Mwanafunzi anaetumia nguvu na muda mwingi kujifunza kitu kile kile kwa msaada mkubwa ili aelewe, akifaulu ni Genius?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,034
Maana nashangaa nashindwa kuelewa watu wanawaitaje hawa watu magenius na utawalinganisha vipi na wale ambao wanaweza kujifunza haraka bila kurudia rudia na wana msaada mdogo wa material na walimu.

Unakuta mwanafunzi topic 1 tu anaiwekea nguvu kubwa mnooo! Yaani anairudia rudia sana ili iwe kama chorus, muda huo kuna vitabu vingi vya yeye kuelewa zaidi, hapo kuna walimu wapo muda wowote na tena wamejikita kuwafundisha namna ya kujibu maswali ya kwenye mtihani. Kwa huyu mwanafunzi hadi anakaribia mitihani yake kuna kipya kipi hapa zaidi ya kwenda kurudia kiitikio?

Hapo sasa upande mwengine unakuta kuna mwanafunzi ambae kitabu alichonacho ni cha kuazima, walimu wanafundisha tu darasani hakuna msaada baada ya hapo, ni yeye kuamua asome au apuuzie hakuna wa kumcontroll, mwanafunzi huyu unakuta uwezo wake wa kujifunza haraka ndio unambeba na pia uwezo wa kutatua maswali mapya unamsaidia kujibu maswali ambayo anakutana nayo kwa mara ya kwanza.

Hapo yupi ni genius, kasuku wa kurudia kiitikio ama huyo anaeweza freestyle kutoka kichwani papo hapo?
 
Nilisoma peke yangu topic ya organic chemistry a level kwa kutumia knowledge ya o level. Je, na mimi ni genius?
 
The end justifies the means negro.
Isikupe presha maana kila mtu anashunda mechi zake.
 
Nadhani hata Einstein alikua ni mtu wa kusoma sana na kufanya tafiti nyingi kwa kurudia rudia sana..ubongo bila kupata chakula chake hautaweza kufikia kiwango chake
 
Back
Top Bottom