Mwanafunzi wa Feza ashangaa wanaofeli mtihani wa NECTA

Mwanafunzi wa Feza ashangaa wanaofeli mtihani wa NECTA

Moja kati ya tatizo la watanzania ni kutokujali mawazo ya mtu..

Huyo dogo anaongelea uhalisia wake na mazingira yake halisi so mlitaka aongelee kitu hajawahi kukiona?

Ni neema kuzaliwa katima familia ya kipato cha juu na kufanyiwa uwekezaji katika elimu yake na makuzi kiujumla kama haukupata bahati basi kaa kimya..
 
Ana point but bado ni mdogo na ana exposure ndogo.Hafahamu mazingira magumu wanayosoma wanafunzi wengine mf kukosa walimu,miundombinu mibovu nk.Yeye dunia yake ni shule-nyumbani hawezi kuelewa tofauti na hapo.Kasoma shule yenye kila kitu kuanzia walimu vitabu nk sio kosa lake hawezi kuelewa
 
Sihitaji kupeleka mtoto shule alafu aanze kusahau Kiswahili na kujirembua (kuongea kwa ishara) namna hii. ukileta mtoto wa kizungu hapo utakuta anaongea straight tu, ila wa kibongo lazima alete mbwembwe. au angeletwa hata wa international school of TAnganyika tu. hata hivyo, nampongeza mzazi na mtoto kwa hatua hiyo.
Nimemuona huyu mtoto akihojiwa akiwa na baba yake, hawa kwao wanazo kwani baba yake ni mtaalamu wa IT serikalini na wote wamesoma Feza, wapo watatu, sasa ukiangalia ada ya Feza ndio utajua huyu mtoto ni mayai, baba yake anadai watoto wake wana uwezo wa masomo sababu toka wakiwa watoto huwanunulia game zinazowajenga kiakili, sisi watoto wetu kutwa wanaangalia bongo movie za akina Mkojani, Joti na filamu zao za kipuuzi.
 
Kuna tofauti ndogo sana baina ya kiburi na kujiamini.

Japo dogo anahisi kaongea kwa kujiamini, kihalisia kinachosikika hapo ni kiburi, majigambo na dharau.

By the way, bwana mdogo kesha left group. Uzungu mwingi una madhara yake nao. Nina hakika hapo alipo anaji identify kama 'they/them'.
Sawa ana akili nyingi, je marinda yapo?
Duuuh ipa watu mnafikiria mbali.
 
Du Nkuyu Primary/sekondari school hehe mtu akifaulu ana divisheni III
Harafu halmashauri imefurusha wanafunzi wote masikini walio jaribu kukaa makambini angalau kuongeza muda wa kujisomea. Hii ilitokana na baadhi ya shule zenye tabia hiyo ovu kuanza kuwa na dv 1 saba hadi kumi hivi... serikali imewafurusha masikini hawa na kuwataka wakasome huko huko kwa bibi zao. Ndo mambo ya Nkuyu huku
 
Nikikiangalia hiki kibunda cha vyeti vya kidato cha nne(nimerudia kweli mpaka kupata credit 3) Nikalinganisha na maneno ya dogo.Daah naona vitone tu vinatoka kwenye macho.
 
That’s a fact: zaidi ya asilimia 50 ya wanafunzi Feza Schools ni waumini wa Uislamu. Nashangaa kwanini Wdturuki wenye mrengo mkali wa Kiislamu wafungue shule Tanzania: lengo lao ni nini haswa? Wanataka nini na akili za watoto wa Kitanzania? Mimi sioni hili suala limekaa vizuri haswa ukichukulia Uturuki haina uhusiano wowote maalum wa kihistoria na Tanzania. Waturuki wenyewe wakipata nafasi wapo tayari kuhamia Ulaya haswa Ujerumani ambapo wapo wengi sana. Nimeishi Norway, kuna wahamiaji wengi wa Kituruki ambao kazi yao ni biashara ya corner food stores kama Wahindi wa UK na migahawa ya kuuza doner kebab ma pizza. Sasa Waturuki kweli wana nia gani na Tanzania? Labda watakuwa wana manufaa kwa Waislamu wenzao.
Chief sema huna hela, naona unatoa excuse km zote kujustify uchoka mbaya wako
 
SSafi ANA My Baby. Wakumbushe Wenzio Wajibu wao wakiwa Shule ni Nini. Ingawa wewe WA Kishua bado unakaza Msuli WA kusoma. Keep it up👏👏👏
 
Hao ni vilaza, wachawi, wenye wivu na husda. Pia wapewe kombe au kama vipi serikali ianzishe tuzo ya maskini bora wawe wanashindana maana haiwezekani binadamu mwenye akili timamu ajivunie shida na umaskini. Ni punguani tu atajisifia ujinga na kumponda aliyefanikiwa.

Hapa angekuwa wa mwisho na kupata dungu hao wangekuja kumpongeza, akili zao ziko reverse.
Kwanza huyo dogo hapo alipo tiyari anawazidi akili na uzee wao. Katoa ushauri, maoni na kajibu maswali ila wanamkasirikia kama vile kaweka sheria.
1. Kasema wanafunzi wajipime na mitihani mingine maana NECTA ni rahisi. Kama mtu unaona ni upuuzi sio kesi, kawaazishie wanao ligi ya singeli na kucheza rede wasubiri NECTA.

2. Kasema NECTA ni rahisi. Ni maoni yake, kama unapinga mwambie mwanao NECTA ni ngumu akiingia kwenye mtihani azimie.

3. Kashangaa wanaofeli. Ajabu iko wapi? Mbona humu kuna watu mnashangaa wanaofaulu kama yeye, tena yeye hajawatafutia visingizio waliofeli ila nyinyi mnataja mara umaskini, mara yeye kisa wana hela.

Au serikali ianzishe tuzo ya umaskini maana watu wanaupenda sana. Ndio maana mwanasiasa akijiita mnyonge raia wanajigaragaza mtaani, wakati familia yake haijui shida.
Hizo tuzo za maskini zitawafaa sana, watu huwa wanaona umaskini ni sifa ya kujivunia.
 
That’s a fact: zaidi ya asilimia 50 ya wanafunzi Feza Schools ni waumini wa Uislamu. Nashangaa kwanini Wdturuki wenye mrengo mkali wa Kiislamu wafungue shule Tanzania: lengo lao ni nini haswa? Wanataka nini na akili za watoto wa Kitanzania? Mimi sioni hili suala limekaa vizuri haswa ukichukulia Uturuki haina uhusiano wowote maalum wa kihistoria na Tanzania. Waturuki wenyewe wakipata nafasi wapo tayari kuhamia Ulaya haswa Ujerumani ambapo wapo wengi sana. Nimeishi Norway, kuna wahamiaji wengi wa Kituruki ambao kazi yao ni biashara ya corner food stores kama Wahindi wa UK na migahawa ya kuuza doner kebab ma pizza. Sasa Waturuki kweli wana nia gani na Tanzania? Labda watakuwa wana manufaa kwa Waislamu wenzao.
Mbona hii ni nje ya mada???
 
Watu wamekasirika wakati dogo kaongea ukweli tupu.
Kwa sasa mwanafunzi hapaswi feli wakati notisi zimejaa kila mahali.

Wazazi hawafatilii maendeleo ya watoto wao hivyo mtoto aende au asiende shule haiwahusu.

Watawala na watawaliwa huandaliwa na wazazi
Swala la akili class lipo kipekee kuna mtu hata akaze msuli vpi hatoboi ila mwingine yeye ni kugusa tu.
 
Back
Top Bottom