Emanueli misalaba
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 1,111
- 1,658
Wana Jf Salaam , bila shaka mko poa poa na weekend hii.
Kwa mda sasa nimekua nikisikia hii sherehe ya mwaka kogwa ambayo huazimishwa huko Makunduchi,
Juzi ilibidi nimpigie simu mtu anaishi huko ili nimuombe anipe picha kamili huwa ikoje, aliniambia,
1. Kabla ya siku ya kwanza ya mwaka kogwa, wazee huchinja Mnyama kwenye mizimu yao kisha watu wenye kutaka kuchukua huwa wanaenda kwenye mzimu na kupewa nyama huko kwenye mizimu yao.
2. Kesho yake Siku ya mwaka kogwa yenyewe, huambatana na mambo mengi ikiwemo watu kuwa makundi mawili kundi la kaskazini na kundi jingine la kusini na kupigana kwa fimbo Zamani na kwa sasa hutumia migomba, kwa kuanzia asubuhi hadi around ya saa 6 adhuhuri,
3. Siku hiyo hiyo huwa kuna kibanda kimejengwa na mtu huingia ndani yake, kisha kibanda huchomwa moto na mtu aliye ndani hutakiwa atoke kwa kasi ndani yake asije kuteketea ndani yake,
4. Siku zinazofuata huwa ni kuburudika kwa mziki.
Wadau hayo ndiyo mambo ya Mwaka kogwa, nilikuwa na maswali mengi kwa huyo mkaazi wa huko Makunduchi ila alikuwa mengine hawezi kunijibu.
Wajuvi na wabobevu wa mambo ndugu zangu Mshana Jr, Shimba ya Buyenze, Rakim, TumainiEl, Herbalist Dr MziziMkavu, Robert Heriel Mtibeli nk
Mwaka kogwa upi uono wenu kwa radar ya kiroho?
Kwa darubini ya imani hili jambo limebeba nini nyuma ya pazia?
Vipi ambaye anamwamini Mungu mmoja na mtume wake (s.a w) kisawasawa akishiriki kwenye sherehe hizi hapati hatia nafsini mwake?
Baadhi ya viongozi wa serikali kushiriki hii sherehe je jambo hili ni jambo ambalo laweza kuleta faida au hasara za kiroho kwa taifa lote au ni kwa eneo husika tu?
Natanguliza shukurani nyingi saaaaaaana asanteeeeen"