MWAKA 2023: Mwaka wa Tafakuri na Katiba Mpya - 1

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
Mwaka 2023 ukawe mwaka wa Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya, Ukawe mwaka wa utekelezaji wa mapendekezo ya kikosi kazi cha Rais kuhusu Demokrasia nchini.

Heri ya mwaka mpya Watanzania, hongereni sana kwa kufika mwaka 2023 pamoja na changamoto zote za Nchi yetu, vikiwemo maji, umeme kukatika na mfumuko wa bei kwenye bidhaa masokoni.

Upo uwezekano mkubwa sana kutokana na hali ya uchumi wetu na Dunia pamoja na mashinikizo ya jumuiya za kimataifa mwaka 2023 kukawa na pendekezo la mabadiliko katika katiba yetu.

Binafsi mimi kama mtanzania nimeshazoea shida hizi za kukatika kwa Umeme,maji kukatika mwezi,mfumuko wa bei kwenye bidhaa masokoni,na mambo madogo madogo kama kutoa rushwa ili uwekewe Umeme usipotoa unaambiwa subiri wenzako wa mwaka juzi bado hawajaunganishwa.

hivyo hivyo idara ya maji form utaambiwa imepotea na kwa sababu hawakupi copy yoyote unapoiwasilisha,hauwezi kuwafanya chochote, watakwambia tu nenda tena kalete barua nyingine toka kwa mwenyekiti wa mtaa uliyoleta mwanzo imepotea. Tumeshazoea yote, kwa mtazamo wangu tunahitaji katiba mpya kutokana na sababu zifuatazo:

1. Katiba ya sasa ilipendekezwa na kuasisiwa kwa muda mfupi na kamati kuu ya chama tawala. Mchakato wote ulifinywa kwa takribani mwezi mmoja bila kuhusisha maoni ya wananchi. kwa hiyo hii tuliyonayo sio katiba ya Umma.

2. Mamlaka ya umma yaliyowekwa kwenye ibara ya 8 yako kama pambo, hayawezi kuhojiwa kikamilifu mahakamani. Ndio maana huwezi kwenda kumwondoa mbunge mahakamani hata kama hawatumikii (there is no power of reccall).

3. Suala umiliki wa ardhi halijafafanuliwa vizuri kikatiba. Ndio maana tunaswagwa kupisha migodi na mashamba ya wawekezaji wa kigeni.

4. Kuna utata kuhusu Muungano. Kwa mfano ardhi sio suala la Muungano wakati ambapo Muungano ni kuunganisha ardhi!

5. Haki ya kupiga kura haiko kwenye haki za msingi za kikatiba badala yake imetajwa kwenye ibara ya 5 ambayo si sehemu ya haki za msingi. Katika Muktadha huu mamlaka ya kuhoji haki ya kupiga kura mahakamani yanakuwa katika mtanziko (tutaona kwenye Kesi ya Mtikila kama suala hili likiibuka).

6. Hakuna suala la uraia. Je, watanzania ni wakimbizi? Kwa mujibu wa katiba ya sasa je, raia wa tanzania ni nani?

7. Haijatamkwa wazi katika katiba kwamba ndio sheria mama.

8. Rais amepewa mamlaka ya kuteua tume huru ya uchaguzi bila checks and balance hatimaye kuharibu haki na uhuru wa mfumo wa kuingia madarakani ambao ni mhimili muhimu wa katiba.

9. Rais amepewa madaraka makubwa tena ya mwisho. Kichekesho ni kuwa rais ana mamlaka hata ya kulivunja Bunge kama litakataa kupitisha bajeti ya serikali yake!

10.Katiba hii haitambui na kuzilinda haki nyingi za msingi mathalani za vijana, mazingira,utamaduni nk. Orodha ni ndefu.

11. Haifafanunui haki na wajibu wa vyama vya siasa nchini. Je kiongozi wa upinzani ana hadhi gani katika katiba ya sasa? Upinzani una umuhimu gani kwa taifa?

12. Haki ya elimu haimo kwenye katiba, kinachotajwa ni haki ya kujielimisha tena haiko katika orodha ya haki za binadamu zilizotajwa kwenye katiba.

13. Mambo nyeti kama vita dhidi ya rushwa, umiliki wa uchumi nk hayajafafanuliwa na yale yaliyodokezwa katika ibara ya 9 hayawezi kuhojiwa mahakamani.

14. Serikali kuu inaingilia serikali za mitaa. Kadhalika pana mwingiliano baina ya wakuu wa mikoa, wilaya, wabunge, madiwani. Mfumo mzima wa utawala ni mkorogo wenye utata.

15. Rais anateua viongozi wakubwa wa nchi kama mwanasheria mkuu, Jaji Mkuu, Mkurugenzi wa mashtaka bila kushauriana na mtu yoyote wala kuthibitishwa na chombo chochote.

16. Bunge haliruhusiwi kupendekeza muswada unaoweza kuigharimu pesa serilai bila muswada huo kupitia serikalini. Bunge limewekwa kuwa mpagazi/kuli wa serikali.

17. Hakuna mahakama ya Katiba. Mahakama kuu imepewa mamlaka ya kusikiliza masuala ya kikatiba wakati mahakama kuu sio suala la muungano hivyo maamuzi yake hayana nguvu ZNZ.

18. Hakuna mamlaka ya kuwalinda wananchi wasitonewe na vitendo vya watawala.

19. Tume za serikali yenyewe mathalani ya Nyalali, kisanga nk zimesema katiba hii haifai!

20. Hakuna kifungu cha wazi kufafanua namna ya kurekebishwa kwa katiba. Hivyo kuna mwanya wa hata Bunge kurekebisha katiba yote!

21. Ibara ya 152 inayotoa ufafanuzi haijitoshelezi kabisaaaaaaaaaa. Kwa mfano neno ambalo viongozi wanalitumia mara kwa mara kuhalalisha maamuzi yao guesss whaat "MASLAHI YA UMMA" halijafafanuliwa ni nini hasa!

22. Katiba imeeleza bayana namna ya kulipa deni la nje, ingawa iko kimya kuhusu madeni ya ndani.

23. hakuna kifungu cha kuilazimisha serikali kulipa fidia wananchi wake inapodhirika kimahakama kuwa ilivunja haki

24. Tumeshaweka viraka vingi sana mpaka sasa nguo katiba haijulikani ina rangi gani-tununue nguo mpya!

Sababu ni nyingi zinakaribia umri wangu wa miaka arobaini,labda watueleze-ni kwa nini hawataki KATIBA MPYA?

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the effect of Micro-Financing on poverty reduction.
 
Katiba ya sasa inatosha na ni Bora sana
 
Leo 13:15hrs 01/01/2023

Mwaka 2023 ukawe mwaka wa Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya,Ukawe mwaka wa utekelezaji wa mapendekezo ya kikosi kazi cha Rais kuhusu Demokrasia nchini,Heri ya mwaka mpya Watanzania,hongereni sana kwa kufika mwaka 2023 pamoja na changamoto zote za Nchi yetu,vikiwemo maji,umeme kukatika na mfumuko wa bei kwenye bidhaa masokoni,Upo uwezekano mkubwa sana kutokana na hali ya uchumi wetu na Dunia pamoja na mashinikizo ya jumuiya za kimataifa mwaka 2023 kukawa na pendekezo la mabadiliko katika katiba yetu.

Binafsi mimi kama mtanzania nimeshazoea shida hizi za kukatika kwa Umeme,maji kukatika mwezi,mfumuko wa bei kwenye bidhaa masokoni,na mambo madogo madogo kama kutoa rushwa ili uwekewe Umeme usipotoa unaambiwa subiri wenzako wa mwaka juzi bado hawajaunganishwa,hivyo hivyo idara ya maji form utaambiwa imepotea na kwa sababu hawakupi copy yoyote unapoiwasilisha,hauwezi kuwafanya chochote,watakwambia tu nenda tena kalete barua nyingine toka kwa mwenyekiti wa mtaa uliyoleta mwanzo imepotea,tumeshazoea yote,Kwa mtazamo wangu tunahitaji katiba mpya kutokana na sababu zifuatazo:

1. Katiba ya sasa ilipendekezwa na kuasisiwa kwa muda mfupi na kamati kuu ya chama tawala. Mchakato wote ulifinywa kwa takribani mwezi mmoja bila kuhusisha maoni ya wananchi. kwa hiyo hii tuliyonayo sio katiba ya Umma.

2. Mamlaka ya umma yaliyowekwa kwenye ibara ya 8 yako kama pambo, hayawezi kuhojiwa kikamilifu mahakamani. Ndio maana huwezi kwenda kumwondoa mbunge mahakamani hata kama hawatumikii(there is no power of reccall)

3.Suala umiliki wa ardhi halijafafanuliwa vizuri kikatiba. Ndio maana tunaswagwa kupisha migodi na mashamba ya wawekezaji wa kigeni.

4.Kuna utata kuhusu Muungano. Kwa mfano ardhi sio suala la Muungano wakati ambapo Muungano ni kuunganisha ardhi!

5. Haki ya kupiga kura haiko kwenye haki za msingi za kikatiba badala yake imetajwa kwenye ibara ya 5 ambayo si sehemu ya haki za msingi. Katika Muktadha huu mamlaka ya kuhoji haki ya kupiga kura mahakamani yanakuwa katika mtanziko(tutaona kwenye Kesi ya Mtikila kama suala hili likiibuka)

6. Hakuna suala la uraia. Je, watanzania ni wakimbizi? Kwa mujibu wa katiba ya sasa je, raia wa tanzania ni nani?

7. Haijatamkwa wazi katika katiba kwamba ndio sheria mama.

8. Rais amepewa mamlaka ya kuteua tume huru ya uchaguzi bila checks and balance hatimaye kuharibu haki na uhuru wa mfumo wa kuingia madarakani ambao ni mhimili muhimu wa katiba

9. Rais amepewa madaraka makubwa tena ya mwisho. Kichekesho ni kuwa rais ana mamlaka hata ya kulivunja Bunge kama litakataa kupitisha bajeti ya serikali yake!

10.Katiba hii haitambui na kuzilinda haki nyingi za msingi mathalani za vijana, mazingira,utamaduni nk. Orodha ni ndefu

11. Haifafanunui haki na wajibu wa vyama vya siasa nchini. Je kiongozi wa upinzani ana hadhi gani katika katiba ya sasa? Upinzani una umuhimu gani kwa taifa?

12. Haki ya elimu haimo kwenye katiba, kinachotajwa ni haki ya kujielimisha tena haiko katika orodha ya haki za binadamu zilizotajwa kwenye katiba

13. Mambo nyeti kama vita dhidi ya rushwa, umiliki wa uchumi nk hayajafafanuliwa na yale yaliyodokezwa katika ibara ya 9 hayawezi kuhojiwa mahakamani.

14. Serikali kuu inaingilia serikali za mitaa. Kadhalika pana mwingiliano baina ya wakuu wa mikoa, wilaya, wabunge , madiwani. Mfumo mzima wa utawala ni mkorogo wenye utata

15. Rais anateua viongozi wakubwa wa nchi kama mwanasheria mkuu, Jaji Mkuu, Mkurugenzi wa mashtaka bila kushauriana na mtu yoyote wala kuthibitishwa na chombo chochote

16. Bunge haliruhusiwi kupendekeza muswada unaoweza kuigharimu pesa serilai bila muswada huo kupitia serikalini. Bunge limewekwa kuwa mpagazi/kuli wa serikali

17. Hakuna mahakama ya Katiba. Mahakama kuu imepewa mamlaka ya kusikiliza masuala ya kikatiba wakati mahakama kuu sio suala la muungano hivyo maamuzi yake hayana nguvu ZNZ

18.Hakuna mamlaka ya kuwalinda wananchi wasitonewe na vitendo vya watawala

19. Tume za serikali yenyewe mathalani ya Nyalali, kisanga nk zimesema katiba hii haifai!!!!!

20. Hakuna kifungu cha wazi kufafanua namna ya kurekebishwa kwa katiba. Hivyo kuna mwanya wa hata Bunge kurekebisha katiba yote!!!!

21. Ibara ya 152 inayotoa ufafanuzi haijitoshelezi kabisaaaaaaaaaa. Kwa mfano neno ambalo viongozi wanalitumia mara kwa mara kuhalalisha maamuzi yao guesss whaat "MASLAHI YA UMMA" halijafafanuliwa ni nini hasa!

22. Katiba imeeleza bayana namna ya kulipa deni la nje, ingawa iko kimya kuhusu madeni ya ndani.

23. hakuna kifungu cha kuilazimisha serikali kulipa fidia wananchi wake inapodhirika kimahakama kuwa ilivunja haki

24. Tumeshaweka viraka vingi sana mpaka sasa nguo katiba haijulikani ina rangi gani-tununue nguo mpya!!!!

Back
Top Bottom