Mwakyembe asisitiza: Hatukubali TLS kujiingiza katika siasa

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
HATUTAKUBALI TLS KUJIINGIZA KATIKA SIASA-MWAKYEMBE

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Mhe. Dkt Harrisson Mwakyembe amesema Serikali haiwezi kuona Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kinajiingiza katika siasa na kama TLS wanataka hivyo, basi Serikali haitasita kuifuta Sheria ya TLS Sura ya 307 iliyoanzisha chama hicho cha Wanasheria.

DKt Mwakyembe alikuwa akizungumza hayo na ugeni wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) uliokwenda kumtembelea Ofisini kwake mjini Dodoma ukiongozwa na Rais wao Bw. John Seka.

tmp_11503-FB_IMG_1488814653742867370480.jpg
tmp_11503-FB_IMG_14888146583261568903272.jpg
My take ==Hayo mamlaka ya kufuta Chama cha Wanasheria Tanganyika Mwakyembe anayatoa wapi?

Wakili msomi Joseph Kinango alisema tamko la Waziri Mwakyembe kuwa ataifuta TLS ni batili na halina mashiko kisheria. Kwa lugha ya kisheria "Its null and void abinitio" yani ni tamko batili hata kabla Mwakyembe hajalitamka. Yani wakati Mwakyembe anafikiria kutamka tayari lilikua batili.
 
Watatafuta kila sababu ya kuchukua control. Ila ukweli unabaki palepale, wanasheria wakijitambua nchini viongozi wengi watakua kwenye wakati mgumu sana maana wanafanya madudu mengi sasa hivi kinyume cha sheria.
 
Mambo mengine ni haibu kusema yamezungumzwa na mtu mwenye weledi wa kiwango cha PhD,hivi TLS katika muundo was serikali inaingia sehemu gani? Kama ni moja ya taasisi za serikali ndiyo serikali inaweza kutoa maelekezo yake lakini kama ni chama cha wataalamu kama kilivyo chama cha walimu au chama cha wakandarasi basi kunavitu ambavyo serikali ilikuwa inawakandamiza wataalamu wetu was sheria ili wasiweze kuihoji serikali hii ya ccm,
Ningeshauri kama mahakimu wote na mawakili wote ni wanachama was hiki chama basi waonyeshe umoja na mshikamano
 
Wakili msomi Joseph Kinango alisema tamko la Waziri Mwakyembe kuwa ataifuta TLS ni batili na halina mashiko kisheria. Kwa lugha ya kisheria "Its null and void abinitio" yani ni tamko batili hata kabla Mwakyembe hajalitamka. Yani wakati Mwakyembe anafikiria kutamka tayari lilikua batili.
Daaa sheria bhn.. Yaan kabla haijatamkwa tayar ni batili.. Duuuuuuu
 
HATUTAKUBALI TLS KUJIINGIZA KATIKA SIASA-MWAKYEMBE

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Mhe. Dkt Harrisson Mwakyembe amesema Serikali haiwezi kuona Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kinajiingiza katika siasa na kama TLS wanataka hivyo, basi Serikali haitasita kuifuta Sheria ya TLS Sura ya 307 iliyoanzisha chama hicho cha Wanasheria.

DKt Mwakyembe alikuwa akizungumza hayo na ugeni wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) uliokwenda kumtembelea Ofisini kwake mjini Dodoma ukiongozwa na Rais wao Bw. John Seka.View attachment 477476 View attachment 477477
My take ==Hayo mamlaka ya kufuta Chama cha Wanasheria Tanganyika Mwakyembe anayatoa wapi?

Wakili msomi Joseph Kinango alisema tamko la Waziri Mwakyembe kuwa ataifuta TLS ni batili na halina mashiko kisheria. Kwa lugha ya kisheria "Its null and void abinitio" yani ni tamko batili hata kabla Mwakyembe hajalitamka. Yani wakati Mwakyembe anafikiria kutamka tayari lilikua batili.

HAO WALIOENDA KUMTEMBELEA KIPINDI HIKI NAO SIWASOMI, U CAN'T STEP UP WITHOUT GIVEN A CHANCE.
 
Unajua kuna wakati uwa hawa viongozi wetu hawajui wanachofanya...kwa kawaida kwenye hizi association aidha za wafanyakazi au kama hii ya TLS yule anayeogopwa na mamlaka ndio uwa chaguo sahihi. Nadhani wanampigia kampeni Tundu Lissu bila wao kufahamu. Ni ishu ya muda tu, ngoja tusubiri, natabiri Tundu Lissu kushinda kwa kishindo uchaguzi huu wa TLS.
 
HAO WALIOENDA KUMTEMBELEA KIPINDI HIKI NAO SIWASOMI, U CAN'T STEP UP WITHOUT BEING A CHANCE.

Umenena mkuu, hawa nao nadhani wana ajenda yao. Uwezi kumtembelea mtu ambaye ameonyesha kuwa against na taasisi unayoiongoza. Mimi nadhani hawa ndio wanafanya wananchama wa TLS wadhani association yao imekuwa kama kitengo cha serikali vile. This must stop, tunataka TLS itakayosema jambo dunia itetemeke.
 
Back
Top Bottom