Mwalimu Nyerere na ukabila

Eng. Burton A. Bukuku;wakati mimi namwona Kikwete bomu, kuna wengine wanamuona mzuri sana, wakati wengine wanamuona Nyerere mzuri wengine wanajuta hata kumjua!
Hizi ni caliber za binadamu na haijaandikwa mahali kuwa ukiwa unasema ubaya wa Nyerere lazima useme na uzuri wake. Na mtego huu ndio kila siku huwa mnauvaa sana, hakuna mahali kuwa ukisema ubaya wa Nyerere basi laizma useme na mazuri yake.
Nilitaka unieleze makosa ya Nyerere ukiwa mtu huru, jaji huru asiye na upendeleo wowote. Lakini upenzi unazidi sana kuliko kuismamia ukweli.
Ukweli ni kuwa JK ni baba wa taifa, ni kweli alikuwa na mapungufu yake mengi tu, nataka uyaseme hayo --orodhesha na ukiyasema hayataondoa ukweli kuwa Nyerere ana mazuri yake!!
Mkuu Bukuku, nakubaliana nawewe kabisa kuwa mwalimu kama binadamu alikuwa na mapungufu yake. Katika moja ya hotuba zake za mwisho alisema, 'mchukue yale mazuri yetu na muache yale mabaya'. Amekiiri hadharani kwa kinywa chake. Mimi mara zote nimekuwa nikiyasema yale ambayo sikuridhika na utendaji au utekelezwaji wake.

Tatizo linakuja pale kunapokuwepo na chuki, ima ya kuzaliwa au ya kujifunza dhidi ya Nyerere. Fikiria mtu anaposema Nyerere alikuwa mkabila, hiyo ni sawa kwa maoni yake, lakini aende mbali nakututhibitishia kuwa alikuwa mkabila kwa ABCD.

Mtu anaposema alikuwa mdini, fair! lakini athibitishe bila shaka udini wa Nyerere. Tena hili la udini hata mwandishi Mohamed Said tumejadiliana naye mwezi mzima hapa JF hakuweza kuthibitisha kisomi udini wa Nyerere zaidi ya hisia na hadithi za kusikia. Sasa limejirudia ndio maana tunauliza na si kutetea historia ya Nyerere; 1) Tuthibitishiwe ukabila wake. Hadi sasa hakuna aliyethibitisha.
2) Tuthibitishiwe udini wake, hakuna aliyejitokeza n.k.

Hii maana yake ni nini! tutaambiwa siku moja Nyerere alikuwa Mchina, tunakubali. Siku nyingine alikuwa mdogo wake Dikteta Ngweso, tunakubali. Mama yake alizaliwa ukoo wa Hitler, tunakubali. Yote haya yatajumuishwa na mwendesha mashitaka ili aorodhesha makosa 100 ya Nyerere na kutaka hakimu atoe hukumu bila ya uthibitisho. Hapa ndipo wengine tunasema hapana, tuna akili zetu, tumeishi nyakati za mwlm tunamjua tupeni uthibitisho. Kabla ya hukumu tuthibitishiwe madai dhidi yake.
Kwa vile mara nyingi huwa hawana uthibitisho ya mabaya yake basi sisi tuna uthibitisho wa mema yake ndio linapokuja suala kutaja mazuri yake.

Bukuku inapotokea mtu akasema Nyerere alikuwa mbaya sana kwasababu alikataa kuleta TV, hivi kuna njia gani rahisi ya kumsaidia mtu huyu kama si kumweleza uzuri wa mambo mengi aliyoyafanya kuliko TV.
Siwezi kusema tu hapana ulikuwa uamuzi mzuri kutokuwa na TV nakaishia hapo, nitakuwa nimetumbukia katika mtego wa kudhani bila ushahidi, nitaeleza kwanini TV haikuwa muhimu kuliko elimu na afya na hapa ndipo nalazimika kutaja mema ya Nyerere.

Tufanye hivi: Maswali ni mengi hebu tuanze na haya mawili kwanza, tuelezwe ukabila na udini wa Nyerere.
Mkuu Bukuku fungua pazia ili wenye hoja wakuunge mkono nasi tuelimike.Hakuna sababu ya kutaja mazuri tuanze na haya mawaili tu. Ukabila na Udini wa Nyerere kwa vithibitisho!
 
Mkuu Jasusi , hivi wakati wa Nyerere kulifanyika majaribio ya mapinduzi
mangapi? naomba nijuzwe/tujuzwe, maana binafsi nafahamu kidogo mawili tu
lile la mara tu baada ya uhuru na hili la akina anko Tom,Mapunda, Mbogoro,
Zacharia Hans Pope na wenzao
Mtemi,
Nadhani swali lako unaweza kupata majibu katika kitabu cha Godfrey Mwakikagile. Amegusia attempts zote.
 
Nakumbuka mwl ktk hotuba zake alikuwa very open.........kuhusu kuchagua kiongozi alisisitiza sana yafuatayo na kwa uchungu mkubwa.........alisema"...hatutachagua mtu kwa sababu ya dini yake, hatutachagua mtu kwa sababu ya kabila lake na wala hatutachagua mtu kwa sbabu ya mkoa/sehemu atokako.................tunataka mtu mwenye sifa za kuwa kiongozi yaani mtu anayeyajua matatizo ya watz na yuko tayari kuwatumikia.......ndiyo maana alikuwa hataki watu km akina kikwete na lowasa kwani alijua ni wasanii tu wa mtaani ambao hawawezi kutembea ktk kile wasemacho.......................hakutaka sentensi za kwamba kwa kuwa mhula huu rais katoka bara basi ujao atoke visiwani, kwa kuwa rais katoka kaskazini basi huu atoke mashariki..................jamani yule mzee alikuwa na vision za ajabu sana km angeungwa mkono tungefika mbali sana ndiyo maana wenye akili timamu wanatamani azimio la arusha lirudishwe na liwekwe kwenye katiba mpya ya watz
 
Wacha, ulikuwa wapi?
Ni kama vile tumekuwa tunarusha makombora kutoka kwenye handaki bila kujua kuwa kuna mwenzetu anakuja kutupa ahueni.
It is good to see you here man, and now I can take a break!


Jasusi

Vipi mkongwe naona hawa kuku wanaleta shida ile misukule imevimbiwa lakini bado inataka kula, wakati wake wa kupasuka matumbo umekaribia.
Hivi hawa kuku aliowaswaga huku ni nani kama sio M k w e r e kwa ushirikiano wake na vifisadi dagaa. Hata aibu halina kibabu kizima akili zake hovyo.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Atleast kuna watu mnajaribu kumtetea jk Nyerere na kumake sense katika maelezo yenu. Ngoja nijipe muda zaidi wa kumsoma huyu JK nyerere anayesema amesaidiana kufight uhuru na wazee ila wengi naona wameishia vifo visivyo na majibu mpaka leo. THE DARK SIDE OF NYERERE AND MAISHA SYKES by Mohamedi Saidi vinanipa mwanga kiasi kumfahamu.
 
Ahsate sana Mkuu, nimeupenda mno huu mchango wako.



Mafisadi wameshindwa kuongoza nchi sasa wanakuja na tabia ya kumlaumu mwalimu kwa kushindwa kwao kuongoza nchi. They should deliver without pointing fingers to others. Utajiri waliojichukulia utawatokea puani sooner rather than later.

Mwalimu ataendelea kusifiwa kwa yale aliyofanya kwa wengi ambao wanakubali kwamba alikuwa one of the great leaders katika generation yake, wale wanaomkandia kwanza hawawezi hata kukaribia chembe ya yale aliyofanikiwa na ni failures katika maisha yao binafsi. Kuna wengine wanakuja na maswala ya kizandiki ili kupotosha hoja muhimu kwa taifa hili, kama Nyerere alikuwa ni failure sijui hawa ambao nimisukule pale Magogoni tuwaweke katika sehemu ipi?


Mwalimu aliacha hii nchi ipo katika utajiri mkubwa katika kila sekta ukianzia reli, air travel, kampuni ya simu na mashirika muhimu ya umma ambayo ndio mafisadi sasa wamejichukulia na kufanya yao na kuwakamua walipa kodi. Hata nchi kubwa kama Uingereza, Germany na Marekani nguzo kuu bado zinasimamiwa na serikali wakati hapa kwetu wamejichukulia bure na sasa wanafikiri wataweza kuendelea kushiba baada ya kuvimbiwa. Hawa kuku walioletwa hapa kupotosha mambo muhimu hawawezi kufanikiwa kwa sababu Tanzania aliyoiacha mwalimu inazaliwa upya na watakiona cha mtema kuni.


Mwalimu aliandika vitabu vingi sana kama una nia ya kumwelewa nenda kavisome …. …. …. … Wakati ni huu!
 
Ahsate sana Mkuu, nimeupenda mno huu mchango wako.


Mkuu za masiku? Naona Internationals karibu zinaisha, Rafa nilitazama mechi zake kule China naona kawashitukia media na aliamua kupumnzika kidogo, hopefully atapumnzika vizuri na baadaye kutinga O2 kwenye funga mwaka. The boy is good. Have a nice day na shukrani za dhati kwa michango yako hapa JF.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nashukuru sana Mkuu nami pia nakupa shukrani za dhati kwa michango yako hapa jamvini kwetu. Mtu wetu Rafa naona labda kachoka lakini kweli performance yake kuanzia spring hadi sasa sikutegemea iwe nzuri kiasi kile hasa ukitilia maanani kwamba alikuwa kaumia na hakucheza kwa kipindi kirefu ili kujitibia goti lake, nahisi kateleza tu baada ya mapumziko mafupi ataendelea kufanya vitu vyake katika mashindano ya kufungia mwaka kabla ya kutinga Australia January, 2014.

Mkuu za masiku? Naona Internationals karibu zinaisha, Rafa nilitazama mechi zake kule China naona kawashitukia media na aliamua kupumnzika kidogo, hopefully atapumnzika vizuri na baadaye kutinga O2 kwenye funga mwaka. The boy is good. Have a nice day na shukrani za dhati kwa michango yako hapa JF.
 
Hivi nyie mliwai kuangalia tv ya zanzibar. hapakuwaga na kitu isipokuwa jamaa aliyekua anapuliza tarumeta flani hivi zakienyeji. hangalau kilimanjaro milimani KBC ilikuwa na kitu chakuangalia.
 
Sio kuongozwa tu Madaraka Mbalimbali Nchini yangeegemea hayo Makabila na Usawa usingekuwepo Mfano Mzuri angalia Jirani zetu Kenya na Kabila la Kikikuyu wao walipendwa na wakoloni; wana Elimu zaidi ya wengine; Ardhi Zaidi ya Wengine; Mji bora zaidi ya wengine (NAIROBI) Wengi wana Madaraka na ni Mabwanyenye
UKweli ni kwamba Nairobi ni mji wa wamaasai, hata neno Nairobi ni la kimasai. Tatizo, upendeleo uliwafanya wakikuyu kuutawala. Upendeleo ukaongezwa na Kenyatta.
 
yaani nyerere mawazo yake yalikuwa finyu mpaka na yeye yamem cost

kutokuwepo kwa tv matokeo yake hotuba zake za tv zipo mbili tu....
na zilichukuliwa akiwa sio rais...na ni itv na channel ten tu ndo wanazo....
zingine nzuri hazipo kwenye tv

kitabu ni historia ya edwin mtei kimezinduliwa hivi karibuni

waulize watu wa chadema watakupa
Siasa za misikitini zimekupofusha kabisa akili.
 
Hahahha....mi nilivyosikia ni kwamba hakutaka watuwawe na tv ili wasijue yanayoendelea nje ya sehemu walipo...sasa yeye kwasababu anayo anakuja kuwadanganya ana maono haya na yale kuhusu ulimwengu unapoelekea.Siku ya pili watu wakisikia zile habari kwenye redio au sijui kwenye magazeti basi wanazidi kumwamini maana anajua mambo!!!Ntakitafuta!!!
Hahahah
 
Mpaka sasa mwalimu ndiye aliyefanya makabila mengine wawachukie wahaya kupitiliza. Mwalimu alipandikiza mbegu mbaya kwa watanzania kwamba wahaya wanabaguana, wana ukabila kuliko makabila mengine kitu ambacho sio kweli.

Wahaya ni watu wapole, wasafi, wanyenyekevu na wenye busara sana. Kitu pekee ambacho wahaya hawakipendi ni kudharauliwa, yaani hata uwe na pesa, nyumba, magari n.k yeye kwake anaona ni kitu cha kawaida hatishiki wala kubabaika. Utakuta hajajenga, ila akija kwako hata uwe umejenga kiasi gani, yeye atasema ni kanyumba.

Wahaya ndiyo kabila linalochukiwa Tanzania kuliko yote. Wengi hupenda kumuona Muhaya akiteseka au hata akianguka zaidi, hapo ndipo furaha yao hutimia vizuri. Lakini hii chuki haikuja bure, mwalimu ndiye chanzo aliiharibu image ya wahaya kwa watanzania kwa kuwaita wabaguzi na wakabila, propaganda hii inaenea na kusambaa hadi leo. Inawezekana alifanya hivyo kwa itikadi zake za kisiasa na utawala kwa kuwaogopa wahaya.

Wahaya ni wamoja, wana hadi vyama vya koo zao ili kuhamasisha umoja na mshikamano, wanaishi kijamaa zaidi, sasa sijui huko kubaguana alikokueneza mwalimu alikutoa wapi.

Namchukia sana mwalimu, kila nionapo picha yake, hasira unipanda misri ya cobra. Kwanza ndiye chanzo cha umasikini wa Tanzania kutokana na sera zake mbovu.
 

Similar Discussions

10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom