Utachukua hatua gani kichama Mkuu?Lukuvi na wenzake wamenichefua sana hata sitaki kuwasikia.
CCM hawawezi kuja hapa maana wanajua Lukuvi alimwakilisha Waziri Mkuu.Hivyo wanaweza kutumia mwanya huo kuisukumia serikali.Serikali nayo inaweza kumkataa Lukuvi kuwa haikumtuma kusema hayo bali ni mawazo yake binafsi.My take:Kwakuwa CCM imejaa wengi wenye mitazamo ya Lukuvi na Werema,Wana sisiem wafanye maamuzi magumu kushirikiana na UKAWA kuiweka pembeni 2015, kama ishara ya kupinga madhila yanayoendelezwa na viongozi wasio na utashi wa kweli huku wakiwa na dhamana kubwa kiserikali kuongoza nchi hii.Hii itaidaidia CCM kuzaliwa upya na kuweza kujipanga tena kutekeleza malengo yake mahususi na asili.Vinginevyo tutakuwa tuna bytime
Bila shaka kauli za Lukuvi na Werema zitasaidia kum'badilisha mtazamo Madam Faiza.
Hivi karibuni,Madam FaizaFoxy umejitokeza kukosoa waziwazi na kuhitaji ufafanuzi wa wana-CCM wenzako juu ya kauli za viongozi waandamizi wa kiserikali. Ni jana tu hapo, umewaita MwanaDiwani na Nape Nnauye waje waielezee kauli ya Waziri William Vangimembe Lukuvi aliyoitoa kanisani juu ya maneno yake ya kibaguzi na ya kidini. Kilichotokea unakijua. Wahusika walikuja (nadhani ni MwanaDiwani) wakiwa hawana majibu.
Nichukue nafasi hii kukuomba Madam FaizaFoxy kurudi njia kuu.Kutetea chama chako. Ukipenda boga,penda na ua lake. Unachofanya sasa hapa JF ni kukidhalilisha chama chako pendwa cha CCM.Nasema hivi kwakuwa,ndani ya CCM hakuna wakueleza kwa ufasaha juu ya kauli za Lukuvi,John Damian Komba na Jaji Fredrick Mwita Werema. Hata wenyewe hawawezi kuelezea. Labda ungesema wasifie kauli hizo na kukejeli upinzani.
Madam FaizaFoxy, wewe wajua.Wajua bila ya shaka yoyote.Kwamba,ndani ya chama chenu cha CCM kuna waongeaji na si wasemaji. Kuna wanamaneno mengi na si wenye hoja nyingi. Kwamba, ni rahisi kukashifu kuliko kusifu;kurubuni kuliko kubuni;kuponda zaidi ya kupenda. Madam FaizaFoxy,kama wakipenda chama chako,usiwaite kwenye mijadala tena. Ni Nape Nnauye aliyekimbia Mjadala wa Serena Hotel.
Nakuomba sana Madam FaizaFoxy.
Wewe nawe, si bora ungejiita mkandarasi ningekuelewa, hiloo la "mukandarasi" sikuelewi kabisa.
Embu tuwe fair kidogo kosa la Lukuvi liko wapi?
Salmini Amour amewahi kunukuliwa jukwaani kwenye mkutano wa CCM Zanzibar akiwaita wanaodai serikari tatu ni Manyan'gau na wapenda utumwa. Akimalizia na kusema uhuru wa nchi unapatikana mara moja sasa wapinzani, Uamsho na wana CCM wenzake wanaodai serikari tatu wanapigania uhuru gani tena? Mbona amkuwaka na kauli za kebehi au kuuliza kama ndio msimamo wa CCM.
Serikari imewahi kuwazuia wazi SMZ kujiunga na OIC ambacho ni chombo cha waarabu mara kadhaa, na agenda hiyo aijesha. Kuna watu huko ZnZ wanaodai kurudisha old ties na Oman, kuna watu wanaowaita wabara watwana, kuna watu wanaotaka far right Islamic thinking imposed in Zanzibar na ukizingatia hakuna ukandamizaji wa Imani and the islands are dominated by Muslim; watu hao wanadai nini zaidi ya ubaguzi na mipaka ya ideology zao itaishia wapi huwezi ku-gurantee eti itakuwa huko huko ZnZ.
Msikilize vizuri Lukuvi, ccm inang'ang'ania serikali 2 ili kuthibiti uislam Zanzibar?
Mtazamo wangu uko pale pale siku zote, kusimama kwenye ukweli, ndiyo maana mpaka hii leo hunioni kumsifia kinafik Nyerere kwa makosa aliyoyafanya, ingawa ni muasisi wa CCM na mimi ni mwanachama hai wa CCM.
Ikiwa Kinana anaweza kutembea nchini na kukemea Serikali katika mapungufu yake, ni wakati muafaka na sisi wapenzi wa CCM tukemee mapungufu ya wana CCM wanaokiharibia sifa chama chetu tunachokipenda.
Tuliojaaliwa kupitia vitabu japo "kiduchu" hiyo inaitwa "Checks and Balances".
Hiyo ni tafsiri yako wewe kudhibiti maana kunaendana na sheria sambamba ambazo zinazosema misikiti isijengwe, kusiwe na mihadhara ya kidini na mengineo yenye ku-deprive imani ya kiisalam na njia zake. Hivyo ndio unavyo control kitu, siyo kauli ya mtu au maoni yake binafsi, sasa ni lini CCM imefanya udhibiti wa uislamu? au wa dini yeyote au kabila lolote, for that matter.Msikilize vizuri Lukuvi, ccm inang'ang'ania serikali 2 ili kuthibiti uislam Zanzibar?
Faiza sema ukweli wako, huu ni wakati wako mzuri kujiuliza ni kipi hasa cha msingi kinachokuweka CCM. Siamini kama kweli uanachama wako CCM umesimama kwenye nguzo halisi (real) za chama hicho hivi leo. Lukuvi ndio sura halisi ya CCM leo hii; usipokubaliana naye, jiulize vizuri ni CCM ipi hasa uliyomo? Halafu, usipoteze muda na Mwanadiwani au Nape. Sipendi kutumia kauli zinazotumiwa na baadhi ya watu kama akina Nkamia kuhusu watu wa aina hiyo. Kifupi ni kuwa, hao ni vipaza sauti tu; hawana majibu. Wewe nenda moja kwa moja kwa mwajiri wa Lukuvi akufahamishe kama kuna uwezekano wowote wa kumtenganisha Lukuvi (na kauli yake) na CCM na Serikali na hata na mkuu mwenyewe aliyemteua.
Kutokana na kuwa na michango inayosisimua jukwaa, unaonaje ukiwa mtu huru usiyefungamana na vyama ili uendelee kushusha nondo kila pande bila hiyana? Unapojinasibu na uanachama wa CCM halafu unawasaili akina Lukuvi, Nape na Mwanadiwani wanapoitetea "misingi halisi" ya CCM yao ya leo hii, unatuletea mkanganyiko na kushusha viwango vya tafakuri yako tunayoifahamu. Hebu sema ukweli wako, ni nini hasa kinachokukosha huko CCM? Na kweli ikuweke huru.
Checks and balances ndani ya CCM hii ya leo? Faiza hebu acha utani, tuna mambo muhimu ya kushughulikia kulikwamua taifa. CCM yote iko completely unbalanced; inahitaji total overhaul. Hiyo ndiyo kazi unayotakiwa kuizungumzia kama uko tayari kukifufua chama na kukirejesha kwa wananchi.
Kikwete na Kinana.