Ni kweli sijafuatilia. Ni kweli kuna bifu kati ya JD na Clouds.
Je ni kweli kuna bifu kati ya MwanaFA na Jide? Kuna kosa gani kwa Jide kufanya biashara siku ambayo MwanaFA pia anafanya biashara? Ni kwa nini Jide akifanya show yake, MwanaFA "hatakiwi" kufanya show yake?Je ni kweli kuwa siku hiyo wanamuziki wote hawatafanya show zao isipokuwa Jide na MwanaFA? Labda mtueleweshe vizuri eneo hili sisi ambao hatufuatilii haya mambo ya wanamuziki kila siku.
1. Ni kweli kwamba Jide haba bifu na MwanaFA, na MwanaFA anaweza kufanya show yake any day hata kama inagongana na ya Jide.
2. Ni kweli kwamba MwanaFA ni mmoja wa wakurugenzi kwenye taasisi ya THT (solely owned by Clouds FM owners), hope hili unalifahamu.
3. Kwa namba 2 hapo juu, kwa sababu ya uhusiano uliopo kati ya MwanaFA na Clouds FM unaweza ku-impair maamuzi ya MwanaFA juu ya upande upi awe kwenye hii bifu ya Clouds FM na Jide.
4. Moja ya mbinu Clouds FM wanazozitumia ni kumshindanisha Jide na wasanii wenzake au na bendi zingine, na hivyo ndivyo imekuwa kwa MwanaFA this time, hii show ya FA promoters wake ni Clouds FM kuanzia tarehe, matangazo, wasanii waandamizi, ukumbi mpaka kiingilio.
5. Last time Ruge alisema Skylite Band imepokea kijiti cha kuwa bendi pendwa kwao Coluds FM badala ya Machozi Band, so hii ni bendi nyingine inatumika kupambana na Jide (Mmiliki wa bendi ni Sebastian Ndenge kwa mujibu wa Ruge) na wameschedule ratiba y sawa sawa na Machozi Band.
NOTE: Ukisoma namba 4 hapo juu utakumbuka mbinu hii ilitumika pia kupambana na Vinega kipindi kile cha nyuma, tar 26/11/2012 Vinega waliplan show na Clouds wakapanga show yao pia tena kwa kuahidi kuwaleta wasanii wa nje DMX na Fabulous, ilikuwa vita hevi sana ile na kina MwanaFA walitumika pia kwenye ile vita.
Conclusion: Transitively, MwanaFA ana bifu na Jide, ie Kama Jide ana bifu na Clouds FM wakati Clouds FM na MwanaFA ni wamoja, then MwanaFA ana bifu na Jide.