CCM mnataka hayati Magufuli agombee 2025?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,305
33,924
Ni kama sielewi CCM inataka nani awe mgombea wao ngazi ya Urais kwenye uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kati ya Hayati John magufuli na Wana CCM wengine walioko hai.

Kwenye mitandao ya kijamii hivi Sasa ni kama limezuka Kundi kubwa Sana la wana CCM linalofanya jitihada za kuhakikisha kuwa kila siku kunakuwa na habari za Hayati Pombe John Magufuli mitandaoni.

Ni kama vile wanatushawishi tuone ubora wake na achaguliwe kwenye uchaguzi ujao.

Magufuli alishafariki, Sasa hizo harakati za mitandaoni kumnadi lengo lake ni nini hasa!!??
 
Tuliosoma falsafa na historia tumekutana na hoja kwamba mtu hafariki mpaka siku mtu wa mwisho anapoacha kumuwaza.

Yani ukimfikiria, ukimkumbuka, ukimtaja, anaendelea kuishi katika mawazo yako.

Labda wanataka Magufuli aendelee kuishi katika mawazo ya watu.

"No one is finally dead until the ripples they cause in the world die away, until the clock wound up winds down, until the wine she made has finished its ferment, until the crop they planted is harvested. The span of someone’s life is only the core of their actual existence."

Terry Pratchett, Reaper Man (Discworld, #11; Death, #2)
 
Back
Top Bottom