Mwana FA v/s Lady Jay Dee....!!!

Mwana FA v/s Lady Jay Dee....!!!

Ruge Matak@ tuu ugomvi wake anataka uhamie kwa wasanii ila huu FA nae anatafuta kudharauliwa tuu naamini hategemei sanaaa muziki sasa hizi njaa hata sijui zinatokea wapi jamani au wana jengine kati yao Jide aje hapa jamvini atueleze, juzi Ommy dimpozz ameongea point sana wasanii washikamane na Ngwea ndio awe msanii wa mwisho kufa masikini sasa sijui hawakumsikia? Clouds isimame kama yenyewe na wasanii wasimame kama wenyewe, Clouds walitaka kumpelekesha Dimond wakagonga mwamba wakamwomba radhi ili waendelee kugonga ngoma zake nadhani hili litafata pia kwa Sister Jide hawana lolote tena nakushauri sister wakija kukutaka radhi waambie kugonga ngoma yako kwenye station yao kwa mara moja tuu sh. 200,000 ili uubadili mziki wetu na uwe ajira kamili haya maradio station wanavuna sana juu ya migongo ya wasaniii
 
Hapo mbona mm naona yapo sawa maana huyu ana mashabiki wake na Jide ana mashabiki wake
 
hahahahaha..kazi imeanza...lakini tujiulize mbn hizi bendi za twanga,akudo huwa zinapiga siku moja na watu wanaenda..?

ila katika hili FA kazingua...hata maudhui ya show utaona kabisa anataka kumuharibia mwenzake...ila mungu mkubwa wote mtapata watu binafsi nitapita kote huko nishuhudie
 
sawa hatukatai ila tarehe zinagongana two times??!!! What a coincidence?
 
....Jide mara ya kwanza show yake alipanga may 31 na mwana FA naye kapanga tarehe hiyo hiyo,waungwana tukasema labda imetokea hivyo tu kwa bahati mbaya!! .... Sasa Jide kapanga tarehe 14 June eti na jamaa naye kapanga tarehe hiyo hiyo!!!....
Kwani si kila mmoja anajitegemea na ana mashabiki wake? Au wanatumia ukumbi mmoja?

Au unataka kutuambia kuwa katika hiyo tarehe 14 June ni Mwana FA na Jide pekee ndio watakaofanya biashara ya mziki(show)? Sijaona hoja ya msingi katika hili. Muziki ni biashara kama biashara zingine sasa kwa kuwa katika mtaa wetu kuna maduka ya nguo mengi basi mimi nisifungue duka langu kwa sababu wewe umefungua la kwako? Acheni kugombanisha watu bila sababu za msingi bana!
 
Hapo mbona mm naona yapo sawa maana huyu ana mashabiki wake na Jide ana mashabiki wake

ishu sio mashabiki bali kuharibiana. Mimi nauza nyanya, kwanini na wewe uje kuuza nyanya karibu yangu? tafuta biashara nyingine njoo uiweke karibu yangu. jide kapanga tarehe ya show na yeye anapanga siku hiyohiyo yaani wagawane mashabiki wakati wangefanya siku tofauti wangepata wengi zaidi. mashabiki wa mziki ndo walewale. mia
 
Wanaume hatuna sifa kama huyu mwanafatuma
 
Not necessarily. Kwa nini JD asingesogeza wiki moja mbele ya show yake?

JD ndiye wa kwanza kupanga tar 31 May 2013, jamaa nao wakapanga tar hiyo hiyo. Baada ya msiba akapanga tena tar 14/06 jamaa wakapanga tar hiyo hiyo. So kama akibadili watabadili pia na itakuwa haina maana unapanga wanapanga unapangua.

Acha waumane lakini inaonyesha wasanii wenyewe wanavyoharibiana wao kwa wao either kwa maslahi binafsi au kwa kutumika.

Kama unakumbuka vizuri hata Vinega walimlaumu mwanaFA that time ya harakati zao.

Anyway wengine tunaishia kwenye keyboard tu, hatuna impact yoyote mifukoni kwao kwa sababu hata kama wangetofautisha sidhani kama tungeenda kote (67% ya sisi tunajadili hili hatwendi kwenye show, hatununui CD wala tape kuwaunga mkono wasanii hawa hawa).

Ni zamu kwa zamu, JD alinjoy coverage ya Clouds FM, na sasa ni wenzake kama Ruge alivyosema. Siku MwanaFA naye atakuja kuwa replaced tutamsikia.
 
Kwani si kila mmoja anajitegemea na ana mashabiki wake? Au wanatumia ukumbi mmoja?

Au unataka kutuambia kuwa katika hiyo tarehe 14 June ni Mwana FA na Jide pekee ndio watakaofanya biashara ya mziki(show)? Sijaona hoja ya msingi katika hili. Muziki ni biashara kama biashara zingine sasa kwa kuwa katika mtaa wetu kuna maduka ya nguo mengi basi mimi nisifungue duka langu kwa sababu wewe umefungua la kwako? Acheni kugombanisha watu bila sababu za msingi bana!

Hujafatilia issue ikoje mkuu, hakuna kificho kwamba Clouds FM wana bifu na Jay Dee, na wameahidi kumshusha iwezekanavyo. Kosa mmoja wanalolisahau ni kwamba anaweza akapata sympathy ya watu na hii bifu ikamboost zaidi. Wasingemjibu wakamkalia kimya.
 
  • Thanks
Reactions: SMU

Ni kweli sijafuatilia. Ni kweli kuna bifu kati ya JD na Clouds.

Je ni kweli kuna bifu kati ya MwanaFA na Jide? Kuna kosa gani kwa Jide kufanya biashara siku ambayo MwanaFA pia anafanya biashara? Ni kwa nini Jide akifanya show yake, MwanaFA "hatakiwi" kufanya show yake?Je ni kweli kuwa siku hiyo wanamuziki wote hawatafanya show zao isipokuwa Jide na MwanaFA? Labda mtueleweshe vizuri eneo hili sisi ambao hatufuatilii haya mambo ya wanamuziki kila siku.
 
huyo mwana ---- ni mjinga sana,jamani how can some one be evil like that jamani.kuna baadhi ya watu wana roho mbaya sana yaani yote haya ni kupunguza mapato kwa Jide,jamani mwana ---- stop this jamani,how can you do that no Judith jamani
 
Back
Top Bottom