Mwakyembe amechoka, apumzishwe!

Mwakyembe amechoka, apumzishwe!

huku nyuma ALITAKA KUFA AKASHINDWA
ALITAKA KUTAJA UHUSIKA WA JK KWENYE RICHMOND AKASHINDWA
ALISEMA ATAMFUNGULIA LOWASA KESI ZA UFISADI AKASHINDWA
ALISEMA ANGEMFUNGA MASOGANGE AKASHINDWA,ALITAKA KUPANUA BANDARI AKASHINDWA,AKATAKA KUBORESHA RELI AKASHIDWA
Really he is a total failure in all circumstances
 
Angekuwa anajitambua, angejiuzulu. Hii ni aibu kubwa sana.
 
Safii sana ndio maana JF ni Home of Great Thinkers. Unajua ki Ukwelii Nime waza na kuwazuka na hasira nyingi sana zikaja, nika ona ngoja nije kwa ndugu zangu wa Jf nao nawasikie ki ukweli mi naona huyo Mwakyembe jamani achunguzwe atakuwa hayupo sawa sawa, yanii haiingii Akiliniii kabisaa Eti Cheti cha kuzaliwa na Ndoa, Hapa kuna relation gani!? Ina maana Cheti ndio nini sasa kwenye ndoa. Ina maana kwamba cheti cha kuzaliwa kinaweza kuwafanya watu wawili walio pendana kwa dhati wasi oane eti kwa sababu mmoja au wote hawana chet cha kuzaliwa!? yanii nashindwa hata ku elezea ni kwa jinsi Ganii hichi kitu haki make Sense. Ngoja niishie tuu hapa kwa maana naweza andika yasiyo na busara kwa Hasira niliyo nayo.
 
Dr mwakyembe ni moja ya vichwa nilivyokuwa navikubali sana pale bungeni hasa kwa uwezo wake wa kujenga hoja na kusimamia kwenye ukweli wakati huo alikuwa mbunge wa kyela. Hali hiyo ilimfanya Rais mstafu Jakaya Mrisho kikwete ampe unaibu waziri baadae uwaziri kamili lakini alipata maswahibu yaliyompelekea kwenda kutibiwa india na mungu akamsaidia akarejea salama nyumbani lakini toka arejee miaka kadhaa iliyopita Dr mwakyembe amekuwa mtu asiyeweza kujenga hoja amekuwa mropokaji wa kwanza nasubutu kusema katika mawaziri waropokaji wa awamu hii ya tano mwakyembe ni mmoja wapo anaongoza kwa kutoa matamko yasiyokuwa na mantiki wala faida kwa serikali. Dr mwakyembe ni mbobezi wa sheria ya katiba (constitutiona law) sambamba na mwenzake prof Issa Shivji lakini mwanasheria huyu amegeuka kituko badala ya ushajaa nikiikumbuka kamati teule aliyoiongoza kwenye richmond nataman kulia ninaposikia akitoa matamko ya ovyo kama vile uwezo wa kufuta TLS, Hamna kufunga ndoa mpk uwe na cheti cha kuzaliwa wakati anajua havihusiani chochote najiuliza ni uwaziri ndo unamwangusha na kuwa hivyo aule ugonjwa umemwasiri maana naweza nikamlaumu mtu kumbe yu mhoma maskini mwakyemba
 
Mwakyembe dish limeyumba na anahitaji msaada wa haraka mno, tena wanataaluma wenzie manake miaka 10 nyuma asingefanya haya itakuwa na laana za Mwakipesile ndio zinampata sasa.

Bado Lukuvi na yeye ukisikia matamko yake utajua anahangaika kumfurahisha bwana mkubwa. Wananchi ni wakati wenu kuweka kumbukumbu ili wakija tena watueleweshe kwanini walilazimisha kutuonea bila sababu.
 
Kiongozi aliepatikana kwa rushwa na dhuluma huwa hajali wananchi wake maana anajua uwepo wake kitengoni hauitaji wananchi
 
Namhuzunikia sana,,, alikuwa jembe sana Mwakyembe lakini lile tamko hata sikuamini kama kweli limetoka kinywani mwake...
Ni dhahiri hafiki jimboni kwake,, kwani angekuwa anajua kama wanajimbo lake ailimia kubwa hawana vyeti vya kuzaliwa na wanaoana
 
Wana bodi,

Umofia kwenu. Namwandikia ndugu yangu DR. Harrison Mwakyembe nikiwa nimetoa macho siamini kama huyu ndiye yule mwanasheria machachari wa enzi za Samuel Sitta (RIP). Kama ni yeye basi nadhani kuna tatizo kubwa kichwani kwake. Kifupi mwanasheria huyu ni mwongo hatakiwa kuaminika tena, kapoteza kila kitu kilichokuwa kinawafanya watanzania wamwamini. Kwa tathmini ya haraka, Dr. Mwakyembe amebakiza kiki moja tu ya kumfanya atengeneze headlines kwenye media nayo ni kumkamata Mange Kimambi... zingine zote kafeli kwa aibu mbaya... Nimeona andiko la Uhamiaji la kumkamata Mange pindi akitua nchini. Mwakyembe unatia aibu sana kaka. Hebu tujikumbushe
1. Wewe na marehenu Sitta (sorry marehemu hatetwi) mlituaminisha ufisadi wa fisadi papa wetu Lowasa kupitia Richmond. Mliimba wimbo huu mkamwambukiza Dr. Slaa na baadae wana Chadema. Kipindi cha uchaguzi uliopita, ukijua kuwa si kweli ulitokea Star TV ukaaminisha watanzania na hata Rais Magufuli kuwa ufisadi wa Lowasa ni kesi ya jinai inapelekwa kortini muda wowote. Rais kaingia kingi, akaanzisha mahakama ya mafisadi na mwishoe imekuwa aibu kubwa. Mwakyembe umepatwa nini kaka yangu? Ni ile sumu? Bado nawaza.

2. Ukiwa msomi mzuri, uliikana tasnifu yako ya sheria kutoka ujerumani kipindi cha uandishi wa katiba mpya. Unastahili kuendelea kuitwa PhD holder? Tasnifu yako ni ipi inayokutambulisha duniani kuhusu udaktari wako? Bado una msimamo wa kisomi uliosimamia wakati wa VIVA au msimamo wako ni huu uliouonyesha kipindi cha bunge la katiba? Au ni ile sumu kaka yangu? umekuaje wewe?

3. Wewe ni mwanasheria, mwanachama wa jumuiya ya mawakili wa Tanganyika, kwa makusudi kabisa umeamua kujitoa akili kidogo uliyobakiwa baada ya bunge la katiba na sasa unawavuruga wenzako. Ni nini kaka yangu kinakusibu? Hivi uchaguzi huu wa TLS unakusumbua nini hadi uonekane mbumbumbu kuliko kina Lusinde? Nini kinakusibu kaka yangu? Ni ile sumu au bashiteism?

4. Umekurupuka kuhusu vyeti vya kuzaliwa kutumika wakati wa kufunga ndoa. Ulilenga kuua mjadala wa TLS ulifeli matokeo yake hata Rais kaamua kukudhalilisha, nini kilichobaki ukajivunia kwa wanao na wana Kyela? Mwakyembe uko salama upstairs au unahitaji msaada kaka yangu?

5. Ukiwa waziri wa Katiba na sheria, ukiwa mwanasheria na mwanahabari, ulikuwa msitari wa mbele kutetea sheria kandamizi inayoua ustawi wa vyombo vya habari bila kujali madhara makubwa kwa jamii pana ya watanzania. Ni ile sumu kaka yangu au kuna kingine?

Mwisho, nakuona umebakiwa na silaha moja tu ili uendelee kuwa kwenye game hii. Nayo ni kujitoa kifua kwa kiki ya kumsaka na kumkamata Mange Kimambi. Hii pekee ndo wafuwasi wako watakuona bado una uwezo ambao hauna. Ila hii kiki ukiitumia ndo inakwenda kukupoteza kabisa na hatimaye nafasi yako atapewa Lusinde Kibajaji. Tunakuombea urudiwe na akili yako ya kawaida otherwise ushaanguka kaka.
 
Mashaka yangu juu yake yalianza pale alipokuwa akimnadi yule mmarekani Robert Shumake kwamba angewekeza kwenye treni ya kutoka airport hadi mjini (Dar) huku akisema "yule baba ana helaaaa". Kumbe tapeli tu.
 
Kwa mwezi huu dr waziri wa Sheri's amefanya haya.

1.LISU ASIWE MGOMBEA WA TLS...AKASHINDWA.

2.AKATAKA KAFUTA CHAMA WA WANASHERIA TANGANYIKA...AMESHINDWA.

3.AKATAKA UCHAGUZI UAIRISHWE WA TLS... AKASHINDWA.

4.AKAPELEKA KESI MAHAKAMANI KUBADILI VIFUNGU VYA TLS...AKASHINDWA.

5.AKATAKA WATU WASIOE BILA VYETI VYA KUZALIWA...AKASHINDWA....

HUYU NDIO WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA NCHINI VYETANAM!!!


Mkuu,

SIKU YA KUFA NYANI MITI YOTE HUTELEZA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom