Mwafaka wa Umeya wa Arusha wapatikana

Mwafaka wa Umeya wa Arusha wapatikana

@njilembera. Nitukane tu unasubiri nini? Na ndio kazi yenu hamuna ustaarabu. Kwani hujui . Ndio wameniibia. Haijalishi mchaga akiwa tajiri au maskini aghlabu wote ni wezi tu.

Kuna tajiri mmoja wa kichaga jina namhifadhi lkn anamiliki campuni ya mabasi ya abiria lkn anakodisha majambazi wateke magari ya watu halaf anayabadilisha kidogo anayatumia. Wapo wengi weye peleleza tu.
 
Kijana Crashwise nakupongeza mkuu;haya mazungumzo yamefanyika lini na wapi mbona nimemwona Mbowe bungeni leo au walifanya over the weekend?

Hapo panataka maelezo ? Wenyewe waliamuwa kwa kujuwa kuwa wao na wananchi wao ndio wanaopata madhara. Wakubwa kazi yao kuja na kuhamasisha na kuachia wenye meno watafune> pengine hali hii ndiyo iliyotokea kule Zanzibar.
 
ulikuwa ni ubabe wa CCM hasa makamba...

Ulikuwa ubabe wa CCM na ujinga wa CDM! kilchobadilika kipi hapa kama ubabe upo palepale kwani mwishi wake CDM wamekubali kuwa aliopo ni halali . Kwa kuondowa ujinga CDM wamefanya jambo la ustaarabu kukubali yaishe kwa manufaa ya wananchi. Walitakiwa CDM watambue busara hii mapema na sio kungojea hadi damu imwagike.
 
Ubabe wa CCM upi jamani? Uchaguzi ule CCM ulishinda kihalali. Walishinda madiwani wengi kuliko Chadema katika uchaguzi. Walikuwa na haki ya kusimamisha Meya pale. Haki ya Chadema kusimamisha Meya ilitoka wapi? Badala yake Chadema wakaja CDM na mizengwe yao ya madai kwamba Diwani Chatanda hakubaliki wakati alipitishwa rasmi na CCM na alikidhi masharti ya makazi. Chadema wakachagua njia ya msuguano, ya kutumia nguvu na maandamano yasiyo na tija. Yamewafikisha wapi? Ona leo hii wamekaa kitako na kufikia muafaka. Kilichowashinda kufanya hivi toka mwanzo ni nini? Jamani tusikubali kutumiwa na wanasiasa uchwara kwa maslahi yao binafsi.
 
So tatizo ilikua ni kupata nafasi za uongozi tu
na sio mchakato wa uchaguzi kubakwa?

shame on mbowe,you can't stand for what is right!
Yaani hii itatumika kisiasa dhidi yenu kwamba "mna uchu wa madaraka"
hadi mjute,

Am watching

Kwani issue ilikuwa KUGAWANA MADARAKA au ilikuwa KUKATAA KUKIUKWA KWA SHERIA YA UCHAGUZI ZA SERIKALI ZA MITAA mbapo Mbunge wa viti maalum(CCM)Tanga Mama Chitanda kupiga kura yake Arusha sehemu ambayo yeye sio mwakilishi?

CHADEMA ni waroho wa madaraka au?
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Chadema, CCM mwafaka Arusha [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Monday, 20 June 2011 20:57 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]0diggsdigg

Peter Saramba na Moses Mashalla, Arusha
HATIMAYE mgogoro wa uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Arusha umepata ufumbuzi baada ya pande zinazohusika kufikia muafaka wa kupokezana madaraka.

Katika muafaka huo uliofikiwa baada ya majadiliano yaliyodumu kwa zaidi ya miezi miwili CCM kitaendelea kushikilia nafasi ya umeya huku Chadema kikipewa unaibu kwa kipindi cha miaka minne mfululizo.

TLP kitachukua nafasi ya unaibu meya kwa kipindi cha mwaka mmoja baada ya ile minne ya Chadema kukamilika

Makubaliano mengine ni Chadema na CCM kuongoza kwa kupokezana kamati mbili za kudumu za uchumi, elimu na afya na ile ya mipango miji, mazingira na ujenzi ambapo kikao cha jana kiliwachagua John Bayo (Chadema) na Ismail Katamboi (CCM) kuongoza kamati hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani wa Manispaa kilichomchagua diwani wa Kimandolu, Estomi Mallah kuwa naibu meya, mwenyekiti wa kamati ya muafaka, Michael Kivuyo alisema uamuzi huo umejali maslahi ya umma na kuweka pembeni itikadi na maslahi ya vyama.

“Tumekubaliana kusahau yote yaliyotokea nyuma, tumeanza ukurasa mpya kwa maslahi ya wananchi ambao wanahitaji kuunganishwa na viongozi wao katika harakati za maendeleo ambayo hayajali itikadi,” alisema Kivuyo.

Kwa upande wake, Meya liyekuwa akipingwa uchaguzi wake, Gaudance Lyimo alisema “Nimeufurahia muafaka huu. Kimsingi tungeweza kuendelea na shughuli zote, lakini ingekuwa ngumu kutekeleza majukumu yetu katika hali iliyokuwepo,”

Alisema ni afya kwa maendeleo ya Manispaa ya Arusha kufanya kazi pamoja na madiwani wa vyama vyote, hasa Chadema yenye idadi kubwa kwa maendeleo ya umma uliowaamini na kuwachagua.

Meya Lyimo ambaye ni diwani wa Kata ya Olorieni aliwagiza watendaji wote wa Manispaa kuwapa ushirikiano unaostahili madiwani wote katika utekelezaji wa majukumu yao bila kubagua wala kuangalia itikadi za vyama vyao.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha aliyekuwa mmoja wa wajumbe walioshiriki vikao vya kutafuta muafaka huo alisema tatizo la uchaguzi wa meya na mauaji yaliyotokea yalikuwa ni jambo la kusikitisha ambalo katika muafaka huo wamezingatia makubaliano yatakayohakikisha hayatajirudii siku zijazo.

“Natoa wito sasa kwa madiwani wote kutekeleza wajibu wao kuwakilisha na kutetea maslahi ya wananchi bila kujali itikadi za vyama vyao kwai kiongozi akishachaguliwa anawakilisha watu wote wenye itikadi tofauti na hata wasiokuwa na vyama,” alisema Mushi.

Naibu Meya mpya kwa upande wake, aliahidi ushirikiano wa dhati kwa Meya na madiwani wote ili kuharakisha na kufanikisha maendeleo ya Manispaa ya Arusha yaliyokwama kwa kipindi kirefu kutoka na mgogoro uliokuwepo.

“Naamini sasa mstahiki Meya atapata usingizi baada ya muafaka huu kwani alikuwa akiwiwa vigumu kutekeleza majukumu yake. Wananchi wa Arusha sasa watarajie kuona na kupata maendeleo yaliyokusudiwa,” alisema Mallah.

Zaidi ya Mkuu wa Wilaya na mwenyekiti wao, Kivuyo, kamati ya kutafuta muafaka wa mgogoro huo uliosababisha vifo vya watu watatu Januari 5, mwaka huu, iliundwa na wajumbe 10, watano kutoka CCM na wengine Chadema.

Kutoka Chadema wajumbe walikuwa wa kamati hiyo iliyoanza vikao vyake tangu Aprili mwaka huu walikuwa John Bayo, Samson Mwigamba, Efatha Nanyaro na Amani Golugwa wakati CCM iliwakilishwa na Abdulrasul Tojo, Ismail Katamboi, Lilian Mmasi, Karim Moshi, Musa Sunja na Meya Lyimo.

Baada ya kikao cha muafaka na uchaguzi wa naibu meya na wenyeviti wa kamati mbili za kudumu, madiwani wote walisimama, kushikana mikono na kuimba wimbo maarufu wa kuhimiza mshikamano maarufu kwa jina la ‘solidarity forever’.

Wimbo huo uliashiria mwisho wa mgogoro na mwanzo wa ushirikiano. [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Makubaliaono ni kitu kizuri sana duniani. Hasa pale yanapookoa maisha ya watu wasio na hatia. Nikiwa kama mwana chama wa chadema. Nisingependa muafuaka ambao haujali maisha ya watu waliopoteza maisha yao. Wao wanakuwa wapi? wameecha familia amabazo zinateseka. Je kama wana siasa wanakubali uhuni ulifanyika kuuwa watu bila hatia je wafiwa wanapewa fidia gani?

Neno muafaka hususani kwa swala la Arusha is a joke. Tuliandamana na kupiga mayowe tukiamni haki za msingi ziliporwa kwenye demokrasia. Muafaka wa kweli ni kurudia uchaguzi. haya mambo ya ushindi wa mezani hayatusaidii kwa uhai wa demokrasia ya kweli. Hii imekuwa mbinu wa watawala wa Afrika kufunika kombe. Wanatumia miafaka na sharing of power ku-difuse pressure inajengwa kutoa wasio takiwa madarakani.

Mpaka uchaguzi huru na wahaki utakapofanyika, kilichotokea Arusha ni mazingaombwe yasiyo na kichwa wala miguu. Demokrasia inagharama zake. Mandela alipotakiwa atoke jela kwa masharti aligoma, alikuwa tayari kufia jela kuliko kuuza uhuru wake. Mwisho wa siku alitoka na uhuru asilimia mia. Alikubali mateso, kifungo na madhila yote kwa ajili ya haki. Lyimo sio meya wa Arusha. Tunataka uchaguzi mpya.
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Chadema, CCM mwafaka Arusha
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"]Send to a friend
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"]Monday, 20 June 2011 20:57
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]0diggsdigg

Peter Saramba na Moses Mashalla, Arusha
HATIMAYE mgogoro wa uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Arusha umepata ufumbuzi baada ya pande zinazohusika kufikia muafaka wa kupokezana madaraka.

Katika muafaka huo uliofikiwa baada ya majadiliano yaliyodumu kwa zaidi ya miezi miwili CCM kitaendelea kushikilia nafasi ya umeya huku Chadema kikipewa unaibu kwa kipindi cha miaka minne mfululizo.

TLP kitachukua nafasi ya unaibu meya kwa kipindi cha mwaka mmoja baada ya ile minne ya Chadema kukamilika

Makubaliano mengine ni Chadema na CCM kuongoza kwa kupokezana kamati mbili za kudumu za uchumi, elimu na afya na ile ya mipango miji, mazingira na ujenzi ambapo kikao cha jana kiliwachagua John Bayo (Chadema) na Ismail Katamboi (CCM) kuongoza kamati hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani wa Manispaa kilichomchagua diwani wa Kimandolu, Estomi Mallah kuwa naibu meya, mwenyekiti wa kamati ya muafaka, Michael Kivuyo alisema uamuzi huo umejali maslahi ya umma na kuweka pembeni itikadi na maslahi ya vyama.

“Tumekubaliana kusahau yote yaliyotokea nyuma, tumeanza ukurasa mpya kwa maslahi ya wananchi ambao wanahitaji kuunganishwa na viongozi wao katika harakati za maendeleo ambayo hayajali itikadi,” alisema Kivuyo.

Kwa upande wake, Meya liyekuwa akipingwa uchaguzi wake, Gaudance Lyimo alisema “Nimeufurahia muafaka huu. Kimsingi tungeweza kuendelea na shughuli zote, lakini ingekuwa ngumu kutekeleza majukumu yetu katika hali iliyokuwepo,”

Alisema ni afya kwa maendeleo ya Manispaa ya Arusha kufanya kazi pamoja na madiwani wa vyama vyote, hasa Chadema yenye idadi kubwa kwa maendeleo ya umma uliowaamini na kuwachagua.

Meya Lyimo ambaye ni diwani wa Kata ya Olorieni aliwagiza watendaji wote wa Manispaa kuwapa ushirikiano unaostahili madiwani wote katika utekelezaji wa majukumu yao bila kubagua wala kuangalia itikadi za vyama vyao.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha aliyekuwa mmoja wa wajumbe walioshiriki vikao vya kutafuta muafaka huo alisema tatizo la uchaguzi wa meya na mauaji yaliyotokea yalikuwa ni jambo la kusikitisha ambalo katika muafaka huo wamezingatia makubaliano yatakayohakikisha hayatajirudii siku zijazo.

“Natoa wito sasa kwa madiwani wote kutekeleza wajibu wao kuwakilisha na kutetea maslahi ya wananchi bila kujali itikadi za vyama vyao kwai kiongozi akishachaguliwa anawakilisha watu wote wenye itikadi tofauti na hata wasiokuwa na vyama,” alisema Mushi.

Naibu Meya mpya kwa upande wake, aliahidi ushirikiano wa dhati kwa Meya na madiwani wote ili kuharakisha na kufanikisha maendeleo ya Manispaa ya Arusha yaliyokwama kwa kipindi kirefu kutoka na mgogoro uliokuwepo.

“Naamini sasa mstahiki Meya atapata usingizi baada ya muafaka huu kwani alikuwa akiwiwa vigumu kutekeleza majukumu yake. Wananchi wa Arusha sasa watarajie kuona na kupata maendeleo yaliyokusudiwa,” alisema Mallah.

Zaidi ya Mkuu wa Wilaya na mwenyekiti wao, Kivuyo, kamati ya kutafuta muafaka wa mgogoro huo uliosababisha vifo vya watu watatu Januari 5, mwaka huu, iliundwa na wajumbe 10, watano kutoka CCM na wengine Chadema.

Kutoka Chadema wajumbe walikuwa wa kamati hiyo iliyoanza vikao vyake tangu Aprili mwaka huu walikuwa John Bayo, Samson Mwigamba, Efatha Nanyaro na Amani Golugwa wakati CCM iliwakilishwa na Abdulrasul Tojo, Ismail Katamboi, Lilian Mmasi, Karim Moshi, Musa Sunja na Meya Lyimo.

Baada ya kikao cha muafaka na uchaguzi wa naibu meya na wenyeviti wa kamati mbili za kudumu, madiwani wote walisimama, kushikana mikono na kuimba wimbo maarufu wa kuhimiza mshikamano maarufu kwa jina la ‘solidarity forever’.

Wimbo huo uliashiria mwisho wa mgogoro na mwanzo wa ushirikiano.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
sasa mkuu ulitaka muafaka usifikiwe?labda utoe ufafanuzi kinachokera ni muafaka uliofikiwa au ni maamuzi yaliyofanywa mwanzoni angali kwa muafaka ungepatikana kwa mazungumzo.
 
Issue ilikuwa taratibu za kumpata Meya zilikiukwa. Meya alipatikana kiwizi, au sheria zilivunjwa. Sasa tulitegemea muafaka wowote unaendana na uchaguzi mpya wa Meya sio kupeana madaraka. Mimi sipendi siasa za mkato. Ndio siasa za Afrika wanafanya unyama wakijua wakikaa mezani wata-settle for less. Huwezi kutetea Demokrasia wakati uko cheap.
 
walichofanya ni kizuri.hakuna maslahi kwa umma kuendelea kuvutana tuuuuu kusikoisha. waache wafanye kazi sasa tuone
 
Kwanini walikataa muafaka wa kupiga kura upya? Ingekuwa nafuu hata kama wangekubaliana kumpa kura Lymo. Sasa CDM Arusha wanaonekana kama hawana msimamo. Na itakuwaje kwa upande wa Maaskofu waliokataa kumtambua Meya mpaka uchaguzi urudiwe? Watashirikiana na Lyimo?
 
Acha unazi usio na tija wewe. Unafurahia sn kuona Arusha inaendelea kubaki na marundo ya taka mitaani, kisa halmashauri ina migogoro? Lazima ujue demokrasia ina PRICE yake, ambapo pamoja na kusimamia sana haki, unaweza kulazimika kukubaliana na matakwa ya kaburu ,just for betterment of the society at logger-heads. Usitegemee kuwa bingwa wa kila mgogoro broda.
 
tatizo lilikuwa ni umeya? Au demokrasia ilibakwa? kwa kukiuka taratibu za uchaguzi so cha muhimu kilikuwa kurudiwa kwa uchaguzi uliovurugwa no matter who will win or loose. Na sio umeya unless tuambiwe tuliandamana kudai UMEYA na sio UCHAGUZI WA MEYA NI BATILI URUDIWE sasa which is which tuwekane sawa kabisa
 
Issue ilikuwa taratibu za kumpata Meya zilikiukwa. Meya alipatikana kiwizi, au sheria zilivunjwa. Sasa tulitegemea muafaka wowote unaendana na uchaguzi mpya wa Meya sio kupeana madaraka. Mimi sipendi siasa za mkato. Ndio siasa za Afrika wanafanya unyama wakijua wakikaa mezani wata-settle for less. Huwezi kutetea Demokrasia wakati uko cheap.
Mkuu hata JK mwenyewe aliiba kura kwa kusaidiwa na usalama wa taifa na NEC hakuna asiyefahamu hilo na ndio maana mpaka leo hii ukienda kwenye tovuti ya NEC matokeo ya urais hayawekwa maana CHADEMA wanayo matokeo halisi, na NEC wakiweka ya kwao wataumbuka, tunachojua kwamba Meya wa CCM ni fake! Na halimashauri inaongozwa na CHADEMA yeye pale kakaa kwa kuficha aibu ya chama chake. Lisikufadhaishe sana mkuu, ndio maana leo hii Dr Slaa akitoa agizo mara moja Kikwete anayekeleza, maana moyoni dhamira yake inamsuta!
 
A principle is a principle. Jibu swali ni kwa nini hawakukubali kurudia kura. Si wangempa tu huyo Lyimo hizo kura kama maji yaliwafika shingoni?
 
Acha unazi usio na tija wewe. Unafurahia sn kuona Arusha inaendelea kubaki na marundo ya taka mitaani, kisa halmashauri ina migogoro? Lazima ujue demokrasia ina PRICE yake, ambapo pamoja na kusimamia sana haki, unaweza kulazimika kukubaliana na matakwa ya kaburu ,just for betterment of the society at logger-heads. Usitegemee kuwa bingwa wa kila mgogoro broda.

Kwahiyo tusitemee demokrasia Tanzania hasa ya Uchaguzi, kwani Tutazalisha kina Maalimu Seif kibao usoni. Unaibiwa halafu unapewa unaibu unatulia. I dont buy that.
 
Acha unazi usio na tija wewe. Unafurahia sn kuona Arusha inaendelea kubaki na marundo ya taka mitaani, kisa halmashauri ina migogoro? Lazima ujue demokrasia ina PRICE yake, ambapo pamoja na kusimamia sana haki, unaweza kulazimika kukubaliana na matakwa ya kaburu ,just for betterment of the society at logger-heads. Usitegemee kuwa bingwa wa kila mgogoro broda.

Mkuu mimi sikubaliani na wewe. Tuseme tu kwamba CHADEMA wamekuwa walaini nadhani kwa sababu wanaona wamezidiwa na nguvu ya chama kilichoshika dola. Kimsing ilitakiwa ufanyike uchaguzi mpya au CHADEMA ilibidi wasusie tu ili kijulikane kwamba hawaridhiki na yaliyotokea.
 
kwanini walikataa muafaka wa kupiga kura upya? Ingekuwa nafuu hata kama wangekubaliana kumpa kura lymo. sasa cdm arusha wanaonekana kama hawana msimamo. Na itakuwaje kwa upande wa maaskofu waliokataa kumtambua meya mpaka uchaguzi urudiwe? Watashirikiana na lyimo?

imetoka hiyo.
 
Was this a mistake of CDM _ Arusha or of CDM as whole? What was so hard about casting votes again, and giving them to Lymo?
 
Back
Top Bottom