Mwana JF unamaoni gani kuhusu mjadala wa Dini ulioandaliwa kati ya Dkt. Sule na Pastor Ndacha tarehe 16 na 17 December 2023

joex

JF-Expert Member
Feb 18, 2011
787
640
Wanazuoni wa Dini za Kikristo na Kiislam (Dr Sule na Pastor Ndacha ) wameandaa mdahalo wa Dini hizi mbili hapo Ukumbi wa PTA tarehe 16 na 17 December 2023.

Katika mahojiano yao kupita Vivo online tv, wamejinasibu kuwa mdahalo huo utakuwa wa kistaarabu na wenye kuimarisha imani za waumini wao. ninapenda kupata maoni yako je

1. Midahalo ya dini kama hiyo itatusaidia katika imani zetu

2. Tunakumbuka enzi za nyuma wakati midahalo kama hiyo ilipokuwa inaendeshwa huku nukuu nyingi zikiwa ni zile za biblia tu, je katika enzi zetu ambapo watu wamepata kujua kwa undani kilichoandikwa kwenye Quran na Hadithi za Mtume, je Waislam watahimili mdahalo kama huo.

3. Je unaafiki wanazuoni hao kutoza kiingilio cha Tsh. 20,000 kwenye mdahalo huo.

4. Going forward je midahalo kama hiyo ifanyike waziwazi?
 
Dini huwa zinawagusa WATU ambao hawapo tayari kuwa open minded wao hao viongozi they are living luxury life with all materials things kutoka Kwa Waumini ambazo uziita zaka/fungu la kumi n.k

In short mambo ya kiroho unabidi kuyaheshimu Sana . na sio Kama wanavyofanya hawa waafrica wana Miss use Sana.
 
Haya mambo ya Imani tuyaache kuyashabikia au kuleta mijadala ambayo mwisho wa siku inaenda kutugawa. Sioni sababu gani ya kuwepo mjadala huu wa imani kwani imani ni kitu ambacho kinamgusa mwanadamu zaidi hata ya siasa. Nashauri kama kuna wanaofatilia hili jambo wafanye kila namna hili jambo lisifanyike.
 
Hii midahalo imekuwa ikifanyika kwa miaka mingi, na lengo ni kila mmoja kuvutia upande wake akiamini yupo sahihi

As long as itakuwa ya kistaarabu basi haina tatizo, changamoto ni spana zikikolea upande mmoja na kuzua vurugu hapo itakuwa mtihani sasa

All in all, tunajua upi pumba na upi mchele
 
Dr Sule na Mwl Ndacha nawakubali sana kwa pamoja.

Vijana tuige mfano mzuri wa kutafuta maarifa.

Wako wengine akina Suleiman Mazinge, Mwl Chaka wa Mussa, Akina Francis
 
Zaman ilikua bure, mwishon mnatoa sadaka ulichonacho nasio lazima kutoa, ila maybe kwa vile sku hz wanakodi ukumbi ndiomaan kuna kiingilio
Zamani bure mnapigwa na jua palw Manzese Tip Top huku umesimama kwenye vumbi na Kipaza sauti cha kukwaruza.

Sasa wanaboresha huduma nzuri.

Utakula neno la Mungu ukiwa kwenye kiyoyozi, umekaa kiti kizuri na maji poa pembeni.

Je hapo kuna gharama??
 
Back
Top Bottom