Mwalimu Nyerere na ukabila

Mwalimu Nyerere na ukabila

naheshimu mawazo yako
but tazama mambo kwenye angle tofauti

mwinyi hakuwahi kupanga kuwa rais wa tanzania wala zanzibar
hakuwa na mtandao wala chochote kile

unaweza sema alikuwa an 'accidental president'

lakini aliweza mengi mno ambayo nyerere yalimshinda
na aliwapa wananchi bidhaa muhimu kuliko zote
uhuru wa kuongea na kukosoa hata serikali yao
na uhuru wa kufanya biashara bila usumbufu
lakini alitengeneza Mtandao yeye ndiye sababu kuu ya leo hii kuwa na Kikwete madarakani alimbeba akiwa hata hajafikia cheo cha kuendesha taasisi akampa unaibu uwaziri without enough accolades and the rest is history
 
Mkuu naomba kujibu hoja zako ulizowalenga hawa jamaa

You need to be crazy to defend Nyerere!

No u dont need to be crazy to defend Nyerere the same as u dont need to be crazy but biased to criticise Him terriblly. Tunaweza kuweka sababu zetu sote alafu tukapima . Ukiwa unbiased pamoja na kumcriticise bado utaona Nyerere ni mfano wa viongozi tunaowahitaji sasa but kwa mwelekeo tofauti.

Nyerere anaweza tu kuwa defended when you compare him with other leaders who came after him.

Hapa sijakuelewa mwanzo umesema we need to be crazy to defend him . Alafu hapa unasema tunaweza kumdeffend kwa kumlinganisha na leaders wengine waliokuja baada yake. kwani wewe ulitaka tumlinganishe na kina nani.
au na nini
??

Nyerere terribly failed, but he has vision at least where he faled could easily be repaired by other presidents..it was not so.
Sio kweli kuwa N yerere failed terribly. Unless tujue context ya terribly kwako ni nini Mbona tanzania kuna miaka ni nchi iliyoongoza kufuta ujinga duniani. Na hii ilikuwa chini ya sera za mwalimu. mammbo ya UPE na elimu ya watu wazima. Yes Duniani. But nakubali kuna mambo ali fail lakini sio wa hicho kivumishi cha sfa cha terribly ulichotumia.

Sasa kuja na hizi saikolojikaly explainable eti watu walilia sana.Mkuu watu wameishaandika paper kuhusu hili swala, find some! kuna sababu za kisaikolojia, kuna sababu za kidini na umaskini!

Hapa nakubaliana na wewe haya mambo ya kulia sikubalini nayo.

Umesema Nyerere alikuwa anaongea sana that was true, kweli alikuwa muongeaji, mwongo, na ameharibu nchi kila mtu siku hizi anaongea sana

Let me ask you, Sokoine alikuwa mwongeaji sana? nani unafikiri alikuwa radical wa kutekeleza ujamaa kwa vitendo? caliber yake ya kuongea sana siyo kipimo cha kiongozi bora

Nyerere alikuwa dictator
Mbishi. haambiliki
Nyerere alijifanya anajua kila kitu
Nyerere mehairibu nchi beyond repair

Mkuu nadhani Nyerere alikuwa na mapungufu yake lakini mapungufu ya uongozi wa nyerere sio makubwa kiasi hicho kwamba ndio chanzo cha matatizo yetu yoote . Do u know u dictator wa hitler ndo umeisaidia kuifanya Ujerumani kuwa amaong industrila power?? Before Hitler Ujerumani ilikuwa imeachwa mbali na UK na france. Anywa siendi huku lakini nataka kukuonyesha kuwa a sometime nchi zinahitaji dictators of some sorts . Mfano mwingine ni Uganda. Uliza au fuatilia waganda vizuri . Ukweli ni kwamba Ukweli ni kwamba Idd amin was a good leader to most of ugandan. Upo hapo????????

katika uongozi na uongozi hutakiwi kumsikiliza kila mtu la sivyo sio leader tena. Kutoambilika kwa kiongozi ni jambo baya mara matokeo yakiwa mabaya lakini kutombailika kwa nyerere mambo kulikosababisha matunda mazuri tunaweza tusikujue. So hata wewe uiwa kiongozi usijidanganye kuwa utamsikiliza kila mtu. Hata obama kule unasikia aliapewa alteantive tatu za kumuua OSama yeye akaamua ile ya kumzukia. Inge bakcfire ile leo tungekuwa tunaongea mengine. Na wangejitoeza watu wakisema sisi tulisema bora tupige mabomu tu. Hizo ni siasa.

Kwa mtazamo wangu tanzania tunakosa president mwenye udicator fulani. Mkapa aalikuwa ana udctor fulani lakini naye tatizo ni ufisadi. yaani Jakaya angekuwa ana talanta za Udictor fulani na Uzalendo kama wa nyerere basi tungekuwa mbali.
Nyerere ndiye aliyeweka katiba ya kifalme na kitwana
This is timing hata ungekuwa wewe mazigira ya wakati huo sijui ungefanya nini . na katiba aliyoweka haina tofauti na katiba za nch nyingie za afrika zilizotangulia kupata uhuru. Sasa ulitegema aige kutoka wapi.

Nyerere ndiye aliyeshauri na ku-force vyama vingi vianze BILA KUFORCE MABADILIKO YA KATIBA
BILA KUFORCE TUME YA UCHAGUZI IWE HURU

Sasa Nyerere alishauri kama nani alikuwa ana mamlaka gani kwenye serikali wakati huo? Sasa wewe unamlaumu aliyeshauri badala ya kuwalamumu waliomsikiliza ambao ndio walikuwa na mamlaka na uwezo wa kukubali au kukataa. Ni kosa kusema aliforce sababu hakuwa yeye rais. Kama wenye madaraka waliamua kumsikiliza ni udhaifu wao sio wa nyerere


Tuache unafiki jamani, if we are living with excuse we can miss one for Mwinyi, Mkapa, Kikwete etc!!
Yes tuache unafiki tutoe credit where it deserve pia. J. K Nyerere deserve some credit and some critics Nyerere alionyesha mfano wa leadership. ambao baada yake sioni kama kuna viongozi wana leadership.


Nawasilisha
 
I think now we are clutching straws..., if we can crucify somebody by not knowing what was socially acceptable at those places, be it whatever odd it was and I think its shallow of people if they cant look beyond the mere appearance ..., Hey for me Ghandi was still a good leader although he was wearing a bed sheet....

Vijiji vya Ujamaa was very bad implemented but that does not make it necessarily a bad idea; At least in Nyerere times majority of people where poor and the class gap was not as big sio sasa jirani yako anakula kuku getini kuna mtoto wa masikini ambaye mlo wa mwisho alikula juzi.


I am sure the first part is just an argument from your side but you now know what the point is.

The best ideas are those which works. You cant have it good and failed. Its either black or white, no gray shades. He himself announced to have failed, who are you to keep on depicting the same failures as good? a devils advocate?
 
Binadamu kwanza anatambaa kabla hajaweza kukimbia..., we had to start from somewhere, na mtu mmoja hawezi akafanya all the changes, especially the Ujamaa policy being flawed. Angalia sasa miaka 50 baada ya uhuru ni kipi tumekifanya?

Maybe its time tuanze kujiangalia na sisi wenyewe labda kuna something seriously wrong in our heads..., kama sisi tumeshindwa na tuna wasomi na kukusanya kodi nyingi na tunajipongeza, sidhani kama itakuwa bora kumsingizia Nyerere kwamba hakuna alichokifanya.

After all mwenyewe alisema kuna mengi mazuri na mabaya mengi tumeyafanya.., kwahiyo tuyaache mabaya na kuendeleza mazuri, lakini it seems we are going the opposite way.

Au kwa maeno mengine Mkuu VoR miaka 26 tangu Nyerere ang'atuke madarakani, au miaka 26 ya Mwinyi, Mkapa na Kikwete!? Je nchi yetu imepata maendeleo yoyote ya kujivunia katika kipindi hiki cha miaka 26 ya Mwinyi, Mkapa na Kikwete? Kama kuna maendeleo ni katika nyanja zipi? Je, viwango vya maisha ya Watanzania walio wengi vimeongezeka kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na kabla ya hawa watat kuingia madarakani!?

Ahsanteni sana kwa wale wote mnaomtetea Mwalimu. Mwalimu kama kiongozi alikuwa na mapungufu yake mengi tu na hata yyeye mwenyewe aliyasema hadharani bila woga wala aibu. Sijui kama Watanzania tutapata bahati ya kuyasikia mapungufu ya akina Mwinyi, Mkapa na Kikwete ambayo pia yamehusisha ufisadi na uporaji wa mali za Watanzania tena mchana kweupe. RIP Mwalimu

Kwa maoni yangu kwa miaka michache niliyopata bahati ya kumfahamu Mwalimu sikuona kama alikuwa na udini au ukabila, lakini ndio hivyo binadamu tunaweza kuangalia kitu kimoja na kukawa na mahitimisho 10 tofauti ya kitu kile kile.
 
Habari zenu jamani?!

Naomba nianze kwa kusema ukweli kwamba mimi sikuwepo kipindi cha utawala wa Mwl na hata alipofariki nilikua mdogo sana hivyo sikuwahi kujua kwanini watu wengi walikua wanampenda sana huku bado kukiwa na mambo mengi hasi yanayosemwa juu yake.Nafurahi kwamba mwaka huu nimeweza kutumia muda wangu kiasi nikasoma vitabu kadhaa kumhusu...makusanyo ya hotuba zake pamoja na vitabu alivyoandika mwenyewe.Kutokana na niliyoyasoma niliridhika kwamba sifa zote anastahili...pia kukosolewa maana yeye kama mtu mwingine yeyote yule makosa hatuwezi tuyakwepa.

Katika vitu ambavyo Mwl alivisimamia haswa ni usawa.Hakutaka kabila moja lijione/jisikie liko juu ya jingine na kutengeneza matabaka.Sasa swali langu nnaloomba mnisaidie ni hili....ule msemo au sijui niyaite madai ya kwamba Mwl aliwahi kusema makabila fulani hayafai kupewa uongozi wa juu wa nchi ni wa kweli au ni propaganda za waliomchukia?!Nauliza hivi kwasababu niliyoyasoma juu yake hayaendani kabisa na madai haya...na wala haileti maana kusikia kwamba aliyepigania usawa ndie aliyekua wa kwanza kutengeneza matabaka lilipokuja swala la uongozi!!!

Naomba majibu kama yapo yawe na vielelezo na yasiwe maneno ya kusikika na kufikirika tu ili tusiojua tujifunze kitu.
Asanteni!



Mafisadi wameshindwa kuongoza nchi sasa wanakuja na tabia ya kumlaumu mwalimu kwa kushindwa kwao kuongoza nchi. They should deliver without pointing fingers to others. Utajiri waliojichukulia utawatokea puani sooner rather than later.

Mwalimu ataendelea kusifiwa kwa yale aliyofanya kwa wengi ambao wanakubali kwamba alikuwa one of the great leaders katika generation yake, wale wanaomkandia kwanza hawawezi hata kukaribia chembe ya yale aliyofanikiwa na ni failures katika maisha yao binafsi. Kuna wengine wanakuja na maswala ya kizandiki ili kupotosha hoja muhimu kwa taifa hili, kama Nyerere alikuwa ni failure sijui hawa ambao nimisukule pale Magogoni tuwaweke katika sehemu ipi?


Mwalimu aliacha hii nchi ipo katika utajiri mkubwa katika kila sekta ukianzia reli, air travel, kampuni ya simu na mashirika muhimu ya umma ambayo ndio mafisadi sasa wamejichukulia na kufanya yao na kuwakamua walipa kodi. Hata nchi kubwa kama Uingereza, Germany na Marekani nguzo kuu bado zinasimamiwa na serikali wakati hapa kwetu wamejichukulia bure na sasa wanafikiri wataweza kuendelea kushiba baada ya kuvimbiwa. Hawa kuku walioletwa hapa kupotosha mambo muhimu hawawezi kufanikiwa kwa sababu Tanzania aliyoiacha mwalimu inazaliwa upya na watakiona cha mtema kuni.


Mwalimu aliandika vitabu vingi sana kama una nia ya kumwelewa nenda kavisome …. …. …. … Wakati ni huu!
 
I am sure the first part is just an argument from your side but you now know what the point is.
The best ideas are those which works. You cant have it good and failed. Its either black or white, no gray shades. He himself announced to have failed, who are you to keep on depicting the same failures as good? a devils advocate?
Is the argument if Nyerere had the better ideas??; If we are debating if Ujamaa is better than Capitalism I think that calls for another day, So you want to tell me that Good leaders don't fail, Mkwawa; Mangi Sina to name just a few they failed at the end but does that make them bad leaders?

Ujamaa policies failed; but Nyerere was a good leader and during his time there were many problems, njaa, vita vya Kagera n.k. still he stand in what he believed in and people followed him, now those are recipes of a good leader at least he had a vision of where he wanted to take us towards Ujamaa tofauti na sasa viongozi vision yao ni kumaliza miaka yao 10 na kuondoka na pension to last their kids and grandchildren lifetime
 
Mwalimu kama kiongozi alikuwa na mapungufu yake mengi tu na hata yyeye mwenyewe aliyasema hadharani bila woga wala aibu. Sijui kama Watanzania tutapata bahati ya kuyasikia mapungufu ya akina Mwinyi, Mkapa na Kikwete ambayo pia yamehusisha ufisadi na uporaji wa mali za Watanzania tena mchana kweupe. RIP Mwalimu
You have said it all Mkuu kama watanzania tuna kitu cha kujivunia ni Baba wa Taifa..., watu wanachokifanya ni kupoint mapungufu yake na kusahau yote mazuri aliyoyafanya..., Yaani Afrika nzima visionaries walikuwa ni kina, Kwame Nkurumah; Nyerere na Mandela hao ndio watu wa kujivunia Africa nzima.
 
Ni kigezo gani kinatumika kutambua Nyerere alipendwa au hakupendwa na watu wengi?

Mimi naamini Nyerere alipendwa na watu wengi kuliko rais yeyote aliyepata kutokea Tanzania.

Naamini pia ni Miongoni mwa viongozi mashuhuri Afrika waliopendwa na kuheshimika sana na waafrika.........Ukimuondoa Mandela, Nyerere anafunika vibaya....Anaweza fatiwa na kina Nkrumah, Lumumba, Samora na viongozi wa sampuli hii (wapigania uhuru)………Hawa wa siku hizi ni kama makapi tu.


Kwa Tanzania hii, hakuna kama Nyerere!.......Ndio maana pamoja na kuwa ameshatangulia mbele ya haki, bado watu wanazikumbuka busara zake na wanamkumbuka kwa mema mengi aliyoyafanya, tofauti na maraisi wastaafy wengine ambao hata huwa hawakumbukwi kwa mema zaidi ya mabaya.

Heshima yako mkuu!!
Hapo penye blue na green panakanganya kidogo!! Kwani nawe umetumia vigezo vipi kusema uliyosema?!?

Pale penye brick red napo pana utata mkubwa. Je, unaamini Mandela ni zaidi ya Nyerere? Kwa vigezo vipi?!?

Asante!


 
Is the argument if Nyerere had the better ideas??; If we are debating if Ujamaa is better than Capitalism I think that calls for another day, So you want to tell me that Good leaders don't fail, Mkwawa; Mangi Sina to name just a few they failed at the end but does that make them bad leaders?

Ujamaa policies failed; but Nyerere was a good leader and during his time there were many problems, njaa, vita vya Kagera n.k. still he stand in what he believed in and people followed him, now those are recipes of a good leader at least he had a vision of where he wanted to take us towards Ujamaa tofauti na sasa viongozi vision yao ni kumaliza miaka yao 10 na kuondoka na pension to last their kids and grandchildren lifetime

After 24 Years in power he himself declared he failed, who are you to still argue? Does "I failed" means "I won" to you? creepy.

He didnt say Ujamaa failed, he said "I failed" is he ujamaa or nyerere?
 
You have said it all Mkuu kama watanzania tuna kitu cha kujivunia ni Baba wa Taifa..., watu wanachokifanya ni kupoint mapungufu yake na kusahau yote mazuri aliyoyafanya..., Yaani Afrika nzima visionaries walikuwa ni kina, Kwame Nkurumah; Nyerere na Mandela hao ndio watu wa kujivunia Africa nzima.

Miaka 26 ya Mwinyi, Mkapa na Kikwete tumeona kuongezeka kwa kiwango kikubwa cha ukusanyaji wa kodi ya mapato, tumeona kuongezeka kwa kiwango kikubwa kwa nchi yetu kupatiwa misaada na mikopo toka nchi za Wafadhili pia kwa miaka zaidi ya 10 tunachimba dhahabu yetu ambayo bei yake katika soko la dunia imefikia hadi $1,400 kwa ounce moja ukilinganisha na bei ya $220 ilioanza kuchimbwa mwaka 2000. Je, pamoja na vyote hivi tuna maendeleo ya kuweza kujivunia au kujivunia viongozi wetu kuanzia Mwinyi mpaka Kikwete? kama lipo la kujivunia miongoni mwa Watanzania walio wengi ni lipi hilo!?
 
Miaka 26 ya Mwinyi, Mkapa na Kikwete tumeona kuongezeka kwa kiwango kikubwa cha ukusanyaji wa kodi ya mapato, tumeona kuongezeka kwa kiwango kikubwa kwa nchi yetu kupatiwa misaada na mikopo toka nchi za Wafadhili pia kwa miaka zaidi ya 10 tunachimba dhahabu yetu ambayo bei yake katika soko la dunia imefikia hadi $1,400 kwa ounce moja ukilinganisha na bei ya $220 ilioanza kuchimbwa mwaka 2000. Je, pamoja na vyote hivi tuna maendeleo ya kuweza kujivunia au kujivunia viongozi wetu kuanzia Mwinyi mpaka Kikwete? kama lipo la kujivunia miongoni mwa Watanzania walio wengi ni lipi hilo!?


Cha kwanza ni hiki kinachokufanya tuongee sasa hivi. Naapa wakati wa nyerere tusingethubutu.

Nyerere was against chochote chenye maendeleo.
 
Mantiki (logic) ni kitu kizuri sana kujifunza; kwa sababu haihusiani na ujengaji wa hoja tu bali pia katika kutafuta ukweli. Uzuri wake mwingine ni kuwa ukifuata kanuni zake huitaji mtu kukulazimisha kuuona ukweli bali wewe mwenyewe utauona ukweli kwani ukweli unajionesha wenyewe kuwa ni kweli (self-evident). Fuatana nami:

Leo mna TV
Leo mna Computer
Leo mna radio
Leo mna vyama vingi
Leo mna upinzani
Leo mna wawekezaji lukuki
Leo mna vyama vya ushirikia SACCOS, NGOS n.k
Leo mna wasomi wengi kuliko wakati mwingine wowote
Leo mna utaalamu wa kila aina

Vyote mlivyo navyo sasa havikuwepo wakati tunapata uhuru wala havikuwepo miaka 25 baada ya Uhuru. Lakini wakati ule Taifa hili hili liliweza kujilisha kwa kiasi cha kutosha, lilijenga reli na mitandao ya barabara, lilijenga mabwawa ya kuzalisha umeme liliweza kusomesha maelfu ya watoto wake, liliondoa literacy, liliweza kutoa chanjo za magonjwa yaliyowashindwa wakoloni. liliweza kufanya mambo mengi (viwanda vya nguo, baskeli, vipuri, vyuma, radio, n.k ) vyote hivi vilikuwepo chini ya Dikteta Mwandamizi Nyerere


Dikteta huyo aliyeharibu nchi "beyond repair" akaamua kuachia madaraka kwa hiari yake mwaka 1985 bila kutaka kupewa kinga ya maovu yake akiwa madarakani na akaashi miaka mingi baadaye huku watu wenye kujua maovu yake (hakuna dikteta asiye mwovu) hakuna hata mmoja aliyewahi kufungua kesi dhidi yake. Huyu Dikteta Mwandamizi aliyeliangamiza taifa akawa wa kwanza kutetea vyama vingi na kuliamsha taifa alipoona linatoka katika misingi yake - na amebakia kiongozi pekee aliyeweza kuwanyoshea vidole watawala walioko madarakani bila watawala hao kuamua kumchukua hatua - hasa kwa vile alikuwa ni dikteta!

Dikteta Nyerere aliyewabagua watu ndiye kiongozi pekee ambaye serikali zake zimewahi kuwaweka watu wa dini, rangi na makabila mbalimbali. Waislamu, Wakatoliki, Wahindi, Wazungu, Waarabu wameweza kushika nafasi katika serikali yake. Dikteta huyu mwandamizi ndiye aliyeweza kusema kuwa kabla "wachache wetu hawajaishi katika anasa, wengi wetu wapate mahitaji yao muhimu" na hivyo akaanzisha na kufuatilia kampeni ya chakula bora, nyumba bora, mtu ni afya, siasa ni kilimo n.k na watu walimuamini na kumfuata kwani hawakuwa na shaka na malengo yake.

Hakuwa na mashaka kuwa Nyerere alikuwa anajinufaisha na matatizo yao; wala hawakuwa na shaka kuwa alitumia nafasi yake vibaya kuishi kama madikteta wengine wa zama zake. Dikteta Nyerere, alionekana akishiriki kupanda miti bila kuwekewa mikeka, Dikteta Nyerere hakuwa anatembea akizungukwa kila anakopita na bodigadi wake kumsimamia nyuma kama mfalme fulani. Dikteta huyu Nyerere kama wengine walivyoonesha hakuna kazi kushiriki kampenzi za ujenzi wa nyumba bora yeye mwenyewe akishiriki kushika matope kukanda udongo na kupanda kwenye ngazi kujenga nyumba. Huyu ndiye dikteta Nyerere ambaye aliiharibu nchi beyond repair.

Wakaja viongozi wasio madikteta Mwinyi, Mkapa na Kikwete. Viongozi hawa wameonesha uzalendo mkubwa na kuonesha ni jinsi gani wanaongoza kwa kufuata demokrasia. Nyerere tuliambiwa alikuwa anawahamisha wapinzani wake wa kisiasa; hawa wa leo wanafanya nini na wapinzani wao wa kisiasa? Tunaambiwa Nyerere hakuacha nchi yenye Katiba nzuri na kuwa alilazimisha watu kupiga kura ya "ndio au hapana"; hawa wa leo hata kura ya ndio au hapana haipigwi na watu wameingia Bungeni bila kupigiwa kura hata moja lakini wanaitwa ati "wabunge wa kuchaguliwa wa jimbo"; Dikteta Nyerere hakutaka watu wajue saana na hivyo akaja na "kisomo cha watu wazima" na kuhakikisha watanzania wote wana uwezo wa kusoma na kuandika - hadi kufikia asilimia 98; hawa wazalendo wazuri viongozi mahiri wameweza kufanikiwa kuvurunda kazi hiyo ya dikteta Nyerere kiasi kwamba literacy level iko chini ya asilimia 70!!

Tunaambiwa kuwa Dikteta aliyeharibu nchi, ndiye aliyesaidia kujenga misingi ya elimu akiamini kuwa elimu ndio ufunguo. Milango ya elimu ikafunguliwa kwa kila mtoto wa Kitanzania na kitu pekee ulichotakiwa kuwa nacho ni kufanya vizuri; hakukuwa na kikwazo cha mtoto wa Kitanzania kwenda shule; haikujalisha unatoba Kigoma au unatoka Arusha; ukifaulu unaenda kusoma kwa gharama za serikali tena hadi chuo Kikuu. Leo hii, viongozi wetu wazuri na wa mfano wameinua sana elimu ya juu kwa kuifanya iwe bidhaa adimu kwa walionacho!

Dikteta Nyerere aliweza kujenga shirika la ndege la Tanzania - ndege zake zikaweza kuruka na kutua hadi London! Zikiwa na nembo ya twiga wetu na zikipata sifa na marubani wake majina yao watu wanayakumbuka! Leo chini ya viongozi wa demokrasia wasio na madikteta hakuna ndege hata moja inayoruka ikiwa na alama ya taifa; acha kwenda London tu kutoka Dar hadi Dodoma hakuna!

Dikteta Nyerere aliachiwa reli ya kati na Mkoloni, chini yake ikapanuliwa na ikaongezewa na reli ya Uhuru ! Tulkawa taifa la kwanza Afrika kujenga reli mpya kabisa baada ya uhuru! Watawala wetu wa sasa wameshindwa kujenga hata reli toka Mtwara Dar miaka karibu 40 tangu Nyerere alipomaliza kujenga reli ya Uhuru. Tena, wao wakipokea misaaada zaidi kuliko Nyerere!

Baada ya matatizo ya uasii ya 1964 Dikteta Nyerere alitambua tatizo la jeshi kuwa lilirithi mawazo ya kikoloni na halikujengwa na wananchi wake; Nyerere akawa kiongozi wa kwanza Afrika kuvunja jeshi lake na kuliunda kuanzia chini. Jeshi hilo likawa na nidhamu na kujitofautisha katika Afrika na kubakia kuwa jeshi la wananchi wa Tanzania. Liliheshimika, lilipendwa na lilibeba fahari. Hata baada ya kuondolewa siasa, jeshi letu lilibakia kuwa ni la ulinzi. Jeshi lilipoondolewa katika siasa halikujiingiza katika malumbano ya kisiasa wakati Nyerere yuko hai. Wakati wa vuguvugu la 1995 ambapo watu walijitokeza kuipinga serikali ya CCM na mvuto wa Mrema ulikuwa kama wa Slaa na CCM ilitishiwa madarakani JWTZ halikujitokeza kusema au kufanya jambo lolote kuonesha upendeleo. LILIKAA PEMBENI - Wakati Dikteta mwenyewe yupo!

Mwaka jana JWTZ lililoheshimiwa na kujitofautisha kuwa ni la wananchi likaingia katika siasa chini ya viongozi wazalendo waliokubuu katika demokrasia wenye kuheshimu siasa za vyama vingi! Naam Dikteta Nyerere akazidiwa tena na wanademokrasia wapendwao.

UKINIPA UCHAGUZI KATI YA DIKTETA NYERERE NA HAWA - NITAMCHUKUA DIKTETA NYERERE ANYDAY OF THE WEEK!

Leo mna TV
Leo mna Computer
Leo mna radio
Leo mna vyama vingi
Leo mna upinzani
Leo mna wawekezaji lukuki
Leo mna vyama vya ushirikia SACCOS, NGOS n.k
Leo mna wasomi wengi kuliko wakati mwingine wowote
Leo mna utaalamu wa kila aina

Na Nyerere aliondoka 1985 (miaka 26 iliyopita) , alikufa 1999 (Miaka 12 iliyopita) na kuwaachia wasio madikteta na vyote ambavyo havikuwepo wakati wake kutokana na udikteta wake leo vipo tena bwelele! Tatizo liko wapi? Mbona mnalalamika, mbona wananchi wenu hawana furaha, mbona mmekuja na jaribio jingine dhaifu la "mpango wa maendeleo wa miaka 5"? Mbona mnataka kurudia misingi ile ya kidikteta? Mbona hamuwezi kuzungumza bila kutaja jina lake? Mbona elimu yenu imevurugwa? Mbona nishati yenu imevunjwa vunjwa, mbona madini yenu hayawapi neema mliyowaahidi wananchi wenu?

Wanasema "tatizo ni Nyerere!". Ati "Nyerere ameacha".. ati "Nyerere amejenga". Yuko kaburini kageuka samadi miaka mingi iliyopita. Wasomi nyinyi, watawala nyinyi, nini kinawashinda? Wanasema tatizo ni "Fikra za Nyerere". Amewaachia madaraka mwaka 1985, hata mlipoua fikra zake kule Zanzibar aliwasema tu nakuwaonesha mmefanya upumbavu lakini hakunya lolote; angeweza kurudi madarakani kama angetaka. Mnajua kabisa angeweza - soma Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania. Jeshi lilimtaka arudi - alikataa. Akawaambia "vijana" wamuache Rais afanye kazi yake na afanye makosa! Dikteta mwenye kukataa madaraka!!! Oh.. huyo ndiye Dikteta nimpendaye!!

Tatizo nini? Nyerere! wanasema.

Logic - mantiki.
 
No u dont need to be crazy to defend the same as u dont need to be crazy to criticise nyerere . Tunaweza kuweka sababu zetu sote alafu tukapima . Ukiwa unbiased pamoja na kumriticise bado utaona nyerere ni mfano wa viongozi tunaowahitaji sasa but kwa mwelekeo tofauti.



Hapa sijakuelewa mwanz umesema we need to be crazy to defend him . alafu hapa unasema tunaweza kumdeffend kwa kumlinganisha na leaders wengine walikuja baada yake. kwani wewe ulitaka tumlinganishe na kina nani.
au na nini



Sio kweli kuwa N yerere failed terribly. Unless tujue context ya terribly kwako ni nini Mbona tanzania kuna miaka ni nchi iliyoongoza kufuta ujinga duniani. Na hii ilikuwa chini ya sera za mwalimu. mammbo ya UPE na elimu ya watu wazima. Yes Duniani. But nakubali kuna mambo ali fail lakini sio wa hicho kivumishi cha sfa cha terribly ulichotumia



Hapa nakubaliana na wewe haya mambo ya kulia sikubalini nayo.



Mkuu nadhani Nyerere alikuwa na mapungufu yake lakini mapungufu ya uongozi wa nyerere sio makubwa kiasi hicho kwamba ndio chanzo cha matatio yetu yoote . Do u know u dictator wa hitler ndo umsaidia kifanya Ujerumani kuwa amaong indutrila power. Beofer hitler Ujerumani ilikuwa imeachwa mbali na UK na france. Anywa siendi huku lakini nataka kukuonyesha kuna sometime nchi zinahitaji dictator. Mfano mwingine ni Uganda. Uliza au fuatilia waganda vizuri . Ukweli ni kwamba Ukweli ni kwamba Idd amin was a good leader to most of ugandan. Upo hapo????????

katika uongozi hutakiwi kumsikiliza kila mtu la sivyo sio leader tena. Kutoambilika kwa kiongozi ni jambo baya mara matokeo yakiwa mabaya lakini kutombailika kwa nyerere mambo kulikosababisha matunda mazuri tunaweza tusikujue. So hata wewe uiwa kiongozi usijidangaynye kuwa utamsikiliza kila mtu. Hata obama kule unasikia aliapewa alteantive tatu za kumuua OSama yeye akaamua ile ya kumzukia. Inge bakcfire ile leo tungekuwa tunaongea mangine. Na wangejitoeza watu wakisema sisi tulisema bora tupige mabomu tu. Hizo ni siasa.

Kwa mtazamo wangu tanzania tunakosa president kwente udicator fulani. Mkapa aalikuwa ana udctor fulani lakini naye tatizo ni ufisadi. yaani Jakaya angek uwa ana talanta za Udictor na Uzalendo kama wa nyerere basi tungekuwa mbali.

This is timing hata ungekuwa wewe mazigira ya wakati huo sijui ungefanya nini . na katiba aliyoweka haina tofauti na katiba za nch nyingie za afrika zilizotangulia kupata uhuru. Sasa ulitegema aige kutoka wapi.



Sasa Nyerere alishauri kama nani alikuwa ana mamlaka gani kwenye serikali wakati huo? Sasa wewe unamlaumu aliyeshauri badala ya kuwalamumu walimsikiliza ambo ndio walikuwa na mamlaka na uwezo wa kukubali au kukataa. Ni kosa kusema aliforce sababu hakuwa yeye rais. Kama wenye madaraka waliamuakumsikiliza ni udiafu wao sio wa nyerere



Yes tuache unafiki tutoe credit where it deserve pia. J. K Nyerere deserve some credit and some critics Nyerere alionyesha mfano wa leadership. ambao baada yake sioni kama kuna viongozi wana leadership.


Nawasilisha

Mtazamaji asante kwa kuwakilisha

Kwanza sijafanya comparison ya hawa viongozi waliofuata baada ya Nyerere...wote ziro

Leo hii tunalilia katiba Nyerere aliiweka katiba ya ku-mfavor yeye

Kuteua

Jaji mkuu
Mkuu wa majeshi
CAG
Chair wa tume ya uchaguzi
mkuu wa takukuru(not sure)
etc

Nyerere aliweka msingi wa gorofa moja wakati tunataka gorofa kumi! ndyo maana kazi zake nyingi zimekufa na hazikumbukwi tunabaki kutetea tu


Nyerere hakuwa kiongozi, Nyerere alikuwa mwanafalsafa aliyetamani vitu viwe kama anavyotaka lakini akashindwa njia ya kufika hapo.

sifa ya kiongozi bora

Hutengeneza viongozi kama yeye...........hakuna na hakuwepo

kuthibitisha kauli ya mwanzo kuwa alikuwa haambiliki , Leo hii hakuna kama yeye nyote mnaishia kuandika kumtetea lakini mnaishi kama mabepari! deny it!!

Swala la katiba ni very serious, you will soon hear and see ..... kuwa lawama za katiba zitarudi kwa Nyerere.

Katiba ni dira ya taifa , kama katiba ya Tanzania inaweza kumfanya rais kuwa dikteta kwa maneno yake mwenyewe Nyerere , kitu gani kinachoonyesha yeye hakuwa aliyesema angekuwa??

Na alifanya nini kuzuia isiwe kwa marais wanaokuja

nitamsifu kwenye mengi sana, nitamuunga mkono hata kwenye siasa yake ya ujamaa kuwa alishindwa akiwa na nia njema. ILA SITAKUBALIANA NA HILI LA KATIBA. WHENEVER YOU HEAR OPPOSITION AND OTHER ACTIVIST ARE CRYING FOR NEW CONSTITUTION RUN TO HIS GRAVE AND ASK HIM why he left us with constitution like this??

Mkuu au haujasikia kilio cha katiba? hujagundua tu anasemwa nani hapa? au ndiyo utauliza wenginewalifanya nini? si wanajinoma kama yeye?? katiba tamu kwa rais jamani na ni chungu kwa raia!!

au ili kumtukuza Nyerere tusibadli katiba??

Mkuu wanasemwa akina washington isiwe Nyerere

If we areliving in the world of logic then Nyerere failed......if we are living with double standard let swim in the world of excuse kwani kujitetea kunashindikana

Next few years watu watamtetea Kikwete kwa KILIMO KWANZA japo leo tunasema hafai

TUKIWA NA STANDARD NA KUITA KIJIKO KIJIKO BASI TUTUMIE KOTE, KAMA NDI HIVYO BASI MARAIS WOOOTE WAZURI SANA SANA, JAPO UZURI WAO UTAKUWA asilimia 0.0002% lakini si ni uzuri!!!
 
Mwanakijiji:- Brother sitaongea tena baada ya wewe kusema,, umesema yote kaka na ni ukweli mtupu na inatia uchungu ,mkubwa sana. Watu kama wewe ni wachache mno.
 
After 24 Years in power he himself declared he failed, who are you to still argue? Does "I failed" means "I won" to you? creepy.

He didnt say Ujamaa failed, he said "I failed" is he ujamaa or nyerere?

Accepting and identifying failure ni one way ya ku recify problem. Je Huoni bado ni mfano wa kuigwa . We umewai kusikia mwanasiasa gani anakubali publicly alipofail. umewai kusikia mwanasiasa yeyte wa kiafrica ana declare failure

Si unaona hawa wa sasa ndio hivyo Mgao wa umeme zaidi ya miaka 10 wanasema ni challenge? as if mgao ni tetemeko la ardhi au mafuriko? Hawataki kusema ni failure
 
Mtazamaji asante kwa kuwakilisha

Kwanza sijafanya comparison ya hawa viongozi waliofuata baada ya Nyerere...wote ziro

Leo hii tunalilia katiba Nyerere aliiweka katiba ya ku-mfavor yeye

Kuteua

Jaji mkuu
Mkuu wa majeshi
CAG
Chair wa tume ya uchaguzi
mkuu wa takukuru(not sure)
etc.................................................


Mkuu kifupi ukisikia Jina Nyerere linakuwa associated na underveloped Ya Tanzania basi ujue kuna watu wanaficha underperfoemnce na irepsonsibility yao nyuma ya mapungufu machache ya nyerere.

By those 1960's , in those era with two major blocs( USSR Vs USA) Nyerere did wht every other Good leader could have done.
 
tehe tehe tehe....!! nape naona kaongeza kidogo per diem kutoka buku mbili mpaka....au kuna watu wa "zamu yetu"wametuma watu wao mtandaoni!!! Ndiyo maana Mbayuwayu anamwita Nyerere mzee Nyerere tofauti na wengine wanavyoita baba wa Taifa!!
Hii thread inahusu ukabila ila naona yameingia mambo mengi tu!! Mimi nilikuwa hata sijijui wakati wa vita vya kagera !!Ila mzazi wangu ananiambia life ilikuwa nzuri sana kabla ya vita..! Kwa wafanyakazi mshahara ulikuwa unakutana na mshahara mwingine ila baada ya ya vita ndiyo hivyo tukafunga mkanda !!

Inasemekana miaka ile Shilingi yetu tano ilikuwa ni sawa na dollar moja ya Marekani na shilingi yetu ishirini ilikuwa ni sawa na UK pound 1. Wakaja wachakachuaji wakaichakachua shilingi yetu kwa kisingizio cha kupata misaada na mikopo toka IMF, WB pamoja na nchi za wafadhili. Hili la kuichakachua shilingi yetu Nyerere alilikataa kata kata.

Sasa ukiwauliza hao waliochaikachua shilingi yetu ni faida gani tuliyoipata baada ya uchakachuaji ule na misaada na mikopo chungu nzima toka nchi za wafadhili, IMF na WB wanang'aa macho. Pia wengi wanasahau kwamba Nyerere alipigwa vita sana na nchi za Magharibi ili kuhakikisha hapati mafanikio na wakaenda kuwakumbatia watu kama akina Mobutu na mafisadi wengine wa Afrika.
 
Cha kwanza ni hiki kinachokufanya tuongee sasa hivi. Naapa wakati wa nyerere tusingethubutu.

Nyerere was against chochote chenye maendeleo.

Siwezi kumsifu rais kwa kuruhusu (japo kiduchu, maana sheria ya vyombo vya habari hawataki kuibadilisha) uhuru wa kujieleza kwasababu kwa kufanya hivyo hatupi zawadi, bali haki yetu ya kikatiba.

Halafu, suala la uhuru wa vyombo vya habari halikwepeki kwa sasa kwa sababu ya teknolojia (social netowrks etc) na utegemezi wa nchi yetu kwa misaada kutoka nchi za nje. Rais hawezi tena kuzuia uhuru wa kujieleza na bado akaenda kwa wafadhili kuomba hela.

Sitegemei tumsifu rais kwa hili, rais aliyepewa madaraka makubwa sana kwenye katiba yetu. Tumsifu kwa vision na mambo mengine na sio routine activities.
 
Mwalimu Nyerere hakuwabagua wala ndizi - Wahaya, Wachaga na Wanyakyusa - au watu wa makabila mengine katika uongozi wa nchi yetu. Kuna wala ndizi wengine lakini tunapo zungumzia wala ndizi, tunatumia jina hilo kumaanisha watu wa makabila hayo matatu.

Nyerere angefanya hivyo na kusema raisi na waziri mkuu asitoke makabila hayo, angekuwa anakwenda kinyume cha uongozi wake na imani yake kwamba sisi sote ni sawa.

Nimezungumza na watu mbali mbali kutoka enzi ile pamoja na wapinzani wake kuhusu suala hilo lakini bado sijamsikia hata mmoja na mwenye ushahidi wa kuridhisha kwamba Mwalimu alisema, kwa manufaa ya taifa, Mchaga, Mnyakyusa au Mhaya asiwe nafasi ya kuwa raisi au waziri mkuu wa Tanzania. Sijazungumza na kila mtu anaye sema au anaye amini hivyo, lakini nimezungumza na wengi wa kutosha, pamoja na wale walio kuwa karibu naye sana ambao baadaye wakajiunga na vyama vya upinzani.

Kuna kiongozi mmoja wa taifa aliyekuwa karibu sana na Nyerere niliye zungumza naye Dar mwaka 1974. Nilifahamiana naye sana, na nilikuwa nyumbani kwake siku moja. Tulikuwa tunazungumzia mambo mbali mbali pamoja na ukabila nchini, ikiwa tunao au hatuna, kuweza kuhatarisha umoja wa nchi yetu. Katika mazungumzo hayo, akamtaja Mwalimu Nyerere na Kawawa kuhusu uongozi wao. Alisema Nyerere hana ubaguzi na hana upendeleo. Akaendelea kusema: "Nyerere ni mpole lakini ni mkali sana when you encroach on his authority." Those were his exact words, quoted verbatim. Kuhusu Kawawa, alisema sentensi yote katika Kiingereza: "He is an excellent administrator and very hardworking."

Alisema hayo yote bila mashaka yotote. His statements were categorical, unequivocally so.

Aliendelea kusema kwamba Nyerere aliamini kabisa kwamba Watanzania wote wana haki za uraia na kwamba hata watu ambao si weusi ni Wafrika kama sisi. Alisema Nyerere hatofautishi kati ya Watanzania weusi na wenye asili ya Kiarabu au ya Kihindi au wenye asili nyingine. Wote ni Wafrika na ni Watanzania ikiwa ni raia wa Tanzania. And he practised what he preached. Hakuwabagua serikalini au mahali popote. Enzi ya Nyerere tulikuwa na mawaziri na viongozi wengine wenye asili ya Kihindi na Kiarabu. Tulikuwa na wazungu pia katika baraza la mawaziri na sehemu zingine. Wengi wenu mnamkumbuka Amir H. Jamal na Derek Bryceson. Waziri wa fedha, Sir Ernest Vasey ambaye hakuwa raia, was there only temporarily.

There were two top-notch intellectuals in our first cabinet: Nyerere himself and Jamal. They were later joined by another bona fide intellectual, Abdulrahman Mohamed Babu, baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Uafrika wa wenzetu hao, hasa Waarabu wa Afrika Kaskazini, ni suala ambalo niliwahi kumuuliza Walter Bgoya mwaka 1971 alipokuwa head of the North Africa and Middle East Division, Ministry of Foreign of Affairs. Miaka ile, the official name of the ministry did not include "of International Cooperation." Ilikuwa inaitwa Ministry of Foreigin Affairs tu. Nilimuuliza kuhusu Pan-Arabism na ikiwa aliona kuna conflict kati ya Pan-Africanism na Pan-Arabism na ikiwa nchi za Kiarabu Afrika Kaskazini zilikuwa more commited to Pan-Arabism kuliko Pan-Africanism. Alisema hakuna conflict yoyote kati ya -isms hizo mbili and in terms of commitment to Africa by North African countries although they were predominantly Arab. Walter Bgoya was then known as a revolutionary intellectual and a fountain of ideas. closely associated with Walter Riodney then teaching at UDSM.

Nyerere also had gone record kwa kusema wazi kabisa kwamba Algerians, Egyptians and other Arabs in North Africa ni Wafrika kama sisi. Nchini Tanzania, his desire to see Dr. Salim Ahmed Salim become president of Tanzania, a predominantly black country, demonstrated his commitment to non-racialism and equality. Unfortunately, racists, black racists, won, walipo mpinga na kumzuia Salim kuwa raisi wa nchi yetu, one of the best presidents Tanzania never had. We have paid a heavy price kwa sababu ya ubaguzi.

Ni kiongozi huyo, Mwalimu Nyerere, ambaye watu wanasema hakutaka Mchaga, Mhaya au Mnyakyusa aingie Ikulu au awe waziri mkuu wa Tanzania. Ni kiongozi huyo huyo ambaye pia aliwateua Wachaga, Wahaya na Wanyakyusa wengi kuwa viongozi wa taifa letu katika sehemu mbali mbali. Ni watu kutoka makabila hayo matatu walio kuwa wengi katika madaraka ya juu kuliko watu wa makabila mengine. Tunaweza kusema aliwapendelea? Kulikuwa na sababu za kihistoria ambazo zimejadiliwa hapa Jamii Forums na mahali pengine kwa nini mambo yalikuwa vile.

Watu kutoka makabila hayo wamelitumikia taifa letu kama watu wa makabila mengine. Wasingekuwa na uzalendo halisi, Nyerere asingewapa madaraka aliyowapa chini ya uongozi wake. Na ikiwa Nyerere aliogopa kwamba Mhaya, Mchaga au Mnyakyusa atawajaza serikalini watu wa kabila lake akiwa raisi au waziri mkuu na nchi hii itatawaliwa na watu wa kabila moja, asingewateua Wachaga, Wanyakayusa na Wahaya kuwa na madaraka ya juu serikalini, katika mashirika ya umma, na sehemu zingine za uongozi nchini. Ni sehemu hizo, wizarani, katika mashirika na kadhalika ambamo ni rahisi viongozi kuwapendelea watu wa makabila yao. Si lazima wapate uraisi au uwaziri mkuu kuweza kuwapendelea ndugu zao wa kikabila.

Ikiwa Nyerere aliwaamini watu wa makabila hayo matatu kuwa viongozi wa taifa letu sehemu mbali mbali, hakuna sababu yoyote kusema kwamba hakuwaamini kuingia Ikulu kuwa raisi, au kuwa waziri mkuu.

Katika mjadala mwingine, niliwahi kutoa mfano wa Mnyakyusa mmoja, Amon Nsekela, ambaye Mwalimu Nyerere alimwamini sana na madaraka. Alimwamini Nsekela kwa sababu ni Myankyusa? Najua yaliyotokea kuhusu Nsekela na watu wengine lakini natoa mfano mmoja tu wa Nsekela. Kama nilivyo wahi kusema, bila Mwalimu Nyerere kumlinda Nsekela, Nsekela would have been history as far back as the early seventies and even before then in 1970. Kulikuwa na wana Usalama wa Taifa, at the behest of and in collusion with some senior politicians and government officials, who wanted to destroy Amon Nsekela. They tried everything they could to destroy him, to no avail. Some are dead and some are still living. All the reports which were written by some intelligence officiers against Nsekela in order to destroy him were rejected by Nyerere. He refused to sign them. No need to go further.

Pia miaka ile, Nsekela alikuwa ni Mtanzania ambaye aliteuliwa na Mwalimu Nyerere sehemu mbali mbali kuliko wananchi wengine. He had the largest number of posts among all Tanzanians in the early seventies, thus inflaming passions among his detractors. Mwalimu alifanya hivyo, kumpa Nsekela vyeo vingi, kwa sababu alikuwa anawapendelea Wanyakyusa?

Daktari wa kwanza wa Mwalimu Nyerere, Mwakosya, alikuwa ni Mnyakyusa. Mlinzi wake kwa muda mrefu, Mwangota, alikuwa ni Mnyakyusa. Daktari wake mpaka mwisho wa maisha yake, Mwakyusa, alikuwa ni Mnyakyusa. Aliwapendelea Wanyakyusa?

Ikiwa aliwaamini kiasi hicho, kwa nini watu wanasema hakuwaamini Wanyakyusa kuwa viongozi wa taifa letu - kuwa raisi au kuwa waziri mkuu? Kuna hata mfano wa mlinzi wake, Mwangota, aliyemwamini kumlinda. Na alitimiza wajibu wake nyakati zote, hata ku risk maisha yake, as he was expected to, in order to protect the president. Kuna wakati Mwalimu alikuwa anatembelea nchi moja ya Ulaya Mashariki (sitaki kuitaja) na alinusurika kuchomwa kisu. Mwangota sprang into action right on time and grabbed the knife and the assailant. He got cut between his thumb and index finger. But he did nothing heroic. He did what he was supposed to do, even if he had to sacrifice his life to protect the president.

Ingawa watu wa makabila hayo matatu walikuwa wengi serikalini na sehemu mbali mbali za madaraka ya juu baada ya nchi yetu ya Tanganyika kupata uhuru na miaka iliyofuata, hawakuteuliwa wengi kuwa mawaziri. Nakumbuka kulikuwa na Wachaga wawili, Solomon Nkya Eliufoo na Nsilo Swai (nakumbuka alikuwa na jina refu - Asanterabi Zephaniah Nsilo Swai). Kulikuwa na Mhaya mmoja, Clement George Kahama, na baadaye kidogo, Mnyakyusa mmoja, Jeremiah Kasambala.

Nyerere hakuwabagua watu wa makabila hayo, hawakunyima uwaziri, ingawa wengi wao walikuwa tayari na madaraka ya juu nchini Tanganyika baada ya uhuru. Halafu tunasikia Nyerere hakutaka Mhaya, Mchaga au Mnyakyusa kuwa raisi au waziri mkuu wa Tanzania.

Hata watu ambao siyo Watanzania wanao julikana kuwa wapinzani wa Nyerere, politically and ideologically, hawaja mlaumu na kusema aliyabagaua makabila fulan nchini mwetui. Mmoja wao ambaye ni maarufu sana ni Ali Mazrui ambaye wapinzani wa Nyerere hapa Jamii Forums na mahali pengine wamejaribu kumtumia na kusema alimnyoosha Nyerere. Sijui wamesoma kiasi gani cha maandishi ya Mazrui kuhusu Nyerere, vtabu vyake na articles, kuanzia na articles zake katika "Transition" wakati journal hiyo was being published in Kampala under the editorship of Rajat Neogy miaka ya 1960s when Mazrui was just a young professor in his thirties and head of the Political Science Department at Makerere, fast-tracked to professorship by Professor Colin Leys, then head of the department and until recently a professor at York University in Canada.

Kuna mengi ambayo Mazrui ameandika katika vitabu vyake na artcles zake in different scholarly journals and other publications kuhusu Nyerere pamoja na alivyo tofautiana naye kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Ujamaa, one-party system, Tanzania's recognition of Biafra, the East African Community, failure to form an East African federation, na kadhalika. Lakini hajawahi kumlaumu Nyerere kuhusu ukabila na kusema kwamba kuna makabila aliyo yabagua nchini Tanzania na kusema watu wa makabila hayo wasipwe uraisi au madaraka kuwa waziri mkuu. Ingawa walitofautiana ideologically, mengi ambayo Mazrui ameandika na kusema kuhusu Nyerere ni sifa, pamoja na aliposema miaka michache iliyopita:

"The most intellectual of East Africa's Heads of State at the time was Julius K. Nyerere of Tanzania - a true philosopher, president and original thinker. He philosophized about society and socialism, and translated two of Shakespeare's plays into Kiswahili - Julius Caesar and The Merchant of Venice. The Swahili translations were published by Oxford University Press beginning in 1963, the year of Kenya's independence. East Africa had vivacious and scintillating intellectual magazines - such as Transition magazine based in Kampala and East Africa Journal based in Nairobi. Contributors to those magazines were intellectuals from the campuses, from the wider civil society and from the governing class." (Ali A. Mazrui, "Towards Re-Africanizing African Universities: Who Killed Intellectualism in the Post Colonial Era?," In Memoriam:This lecture is dedicated to Dr. C. Odhiambo-Mbai who had invited Mazrui to give it, and who was later tragically assassinated in Nairobi, Kenya, on Sunday, September 14, 2003).

Much as he respected Nyerere as "a superb intellectual," a term he once used in some of his writings to describe Mwalimu, Mazrui would have been among the first people to criticize him if he discriminated against members of some ethnic groups in Tanzania. He probably would not have questioned his credentials as an intellectual. But he would have denounced Nyerere's position. And he may even have described it as a betrayal of intellectualism - for, what kind of intellectual, especially of Nyerere's calibre, would stoop so low and try to justify tribalism and exclusion of the members of some tribes from the highest office in the land?

Mazrui himself has been a victim of racism from both sides - from fellow Africans who contend that he is not really African because of his Arab heritage in spite of the fact that Arabs in Africa are also Africans and he is a product of black African ancestry as well; and from whites and others who have discriminated against him because of his black African and Arab heritage. He would be the last person to condone discrimination by a leader, Mwalimu Nyerere, whom he respected highly. He said even as recently as 2008 that intellectually, he had higher regard for Nyerere than most politicians anywhere in the world. Is this the kind of politician who would discriminate against some of his people or against anybody else?

Mazrui has, of course, also been denounced by other people including fellow Africans for a different reason, although this may be beyond the scope of what we are discussing here. Kuna high-ranking official katika wizara yetu ya mambo ya nchi za nje, who later became an ambassador, ambaye aliniambia mwaka 1972 (in Dar) kwamba: "Mazrui works for the CIA." And he said so emphatically. Aligusia mambo fulani kuhusu Tanzania, serikali ya Makaburu, ukombozi wa nchi za Afrika kusini, na kadhalika, kuthibitisha alichosema. He only seemed to confirm what I had heard before from another highly placed source in Dar. About two years later in 1974, some damning evidence aganst Mazrui about his questionable ties to the CIA surfaced. And years earlier, in the sixties, Nkrumah also had denounced Mazrui along those lines, in fact even in stronger language, when Mazrui was teaching at Makerere.

Mazrui was a student at Columbia University studying for his master's degree in politial science when he first met Nkrumah in New York.

But that is another subject.

Watu wanao sema Nyerere aliwabagua watu wa makabila fulani li wasipate uraisi au uwaziri mkuu wanawapotosha wananchi wengi, hasa wale ambao walikuwa bado hawajazaliwa au ambao walikuwa watoto wadogo enzi ya Nyerere, kuliko sisi tulio kuwepo tangu Nyerere alipokuwa anagombea uhuru miaka ya 1950s. Nakumbuka sana miaka ile. Pia namkumbuka sana Nyerere alipokuwa na umri wa miaka thelathini na kitu tu, akigombea uhuru. Kila alipokuwa anakaribia kuingia mjini, alikuwa anapanda na kusimama nyuma ya Land Rover, watu wakimpungia mikono. Ndiyo ile Land Rover ya Dossa Aziz?

Nyerere had massive support across Tanganyika, later Tanzania. He also embraced everybody. It is an insult to his legacy to say that he did not want a Haya, a Nyakyusa or a Chaga to be president or prime minister of our country.
 
Back
Top Bottom