Mwaka unaisha ila tujikumbushe sasa

Mwaka unaisha ila tujikumbushe sasa

Lunyungu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Posts
8,873
Reaction score
1,919
Wana JF
Waandishi wetu na nadhani hata sisi wananchi tumekuwa na tabia ya kusahau mambo baada ya kuanza kwa ushabiki.Na muda mwingi mambo serious huwa tunayapa ushabiki mkubwa na mambo ya kijinga tunayapa uzito wa hali ya juu .Mimi naomba tukikumbushe mambo haya 2 na kama nawe una lako ongeza kwenye orodha tuone tunamalizaje mwaka na yana status gani popote yaliko .

1.Msemakweli na walio foji vyeti vya Elimu ya juu .
Alisema na aka andika kitabu kwa uwazi.Nikasikia wahusika wanasema wanaenda mahakamani .Lakini hata leo hakuna aliye enda kudai haki ya kuchafuliwa .Na watu hawa bado wana heshima kubwa kwenye jamii hata baada ya dhambi kubwa hiyo waliyo ifanyia jamii .Je unaweza kuniambia kwa nini hawakwenda mahakamani kudai kusafishwa majina wakiwa na ushahidi wa Elimu zao ?

2.Kesi ya Rizwan dhidi ya Slaa na Mtikila nayo imeishia wapi na kuna lolote linaendelea ?

naomab kuwasilisha

Angalizo: Kwa wale wasio kuwa wachambuzi na majibu ya kistaarabu tafadhali piteni tu waache wenye nia ya mijadala kwa faida ya wengi waseme .
 
ushahidi wa david kafulila kuwa zambi(ccm) na mwenzake(mbunge wa ccm simkumbuki) waliomba rushwa kwa wakurugenzi wakati kamati ya bunge ya serikali za mitaa ilipokuwa inakagua halmashauri mbalimbali....makinda kapiga kimya mpaka kafulila kafukuzwa uanachama nccr.
nafikiri wanataka lema ashindwe kesi ya ubunge..
 
Kauli ya utata toka kwa Pinda kuwa Zanzibar sio nchi, wenzie wakamzima kwa kuweka kipengele hicho kwenye Katiaba yao baada ya mabadiliko ya kumi.
 
Wana JF
Waandishi wetu na nadhani hata sisi wananchi tumekuwa na tabia ya kusahau mambo baada ya kuanza kwa ushabiki.Na muda mwingi mambo serious huwa tunayapa ushabiki mkubwa na mambo ya kijinga tunayapa uzito wa hali ya juu .Mimi naomba tukikumbushe mambo haya 2 na kama nawe una lako ongeza kwenye orodha tuone tunamalizaje mwaka na yana status gani popote yaliko .

1.Msemakweli na walio foji vyeti vya Elimu ya juu .
Alisema na aka andika kitabu kwa uwazi.Nikasikia wahusika wanasema wanaenda mahakamani .Lakini hata leo hakuna aliye enda kudai haki ya kuchafuliwa .Na watu hawa bado wana heshima kubwa kwenye jamii hata baada ya dhambi kubwa hiyo waliyo ifanyia jamii .Je unaweza kuniambia kwa nini hawakwenda mahakamani kudai kusafishwa majina wakiwa na ushahidi wa Elimu zao ?

2.Kesi ya Rizwan dhidi ya Slaa na Mtikila nayo imeishia wapi na kuna lolote linaendelea ?

naomab kuwasilisha

Angalizo: Kwa wale wasio kuwa wachambuzi na majibu ya kistaarabu tafadhali piteni tu waache wenye nia ya mijadala kwa faida ya wengi waseme .

malipo ya dowans, kuuzwa kwake, jairo kuomba rushwa na kusafishwa,makinda kutangaza posho mpya .........
 
Baada ya milipuko ya mabumu mbagala JK alitoa ahadi kuwa hakutatokea milipuko tena TZ lakini baada ya muda yakalipuka mabomu mengine gongo la mboto.
 
Edward Lowasa alishauri kukaa meza ya makubaliano baina ya CCM na CDM kwenye sakata la meya arusha ili kuepusha ghasia lakini ushauri huu ulipingwa na Mzee Makamba tena kwa kejeli na majigambo na matokeo yake watu watatu wakapoteza maisha Arusha ktk ghasia zilizotabiriwa na Lowasa kuhusiana na sakata hilo meya wa arusha.
 
Ifikapo Dec 2011 mgawo wa umeme utakua historia na umeme wa ziada tutauza nje
 
Unadhani watawala wetu wana akili timamu kweli au wao hutuona sisi wananchi majuha ?
 
Ahadi ya Kigoma kuwa Dubai ya Africa.
 
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Misenyi
Bajaji 400 za wajawazito
Kamanda Lema kukaa gereza la Kisongo kwa siku 14
David Jairo
Rais wetu mpendwa na safari za nje zisijoisha
Rais wetu mpendwa na matatizo ya kuanguka hovyo
Kafulila kuvuliwa uanachama wa NCCR na kuangua kilio
Rostam Aziz
Mauaji ya Arusha ya Jan. 5
.................................................
.................................................
 
Sijui kwa nini watanzania wengi ni maskini.
 
Unadhani watawala wetu wana akili timamu kweli au wao hutuona sisi wananchi majuha ?

Viongozi wetu ni majiniasi ila wananchi ndio mbumbu!!

Kati ya mtu anayeuza vitu vyake vya thamani kwa hasara na mnunuzi nani kati yao ni kilaza???
 
Back
Top Bottom