Mwalimu Nyerere na ukabila

Namchukia sana mwalimu, kila nionapo picha yake, hasira unipanda misri ya cobra. Kwanza ndiye chanzo cha umasikini wa Tanzania kutokana na sera zake mbovu.
Umasikini huo ni wa watanzania wote au wako na familia/ukoo ndo unakufanya umchukie marehemu?

Unafahamu kuna watu wamezaliwa baada ya 1999 na wanapesa nzuri tu hapa TZ?

Unafahamu baada ya Mwalimu, kuna maraisi watano wame/wanaiongoza hii nchi?

Unafahamu kuwa Mwalimu alitawala miaka 24 ya mwanzo wa Tanganyika/Tanzania, miaka 36 ikiwa imetimia sasa tangu yeye atoke madarakani?

Miaka 24, akiwa na wasomi pengine wasiozidi 70, ni sawa na miaka 36, wasomi na teknolojia lukuki, na vichwa vitano kama maraisi, bado ulaumu sera za Mwalimu? Mmeshindwa vipi kuzibadili mkaendelea na mkaachana na umasikini? Singapore, Thailand, Malaysia mlikuwa nao sawa enzi za Mwalimu, imekuaje sasa?

Kama itasaidia kubadili sera za mwalimu na kufuta umasikini, huna budi KUZIDA CHUKI dhidi ya marehemu.
 
Hao wanaowwchukia Wahaya ni kina nani?
Maana unasema ndio Kabila linalochukiwa nchini
Mbona mimi nawajua wengi na siwachukii wala sioni wakibaguliwa?

Nyie ndio mnaoendekeza haya mambo
Kama unafanya mambo yako nani anakujali?
 
Wamissionari walijenga shule Bukoba katika harakati za kueneza dini. Hii ilipelekea Wahaya kuwa ni kabila lenye wasomi wengi kabla ya uhuru, sambamba na Wachaga na Wanyakyusa.

Kuna Wahaya walio anza harakati za kuupinga Ukoloni Zamani kabla ya Nyerere, tatizo ni ego hawakuwa tayari kuunganisha nguvu. Kutokana na kujiamini kwao waliweza kumkosoa Nyerere waziwazi na Nyerere hakuwa mtu akiykubali kukosolewa.
 
Huna uelewa wowote zaidi ya kukariri mambo.
 
Mpaka sasa mwalimu ndiye aliyefanya makabila mengine wawachukie wahaya kupitiliza. Mwalimu alipandikiza mbegu mbaya kwa watanzania kwamba wahaya wanabaguana, wanaukabila kuliko makabila mengine kitu ambacho sio kweli.

Wahaya ni watu wapole, wasafi, wanyenyekevu na wenye busara sana. Kitu pekee ambacho wahaya hawakipendi ni kudharauliwa, yaani hata uwe na pesa,nyumba, magari n.k yeye kwake anaona ni kitu cha kawaida hatishiki wala kubabaika. Utakuta hajajenga, ila akija kwako hata uwe umejenga kiasi gani, yeye atasema ni kanyumba.

Wahaya ndiyo kabila linalochukiwa Tanzania kuliko yote. Wengi upenda kumuona Muhaya akiteseka au hata akianguka zaidi, hapo ndipo furaha yao utimia vizuri. Lakini hii chuki haikuja bure, mwalimu ndiye chanzo aliiharibu image ya wahaya kwa watanzania kwa kuwaita wabaguzi na wakabila, propaganda hii inaenea na kusambaa hadi leo. Inawezekana alifanya hivyo kwa itikadi zake za kisiasa na utawala kwa kuwaogopa wahaya.

Wahaya ni wamoja, wana hadi vyama vya koo zao ili kuhamasisha umoja na mshikamano, wanaishi kijamaa zaidi, sasa sijuhi huko kubaguana alikokueneza mwalimu halikutoa wapi.

Namchukia sana mwalimu, kila nionapo picha yake, hasira unipanda misri ya cobra. Kwanza ndiye chanzo cha umasikini wa Tanzania kutokana na sera zake mbovu.
Aliipandikiza kivipi, lini?
 
Habari zenu jamani?!

Naomba nianze kwa kusema ukweli kwamba mimi sikuwepo kipindi cha utawala wa Mwl na hata alipofariki nilikua mdogo sana hivyo sikuwahi kujua kwanini watu wengi walikua wanampenda sana huku bado kukiwa na mambo mengi hasi yanayosemwa juu yake.Nafurahi kwamba mwaka huu nimeweza kutumia muda wangu kiasi nikasoma vitabu kadhaa kumhusu...makusanyo ya hotuba zake pamoja na vitabu alivyoandika mwenyewe.Kutokana na niliyoyasoma niliridhika kwamba sifa zote anastahili...pia kukosolewa maana yeye kama mtu mwingine yeyote yule makosa hatuwezi tuyakwepa.

Katika vitu ambavyo Mwl alivisimamia haswa ni usawa.Hakutaka kabila moja lijione/jisikie liko juu ya jingine na kutengeneza matabaka.Sasa swali langu nnaloomba mnisaidie ni hili....ule msemo au sijui niyaite madai ya kwamba Mwl aliwahi kusema makabila fulani hayafai kupewa uongozi wa juu wa nchi ni wa kweli au ni propaganda za waliomchukia?!Nauliza hivi kwasababu niliyoyasoma juu yake hayaendani kabisa na madai haya...na wala haileti maana kusikia kwamba aliyepigania usawa ndie aliyekua wa kwanza kutengeneza matabaka lilipokuja swala la uongozi!!!

Naomba majibu kama yapo yawe na vielelezo na yasiwe maneno ya kusikika na kufikirika tu ili tusiojua tujifunze kitu.
Asanteni!
Kwa Sasa ni Lile lililodekezwa kuliko yote na likabweteka Hadi Sasa limeanza lialia linabaguliwa 🏋️
 
Aliyataja makabila yanayokula ndizi kwa sana ambayo yalitafsiriwa kama Wachagga,Wahaya na Wanyakyusa ambao walikuwa juu kielimu na uwingi na alipendelea nafasi za juu(urais,makamu na waziri mkuu) ushikwe na makabila madogo ili makabila haya yasi-manopolize power.Hajatamkaa hadharani lakini aliwaambia watu wengi in private angependa iwe hivo.
Kila aliempinga alionja joto yajiwe

waulize kina bibi titi,kambona,edwin mtei na wengine weengi
Alimtumia kawawa kuua nguvu za kiuchumi za wachagga na wahaya Ili kuwainua wengine, athari zinaoneka leo
 
Asante kwa kunirekebisha ila bado naamini waliompenda wanazidi walio/wanaomchukua...au labda tuseme hawakumtambua sawasawa kiasi cha kuamini aliwatakia mema hivyo hawana malalamiko juu yake. Binafsi naamini alikua dikteta wa kichinichini..wale waliokua karibu yake tu ndo wanaojua ni kwa jinsi gani hakupenda upinzani!!
Wajinga walikuwa wengi isingekuwa Rahisi kutambua hila alizotumia
 
Wamissionari walijenga shule Bukoba katika harakati za kueneza dini. Hii ilipelekea Wahaya kuwa ni kabila lenye wasomi wengi kabla ya uhuru, sambamba na Wachaga na Wanyakyusa.

Kuna Wahaya walio anza harakati za kuupinga Ukoloni Zamani kabla ya Nyerere, tatizo ni ego hawakuwa tayari kuunganisha nguvu. Kutokana na kujiamini kwao waliweza kumkosoa Nyerere waziwazi na Nyerere hakuwa mtu akiykubali kukosolewa.
Watanzania muwaelewe wahaya ni watu wazuri ila egoism iko damuni kuiacha ni mgumu ni intrinsic na DNA, tofauti na wachaga
 
Back
Top Bottom