Mwaka 2012 niliichallange Serikali ya CCM na Hayati John Pombe Magufuli kuhusu mikopo!

Mimi ni muumini wa Uhuru wa kweli na kujiamini kama mtanzania !
Kauli mbiu yangu wakati naingia JF ni moja tu inatambulika kama "KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA"

Kaulimbiu hii inamaanisha kuwa tunaweza kufanya makubwa iwapo tutajiamini au tutachagua kujiamini.
sisi ni watu wenye akili,uwezo na vipaji.na pengine sisi ni watu teule kihistoria.Imagine mabaki ya mtu wa kale zaidi bado yanainesha yapo Tanzania.

Tukishindwa kujiamini kamwe hatutakuwa huru na kizazi chetu kitatawaliwa daima milele.hatuna budi kwa namna yoyote ile tunatakiwa kujiamini na kuvunja utegemezi kwa mabeberu.
Hii ni mission na lazima iwe successful tukiamua.

mwaka 2012 niliwahi kumhoji waziri wa miundombinu wa kipindi hiko akiwa kwenye pick ya mafanikio ...Mhe. Rais Hayati Dr John Pombe Magufuli(Swahiba wangu wa ukweli)
Nilimuhoji juu ya mafanikio katika miundombinu ya barabara ...nilimuhoji kwa nini inakuwa ni ya misaada au pengine mikopo?
Nilimuhoji humuhumu JF !
Hakuwahi kunijibu verbally au kwa kuandika humu jamvini lakini inawezekana alinijibu baada ya kuingia Ikulu ya Magogoni ...hapo alinijibu kwa matendo yaani kuanzisha miradi kutokana na rasilimali zetu na kodi zetu kwani inawezekana.

NILIMFURAHIA KWA HILI.
Pia niliwahi kuhoji kwa nini matangazo haswa kwenye hamasa za afua za tiba kinga yanaandikwa au kutangazwa kuwa ni hisami ya walami ??yaani choo cha shule kikijengwa na mlami kinaandikwa choo hichi kimejengwa kwa hisani ya watu wa marekani???
Huu ni ukakasi na ukoloni mamboleo na ni udhalilishaji kwa chama,Serikali na wananchi.
Baadae matangazo ya namna hiyo yaliondoka(naamini Magufuli alinijibu kwa vitendo)
Niliwahi kuhoji kwa nini mjamzito ambaye ana mume wake tajiri wa kimasai ambaye ana mbuzi,kondoo na Ng'ombe inakuwaje mle wake ajifungue bure kwa hisani ya watu wa Marekani/Uingereza??
nilihoji na kupendekeza tuwe na njia bora ya health care financing.
Katika muendelezo wa kuhoji na kupendekeza niliuliza swali kwa wagombea urais mwaka 2015 katika mdahalo ulikuwa hosted hapa JF ....Niliuliza juu ya sera na msimamo wa wagombea kuhusu universal healthcare insuarance yaani bima ya afya kwa wote hususani bima ya afya ya jamii(CHF)
Nimehoji na kushawishi na kuwajengea uwezo watanzania juu ya kujitegemea na kujikwamua na utegemezi wa kijinga.

Leo hii bado nitaendelea kuihoji na kuipa somo Serikali ya CCM juu ya dhana ya kujiamini,kujisimamia na kuleta maendeleo kwa Kutumia rasilimali tulizonazo.
Dhana hii ni reflection ya Uhuru wetu kamili.

Leo hii nitaendelea kuhoji mikopo inayotupelekea tuandike shule zetu zimejengwa kwa hisani ya msaada wa covid 19.
Nitaendelea kupinga mikopo ya masharti iwe imepangwa au kutekelezws awamu ya tano au ya sita.

Nitaasa kuwa ni vyema tukarejea misingi ya Kujitegemea tulioachiwa na the late Julius Kambarage Nyerere.

Tusimamie UHURU wetu kwa matendo.

Iwapo tumekopa kama Marekani anavyokopa basi miradi yetu isiandikwe kuwa imejengwa kwa hisani ya IMF.Kukopa ni ruksa ila sharti la kuandika kuwa mtoto wangu anasomeshwa kwa Hisani ya IMF ni udhalilishaji ...TUJIREKEBISHE HARAKA.
Mada hii inawajia....

KWA HISANI YA MTU WA TANZANI!
Hii siyo thread yenye quality. Ni mkusanyiko wa maneno yaliyowekwa pamoja bila mpangilio.

Huwezi ukakopa halafu uweke na masharti kwa mkopaji. NONSENSE
 
Hii siyo thread yenye quality. Ni mkusanyiko wa maneno yaliyowekwa pamoja bila mpangilio.

Huwezi ukakopa halafu uweke na masharti kwa mkopaji. NONSENSE
umeisoma na kuielewa mada?mbona comment yako ipo dissconected?
 
Nilisoma Ulaya majengo ya Idara yote na vifaa vya ile idara tena vya kisayansi kweli kweli viliandikwa vimefadhiliwa na UNESCO why Watanzania tunapenda kudanganyana na kuogopeshana kuhusu mikopo na misaada?
 
Ulaya ipi?tupe picha by the way UNESCO sio IMF!lete picha na ushahidi wa Madarasa ya Ulaya yaliyoandikwa covid 19
 
Ningejisikia fahari kama madarasa yangeandikwa: darasa hili limejengwa kwa tozo za miamala ya simu.
 
Ulaya ipi?tupe picha by the way UNESCO sio IMF!lete picha na ushahidi wa Madarasa ya Ulaya yaliyoandikwa covid 19
Ulaya Magharibi na nimesema Unesco siyo IMF na tuliosoma Ulaya wote tunajua kuwa ni ujinga kukamua watu wako kwa kodi kwa ajili ya miundombinu maana finally hiyo miundombinu inakuwa mali ya dunia mzima. Imagine ukijenga barabara ikafika burundi siku UN wakiwa na mission Burundi wataitumia tu hiyo reli yako au barabara kwa manufaa yao na Warundi na huwezi kuwazuia. Then why unaijenga kwa kuumiza watu wako?
 
Ulaya Magharibi nchi gani specific?
Kuna mtanzania atatumia hiyo barabara ya ulaya?
 
mbaya zaidi mtu anakopa bado tena anaendelea kuwapiga kwenye tozo ; fedha anazokopa anasema anajenga madarasa sijui na kuendeleza miradi gani isiyoonekana wakati huo huo anakwambia nakukata tozo tujenge shule kitu hicho hicho kimoja

matokeo yake hakuna miradi inayoendelea zaidi ya porojo tu huku deni likingezeka na bado unakamuliwa tozo na bado anakwambia hapendi pesa za dhuluma
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom