Mwali: Mmiliki wa DOWANS ni huyu!

Mwali: Mmiliki wa DOWANS ni huyu!

Status
Not open for further replies.
Siamini kama Nyalandu hamjui mmiliki wa Dowans, anamjua lakini kama alivyosema bro Utingo, yuko kimaslahi zaidi!
 
Bosi wake JK hamjui mmiliki wa Dowans sembuse huyo Nyalandu, msimlaumu sana analinda ugali wake, kama huamini muulize Six na Mwakyembe
 
Sikutarajia jibu la tofauti kutoka kwa Nyalandu,kama Pinda hawezi sema,ni naibu waziri Nyalandu????:lying:
 
Of mice and a sinking ship..........panya akiwa kwenye merikebu hudonoa mbao zake bila kujua kwa kufanya hivyo ataibomoa na kuzama nayo
 
Jamani, Ngeleja ameshawataja. Bado hamtaki kukubali??? Dawa wakurugenzi waitwe waje waseme wamelipa kodi kiasi gani, wamefile annual returns lini, wameitisha mkutano wa mwaka wa wanahisa lini na kama hao wanahisa walihudhuria au walituma proxies. Issue ya kumjua mmiliki ni easy sana basi tu hakuna anayetaka kujua!
 
Jamani tusimuonee Nyalandu, hili swala si yeye tu hata swaiba wake JK hawezi kulijibu. Hii ni tamthilia endelevu haiishi leo, akitajwa hatutaelewa vizuri, tuwe na subira ikifika mwisho kila mtu atajua mmiliki wa Dowans bila kutumia nguvu kama ilivo kwa sasa.
 
Sio kama hamjui. Anamjua sana ila kumsema ndio shida inapoanzia. kwani hapendi kazi yake? kwani hana akili anavyoona wenzake wote (Mawaziri) wanavyokwepa kumtaja. Jk nae anamfahamu fika mmiliki wa Dowans shida ni kuwa ndio aliyemuweka hapo alipo. inaleta hasira sana :frusty::frusty::frusty:
 
Siku nikipata nafasi ya kumuuliza swali kiongozi kama huyo nitasema hivi..... swali langu ni fupi tu, tutajie mmiliki wa Dowans.
akileta ubabaishaji na mbinu za kukwepa swali, nitamwomba ajiuzuru palepale.


Amani yetu inatumiwa vibaya
 
Jamani, Ngeleja ameshawataja. Bado hamtaki kukubali??? Dawa wakurugenzi waitwe waje waseme wamelipa kodi kiasi gani, wamefile annual returns lini, wameitisha mkutano wa mwaka wa wanahisa lini na kama hao wanahisa walihudhuria au walituma proxies. Issue ya kumjua mmiliki ni easy sana basi tu hakuna anayetaka kujua!

Kaka Msando naamini unajua kwa nini swali limeendelea kuwa "wamiliki wa Dowans ni kina nani" ingawa Ngeleja alishataja.
Kama majibu ya Ngeleja yalikuwa sahihi mbona waziri Nyalandu hakum-quote kusema "wamiliki walishatajwa na waziri wa nishati"!

Ukweli serikali inawajua lakini hakuna mwenye ubavu wa kuwataja.
Tatizo lenyewe hata ukiwaja hautakuta legal document yenye majina yao - hao ndipo nia ya kisiasa zaidi inahitajika
 
Wakati Dowans (T) Ltd. inasajiliwa bosi wake Nyalandu ambaye sasa ndiye Waziri wa Viwanda alikuwa Naibu Waziri katika wizara hiyo hiyo. So this guy, Dr. Chami knows the full story on Dowans' registration & the issuing of licence to operate business in Tz. It's very simple, just ask the right guy for the right answers, ya nini kurembaremba? Hebu waandishi habari mahiri watie kiguu ofisini kwa Dr. Chami waje hapa JF na jibu kamili, haya mguu sawa na kwa mwendo wa haraka mbeeelee tembea!
 
Jumatano ya tar.12 nilikuwa safarini kuekekea Mara kwa shughuli fulani ya ofisi. Nilipofika maeneo ya mji mdogo wa Tinde Shinyanga nikawasiliana na ndugu yangu aliyepo chuo cha sayansi ya tiba Bugando.

Akanitaarifu kuwa atakuwa kwny kongamano na naibu waziri wa viwanda na biashara Lazaro Nyalandu kuanzia saa 8 mchana pale Nyanza club.

It was within my schedule kupumzika Mwanza then the day after nielekee Sirari, so haikuwa big deal mimi kujongea pale Nyanza Club kumsikiliza bro.Nyalandu.

Kongamano lilihusisha wanafunzi wa vyuo vinne vya elimu ya juu Mwanza, kikiwemo SAUT, CBE,Bugando na OUT.

Mr.Nyalandu alichelewa kidogo kufika bt baada ya kuhutubia ukafuata utaratibu wa maswali, na Bro.Nyalandu alionekana kuyamudu vema.

Ilipokaribia saa 6:00pm mkuu wa chuo cha CBE ambaye ndiye aliyekuwa anaongoza mjadala akatangaza kuwa huo ndo mwisho wa maswali na akamkaribisha Nyalandu kufunga kongamano.

But badala ya kuaga Nyalandu akatoa nafasi moja ya upendeleo kwa mtu mmoja. Fursa hiyo ikamwangukia kijana mmoja wa SAUT aliyeonekana ana morali kubwa ya kuuliza.

Huku akishangiliwa na ukumbi mzima, na akiongea kwa hisia kijana huyo akamwuliza Nyalandu swali lifuatalo ambalo sina hakika kama nimemnukuu ipasavyo.

Alisema "wewe kama waziri wa viwanda na biashara ni wazi kuwa ofisi ya msajili wa makampuni (BRELA) iko chini yako, na kwa kuwa BRELA ndiye msajili wa makampuni yote nchini, it means ofisi yako pia ina taarifa zote za makampuni yaliyosajiliwa nchini. Kwa mantiki hiyo naomba utueleze leo kuwa ni nani mmiliki wa Dowans, na ilisajiliwa lini nchini?"

swali hilo lilibadili hali ya hewa ya kule ukumbini kutokana na watu wengi kushangilia na kupiga kelele huku wengine wakimbeba muuliza swali.

Baadae Nyalandu akajibu akijaribu kkwepa hoja. Wanafunzi wakapiga keleke "MAJIBUUU",
Then Nyalandu kwa kujitahidi sana akasema "kwa kuwa issue ya Dowans ina wazungumzaji wengine, mimi naomba nisiizungumzie kwa leo, but mniruhusu nijibu maswali mengine. Nitaifuatilia maana kwa sasa sina taarifa za kina."

Nadhami kumjua ama kutomjua sio issue, kwani hata yeye huyo mwanafunzi anaweza akawa hamjui mkuu wa chuo cha SAUT. Issue hapo ilikuwa ni kumwuuliza Naibu Waziri iwapo anashabikia kuilipa Dowans.
 
Siamini kama Nyalandu hamjui mmiliki wa Dowans, anamjua lakini kama alivyosema bro Utingo, yuko kimaslahi zaidi!

Kunguru mwoga hukimbiza bawa lake. Nyalandu hivyo hivyo usije mvisha paka kengele wakafa na wewe
 
Wangemuuliza mmiliki wa kai hotel angejibu mara moja
 
:A S 114: :A S 114: :A S 114:
na mie akuuuuuuuuuu ningekuwa bro shem nyala nisingetaja.ndo kwanza probation ya unaib minister,hata miezi 6 haijaisha
 
Nyalandu huna ubavu wowote wa kujibu hoja hiyo, kula vya mwisho kwani 2015
 
kwa walioendelea unastaafishwa kwa manufaa ya umma, yaani hujui kuhusu kazi yako! Hawa vilaza kweli kweli, tena issue inayozungumzwa sana miaka sasa tena ya mabilioni hujui? Sasa mnajua nini nyinyi watawala maana hamna sifa ya uongozi.

Mkuu,
mi nadhani bwana mdogo sio kwamba hajui, ila aliamua kuzuga tu ili asije akatoa tamko akacontradict wakubwa zake.
 
Nyie Vipi yeye hapendi usalama wa maisha yake na familia yake, tena ndoa yake bado ndiyo haina hata miaka mitatu! mwacheni naye dogo ale. Kwa nini msimuulize Pinda wakati wa maswali ya chapchap akiwa bungeni ili awajibu chap chap nani ni mmiliki wa dowans?

mkuu, mi nadhani bora ajiuzulu ili aende akale vizuri na huyo mkewe (miss TZ wa zamani). Hawezi kujitetea kulinda ndoa kwenye masuala ya msingi kama haya.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom