Mwalimu mkuu apewe mamlaka kuruhusu wanafunzi kukariri darasa

togetherTight

Member
May 21, 2017
99
100
NI KUHUSU WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI KUKARIRI DARASA

Mimi ni mwalimu wa shule ya msingi. Nikiangalia agizo la waziri wa elimu Prof. Ndalichako nabaini lina athari kwa wanafunzi ambao uwezo wao ni wa chini.

Katika muda ambao baadhi ya wilaya katika mikoa mbalimbali imekuwa na sera ya kukaririsha wanafunzi kutokana na uwezo wao kuwa mdogo (hususani shuleni nnapofundisha) utaratibu umekuwa na matokeo mazuri sana.

Kwa miaka zaidi ya mitano mfululizo shule imefanikiwa kupeleka sekondari wahitimu wote.

Hatukuruhusu mwanafunzi kuingia darasa la tatu hadi amejua kusoma, kuandika na kuhesabu kwa viwango vinavyokubalika.

Lakini pia afikapo darasa la sita (kwa kushauriana na wazazi na mwanafunzi)mwanafunzi hukariri darasa la sita kama uwezo wake ni mdogo, waliokariri hupewa uangalizi maalumu kitaaluma ndipo mwaka unaofata huwa katika hali nzuri kitaaluma na kusajiliwa kufanya mtihani wa kuhitimu.

Lakini kwa maagizo ya sasa tunaenda kuwapoteza watoto kadhaa wasipate elimu ya sekondari ambayo ni ya lazima kwa sasa.

Ombi kwa waziri, aangalie upya swala hili ili kunusuru watoto hasa huku vijijini ambako walimu ni sita wanafunzi shule nzima ni mia tisa na kadhaa.

Ilitosha kukaririsha mtoto darasa la sita mara moja ili kumsaidia zaidi.

Sisi ndio tulio nao huku tusikilizwe kuliokoa taifa.

Kama swala ni bajeti basi wizara ishughulike na takwimu za kila darasa jisi lilivyoandikishwa likiwa darasa la kwanza.
 
Mbona utaratibu wa mtoto kukariri upo na rahisi tu
Mwalimu mkuu akipewa rungu atatusumbua sana wazazi, wacha serkali iendelee na taratibu kama zilivyo
 
Back
Top Bottom