Mwaka mmoja umetueleza mengi

Huu mwaka mmoja tokea awe madarakani umetuonyesha mengi na sasa tunaweza walau hata kuanza kuhitimisha kuwa kumbe wala hayuko tofauti kivile na wengine na huenda akawa ni bomu kabisa kuliko wote waliomtangulia.

Aliingia kwa mikwara ya kufa mtu. Akafutilia mbali sherehe za uhuru [2015] katika lengo la kuheshimu vipaumbele.

Sherehe za muungano [2016] nazo zikafutwa na pesa ambazo zingetumika kwenye hizo sherehe akaagiza ziende kwenye upanuzi wa barabara ya uwanja wa ndege wa Mwanza.

Pia akabana safari za kipuuzi puuzi za kwenda nchi za nje za watumishi wa umma.

Yote hayo pamoja na jitihada za kupambana na ufisadi yalikuwa ni nuru njema kwa wengi. Baadhi yetu tukadhani labda kweli tupo kwenye zama mpya...lakini wengine tukajipa muda maana muda huonyesha mengi.

Juzi sherehe za uhuru zikafanyika. Maajabu! Manake mwaka jana hakukuwa na sababu ya kusherehekea kwa sherehe kubwa kwa ajili ya gharama kuwa juu lakini mwaka sijui hakukuwa na hizo gharama...

Na sijui hizo za muungano nazo zitafanyika hapo mwakani baada ya kutofanyika mwaka huu?

Sasa leo yamekuja haya ya kufanyia mikutano ya CCM ikulu.

Tafadhali sana MTUKUFU rais....like....seriously? Kwa nini msifanyie hayo mamikutano yenu huko Lumumba?

Wahshi kabisa....you will go down as the worst president in the history of our existence...past...present...and future!

Mikwara yote ile kumbe hamna lolote...bora hata gesi ya CocaCola.

NB: Pia iliwahi kuripotiwa kuwa angetuonyesha pay stubs za mshahara wake. Kumbe ilikuwa ni uongo tu. Mpaka leo hamna kitu na hakuna anayejali [ukiacha mimi labda].
Kaka ni weweeeee?au naotaaaaa?
 
Alichofanikiwa kikubwa ni kutuchanganya akili tu.
Tatizo la Magufuli ni kuwa yeye anaamini ya kuwa ana haki ya kukosoa ila hataki kukosolewa. Jambo hili sio jema kwa ustawi wa taifa letu. Wazungu wana msemo kuwa " if you can dish out then you ought to take it with strides."
 
yaani hamuoni hata umeme wa Tanesco haikatwi
bei za cement kushuka
viwanja kushuka
madalali wamejifia
kila mtu afanye kazi ya kueleweka
 
Kupitia kukamatwa Max huyu anataka wengi tubadili kabisa mitizamo yetu juu yake. Wengine bado tulikuwa na imani kupitia utashi, nia aliyoonesha mwanzo. Lakini kwa hili la Max linaweza kubadili kabisa upepo kuliko wanavyofikiri.
 
Siyo hata suala la Max tu...

Hata ile kufuta sherehe za Uhuru mwaka jana kwa ajili ya gharama halafu na kugeuka tena mwaka huu na kufanya sherehe...watu tumueleweje sasa hapo?

Ni kwamba ilikuwa ni publicity gimmick tu?

Na hii ya kufanyia mikutano ya CCM ikulu...toka aingine leo ndo mara ya kwanza [kama sijakosea] yeye kuendesha mkutano wa chama ikulu.

Yale yale tuliyokuwa tunamnangia Kikwete na yeye ndo anayafanya na zaidi!
 
Mkuu binafsi issue ya Max ni benchmark. Naelewa anasimamia nini na nini kinatokea. Hayo mengine unaweza kujenga justification nyingi lakini hili la Max limenipa picha ya halisi ambayo bila kelele za kutosha HAKUNA atakayesema tena.
 
Nakuelewa sana tu.

Ila kwangu mimi naangalia ile cumulative effect ya mambo.

Slowly but surely anatuonyesha kwamba kumbe wala hayuko tofauti.

Yeye ni walewale na CCM ni ileile.
 
godbless lema.....ben saanane......maxence mello......lissu.....who is next?

wahariri wa magazeti wakikaaa kimya wanafata wao
 
NB: Pia iliwahi kuripotiwa kuwa angetuonyesha pay stubs za mshahara wake. Kumbe ilikuwa ni uongo tu. Mpaka leo hamna kitu na hakuna anayejali [ukiacha mimi labda].
.....katika hili hata mimi najali sana na si ajabu ndiyo maana JF inalazimishwa ku - disclose infos zetu ni tujikute tu maiti kwenye viroba + jiwe zito na kutupiwa mto Ruvu!!

.....huu wa awamu ya 5 naona imekuja na staili ya ua, funga ktk viroba + mawe kisha tupia mtoni waliwe na mamba badala ya Msitu wa Mabwepande!!

.....hawana tofauti hawa, ni walewale na ni ileile lakini kwa mtindo tofauti kwa malengo yaleyale na kwa matokeo yaleyale ya Tu - Chukue Chetu Mapema!!
 
Mimi sihofii haya mambo ya kiuchumi au kukosa dawa hospitali, wasiwasi wangu ni kuwa mtu Mmoja anapoona kuwa mawazo yake ndio bora kuliko watanzania wengine, na anapoona kuwa machinga wa Mwanza kubomolewa vibanda baada ya kubembelezwa kwa miaka mingi waondoke, wao wanamgusa Raisi kuliko wakazi wa kivule wanaobomolewa nyumba bila Raisi kusema chochote itasababisha watu wengine waone wametengwa na mkuu wa nchi na hivyo kuamua kumkataa na akikataliwa atalazimisha ushindi na kwa kuwa watu wamechoka wataamua kuingia mitaani na kusababisha machafuko. Wasiwasi wangu ni misingi ya amani ya nchi inabomolewa makusudi kwa ubaguzi miongoni mwa watanzania
 
Huu mwaka mmoja tokea awe madarakani umetuonyesha mengi na sasa tunaweza walau hata kuanza kuhitimisha kuwa kumbe wala hayuko tofauti kivile na wengine na huenda akawa ni bomu kabisa kuliko wote waliomtangulia.

Aliingia kwa mikwara ya kufa mtu. Akafutilia mbali sherehe za uhuru [2015] katika lengo la kuheshimu vipaumbele.

Sherehe za muungano [2016] nazo zikafutwa na pesa ambazo zingetumika kwenye hizo sherehe akaagiza ziende kwenye upanuzi wa barabara ya uwanja wa ndege wa Mwanza.

Pia akabana safari za kipuuzi puuzi za kwenda nchi za nje za watumishi wa umma.

Yote hayo pamoja na jitihada za kupambana na ufisadi yalikuwa ni nuru njema kwa wengi. Baadhi yetu tukadhani labda kweli tupo kwenye zama mpya...lakini wengine tukajipa muda maana muda huonyesha mengi.

Juzi sherehe za uhuru zikafanyika. Maajabu! Manake mwaka jana hakukuwa na sababu ya kusherehekea kwa sherehe kubwa kwa ajili ya gharama kuwa juu lakini mwaka sijui hakukuwa na hizo gharama...

Na sijui hizo za muungano nazo zitafanyika hapo mwakani baada ya kutofanyika mwaka huu?

Sasa leo yamekuja haya ya kufanyia mikutano ya CCM ikulu.

Tafadhali sana MTUKUFU rais....like....seriously? Kwa nini msifanyie hayo mamikutano yenu huko Lumumba?

Wahshi kabisa....you will go down as the worst president in the history of our existence...past...present...and future!

Mikwara yote ile kumbe hamna lolote...bora hata gesi ya CocaCola.

NB: Pia iliwahi kuripotiwa kuwa angetuonyesha pay stubs za mshahara wake. Kumbe ilikuwa ni uongo tu. Mpaka leo hamna kitu na hakuna anayejali [ukiacha mimi labda].
Poleni,
Hiyo ndiyo faida ya kutawala
Ikulu ni ya watanzania wote, lakini chama tawala ndo kina dhamana kwa miaka hii mitano
Mkasirike, mvimbe, ila huo ndo ukweli
JPM amewaambia, vyama vingine vinaruhusiwa kufanyia mikutano ikulu, lkn lazima agenda yenu ijulikane mapema
 
Back
Top Bottom