Mwakyembe amechoka, apumzishwe!

Mwakyembe amechoka, apumzishwe!

Waziri wa sheria anavunja sheria Kwa kutoa matamko binafsi halafu anabaki ofisini? Mimi sijaridhika na tamko la Rais Mwakyembe hatoshi kwenye hii ofisi
 
Una PhD ya Sheria, Unatoa tamko la Kisheria, alafu linatengukiwa na Mtu Mwenye PhD ya Chemistry, Bado huamini Dunia ni Uwanja wa Fujo?...totally madness hii Jamani..ya karne
 
Baada ya tamko la mh waziri wa sheria kuna tetesi kuwa Serikali ilikuwa inaenda kufanya uhakiki wa Vyeti vya kuzaliwa vs vyeti vya ndoa.

Tunashukuru Mh. Raisi amebadilisha nadhani tumepewa muda wa kutubu sisi wakinanii majina yetu yanaenda yanabadilika Kuzaliwa, s/msingi Mpaka chuo.
 
Nilipomsikia nilijiuliza yafuatayo

1,Amefuta ndoa za kimila?
2,Yeye binafsi alipata cheti cha kuzaliwa akiwa na umri gani?
3,Wapiga kura wake ni wangapi wana vyeti vya kuzaliwa?
4,Amepima matokeo ya zuio lake?
 
Kwa mwezi huu dr Mwakyembe amefanya haya machache tuu.
Kwa msisitizo naandika kwa herufi kubwa

LISU ASIWE MGOMBEA WA TLS...AKASHINDWA.

AKATAKA KAFUTA CHAMA WA WANASHERIA TANGANYIKA...AMESHINDWA.

AKATAKA UCHAGUZI UAIRISHWE AKASHINDWA.

AKAPELEKA KESI MAHAKAMANI KUBADILI VIFUNGU VYA TLS...AKASHINDWA.

AKATAKA WATU WASIOE BILA VYETI VYA KUZALIWA...AKASHINDWA....HUYU NDIO WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA.

Kwa ushauri tuu Dr. Mwakyembe jimbo la Kyela lina changamoto nyingi ikiwemo kijiji chenu cha Ikolo hakuna hata lami ka deal nazo hizo issues na sio TLS babaa. Kama sumu haijakutoka kichwani urudishwe India tena.

MWAFWAAAA
Umefanya nikumbuke mbali sana na nikisikia vijiji vya ikolo, ngonga, bujonde,katumbasongwe,butangali,kilwa. Alafu namuona huyu mzee anaongea pumba mjini huku natamani nipewe mamlaka ya mungu leo hii maana katelekeza hivo vijij vina hali mbaya sana hawana maji salama ya kunywa kama miaka 25 sasa lakin eti huku dar anasifiwa poor mnyaki mwenzangu
 
Salaam brothers and sisters

muungwana akitoa tamko lisilofaa na mkuu wake akalifuta kwa kukosa nguvu kisheria, muungwana anapaswa kuwa muungwana kwa kuomba radhi.

Huo ndio uungwana. Ama sivyo mkuu atakuwa anateseka kutoa ufafanuzi kwa watu anaotegemea kuwa ni waungwana. Kuomba radhi sio kujishusha hadhi. Ni unyenyekevu. Unyenyekevu ni siri ya mafanikio.
 
aombe radhi kwa kosa lipi??
kutoa tamko lililotenguliwa?
kukosa umahiri wa kutunga matamko pendezeshi??
kutomshirikisha mwajiri wake kabla ya kutakallam mbele ya umati wa umma??
au kwa lipi??
 
Alijijengea heshima katika awamu ya nne, kwa awamu hii kila siku anadhalilika lakini bado hajiuzulu.
Njaa au uroho wa madaraka? Naamini elimu yake na cheti PHd havitendei haki
 
Mwakyembe wa Siku hizi sio yule wa Mbwembwe za kusoma maoni ya tume ya Richmond. Huyu ni wa kulalamikaa na kuweka picha ya Masogange kwenye IPad take.
Huyu anaeaminisha watu kwamba alihamishwa Wizara si kwa utendaji mbovu na kununua behewa feki bali madawa.
Huyu anaetishia kufuta TLS kwa wivu kwa Lissu.
Ndio aliyeaibika kwa Rais kufuta tamko lake la ajabu la vyeti vya kuzaliwa ambacho hata watu wake Kyela hawana
 
1. Kajifaragua kuwa msiri wake aliyempatia taarifa za usafirishaji wa madawa alifanyiwa fitna, akakamatwa na kufungwa, naye ameshindwa kumtoa. Hayo ni mapungufu ya kiongozi ambaye anaituhumu serikali aliyomo kuwa haitendi haki.

2. Katishia kuifuta TLS endapo itachagua viongozi "wanasiasa" lakini kwa mtizamo wake ni wana CDM.

3. Katangaza sera ya kutopewa cheti cha ndoa kwa wale wasio na vyeti vya kuzaliwa. (Sijui kajitungia ama kachomekewa), Mkulu kachomoa!

Haya matatu haya, yanaweza gharimu mtu, japo simuombei vibaya!
 
Mwakyembe huyu huyu mtaalam wa 'politics of the stomachs'?
 
Ile list ya wale waliomeandama Lowassa juu ya Richmond ni yeye peke yake amebakia.....alishamsafishia mr njia sasa kazi yake kwisha..
 
Kwa mwezi huu dr Mwakyembe amefanya haya machache tuu.
Kwa msisitizo naandika kwa herufi kubwa

LISU ASIWE MGOMBEA WA TLS...AKASHINDWA.

AKATAKA KAFUTA CHAMA WA WANASHERIA TANGANYIKA...AMESHINDWA.

AKATAKA UCHAGUZI UAIRISHWE AKASHINDWA.

AKAPELEKA KESI MAHAKAMANI KUBADILI VIFUNGU VYA TLS...AKASHINDWA.

AKATAKA WATU WASIOE BILA VYETI VYA KUZALIWA...AKASHINDWA....HUYU NDIO WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA.

Kwa ushauri tuu Dr. Mwakyembe jimbo la Kyela lina changamoto nyingi ikiwemo kijiji chenu cha Ikolo hakuna hata lami ka deal nazo hizo issues na sio TLS babaa. Kama sumu haijakutoka kichwani urudishwe India tena.

MWAFWAAAA
Umenifurahisha sana,Leo nimefungua sabato kwa furaha zaidi,umeongea point tupu
 
Kwa mwezi huu dr Mwakyembe amefanya haya machache tuu.
Kwa msisitizo naandika kwa herufi kubwa

LISU ASIWE MGOMBEA WA TLS...AKASHINDWA.

AKATAKA KAFUTA CHAMA WA WANASHERIA TANGANYIKA...AMESHINDWA.

AKATAKA UCHAGUZI UAIRISHWE AKASHINDWA.

AKAPELEKA KESI MAHAKAMANI KUBADILI VIFUNGU VYA TLS...AKASHINDWA.

AKATAKA WATU WASIOE BILA VYETI VYA KUZALIWA...AKASHINDWA....HUYU NDIO WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA.

Kwa ushauri tuu Dr. Mwakyembe jimbo la Kyela lina changamoto nyingi ikiwemo kijiji chenu cha Ikolo hakuna hata lami ka deal nazo hizo issues na sio TLS babaa. Kama sumu haijakutoka kichwani urudishwe India tena.

MWAFWAAAA
Ndugu yetu Msomi (our Learned Colleague), hujachelewa. Be bold enough to tender your resignation since you have failed miserably in all the things that you have been fighting for. Do so while there is still time.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom