siasa katika uwanja sawa,' alisema Dk Mbunda.

Imeeandikwa kwenye Gazeti la Mwananchi
 
Back
Top Bottom