NANDERA
JF-Expert Member
- Mar 18, 2014
- 2,023
- 2,492
Na hawa wanaume ambao wana kipato kizuri, si mashoga wala mahanithi hawaoi kwa nini? tatizo ni wao au wanawake? Iko kama lawama zote tunazipeleka kwenye uchumi. Vipi kuhusu saikolojia? Mi naona kuporomoka kwa maadili kumefanya taasisi ya ndoa kuwa ya kutisha, na pia vijana wamekuwa wakijiingiza kwenye mahusiano mengi na kuumia mapema kabla ya ndoa. Matokeo yake nafsi za vijana wengi wa kike na wa kiume zina majeraha kwa hiyo hawaaminiani. Kila mmoja anajaribu kulinda nafsi yake isiumie.Watu wenyewe hao hao wanaojazana kwenye hii mikutano na makanisani ndio hao hao wanaokwenda kwenye clubs na kucheza ule wimbo wa "no romance without finance, you gotta have a J. O.B, if you wanna be with me, no romance without finance".
Halafu wanaume wakijiangalia wengi hawana ajira, hata wenye ajira wengine hazieleweki.
Halafu badala ya kutatua matatizo ya kiuchumi na kijamii, tunajikita kwenye kuomba mungu zaidi.
Ndiyo maana nikasema desperate people do desperate things.
Pia wanawake wengi kuwa na elimu na kipato kumepunguza kiherehere cha kuolewa kwa sababu wanawake wengi walikuwa wakiolewa ili kupata hifadhi ya kiuchumi. Hata sasa bado wanawake wengi wanategemea kuolewa kama njia ya kutoka kimaisha. Hawa sasa ndo wanapata shida sana maana kutokana na hali ya kiuchumi ilivyo wanaume wengi ni pangu pakavu. Wenye vipato vya uhakika ni wachache na wanawake wanaovitolea macho ni wengi. Hii imeleta shida sana hata kwenye ndoa kwani wanaume wenye vipato waliooa wanavutwa nje ya ndoa na wanawake wengine wanaotaka fedha zao. Wanawake wenye fedha nao wanavuta wanaume wasio na vipato wenye ndoa na wasio na ndoa. Vicious cycle sijui of poverty au kitu gani!!
Kwa hiyo pande zote mbili zina matatizo ila wanaume huona ni udhalili kukiri matatizo yao na badala yake huya-project kwa wanawake. Kama wanawake hawaolewi na kutokuolewa ni tatizo ina maana kwa kiwango hicho hicho na wanaume nao wanapata shida akiwemo mleta mada.
Mafundisho ya mwalimu Mwakasege kuhusu athari za viapo kwenye mahusiano mi naona mengi ni mambo yanayoelezeka hata kwa saikolojia ya kawaida. Mtu aliyefiwa na mwenzi hupata ugumu wa kuoa au kuolewa tena kutokana na mazoea ya mwanzo au majeraha. Vivyo hivyo kwa wachumba na marafiki. Maombi yanaweza kuwa tiba kwa anayeamini, mwingine anaweza kuanza therapy kwa mshauri, mwingine anaweza kujisaidia mwenyewe. Inategemea mtu anaangalia tatizo kutoka pembe gani. Tatizo moja mwingine ataliona ni la kiroho atatumia maombi, mwingine ataliona ni la kisaikolojia atatumia therapy. Mtu akiambiwa "wewe hupati mchumba kwa sababu ya kiapo chako na ex-boyfriend au marehemu mwenza wako" na akaamini katika maombi akavunja kiapo ina maana ataondoa ile negative energy iliyokuwa inamfanya asiweze kuanzisha mahusiano mapya. Pia ile imani kuwa sasa yuko huru inampa motisha hata ya kutabasamu na kuanza kuona wanaume au wanawake kwa attitude mpya.
Halafu kwa uzoefu wangu kutoka kwa jamii yangu ya kijijini na mjini familia nyingi zinatunzwa na wanawake. Wanaume wana haki miliki ya mali lakini walisha familia ni kina mama. Hii sasa inataka kuwa trend mijini hata kwa ndoa ambazo mke na mume wanaingiza vipato. Wanawake wengi walioko kwenye hizi ndoa hawana furaha ila jina la Mrs linawafanya wavumilie. Wengi pia wanaonea watoto wao huruma kwa hiyo walau watoto wanashikila ndoa. Usawa unaelekea kuwa usaha maana kuna waume wanauliza wake zao wanapeleka wapi hela na wake nao wanaouliza wanaume wanapeleka wapi hela wanazidi kuongezeka.
Mi nawashauri kina dada watafute vipato, wajitambue ili wawe huru kihisia, kifedha na kimawazo ndo watafute wachumba.