MwanaDiwani na Nape Nnauye Nawaomba hapa...

MwanaDiwani na Nape Nnauye Nawaomba hapa...

Ndugu, usipotoshe wanaJF. Jaribu kutokuishi katika maisha ya kudhani dhani.

SHeria za JF zimewekwa ili ziwaongoze wanaJF katika mijadala inayolenga katika ujenzi wa Taifa endelevu. Kuvunja taratibu na sheria za JF kwa nia na madhumuni ya kutaka kupitisha hoja zako na zikubalike ni udhaifu wa kiwango cha juu.

MwanaDiwani siyo Nape Nnauye na hawezi kuwa Nape Nnauye katika maisha yake.

Jikite kwenye hoja iliyoko mezani.

Mimi nakwambia NJAA yako imefunga TURBO.
Wewe umesema jf hakuna ofisi za CCM, mara wewe huusiki, usiulizwe, wewe si msemaji. Hilo ni sawa.
Sasa hapa jf unakujaga kama nani??
Unakujaga Kufanya nini??
Lukuvi aliongea kwa niaba ya Pinda ambayo ni serikali Kuu inayoongozwa na Chama SIKIVU.
 
MwanaDiwani na Nape Nnauye,

Nawaomba hapa mtowe majibu kwa haya maswali myepesi kwa majibu muafaka, ambayo kila msomaji humu ataridhika nayo, na kama ana la ziada ataongezea.

1) Jee, alivyohubiri William Lukuvi kanisani kuwa hofu yake ni kuwa Zanzibar "wakiwachwa watawale watasumbua". Nyinyi kama wana CCM wenzangu naomba mje hapa mtueleze kinaga-ubaga, hayo ni maneno ya Lukuvi? au ya CCM? au ya Serikali?

Sitaki kumalizia kasema watasumbua vipi, labda nyinyi na wachangiaji wengine mmalizie.

Mkimaliza hili namba 1) kuna mengine yaja.

Msikilize Lukuvi kuanzia dakika ya 6 sekunde 30

[video=youtube_share;obOYhW6LJUI]http://youtu.be/obOYhW6LJUI[/video]

Mkuu FaizaFoxy katika Uzi ule wa Werema na wazanzibari nilisema team MwanaDiwani haya mazungumzo SI kariba Yao! Wewe anzisha mada ya kumjadili mtu binafsi uone namna team Lumumba watakavyo jaa hapa.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu Faizafoxy mbona unauliza kinyeo cha kuku wakati chini ya mkia unapaona?
Kwa ufupi ni kwamba kilichompa msukumu Lukuvi ni kile kilicho ndani ya mioyo ya viongozi wengi Tanzania na duniani kwa ujumla.
Hawapendi,hawataki,hawaoni raha kuiona jamii ya kiislam inadevelop ktk nyanja yeyote ile.
Huewezi kula ugoro bila kutema mate, Lukuvi yuko ndani ya mfumo kama yale yangekua ni siasa angesemea jukwaani na Si kanisani.
 
Daaaah!!!!
 
Acha kuendekeza njaa, Mchagga na CCM wapi na wapi? Kila siku Nape anatukana na kubagua wachagga majukwaani wewe umeng'ang'ania kama luba. Ile sera ya jikombe ukomborewe haipo siku hizi, we jitume tu kwenye kazi, fanya savings, komalia DUKA lako umaskini utaisha tu. Haihitaji kuwalamba miguu hawa majizi ya chama chenu.
nafikiri wewe hunijui vyema, binafsi sio mwnachama wa ccm kwasababu ya kupewa posho ama hela, na wala hakuna anayenijua kama ni mwanachama zaid ya mwenyekiti wa tawi langu.

ni mwanachama kwasababu nakipenda chama lkn pia sifungwi na sheria kwamba nisikemee pale maovu yanapotendeka na daima siko ili kuitetea ccm ccm inapaswa ijitetee yenyewe kwa matendo yake sasa kama haiwez kujitetea hilo si langu ila langu mimi ni kukosoa pale inapokosea na kuipigia makofi pale inapotenda jambo zuri na kusapoti chama kwa michango yangu. hii ndiyo kazi ya mwanachama aliye hai.

sasa ukimwona mwanachama mbulula huyu utamkuta hawez kukemea ila ndo hata akisemwa vibaya anapiga makofi makofi tuu mie sio wa aina hiyo.
 
Si CCM tu, Uislam ni kwanza kabla ya kila kitu.

Huwezi kutumikia mabwana wawili.

Ningeondosha mashaka na motives zako kama Kukuvi jina lake lá kwanza lingekuwa Hussein, Ramadhan au mengine yanayofanana na hayo. Halafu hizo kauli angezitoa msikitini.

BTW: Mimi siupendi muungano, hivyo ukifa kwangu itakuwa sherehe.
 
asante FF kwa kuuliza hayo maswali, wasiwasi wangu ni kuwa, kwa namna CCM mnavyolindana, na kwa kuwa ubaguzi huo na vitisho hvyo alianza kuvitoa jK mwenyewe, uhesabu maumivu tuu.

Ndai yaccm hakuna mwenye utashi huo, wa kuweza kujibu hoja zako, sembuse Nape, hata ukimuuliza Kinana, hawawezi kujibu, nakupa pole.

labda uamue kuanzisha bifu na wana ccm wenzako.
 
Mimi nakwambia NJAA yako imefunga TURBO.
Wewe umesema jf hakuna ofisi za CCM, mara wewe huusiki, usiulizwe, wewe si msemaji. Hilo ni sawa.
Sasa hapa jf unakujaga kama nani??
Unakujaga Kufanya nini??

Lukuvi aliongea kwa niaba ya Pinda ambayo ni serikali Kuu inayoongozwa na Chama SIKIVU.

Wewe huwa unakujaga kama nani? na unakuja kufanya nini?
 
Ningeondosha mashaka na motives zako kama Kukuvi jina lake lá kwanza lingekuwa Hussein, Ramadhan au mengine yanayofanana na hayo. Halafu hizo kauli angezitoa msikitini.

BTW: Mimi siupendi muungano, hivyo ukifa kwangu itakuwa sherehe.

Now that is preposterous acusation why are you saying FF would not have said anything if Lukuvi was not the one who said those nasty things againt Zanzibaris and muslims in general? She called Nape and the other CCM cadres are they christians only? Why of course Pinda did not ask Kinana to go to the Church and represent him because Kinana is a muslim, and even if he would, definetly Kinana would not say such things aginst muslims of Zanzibar.
However about islamic names do not represent someones allegiance to Islam Kinana as a muslim and in his capacity as SG of CCM would have reprimanded Lukuvi in such manner.
 
Ningeondosha mashaka na motives zako kama Kukuvi jina lake lá kwanza lingekuwa Hussein, Ramadhan au mengine yanayofanana na hayo. Halafu hizo kauli angezitoa msikitini.

BTW: Mimi siupendi muungano, hivyo ukifa kwangu itakuwa sherehe.

Mi napenda ufe leo. Ufe tu basi. Ufe tu. Naam na ufe.
 
Ningeondosha mashaka na motives zako kama Kukuvi jina lake lá kwanza lingekuwa Hussein, Ramadhan au mengine yanayofanana na hayo. Halafu hizo kauli angezitoa msikitini.

BTW: Mimi siupendi muungano, hivyo ukifa kwangu itakuwa sherehe.

Mashaka yako ndio maradhi yako.

Hapa hauna shaka kuwa William Lukuvi aliyoyasema Kanisani ni mazuri sana kwa Taifa hili, au sio?
 
nafikiri wewe hunijui vyema, binafsi sio mwnachama wa ccm kwasababu ya kupewa posho ama hela, na wala hakuna anayenijua kama ni mwanachama zaid ya mwenyekiti wa tawi langu.

ni mwanachama kwasababu nakipenda chama lkn pia sifungwi na sheria kwamba nisikemee pale maovu yanapotendeka na daima siko ili kuitetea ccm ccm inapaswa ijitetee yenyewe kwa matendo yake sasa kama haiwez kujitetea hilo si langu ila langu mimi ni kukosoa pale inapokosea na kuipigia makofi pale inapotenda jambo zuri na kusapoti chama kwa michango yangu. hii ndiyo kazi ya mwanachama aliye hai.

sasa ukimwona mwanachama mbulula huyu utamkuta hawez kukemea ila ndo hata akisemwa vibaya anapiga makofi makofi tuu mie sio wa aina hiyo.

huna tofauti na wale wa mjengoni.. ambao wako pale wamejazana kusubiria tu kauli ya supika mwenye makinda yaaaa ''wanaosema SIYO... SIYOOOOOOOOOO!!!!!!!!!! wanosema NDIYO.. NDIYOOOOOOOO!!!!!!!!!!! waliosema siyo WAMESHINDA!!!!
alafu wanaendelea kutafakari kidhungu namnahii.. KOMBA.jpgKOMBA.jpg
 
MwanaDiwani na Nape Nnauye,

Nawaomba hapa mtowe majibu kwa haya maswali myepesi kwa majibu muafaka, ambayo kila msomaji humu ataridhika nayo, na kama ana la ziada ataongezea.

1) Jee, alivyohubiri William Lukuvi kanisani kuwa hofu yake ni kuwa Zanzibar "wakiwachwa watawale watasumbua". Nyinyi kama wana CCM wenzangu naomba mje hapa mtueleze kinaga-ubaga, hayo ni maneno ya Lukuvi? au ya CCM? au ya Serikali?

Sitaki kumalizia kasema watasumbua vipi, labda nyinyi na wachangiaji wengine mmalizie.

Mkimaliza hili namba 1) kuna mengine yaja.

Msikilize Lukuvi kuanzia dakika ya 6 sekunde 30

[video=youtube_share;obOYhW6LJUI]http://youtu.be/obOYhW6LJUI[/video]
maneno ya kichochezi sana aliyoyasema Lukuvi, kama kweli nchi hii ingekuwa inafuata utawala bora angengolewa madarakani
 
MwanaDiwani na Nape Nnauye,

Nawaomba hapa mtowe majibu kwa haya maswali myepesi kwa majibu muafaka, ambayo kila msomaji humu ataridhika nayo, na kama ana la ziada ataongezea.

1) Jee, alivyohubiri William Lukuvi kanisani kuwa hofu yake ni kuwa Zanzibar "wakiwachwa watawale watasumbua". Nyinyi kama wana CCM wenzangu naomba mje hapa mtueleze kinaga-ubaga, hayo ni maneno ya Lukuvi? au ya CCM? au ya Serikali?

Sitaki kumalizia kasema watasumbua vipi, labda nyinyi na wachangiaji wengine mmalizie.

Mkimaliza hili namba 1) kuna mengine yaja.

Msikilize Lukuvi kuanzia dakika ya 6 sekunde 30

[video=youtube_share;obOYhW6LJUI]http://youtu.be/obOYhW6LJUI[/video]
FAIZA FOX.Mahakama za watu ni kipimo.na kipimo mara nyingi huwa hakisemi uong😵na jinsi watu wanavyounga mkono hoja yako, tena hasa wale wanaotofautiana na wewe kiitikadi.Unajua ni kwa nini, ni kwa sababu umesimamia ukweli.mimi ni mkristu lakini nilikerwa sana na ubaguzi wa kidini wa LUKUVI. Ki ukweli kabla ya mada hii nilikua nakuchukia sana kwa kutetea ujinga wa CCM hata kama ni chama chako.Baba yako akiwa jambazi ni wazi huwezi kumfurahia ingawa kama mtoto huwezi kumkanya,lakini kumuonyesha kwa hisia tu kuwa hupendi ujambazi wake pia ni ujumbe tosha.Sasa kwa bahati mbaya leo kiongozi mmoja wa chama chako amegusa maslahi yako DINI. Umepata ujumbe.Sasa basi hivi ndivyo huwa tunaumia sisi watu tusio na vyama au watu wasio CCM.Hata hivyo "try to imagine" kauli kama hiyo ingetolewa na Mbowe, Slaa, Mzee Ndesambulo au Migwa hapa Tanzania ingekuwaje leo kwa propaganda za kishenzi za CCM,siamini kamaCHADEMA leo hii bado ingekua na usajili wake .Dada yangu kubali kataa Viongozi wa CCM wana dharau na majivuno.Unakumbuka Merry Chatanda aliwaambia Maaskofu kuwa kama wanataka siasa wavue majoho na waingie ktk siasa,hii ilikua dharau.FF sitaki kuamini kuwa kuipenda CCM KUNAONDOA AKILI SITAKI.
 
CCM hawawezi kuja hapa maana wanajua Lukuvi alimwakilisha Waziri Mkuu.Hivyo wanaweza kutumia mwanya huo kuisukumia serikali.Serikali nayo inaweza kumkataa Lukuvi kuwa haikumtuma kusema hayo bali ni mawazo yake binafsi.My take:Kwakuwa CCM imejaa wengi wenye mitazamo ya Lukuvi na Werema,Wana sisiem wafanye maamuzi magumu kushirikiana na UKAWA kuiweka pembeni 2015, kama ishara ya kupinga madhila yanayoendelezwa na viongozi wasio na utashi wa kweli huku wakiwa na dhamana kubwa kiserikali kuongoza nchi hii.Hii itaidaidia CCM kuzaliwa upya na kuweza kujipanga tena kutekeleza malengo yake mahususi na asili.Vinginevyo tutakuwa tuna bytime
 
Hivi karibuni,Madam FaizaFoxy umejitokeza kukosoa waziwazi na kuhitaji ufafanuzi wa wana-CCM wenzako juu ya kauli za viongozi waandamizi wa kiserikali. Ni jana tu hapo, umewaita MwanaDiwani na Nape Nnauye waje waielezee kauli ya Waziri William Vangimembe Lukuvi aliyoitoa kanisani juu ya maneno yake ya kibaguzi na ya kidini. Kilichotokea unakijua. Wahusika walikuja (nadhani ni MwanaDiwani) wakiwa hawana majibu.

Nichukue nafasi hii kukuomba Madam FaizaFoxy kurudi njia kuu.Kutetea chama chako. Ukipenda boga,penda na ua lake. Unachofanya sasa hapa JF ni kukidhalilisha chama chako pendwa cha CCM.Nasema hivi kwakuwa,ndani ya CCM hakuna wakueleza kwa ufasaha juu ya kauli za Lukuvi,John Damian Komba na Jaji Fredrick Mwita Werema. Hata wenyewe hawawezi kuelezea. Labda ungesema wasifie kauli hizo na kukejeli upinzani.

Madam FaizaFoxy, wewe wajua.Wajua bila ya shaka yoyote.Kwamba,ndani ya chama chenu cha CCM kuna waongeaji na si wasemaji. Kuna wanamaneno mengi na si wenye hoja nyingi. Kwamba, ni rahisi kukashifu kuliko kusifu;kurubuni kuliko kubuni;kuponda zaidi ya kupenda. Madam FaizaFoxy,kama wakipenda chama chako,usiwaite kwenye mijadala tena. Ni Nape Nnauye aliyekimbia Mjadala wa Serena Hotel.

Nakuomba sana Madam FaizaFoxy.
 
Back
Top Bottom