Mwakyembe amechoka, apumzishwe!

Mwakyembe amechoka, apumzishwe!

Tangu apate ugonjwa wa kukoboka ngozi na akili ilikoboka by the way kama aliweza kukana chapisho lilompa PHD unadhani kuna mtu hapo? Mwakyembe ukiona alivyokuwa anajinyenyekesha pale ikulu kila akitajwa kasimama na kutoa ishara ya utiifu kwa kuinama kitu ambacho wenzake walikuwa hawafanyi ndio nilijua bado sumu iko mwilini
 
Baada ya kutenguliwa kwa aliyekuwa waziri wa sanaa, habari na michezo mbunge Nape Nauye,
Mh rais alimteua Dr Harison Mwakyembe kuchukua nafasi aliyokuwa anaitumikia Nape na sasa yeye ndio waziri mwenye dhamana ya sanaa, habari na michezo

Ukweli mchungu, rais aliteleza kwa uteuzi wa mwakyembe!
Mwakyembe huijui na huiwezi wizara hii
Kwa rasilimali watu waliobaki ndani ya CCM ni Ridhiwani Kikwete tu ndiye mwenye kuweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi akipewa wizara hii

Mh rais tengua uteuz huu tupe Ridhiwan hapa yeye ataifanikisha wizara hii

Ridhi ni kijana, mwanahabari, mwanamichezo na sanaa pia hayuko mbali nayo so itamfaa sana
Sijui ulitumia vigezo gani kumpa mwakyembe wizara hii ilihali kijana huyu ndio ofis inayomfaa kwa sasa
 
Yaani Mwakyembe kama sio unafiki na tamaa ya madaraka hii wizara angeomba tu apewe mwingine yaani kwa umri, hadhi na elimu yake hapo ni kama wamemdump mbaya yeye mwenyewe hajielewi.
 
Mwakyembe keshaanza gusa maslah ya watu hapa.

Mkuu shukuru alitolewa ile wizara inayohusu mambo ya sheria maana saiv kiki ingekua kubwa mno na kesi mahakamani. Kumfukuza waziri wa masuala ya sheria ndani ya chama cha wanasheria unadhan lingekua jambo dogo lile
 
Yaani Mwakyembe kama sio unafiki na tamaa ya madaraka hii wizara angeomba tu apewe mwingine yaani kwa umri, hadhi na elimu yake hapo ni kama wamemdump mbaya yeye mwenyewe hajielewi.
Hayo ni maoni yako baada ya kuona anafanya kazi kinyume na matamanio yako
Mwakyembe anafanya vizuri kuliko wengi tulivyofikiri,mpaka sasa ameweza kumudu majukumu yake kwenye michezo,sanaa na habari kwa 100%
 
jamii forum inabdi muongezi vitu kadhaa,kuwe na dislike (iwe dole la kati) na hata kuzomea ooohh ili watu kama waziri wawe wanakutana na hzi wanapo fanya mambo za kiboya kama haya..nimejikuta nikisoma mambo ya nchi yetu sasahvi natamani kutukana tu kwanzia bashite------->mkulu
 
MWAKYEMBE AMECHOKA, APUMZIKE/APUMZISHWE.!

By Malisa Godlisten

Jana nilipoona agizo la Waziri Mwakyembe kuwa hakuna mtu ataruhusiwa kufunga ndoa bila cheti cha kuzaliwa nilimpuuza kwa sababu haikua mara yake ya kwanza kutoa kauli za kustaajabisha. Rafiki yangu mmoja alinitania kuwa natarajia kufunga ndoa, je nina cheti cha kuzaliwa?

Nilisema tu kwa kifupi kuwa wendawazimu pekee ndio wanaopaswa kuelewa agizo hilo. Sio kwa sababu "nimebashite" cheti cha kuzaliwa ila kwa sababu agizo hilo ni batili na halina maana. Hata kama watanzania wote wangekua na vyeti vya kuzaliwa bado ningepinga agizo hilo.

[HASHTAG]#Mosi[/HASHTAG]; agizo hilo ni kinyume cha sheria. Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kifungu cha 9 hadi 24 inaeleza kitu kinachoitwa MASHARTI ya ndoa (Preliminaries to Marriage &Restrictions on Marriage). Masharti yanayoelekezwa na sheria hiyo ni pamoja na:

-Umri (miaka 18 au zaidi, kwa mwanamke chini ya 18 apate idhini ya wazazi)
-Utimamu wa akili (asiwepo mgonjwa wa akili kati ya muoaji/muolewaji au wote)
-Hiyari (asiwepo anayelazimishwa, kila mmoja aridhie)
-Kutangaza ndoa (wanaotaka kufunga ndoa wanapaswa kuandikisha mbele ya msajili wa ndoa walau siku 21 kabla ya tarehe ya ndoa)
-Ruhusa ya kupunguza siku hizo 21 inapatikana kwa Msajili Mkuu wa Tanzania, kwa kujaza fomu ya pekee, kutoa sababu ya haraka, na kulipa ada maalumu. Wasajili wadogo hawawezi kutoa ruhusa hiyo
-Kuwa na wadhamini wawili wa ndoa.

Hayo ndio masharti ya ndoa. Ukisoma masharti hayo hakuna mahali sheria imehitaji cheti cha kuzaliwa. Sasa Mwakyembe ametoa wapi hili agizo? Ameota usiku? Ameshauriwa na mkewe? Amepata wapi? Kutoa agizo ambalo ni kinyume na sheria, ni kuvunja sheria. Na sheria inapovunjwa na Waziri wa sheria ni aibu zaidi.

[HASHTAG]#Pili[/HASHTAG]: Kuna watu wanamtetea Mwakyembe kuwa cheti cha kuzaliwa kinapatikana kirahisi. Yani hakuna sababu ya kulalamika kwa kuwa eti ni rahisi kupata cheti cha kuzaliwa. Kiongozi mmoja wa kisiasa akawashangaa watanzania jana akasema watanzania wamezoea kulalamika badala ya kwenda RITA wakachukue vyeti. Yani yeye hakuona ubatili wa agizo la Mwakyembe, alichoona ni urahisi wa kupata cheti pale RITA.

Labda kumsaidia kiongozi huyu na wengine wenye mawazo kama yake, niwaambie tu kwamba hoja sio urahisi wa kupata cheti cha kuzaliwa, hoja ni kwamba agizo la Waziri ni batili na halina mashiko kisheria (null and void abinitio). Sheria ya ndoa haielezi cheti cha kuzaliwa kuwa moja ya requirements za kuoa/kuolewa.

Hatuwezi kuruhusu viongozi watoe matamko ya hovyohovyo ambayo ni kinyume na sheria kwa sababu tu hivyo wanavyovitolea maagizo ni rahisi kupatikana. Itafika mahali watasema watu wasio na kadi za CCM wasipate huduma za afya, na tutaunga mkono kisa tu kadi za CCM zinapatikana kirahisi. Hii sio sawa hata kidogo.!

[HASHTAG]#Tatu[/HASHTAG]: Logic ya cheti cha kuzaliwa ni nini? Yani kuna uhusiano gani kati ya cheti cha kuzaliwa na kufunga ndoa? Kwamba Mwakyembe alitaka kupima nini? Uraia au? Umri? Ukoo? Intention yake nini?

Kama ni uraia, je watu wasio raia hawaruhusiwi kufunga ndoa nchini? Kama wanaruhusiwa, hili agizo lina maana gani? Ninachofahamu ni kuwa kama mtu si raia hakatazwi kufunga ndoa hapa nchini, kama ambavyo watanzania wanaoishi nje ya nchi hawakatazwi kufunga ndoa huko walipo.

Mtu kufunga ndoa Tanzania hakumfanyi kuwa raia wa Tanzania. Na mtanzania aliyeko nje ya nchi kufunga ndoa huko, hakumfanyi kupoteza uraia wake. Sasa kama ndio hivyo logic ya cheti cha kuzaliwa inatoka wapi? Mwakyembe amekula maharage ya wapi?

[HASHTAG]#Mwisho[/HASHTAG]; nimpongeze Rais JPM kwa kufuta agizo hili la "kijinga" ambalo ni kinyume cha sheria. Lakini ni vizuri akampumzisha kazi Dr.Mwakyembe maana ameonesha kuchoka. Kauli zake za siku hizi zimedhihirisha kwamba he is not smart as he used to be. So ni busara ampumzishe tu.

But pia kwa kuwa Mheshimiwa Rais amedhihirisha kwamba anazisikia kelele zetu na anachukua hatua, ni vizuri asikie pia kelele za Bashite na achukue hatua. Haiwezekani kelele za siku moja za vyeti vya kuzaliwa amezisikia na kuchukua hatua, lakini kelele za mwezi mzima kuhusu Bashite hajazisikia. Tafadhali Mheshimiwa Rais chukua hatua na la Bashite pia. Hii itakujengea heshima na kufanya watu waone hauna double stsndards.!

Malisa Godlisten
Ahsante Mkuu, umesaidia Taifa.

MY TAKE:
Sina shaka na elimu ya Mwakyembe..... Nimekuwa nikiyatafakari matamko yake siku hizi nikilinganisha na elimu yake.. Haeleweki kabisa.

Nimeridhika, PASIPO SHAKA; He has absolutely reached the point of retardation...

Hakuna wa kuweza kuidhibiti hali hiyo, hata yeye mwenyewe hawezi.

Kwa hiyo ni wakati muafaka asaidiwe ili kuepusha jambo baya analoweza kulisababisha kutokana na hali aliyofikia.

Kumsaidia ni kumpumzisha..
 
Nimesikitika sana, vitisho anavyo wapa wasanii, eti hakuna msanii aliyefanikiwa kwa kuikosoa serikali.

Fine, Swali la kujiuliza ni nchi ngapi zimepata ukombozi kwa kupitia wasanii. Lugha unayotumia mwakyembe hata wakoloni walitumia lugha kama hiyo na unavyo sema wataishia pabaya sishangai kwani hata wasanii walitusaidia kupata Uhuru walikaa ndani.

Mfano mzuri ni wasanii wa Africa kusini , walivyo changia kupata Uhuru kamili kutoka kwa makaburu.

Wasanii hatutishwi, tunajua tupo kazini, tunajenga nchi yenye usawa na unayo fuata misingi ya haki na sheria.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom