Mwanafunzi wa Feza ashangaa wanaofeli mtihani wa NECTA

Mwanafunzi wa Feza ashangaa wanaofeli mtihani wa NECTA

Yupo SAWA wanaofeli lazima awashangae maaana ni wazembe mitihani ni rahisi Sana Kwa mwanafunzi anaesoma Kwa bidii
 
Sihitaji kupeleka mtoto shule alafu aanze kusahau Kiswahili na kujirembua (kuongea kwa ishara) namna hii. ukileta mtoto wa kizungu hapo utakuta anaongea straight tu, ila wa kibongo lazima alete mbwembwe. au angeletwa hata wa international school of TAnganyika tu. hata hivyo, nampongeza mzazi na mtoto kwa hatua hiyo.
Kabisa, naunga mkono hoja yako
 
Hesabu ni hobby, he wants to be an animator.

Kwanini wasingempeleka tu chuo straight hadi aende A-level? What's better than a kid who knows exactly what they want!
 
Utofauti uliopo kati ya Shule za serikali na Shule za Kulipia ni Mkubwa mno kuanzia Hata kwny Mindset tu ya Mwalimu na Mwanafunzi husika,

Mfano Halisi anzia tu Hata Mtaani kwenu angalia watoto wanaosoma Internationa schools na Hizi za Serikali yani Utaona kabsa Maji na Mafuta vilee vinajitenga.

Watt wa Shule za serikali wakilud nyumbani kazi Kuangalia Singeli na Nyimbo za Amelowa hku wakisindikizwa Na migogoro ya Baba na mama ndani ya Nyumba hivi unafkiri hyo mtoto Saikolojia yake itakuw sawa kweli ?

Mambo ni mengi sana nataman hat nianzishe Thread yangu kabsa nielezee hili kiundani ila Kiufupi Ufaulu wa Mtoto unaanzia Na Misingi ya Wanafamilia/kifamilia.
nimecheka km mazuri vileee.
 
Aisee hata mimi nawashangaa si tu wale wanaofeli ila pia na wale ambao wanafanya hiyo mitihani, ni kupoteza muda tu, bora wajiaandae kuwa maafisa ubashiri na maafisa usafirishaji
 
Ana point but bado ni mdogo na ana exposure ndogo.Hafahamu mazingira magumu wanayosoma wanafunzi wengine mf kukosa walimu,miundombinu mibovu nk.Yeye dunia yake ni shule-nyumbani hawezi kuelewa tofauti na hapo.Kasoma shule yenye kila kitu kuanzia walimu vitabu nk sio kosa lake hawezi kuelewa
Yaani aanze kufikiria habari za kukosa waalimu na mazingira mengine? Yeye yanamhusu vipi?
Kama unataka hivyo basi mngependekeza kuwa na mitihani na marks tofauti kwa kila shule kulingana na status.
 
Sihitaji kupeleka mtoto shule alafu aanze kusahau Kiswahili na kujirembua (kuongea kwa ishara) namna hii. ukileta mtoto wa kizungu hapo utakuta anaongea straight tu, ila wa kibongo lazima alete mbwembwe. au angeletwa hata wa international school of TAnganyika tu. hata hivyo, nampongeza mzazi na mtoto kwa hatua hiyo.
Hizo si ndizo zinaitwa "swaga"?

Wewe nae una swaga zako za kichapwa.
 
Hata mimi nashangaa kwanini mwanafunzi afeli, kwani alipelekwa shule kufanya nini?

Mfumo wetu wa elimu na mfumo kama wanaoutumia FEZA ni tofauti. Kijana kaeleza vizuri kabisa, amefundishwa kuelewa na siyo kuhifadhi, ndicho anaona kinamsaidia.

Mwalimu una moyo gani kumpeleka mwanafunzi wako aende kufanya mtihani ambao wewe mwalimu unafahamu kabisa kuwa anaenda kufeli?

Shule zetu waanze kufata namna ya kufundisha kama Madrassa za Kiislam, huendi topic nyingine mpaka uielewe topic uliyopo. Simpo. Hakuna kufeli.

Nnauhakika FEZA wanatumia mfumo huo.
 
tungefuata namna mnavyofundisha madrasa, tungekuwa nyuma sana kielimu.
 
Yupo sahihi kutokana na mazingira aliyopo. Pale Kuna walimu Tena wazuri, vitabu vya kutosha pamoja na akienda shule hawazi kazi za usafi, kulima Wala kugombania usafiri. Mtoto wa namna hiyo akifeli lazima utamshangaa.
 
Hata mimi nashangaa kwanini mwanafunzi afeli, kwani alipelekwa shule kufanya nini?

Mfumo wetu wa elimu na mfumo kama wanaoutumia FEZA ni tofauti. Kijana kaeleza vizuri kabisa, amefundishwa kuelewa na siyo kuhifadhi, ndicho anaona kinamsaidia.

Mwalimu una moyo gani kumpeleka mwanafunzi wako aende kufanya mtihani ambao wewe mwalimu unafahamu kabisa kuwa anaenda kufeli?

Shule zetu waanze kufata namna ya kufundisha kama Madrassa za Kiislam, huendi topic nyingine mpaka uielewe topic uliyopo. Simpo. Hakuna kufeli.

Nnauhakika FEZA wanatumia mfumo huo.
Mfumo gani?, wakati wanachukua wanafunzi wenye uwezo wa juu kabisa na kuwachuja, hadi kufika form iv ni cream tupu

Shule za serikali za kata ni zoazoa wotee ndani,

Shule za serikali zinazochukua cream kama ilboru, Kibaha nk zinamatokeo sawa na Feza
 
Back
Top Bottom