Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
MWAKYEMBE AMECHOKA, APUMZIKE/APUMZISHWE.!
By Malisa Godlisten
Jana nilipoona agizo la Waziri Mwakyembe kuwa hakuna mtu ataruhusiwa kufunga ndoa bila cheti cha kuzaliwa nilimpuuza kwa sababu haikua mara yake ya kwanza kutoa kauli za kustaajabisha. Rafiki yangu mmoja alinitania kuwa natarajia kufunga ndoa, je nina cheti cha kuzaliwa?
Nilisema tu kwa kifupi kuwa wendawazimu pekee ndio wanaopaswa kuelewa agizo hilo. Sio kwa sababu "nimebashite" cheti cha kuzaliwa ila kwa sababu agizo hilo ni batili na halina maana. Hata kama watanzania wote wangekua na vyeti vya kuzaliwa bado ningepinga agizo hilo.
[HASHTAG]#Mosi[/HASHTAG]; agizo hilo ni kinyume cha sheria. Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kifungu cha 9 hadi 24 inaeleza kitu kinachoitwa MASHARTI ya ndoa (Preliminaries to Marriage &Restrictions on Marriage). Masharti yanayoelekezwa na sheria hiyo ni pamoja na:
-Umri (miaka 18 au zaidi, kwa mwanamke chini ya 18 apate idhini ya wazazi)
-Utimamu wa akili (asiwepo mgonjwa wa akili kati ya muoaji/muolewaji au wote)
-Hiyari (asiwepo anayelazimishwa, kila mmoja aridhie)
-Kutangaza ndoa (wanaotaka kufunga ndoa wanapaswa kuandikisha mbele ya msajili wa ndoa walau siku 21 kabla ya tarehe ya ndoa)
-Ruhusa ya kupunguza siku hizo 21 inapatikana kwa Msajili Mkuu wa Tanzania, kwa kujaza fomu ya pekee, kutoa sababu ya haraka, na kulipa ada maalumu. Wasajili wadogo hawawezi kutoa ruhusa hiyo
-Kuwa na wadhamini wawili wa ndoa.
Hayo ndio masharti ya ndoa. Ukisoma masharti hayo hakuna mahali sheria imehitaji cheti cha kuzaliwa. Sasa Mwakyembe ametoa wapi hili agizo? Ameota usiku? Ameshauriwa na mkewe? Amepata wapi? Kutoa agizo ambalo ni kinyume na sheria, ni kuvunja sheria. Na sheria inapovunjwa na Waziri wa sheria ni aibu zaidi.
[HASHTAG]#Pili[/HASHTAG]: Kuna watu wanamtetea Mwakyembe kuwa cheti cha kuzaliwa kinapatikana kirahisi. Yani hakuna sababu ya kulalamika kwa kuwa eti ni rahisi kupata cheti cha kuzaliwa. Kiongozi mmoja wa kisiasa akawashangaa watanzania jana akasema watanzania wamezoea kulalamika badala ya kwenda RITA wakachukue vyeti. Yani yeye hakuona ubatili wa agizo la Mwakyembe, alichoona ni urahisi wa kupata cheti pale RITA.
Labda kumsaidia kiongozi huyu na wengine wenye mawazo kama yake, niwaambie tu kwamba hoja sio urahisi wa kupata cheti cha kuzaliwa, hoja ni kwamba agizo la Waziri ni batili na halina mashiko kisheria (null and void abinitio). Sheria ya ndoa haielezi cheti cha kuzaliwa kuwa moja ya requirements za kuoa/kuolewa.
Hatuwezi kuruhusu viongozi watoe matamko ya hovyohovyo ambayo ni kinyume na sheria kwa sababu tu hivyo wanavyovitolea maagizo ni rahisi kupatikana. Itafika mahali watasema watu wasio na kadi za CCM wasipate huduma za afya, na tutaunga mkono kisa tu kadi za CCM zinapatikana kirahisi. Hii sio sawa hata kidogo.!
[HASHTAG]#Tatu[/HASHTAG]: Logic ya cheti cha kuzaliwa ni nini? Yani kuna uhusiano gani kati ya cheti cha kuzaliwa na kufunga ndoa? Kwamba Mwakyembe alitaka kupima nini? Uraia au? Umri? Ukoo? Intention yake nini?
Kama ni uraia, je watu wasio raia hawaruhusiwi kufunga ndoa nchini? Kama wanaruhusiwa, hili agizo lina maana gani? Ninachofahamu ni kuwa kama mtu si raia hakatazwi kufunga ndoa hapa nchini, kama ambavyo watanzania wanaoishi nje ya nchi hawakatazwi kufunga ndoa huko walipo.
Mtu kufunga ndoa Tanzania hakumfanyi kuwa raia wa Tanzania. Na mtanzania aliyeko nje ya nchi kufunga ndoa huko, hakumfanyi kupoteza uraia wake. Sasa kama ndio hivyo logic ya cheti cha kuzaliwa inatoka wapi? Mwakyembe amekula maharage ya wapi?
[HASHTAG]#Mwisho[/HASHTAG]; nimpongeze Rais JPM kwa kufuta agizo hili la "kijinga" ambalo ni kinyume cha sheria. Lakini ni vizuri akampumzisha kazi Dr.Mwakyembe maana ameonesha kuchoka. Kauli zake za siku hizi zimedhihirisha kwamba he is not smart as he used to be. So ni busara ampumzishe tu.
But pia kwa kuwa Mheshimiwa Rais amedhihirisha kwamba anazisikia kelele zetu na anachukua hatua, ni vizuri asikie pia kelele za Bashite na achukue hatua. Haiwezekani kelele za siku moja za vyeti vya kuzaliwa amezisikia na kuchukua hatua, lakini kelele za mwezi mzima kuhusu Bashite hajazisikia. Tafadhali Mheshimiwa Rais chukua hatua na la Bashite pia. Hii itakujengea heshima na kufanya watu waone hauna double stsndards.!
Malisa Godlisten