Mwakyembe asisitiza: Hatukubali TLS kujiingiza katika siasa

Mwakyembe asisitiza: Hatukubali TLS kujiingiza katika siasa

Pigo kubwa kivipi hasa?

Ni nini ambacho atafanya huko TLS ambacho hawezi kufanya/kusema sasa?
TLS kwa muda mrefu wameshindwa hata kutoa matamko ya kulaani ukandamijizani mkubwa wa demokrasia unaoendelea nchini kwetu. Ngoja aje Tundu Lissu
 
TLS kwa muda mrefu wameshindwa hata kutoa matamko ya kulaani ukandamijizani mkubwa wa demokrasia unaoendelea nchini kwetu. Ngoja aje Tundu Lissu
Sasa Tundu Lisu akiwa rais wao ndo atafanya nini ambacho hafanyi sasa hivi katika nafasi alizonazo?

I honestly don't see what fuss is all about with him contesting for the position.
 
Majengo yenyewe bado hajakamilika ujenzi unaendelea sijui walikurupuka walikuwa wanakimbiia wapi?
Mimi habari yote sijaisoma nimeangalia hayo majengo tu, naona kama ni ya UDOM, kwa hiyo wizara inatumia majengo ya UDOM?????!!!!!
 
Sasa Tundu Lisu akiwa rais wao ndo atafanya nini ambacho hafanyi sasa hivi katika nafasi alizonazo?

I honestly don't see what fuss is all about with him contesting for the position.
Subiri baada ya uchaguzi ndo utajua
 
Huyu atakuwa siyo mzima akili ile imemwaribu sana akili
Dr. Mwakyembe jimbo lako la Kyela lina changamoto nyingi sana na sio vimeli ambavyo havina strategy kabisa. Watu hawana maji kabisa vijijinibona una deal na ya TLS tuu??? We mzee toka wakupige mabomu kichwa chako hakina akili kabisa.... Ikonyofu elyoo
 
hii nchi ina wasomi wa hovyo sana, huwa hawaamini walichokisoma.Ndio maana nadharau sana degree za watu wa nchi hii. Ukijiuliza anataka achieve nini huwezi hata jua.Ila msomi anashupaa katika ujinha bila aibu.
Huyu ndo alikuwa mwalimu wa Sheria wa Tundu Lissu amemua kuweka akili pembeni kwa maslahi ya chama
 
Du!!! Kazi ipo hivi society ni kielezi cha nini? Unachosema ni kama chama cha magari sio cha wenye magari. Kwa hiyo magari yanaweza kukutana na kufanya mkutano bila wenye nayo kuhusika!!!!!! Strange indeed!!!!
Mheshimiwa: Kuna tofauti kati ya Law (Sheria) na Lawyer/Advocate (Mwanasheria)
Labda unielimishe. Ni chama gani kingine cha professionals ambacho kimeanzishwa kwa sheria ya Bunge? e.g madaktari, wahandisi na kadhalika? TLS imenzishwa kwa sheria ya Bunge (The Tanganyika Law Society Act)
Kama ni chama cha wanasheria, kwa nini wao waanzishiwe chama kwa sheria ya Bunge? Kwa nini professionals wengine wasianzishiwe vyama vyao kwa sheria za Bunge?
Nitoe tongotongo mheshimiwa
 
My take ==Hayo mamlaka ya kufuta Chama cha Wanasheria Tanganyika Mwakyembe anayatoa wapi?

Wakili msomi Joseph Kinango alisema tamko la Waziri Mwakyembe kuwa ataifuta TLS ni batili na halina mashiko kisheria. Kwa lugha ya kisheria "Its null and void abinitio" yani ni tamko batili hata kabla Mwakyembe hajalitamka. Yani wakati Mwakyembe anafikiria kutamka tayari lilikua batili.
kwanza huyo rais wa hicho chama wa sasa, kaenda kwa huyo mwanasiasa, Mwakyembe, kwakua wote ni wanachama wa chama kimoja, yaani CCM.
inaonekana siasa inakua imeingia kwenye chama cha wanasheria pale tu mwanasheria wa mwenye itikadi za upinzani anapotaka kuongoza chama; ila kama mwanasheria mwenye itikadi za CCM akitaka kuongoza chama, siasa inakua haipo! ajabu ya mwaka.
sasa watapaje kiongozi wa hicho chama cha wanasheria asikua na itikadi za upande wowote wa kisiasa? hata ktk mpira. marefa wanaochezesha simba na yanga, hua ni mahsbiki wa upande fulani, ila kwakua wanaongozwa na sheria, hutenda haki bila upendeleo.
 
Mnasikitisha sana, Bado mko kwenye dunia ya ujima kabisa wasomi wa ccm
Nimeeleza namna sheria zetu zinavyopatikana na zinavyorekebishwa. Hiyo dunia ya ujima inahusikaje hapa?

Tunaonaongelea dhana ya demokrasia ya uwakilishi (represantative democrasy. Sera za chama tawala ndizo hutawala kwa kutungiwa sheria kupitia wawakilishj wa wanainchj yaanj bunge. Chama tawala kinapokuwa na wabunge asilimia 75% kinakuwa hakina kizuizi cha kutekeleza sera zake kwanj hata hiyo katiba ya nchi kinaweza kuibadilisha kitakavyo, sembuse hako kasura ka 307 ka sheria! Jitahidi kufikiri nje ya box rafikj yangu Chakaza.
 
Back
Top Bottom