MwanaDiwani na Nape Nnauye Nawaomba hapa...

MwanaDiwani na Nape Nnauye Nawaomba hapa...

Bado kuna mengi sana.. Hili dogo tu ulilogundua
 
Ni maneno ya Lukuvi na si ya CCM

maswali ya faiza foxy hayajibiki zaidi ya lukuvi kuwaomba radhi waislamu. propaganda zina wakati na siyo wakati huu, huamini hili subilini uchaguzi mkuu ndio mtaijuwa misikiti itakavyowasurubu.
 
FaizaFox unachekesha sana, mwanadiwani yuko busy na ukawa hadi auangushe, akishafanikiwa atakuja kukujibu .... watch out my sister
 
Wazanzibar toka zamani wanajisaliti wenyewe na ndio mana ukienda kwao ni maskini wa kutupwa lkn wakija bungeni hawana wanalosema zaid ya kupigia makofi na kuunga mkono hoja.

Sitoshangaa kuona hakuna mbunge atakaye liongelea hili hasa wa zanzibar manake ni waoga wa maisha sana.
 
Chabruma
Je CCM imekuchukua hatua gani kwa mwanachama wake huyu aliyeongea maneno ya uchochezi???

Nikimwambia daktari nina hofu sindano utakayo nidunga itaniua, ni jukumu la daktari kunihakikshia usalama wangu, kadharika wenye jukumu la kumtoa hofu Lukuvi ni wale aliowaona ni tishio kwake, nini maana ya kauli zao na matendo yao.
 
Last edited by a moderator:
MwanaDiwani na Nape Nnauye,

Nawaomba hapa mtowe majibu kwa haya maswali myepesi kwa majibu muafaka, ambayo kila msomaji humu ataridhika nayo, na kama ana la ziada ataongezea.

1) Jee, alivyohubiri Wiilliam Lukuvi kanisani kuwa hofu yake ni kuwa Zanzibar "wakiwachwa watawale watasumbua". Nyinyi kama wana CCM wenzagu naomba mje hapa mtueleze kinaga-ubaga, hayo ni maneno ya Lukuvi? au ya CCM? au ya Serikali?

Sitaki kumalizia kasema watasumbua vipi, labda nyinyi na wachangiaji wengine mmalizie.

Mkimaliza hili namba 1) kuna mengine yaja.

Najua majibu unayo, unangoja kuyapigia mstari tu.
 
Ni maneno ya Lukuvi na si ya CCM

Ni maneno ya CCM alikuwa pale kwa kofia ya Waziri Mkuu...Tunaweza kuyaita ni maneno ya serikali full stop! Nape hawezi kuja jibu hapa ni oversize kwake yy yake ni kujua ukawa wanafanya nini ajibu kwa mipasho
 
Hahahahah, William Lukuvi alichokifanya ni zaidi ya ubaguzi.

Werema, nawaachia Wazanzibari wenyewe, kwani wao ni wanafik, wakiwa Zanzibar wanasema mengine wakija Dodoma wanasema mengine. Astahili yao yawapate kwa Werema. Ingawa si vyema alivyosema na haitoshi, lakini niliona nnawatetea mazumbukuku, sikumuona hata mmoja akirudia hoja hiyo bungeni wala kulalamika kwenye vyombo vya habari. Wazanzibari wanajisaliti wenyewe kwa wenyewe, ni wanafik nambari moja.
Faiza siamini mpk leo hufaham CCM ni kitu gani??huo ubaguzi haujaanza leo kunapotokea watu kama wakina Tundu Lissu,Seif Hamad na wengine kuelezea hayo watu kama nyie ndo mnakua wa kwanza kuwatetea kwa itikadi..awe amezungumza kama yeye na ndivyo alivyoelezea kwenye bunge la katiba kua huo ndio msimamo wake binafsi ambao atausimamia au kimezungumza chama haina tofauti..kwan kama kazungumza yeye binafsi ambae ni mwanachama na kiongozi mkubwa ndani ya chama na serikali ndio inamaana haitaleta uzito wowote..Faiza dada angu fungua macho wakati ni sasa...akili ya kuambiwa usiitumie zaidi kuliko akili yako..
 
Nape yupo nzega mwanadiwani yupo Igunga labda Tandaleone utapata jibu haraka
 
MwanaDiwani na Nape Nnauye,

1) Jee, alivyohubiri Wiilliam Lukuvi kanisani kuwa hofu yake ni kuwa Zanzibar "wakiwachwa watawale watasumbua". Nyinyi kama wana CCM wenzagu naomba mje hapa mtueleze kinaga-ubaga, hayo ni maneno ya Lukuvi? au ya CCM? au ya Serikali?

Sitaki kumalizia kasema watasumbua vipi, labda nyinyi na wachangiaji wengine mmalizie.

Mkimaliza hili namba 1) kuna mengine yaja.
Si ungemalizia kunukuhu sentensi nzima kama alivyosema? Unaogopa eeh?
 
faizaFoxy mara zote huwa ukiweka itikadi za vyama kando (sina hakika na itikadi za dini) hoja yako hugusa hisia halisi za mtanzania asiye na chama kama mimi.

Wasiwasi wangu ni kwamba hutapata majibu stahiki kutoka kwa uliowataja..

Maiti ikitikisika unategemea itaamuka? mbona Pinda alishasema kuwa Zanzibar sio inchi na hao CCM akiwamo na FF hawakuhoji wakati ule?
 
FaizaFoxy itabidi Lukuvi akutake radhi yaishe......maana naona umedhamiria kumshughulikia haswa.......Usisahau na Werema na ubaguzi wake.......

Mbona mnashadadia sana ishu ya Lukuvi wakati ameonyesha hofu tu?je wale wanaoingia misikitini kila kukicha mbona hamuwazungumzii?mimi nina cd zaidi ya kumi za jamaa kwenye misikiti tena juzi kati UKAWA walipotoka nje,mngesikia wanayoyasema hakika wenye mapenzi mema na nchi hii wala msingeongea ya Lukuvi
Siwapendi ccm na wala siitaki mfumo wa muungano wa serikali mbili lakini namuunga mkono lukuvi katika hili.
 
Back
Top Bottom