Mwalimu Nyerere na ukabila

Niweke sawa kauli ifuatayo 'makabila makubwa' a.k.a Wachaga, Wahaya n.k. Ukweli ni kuwa haya ni makabila mdogo. Mkoa wa Kilimanjaro wenye wachaga na wapare una watu milioni 2.5. Mkoa wa Kagera ni chini ya hapo. Wasukuma na wanyamwezi peke yao wakiamua kumchagua rais wa nchi hii atashinda katika sanduku la kura bila kuchakachua au kampeni. Haya ndiyo makabila makubwa.Wahaya na wachaga ni makabila yaliyopiga hatua si makabila makubwa.

Pili lazima tuangalie Nyerere aliichukua nchi katika hali gani. Wakati akiapishwa kulikuwa na wasomi wachache wakitoka makabila ya wahaya na wachaga. Hii ni kwasababu ya historia na mtazamo wa ukoloni na maendeleo ya vyama vya ushirika.

Baraza la mawaziiri wakati wa Nyerere lilikuwa na watu mchanganyiko na kuna wakati wengi walitoka mikoa ya Kagera na Kilimanjaro kwa vile walikidhi mahitaji ya wakati huo kiusomi. Nawakumbuka akina CD Msuya, Mzee Mtei, Elinawinga, Eliufoo, Peter Kisumo, Amir Jamal, Annur Kassam, Joseph Rwegasira n.k. Hata wakuu wa mikoa kama kina Dr Kleruu. Kwahiyo Nyerere kuna wakati alilazimika kuwatumia waliokuwa na uwezo na hii haina maana wao walipaswa kuwa marais! hell no! kuna nafasi moja tu ya rais at a time.

Si lazima msomi awe rais kwasababu usomi pekee si sifa ya uongozi. Watu waliomzunguka Tonny Blair ni wasomi waliobobea lakini Tonny ni Mwalimu wa kawaida tu. Kama usomi ndio sifa ya uongozi pekee basi tusingekuwa na rais Mwinyi. Kama usomi ndio sifa pekee basi Mugabe aliyebobea asingeipeleka Zimbw hapo ilipo. Lakini pia tungekuwa na marais wangapi ili tukidhi haja ya wasomi wa makabila husika?

Nyerere alitaifisha shule kwa nia njema ya kila mtoto apate kidogo. Nilipokuwa Musoma miaka ya 70 mji mzima ulikuwa na shule za Agakhan(Mkendo), Hindu Mandal(Iringo) na Catholic (Mwembeni), kama zisingetaifishwa kamji kale kangekuwa na shule mbili au tatu za serikali. Je wengine wangesoma wapi.? Nguvu ya kujenga shule kwa bajeti ya wakati huo na vipaumbele vya afya isingetosha kuelekeza katika maeneo yote kwa shule tu. Leo kuna maelfu ya wasomi waliokuwa wachunga mbuzi wamefaidika na mpango huo.
Je mpango huo ulikuwa wa haki na sahihi kwa kila mtu? tujadili faida na hasara na si kusema 'mbaya au mzuri tu bila hoja'

TV! Hili linanishagaza sana. Zanzibar ni moja ya nchi chache kuwa na TV tena coloured. Je kuwekeza katika TV kuliwasaidia Wazanzibar kinamna gani!
Kwanini tusiangalie Reli ya Uhuru, Reli ya Tanga-Dar ambazo ni infrastructure za maisha tulizoshindwa kuweka mabehewa tu? Kwanini tusingalie UFI, Urafiki, Mwatex, Mutex, Tanganyika Packers, Swala, Magunia, Moproco, Polyster, Tancut almas n.k vilivyotengeneza maelefu ya ajira na uchumi!
Dar miaka ya 70 na 80 kulikuwa na shift work kama nchi nyingine. Wanafunzi walipata part time na wapo waliofanya kazi mbili kwa siku. Je ilikuwa ni busara kwa Mwalimu kuomba misaada ya kujiimarisha kiviwanda au ni bora angeomba msaada wa kuwa na TV?

Mwalimu akiondoka 'Literacy level' ilikuwa 90-95% na UN ikasema Tz ni mfano, leo tumerudi nyuma na kufikia chini ya 70%, je ni lipi jema kuwekeza katika elimu na maendeleo au kuwaacha watoto wasiende shule wabaki wakiburudika na Joti? Mazingira ya wakati huu na vipaumbele ni tofauti na nyakati baada ya uhuru tusisahau.

Miaka ya 70 mtihani wa darasa la saba ulikuwa wa kitaifa. Kati ya watoto 600 robo tatu ilitoka K'njaro, Kagera na Mbeya.
Ndipo mpango wa nafasi kimikoa ukaanza. Ni kweli mikoa ya K'njaro, Kagera iliathirika sana, lakini ilikuwa ni changamoto nzuri kwani kwa kutumia elimu waliokwishaipata na kutambua umuhimu wake wakaanzisha shule za Private na hakika mwaka 2003 wilaya changa ya Mwanga ilikuwa na sekondari nyingi kuliko mkoa wa Lindi pamoja na 'affirmative action' Lindi iliyopata.
Alichofanya mwalimu ni '' positive affirmativa action' kama ya wabunge maalumu au shule za boarding kwa wamasai na wanyaturu ili kuinua jamii hizo ambazo hazikuwa tayari kiushindani. Tunaweza kulijadili pia kama affirmative action ina umuhimu kwa sasa.

Tusisahau changamoto alizopata mwalimu kama uhaba wa wasomi, kuvunjika EA, vita vya Kagera n.k. Ni ukweli usiopingika kuwa maendeleo yaliyopatikana miaka 23 ya mwalimu ni sawa au makubwa kuliko ya wamu zote tatu.

Kama maendeleo ni TV na kompyuta basi tumepiga hatua sana, lakini kama ni kuwekeza katika infrastructure, viwanda, elimu na afya basi tumerudi nyuma ya mwaka 1961.

Kama Nyerere alikuwa mkabila, Amir Jamal, Annur Kaasam, Leader sterling walikuwa wa kabila lipi dhidi ya kabila lipi? Viongozi hawa wamedumu madarakani katika nafasi nyeti karibu kipindi chote cha Mwalimu.
Tuangalie baraza la mawaziri toka aingie madarakani, makatibu wakuu, wakurugenzi n.k kabla ya kutoa hukumu isiyokuwa na vielelezo vinavyojitosheleza.

Ni ukweli pia kuwa mwalimu alikuwa na mapungufu yake na mimi nakubali kuwa kuua vyama vya ushirika au kutaifisha mashamba na kuyaacha mapori halikuwa wazo zuri ingawa kama mtawala huenda lilikuwa zuri kwake. Nafahamu alikuwa Mwanadamu na sote ni viumbe dhaifu tusio na utimilifu, tupime mazuri na mabaya yake kwa mizania na sio dhania.
 

Nguruvi, laiti ndugu zetu wangeweza kuzungumzia mapungufu ya Nyerere wala isingekuwa shida kukubaliana. Yeye mwenyewe alijua mapungufu yake na hajawahi kuyaficha. Wanaosema kuwa alikuwa haambiliki wanashindwa kutuambia aliambiwa nini akakataa - mfano pekee unaotolewa ni wa Mtei - as if kumkubalia Mtei kungekuwa ni suluhisho la matatizo yote yaliyolikabili taifa. Kama ingekuwa hivyo kweli Mtei si bado yupo hai mbona kina Kikwete hawamsikilizi? Mbona Mkapa hamsikilizi? Mbona Mwinyi hakumsikiliza?

Watu wanashinda kumuangalia Nyerere kwa mwanga wa wakati wake na historia na badala yake wanajaribu kumhukumu kwa vipimo ambavyo hakuna kiongozi duniani wa Afrika anaweza akipimiwa navyo akabakia kuwa kiongozi. Ukiniuliza mimi naweza kudai pasipo shaka kabisa kuwa hakuna wakati uchaguzi ulikuwa wa haki zaidi na wananchi walipata viongozi wao kwa haki kama wakati wa Nyerere! Tena chini ya chama kimoja! Watu wanabeza ati aliwapa watu kura ya "ndio au hapana" kana kwamba huo si uchaguzi! Hivi kwanini wakati wa Nyerere hakukuwa na "kupitwa bila kupingwa?" hata kama alikuwa mtu mmoja wananchi walienda kumpigia kura!!!! Leo tuna Waziri Mkuu ambaye hakuchaguliwa na mtu hata mmoja! tunaambiwa ndio demokrasia!

Wakizungumzia maswala ya uchumi wetu mbaya au kusua sua kwake wanataka tuamini kuwa nchi nyingine zote uchumi wao ulikuwa mzuri kuliko wa kwetu? Really? Hivi uchumi wa dunia ulikuwa miaka ya 1970? Angalia mpango wao wenyewe wa uchumi uliotolewa juni hii wanaseema nini kilisababisha matatizo ya uchumi nchini! Wale wale wanaobeza sera za Mwalimu, utawakuwa wanatukuza China ambayo kimsingi imeendelea unabated na sera zile zile kama za Nyerere tena kwa nguvu zaidi. Hivi mmewassikia hao wa Magharibi wakigangamalia "demokrasia ya vyama vingi" kama prerequisite ya maendeleo?

Jamani, tumeenda kuomba hadi misaada ya mvua kutoka Vietnam.. hivi ni lini Vietnamn imekuwa nchi ya vyama vingi? Mbona leo ina uchumi unaokua kwa kasi zaidi. Wakati mwingine nafikiri bora tungeenda njia ya China na Vietnamn ya kuwa na very strong military and party discipline!! Labda tungeweza kupiga kwa haraka ya maendeleo.
 
That was not my point. The point is that Nyerere used Kiswahili to give Tanzania an identity. That is huge! Hata Kenya wanazungumza Kiswahili lakini Njonjo was opposed to making it a national language. Uganda Museveni ameshindwa kukifanya Kiswahili a national language.
 
lakini alitengeneza Mtandao yeye ndiye sababu kuu ya leo hii kuwa na Kikwete madarakani alimbeba akiwa hata hajafikia cheo cha kuendesha taasisi akampa unaibu uwaziri without enough accolades and the rest is history
Hapana.
Nyerere hakuwa na mtandao, ukilinganisha na huu mtandao wa Kikwete, unless sielewi maana ya mtandao.Aliyempa Kikwete unaibu waziri alikuwa ni Mwinyi ambaye katika term yake ya pili alimpa uwaziri kamili. Check your facts.
 

Wacha, ulikuwa wapi?
Ni kama vile tumekuwa tunarusha makombora kutoka kwenye handaki bila kujua kuwa kuna mwenzetu anakuja kutupa ahueni.
It is good to see you here man, and now I can take a break!
 
Cha kwanza ni hiki kinachokufanya tuongee sasa hivi. Naapa wakati wa nyerere tusingethubutu.

Nyerere was against chochote chenye maendeleo.
Wewe mwongo au humjui Nyerere. Unfortunately wakati wa Nyerere hatukuwa na internet, lakini the man was curious na alitaka kusikiliza upande mwingine unasemaje, hata kama ni kumdhihaki. Nyerere alianzisha column kwenye Daily News " What they say about us" ambayo ilikuwa inachapisha makala kwenye magazeti ya Uingereza ambayo yalikuwa yanakosoa Tanzania na sera zake.
You simply do not know what you are talking about and I wish you would shut the hell up!
 
Mtazamaji asante kwa kuwakilisha

Kwanza sijafanya comparison ya hawa viongozi waliofuata baada ya Nyerere...wote ziro

Leo hii tunalilia katiba Nyerere aliiweka katiba ya ku-mfavor yeye

Si kweli; historically inaccurate. Waulizeni kina Msekwa na watu walioshiriki kuandika Katiba; kina Tendwa wapo hao. Nyerere hakuandika katiba wala kuiweka.


Kuteua

Jaji mkuu
Mkuu wa majeshi

Nchi gani ambayo Rais wake hana mkono katika uteuzi wa Jaji Mkuu au Mkuu wa Majeshi?
CAG
Chair wa tume ya uchaguzi
mkuu wa takukuru(not sure)
etc

Huwezi kuondoa nafasi zote za kuteua Rais vinginevyo hawi tena Rais. Lakini aliondoka miaka 26 iliyopita mbona watu hawajabadilisha?

Nyerere aliweka msingi wa gorofa moja wakati tunataka gorofa kumi! ndyo maana kazi zake nyingi zimekufa na hazikumbukwi tunabaki kutetea tu

Si kweli;


Nyerere hakuwa kiongozi, Nyerere alikuwa mwanafalsafa aliyetamani vitu viwe kama anavyotaka lakini akashindwa njia ya kufika hapo.

nioneshe kiongozi ambaye alifanikiwa kuwafikisha watuw ake alipotaka wafike.

sifa ya kiongozi bora

Hutengeneza viongozi kama yeye...........hakuna na hakuwepo

Sifa ya kiongozi bora ni kufuatwa, siyo kutengeneza viongozi wengine. Usipofuatwa si kiongozi hence the word "kiongozi". Nani alimfuata Mwinyi, Mkapa au wanaomfuata Kikwete?

kuthibitisha kauli ya mwanzo kuwa alikuwa haambiliki , Leo hii hakuna kama yeye nyote mnaishia kuandika kumtetea lakini mnaishi kama mabepari! deny it!!

Ni imani tu; nani alikuwa na mawazo bora ya kumwambia kitu akakataa? Si wote wapo; si wote wanasikilizwa? Waliokuwa wanasemaa haambiliki si leo wameshika madaraka mbona hawayafanyi yale ambayo Nyerere alikuwa hawasikilizi?
Swala la katiba ni very serious, you will soon hear and see ..... kuwa lawama za katiba zitarudi kwa Nyerere.

Watakaofanya hivyo ni wazembe wa kufikiri; wao kama wanataka Katiba Mpya kwanini hawakuandika miaka 15 iliyopita? Kama mawazo yao yamefungwa zaidi na Nyerere kiasi kwamba hawawezi kufikiri nje ya yeye ni bora waachie ngazi. Wanaomlaumu Nyerere kwa suala la Katiba ni watu ambao hawataki kujiangalia wao wenyewe.
Katiba ni dira ya taifa , kama katiba ya Tanzania inaweza kumfanya rais kuwa dikteta kwa maneno yake mwenyewe Nyerere , kitu gani kinachoonyesha yeye hakuwa aliyesema angekuwa??

Well; hakuwa Dikteta madikteta wameshika madaraka sasa. Kwa katiba hiyo hiyo mbona watu hawawapingi - angalia ukipinga hadi ndege ya JWTZ itakubeba kukupeleka mahakamani! Nyerere na Kikwete ni nani Dikteta?

Na alifanya nini kuzuia isiwe kwa marais wanaokuja


huku kutakuwa ni kuchanganyikiwa; kwanini tukimbilie kaburini wakati watu walio na madaraka wako hai? Kwanini tusiamue sisi wenyewe kuandika Katiba ambayo tunafikiri tunaistahili na badala yake tuendelee kulia kama watoto tuliodekezwa ambao tulitaka baba atuachie urithi wa nyumba, shamba, gari, elimu n.k sisi tukue tukunje nne tu na kufurahia. Hivi hatuwezi kufikiria sisi wenyewe leo hii kufanya pale ambapo Nyerere hakuweza au ndio tutabakia kulalamika kuwa kwaniini Baba wa Taifa hakutuachia shule zote zimejengwa, kwanini hakutuachia barabara zote za lami, kwanini hakutuachia Jeshi la Polisi zuri, kwanini hakutuachia vyuo vikuu vingi, kwanini hakutuachia Katiba Mpya, kwanini hakutuachia viongozi wote wazuri; hivi tunafikiria Nyerere alikuwa na miujiza gani hasa katika mwanga wa wasaidizi wake ambao wapo leo hii madarakani? Yaani, mlitaka taifa liwe safi kabisa ili tusihenyeke au kufanya kazi sisi wenyewe tupokee tu kwenye silver platter?

labda mngetaka Nyerere aweke majina ya viongozi wetu wote kwa miaka 200 ijayo ili kila mwaka wa uchaguzi ukija tunaangalia tu "baba katuachia nini" halafu tunachagua.
Mkuu au haujasikia kilio cha katiba? hujagundua tu anasemwa nani hapa? au ndiyo utauliza wenginewalifanya nini? si wanajinoma kama yeye?? katiba tamu kwa rais jamani na ni chungu kwa raia!!

Wanaomsema Nyerere kwa suala la Katiba Mpya hawataki kujiangalia wenyewe. Nyerere hausiki kabisa na lawama ya Katiba Mpya. Jamani wameibadilisha Katiba hii mara ngapi Nyerere akiwa hai na hakufanya lolote? Wangetaka hata kumuweka mfalme wangeweza hawakufanya, leo kwa kushindwa kwao kuongoza wanatafutia pa kuteremkia.

au ili kumtukuza Nyerere tusibadli katiba??

Mkuu wanasemwa akina washington isiwe Nyerere

If we areliving in the world of logic then Nyerere failed......if we are living with double standard let swim in the world of excuse kwani kujitetea kunashindikana

Si kweli; failed on what and compared to who? Mugabe? Moi? kumlinganisha na nani? alifeli kwenye nini?

Next few years watu watamtetea Kikwete kwa KILIMO KWANZA japo leo tunasema hafai

Haijalishi kama watu watamtetea au vipi; ushahidi ndio utaamua. Mtu unaweza kumtetea au kumpinga mtu kwa kujisikia au kwa kudhania na ukachukulia kudhania huko kuwa ni "factual"..

TUKIWA NA STANDARD NA KUITA KIJIKO KIJIKO BASI TUTUMIE KOTE, KAMA NDI HIVYO BASI MARAIS WOOOTE WAZURI SANA SANA, JAPO UZURI WAO UTAKUWA asilimia 0.0002% lakini si ni uzuri!!!

Tatizo ni kuwa huwezi kutumia kijiko kimoja kupimia sufu na sukari ukasema vyote viko sawasawa! Vinginevyo joto lingepimwa kwa rula na umbali kwa kilo!
 
Thank you punainen-red, Mwanakijiji, Jasusi, Wacha, VoR and BAK..........Long live JF..........
 

Mkuu ukiangalia post yangu sijajaza ujuzi wa kiswahili nimeenda kwenye ukweli tu

Ukiangalia jibu lako umekubali ubaovu na ubaya wa Nyerere ila una point moja tu kuwa tulipaswa kubadilisha!!

Ebu nijuze mkuu kwa mtazamo wako chanya kwa Nyerere unafikiri Nyerere alikuwa na makosa yepi na mapungufy yepi? ili sisi wa kizazi hiki tujifunze kupitia hayo
 
moja ya mambo yanayodhirisha Nyerere kupiga vita ukabila ni lile la kuchanganya watu. Mtoto alifaulu Tanga na kwenda kusomea sekondari ya Tabora halafu chuo anakwenda Mbeya, kazi anapangiwa Bukoba. Huko Sekondari kati ya wanafunzi 300 wasambaa ni 5, wadigo 2, wabondei 4. Yaani anakuwa na marafiki 289 na si 11 na kumfanya ajihisi ni mtanzania zaidi kuliko Utanga wake.

Watu wanasema alitaifisha shule kama kukomoa, lakini wanasahau ni Nyerere huyo huyo alitoa 'warrant' za usafiri kwa mtoto kutoka kule Mtimbira asiyeijua hata ifakara ikoje na aliyezaliwa katika lindi la umasikini huku akienda shule hana hata katambuga. Leo mtoto huyo ni professor wa kutumainiwa nchini. Ni nani kutoka 'makabila tangulizi' alinyimwa 'warrant' wakati wa Nyerere!

Wakati EA inakufa Kenya walizuia ndege zote,meli na treni. Nchi haukusimama hata siku moja, Nyerere alihakikisha kwa muda mfupi sana tunakodi ndege ya DETA kutoka msumbiji na kwa muda mfupi sana ATC ikasimama.
ATC sasa ipo ICU tukisubiri tangazo la msiba!

Mwlm akaagiza meli ya MV Bukoba kwa vile meli zote zilikuwa Kenya kwa kujali watu wa kanda ya ziwa.
Kwa muda mfupi treni ya kati ikaendelea na safari, ile ya Tanga-Dar-Moshi huduma kila siku,mkulima anapanda na gunia lake pale mombo asubuhi anarudi kutoka Dar hajambo! Nimepita siku za karibuni reli ya Dar Moshi Tanga imeota nyasi ,nilikata tamaa.

Shule zikifungwa tulikuwa tunatimkia Tanga(TA) kupata kitu kinaitwa 'tempo' kule Mbolea, bandari, sabuni, chuma n.k. huku treni zikifanya shanti na honi kibao. Nimerudi TA nilibubujikwa na machozi, yaani ghost town!

Nimerejea morogoro sikuona harakati za asubuhi za kuwania mabasi ya wafanyakazi wala vijana kwenda kuwahi vibarua wakifunga shule, nimekutana na wauza ndizi kwenye baiskeli na vijiwe vya kilaji jioni kwa waliobahatika na fungu la EPA au Kagoda.Simanzi!
Ilikuwa kawaida kusikia mtoto akisema baba kaenda shift ya usiku, leo Dar shift inaisha saa 9 inaanza shift ya foleni hadi saa 3 usiku.

Kama Nyerere alikuwa mkabila, ameacha nini mkoa wa Mara zaidi ya daraja la Kirumi linalounganisha Kenya na TZ?
Wakati wa vita vya Kagera kule Musoma watu waliomba ruhusa makazini na vijana waliomaliza darasa la saba walilazimisha kujiunga na jeshi na 1/2 ya askari walitoka Mara, Mwanza na Shinyanga, vipi watu hao mashujaa leo wakiwa majeshini tuone ni ukabila wa Nyerere? Mjomba yangu aliposikia watu wanakamatwa makazini kujiunga na jeshi aliingia mitini!!

Mwlm alijenga UDSM na baadaye SUA, IFM, IDM mzumbe, wakasoma watu wa makabila yote. Ni wapi alizuia watu wa makabila fulani wasijiunge na vyuo hivyo? mbona hakuvijenga Musoma ! Ni wapi mtu kutoka Kagera au K'Njaro alinyimwa nafasi chuo cha kilimo ukiriguru kwasababu tu ni mchaga au mhaya? Ni mkoa gani mwlm aliondoka madarakani hakuacha japo 'VETA'?
Mwaka 1980 alinunua Land Rover kwa msaada wa Nordic zikagawiwa kila mkoa kwa ajili ya vituo vya Afya, leo tunanua bajaji halafu tunamzogoa mzee wa watu!

Kwavile mada ya Lizzy ni kuhusu ukabila tujikite hapo na tuje na ushahidi wa ukabila wa mwlm ili tufunguane mawazo.
Vinginevyo mnyonge mnyongeni...................
 
Ni vigumu sana kumtetea Nyerere kwa watu ambao hawako objective.

Kwa mtu anayejua historia ya nchi pamoja na bara la Afrika, na mtu huyo akiwa objective, basi itaonekana Nyerere alikuwa na mapungufu yake as a human pia alikuwa na strength zake. Kwa kulinganisha weakness and strengths za J.K Nyerere as a leader, basi kwa watu ambao wako objective, will come up with conclusion that HE WAS ONE OF AFRICA'S GREATEST LEADER OF ALL TIME. Nafikiri hata Madelaine Albright alisema hivyo wakati wa mazishi ya Nyerere.

Kudai kuwa Nyerere alikuwa mkabila au alikuwa anaonea makabila fulani, is simply absurd. Semeni mengine. Lakini hilo sio kweli.

Ninachoona hapa ni kuwa kuna watu ambao wako subjective katika arguments zao. Wapo ambao "socially" wanafaidika kwa kum-demonize Nyerere kwa vile malengo yao fulani yamejengwa katika misingi ya kwamba Nyerere aliwanyanyasa na alikuwa kiongozi mbaya. Sasa kwa hao watu, kumsifia Nyerere ni kuharibu misingi ya agenda zao. Tumeona hata kwenye threads zingine kuhusu Nyerere ambapo mtu anakomalia swala la sainthood ya Nyerere ilhali huyo mtu wala si mkatoliki na suala zima la sainthood halimhusu kabisa. Lakini watakomalia ili kuondoa hisia zozote kuwa Nyerere was a great leader ili waendelea ku-justify chuki zao zinazoambatana na ajenda zao.

Pia kuna watu ambao wangependa nao waonekane wanajua sana mambo fulani wakati actually hawana ufahamu wa kutosha. Sasa badala ya kuuliza au kutafiti, wao hutumia mbinu ya kushambulia tu, na katika kushambulia huko, somehow, wanajibiwa na wanapata majibu sahihi and they end up learning. Anyway, this not bad. It is a learning technique.

Kwa wale ambao wameamua rohoni kwao kwamba hawatakubali kuambiwa kuwa Nyerere alikuwa na mazuri, tuwaache wabaki hivyo. Historia yetu ya ukweli bado ITASIMAMA TU. Ni wao ndio watakufa na VIJIBA VYA ROHO.
 
Asanteni wote kwa michango mizuri...nimejifunza mengi ambayo sikujua kabla na uelewa wangu kumhusu mwl umeongezeka maradufu!!

Asanteni tena!
 
asanteni wote kwa michango mizuri...nimejifunza mengi ambayo sikujua kabla na uelewa wangu kumhusu mwl umeongezeka maradufu!!

Asanteni tena!

ha haaaa
umeuona moto huo?
Sasa rudi kwenye jukwaa letu lol
 
Asanteni wote kwa michango mizuri...nimejifunza mengi ambayo sikujua kabla na uelewa wangu kumhusu mwl umeongezeka maradufu!!

Asanteni tena!
Lizzy,
Endelea kujielimisha na usiache kusoma. Tafuta vitabu hivi: "The Making of Tanganyika" by Judith Listowell. "We Must Run While They Walk, by William Edgett Smith; The Struggle for Zimbabwe by David Martin na Nyerere and Africa: End of An Era by our own Godfrey Mwakikagile. Hapo utatoka na somo tosha. Keep up the good work.
 

na asisahau vitabi hivi pia

the dark side of jk nyerere
life and times of abdulwahid sykes

sikumbuki waandishi
 
Asante Jasusi...ntajitahidi kadiri muda unavyoruhusu!
 

Mzee kwani madikteta huwa hawaletagi maendeleo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…