Kwanza kabisa niwape pole wanafunzi wa UDSM kwa yaliyotokea, pili niwapongeze kwa umoja na mshikamano usiyoangalia maswala ya siasa kama wengi wetu tunaochangia ujinga katika maswala ya msingi. Nawapongeza maana baada ya tukio lenyewe wanafunzi walikimbia mbiyo kali mpaka kituo cha afya cha chuo kuomba msaada wa ambulance bahati nzuri mwanafunzi mwenzao anayeishi hall six alichukua gari yake akamuwahisha pale dispensary akapewa huduma ya kwanza haraka iwezekanavyo na kukimbizwa Muhimbili.
Kwa masikitiko makubwa nachukua nafasi hii kuwaasa wana JF kuwa makini na statements zinazotuweka katika hali tunayodhani ni sifa kuzitamka au ni kumkomoa mtu au chama kumbe ni kujipalia makaa ya moto. Eti tanzania siyo sehemu nzuri ya kuishi alafu wewe uko wapi? wewe ni mtanzania kweli? au ndicho chama chako kinachokufunza kushadadia? Eti Pinda amesema watu wapigwe tu hivyo majambazi nao wapige waue tu maana wameruhusiwa na pinda, unadhani chama chako kikiingia madarakani ndiyo utakuwa mwisho wa ujambazi, USA hamna ujambazi? chama chako kikiingia madarakani mtaandamana na kuvunja amani bila polisi kuwazuia? Lets think positive as wazalendo siyo kumwaga unga, ugali na mboga.
Mh. John bukuku wa Full Shangwe, mimi nilifika pale hosipitali ya chuo wakati huyu bwana alivyokua ameshapelekwa Muhimbili, ila askari walifika baadae, ni kweli kulikua na uzembe kwa askari. Hilo la kwamba uongozi wa chuo ulipigiwa simu haukufika kutoa msaada kwa wakati si kweli maana walimpeleka hosipitali ya chuo walisema hawakuanza kazi ya kufatuta uongozi wa chuo bali kazi ya kumpeleka mwenzao hosipitali na lilifanyika kwa haraka. Kumbuka baada ya kusikia risari imepigwa vijana walitaharuki na kutawanyika kwanza ndipo wakaanza makelele kuwaita wenzao huku wengine wakikimbia kituo cha afya chuoni kuomba msaada wa usafiri lakini kumbe huku nyuma mwenzao aliyepo hall six kama nilivyoeleza awali alijitokeza na kutoa usafiri kwenda hosipitali na kwenda kituo cha polisi kupata PF3 wakati mwenzao anapewa huduma ya kwanza na hilo lilifanywa kaw haraka sana. Manesi wa Chuo walifanya kazi ya ziada maana ni muda mfupi tu mfanyakazi wa chuo alikua amepelekwa hapo na kufariki kwa ugonjwa.
Mwisho nawasihi ndugu zangu tuache kuchangia mada kiitikadi au kwa kushabikia siasa, tuangalie mustakabali ya nchi yetu kwanza vyama baadae.