Mwafaka wa Umeya wa Arusha wapatikana

Kwenye siasa ukisimamia msimamo bila kuyumba utaingia msituni. Kama kufanya hivyo kutasaidia kuwafanya madiwani wafanye kazi sioni kama Mbowe amekosea
 
Kwenye siasa ukisimamia msimamo bila kuyumba utaingia msituni. Kama kufanya hivyo kutasaidia kuwafanya madiwani wafanye kazi sioni kama Mbowe amekosea

Kwa hiyo kimsingi tukubaliane kwamba CUF kule Zanzibar were absolutely right tofauti na kashfa nyingi ambazo zimewahi kutolewa sio hapa JF tu bali pia na baadhi ya wanasiasa wa upinzani; Oooh wameolewa, oooooh blah blah.
 
Magamba hapo wametumia ubabe kwanini uchaguzi usifanyike kama sheria inavosema 2naenda kulekule kwa kenya kuanzisha nyadifa ambazo hazitambuliki kisheria kuliko chama tawala kuachia wadhifa walioshikilia mwanzo
 
Hatimae ule utata wa meya ulio sababisha watu watatu kupteza maisha umepatiwa ufumbuzi baada ya mazungumzo yaliyokuwa yakifanywa na Waziri mkuu na Freeman Mbowe, kufikia mwafaka kuwa madiwa wakae wakubaliane ndipo leo walipo kaa madiwa wakafikia wamfaka kama ifatavyo...

Meya Gaundence Lyimo CCM
Naibu Meya Mallah CDM alipata kura 22 kati ya 25...2 zilisema hapana na 1 iliharibika
Kamati ya Uchumi na Elimu Bayo CDM
Kamati ya Fedha Lyimo TLP
unaweza kutujuza source ya taarifa yako mkuu, tafadhali
 
soma kwenye thread...Uchaguzi umefanyika na Mallah akapata kura 22 kati ya 25 na kwenye kamati ya Uchumi na Elimu alie changuliwa mwezi wa 12 aliondolewa na kuchanguliwa John Bayo....

mkuu ila kilichofanyika sicho kwakuwa CDM walikuwa wanapigania mfumo mbovu uliyotumika kumpata meya, CDM walipinga sana na kutaka uchaguzi urudiwe ishinde au isishinde ila taratibu na kanuni zifuatwe nasikugawana madaraka kama ilivyotokea.

vile vile CDM walipinga mifumo kama hiyo iliyotokea sehemu mbalimbali kama kenya, ivory cost na kungineko kule kulikotokea mkanganyiko wakupindisha sheria kwa uchu wa madaraka.

kwa hili CDM wakubali yakuwa wamechemsha au nisema kwa msisitizo tumechemsha kukubali kuruhusu mianya kama hii ya kupindisha sheria na kujenga mazoea ya kufanya mazungumzo mbeleni huko.

CDM hapa hatujamaliza tatizo bali tumeongeza tatizo tena kubwa sana, na mjue yakuwa mmemuweka LEMA kwenye wakati mgumu sana kwakuwa siku zoe amekuwa akipigania ukweli sasa nyie kwakuwa ni wengi mmeupindisha ukweli, na kura iliyo haribika ilikuwa ni yadiwani wa kata ya revyolosi mh NANYARO ambaye alipinga sana uchanguzi huwo ambao umewasaliti wananchi.

JF tuache kushabikia ujinga CDM ikikosea lazima tuikosoe kwakuwa ndicho chama cha matumaini ya watanzania na ni chama kinachoenda ikulu, utaratibu kama huu ni wakupinga sana ili siku nyingine usijirudie tena.

haya ni mawazo yangu binafsi kama wengine jinsi walivyotoa mawazo yao
 
Kama ni kweli let us b fair, tofauti ya hii na Wazenji iko wapi? SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA. Tuone ukweli wake halafu tutachambua.
 
Taratibu zilivunjwa, CCM walipora demokrasia. Ushindi wa mezani ni uzandiki. Tunataka uchaguzi mpya wa Meya ili kuilinda Demokrasia. Damu za waliokufa zinathamani kubwa. Lazima serikali ya CCM iwalipe ndugu wa marehemu na watoto wao fidia stahiki na waombe umma msamaha kwa kuuwa wananchi bila hatia.
Mkuu mawazo yako ni sawa ya wengi na niliwauliza wakasema huu ni mwanzo tulimalize kwanza hili kumbuka hata budget haijapitishwa na madiwani....tuwaachie tuone mipango yao
 
So tatizo ilikua ni kupata nafasi za uongozi tuna sio mchakato wa uchaguzi kubakwa? shame on mbowe,you can't stand for what is right!Yaani hii itatumika kisiasa dhidi yenu kwamba "mna uchu wa madaraka"hadi mjute,Am watching
we spika wa redio acha kumwandama kamanda wetu.
 
Hizi ni Habari njema,JE MARY CHITANDA ALIPIGA KURA?MAANA YEYE NDO ALIKUWA CHANZO CHA MATATIZO,
 
huo ni uamuzi wa busara na wakizalendo kuzuia watu wasiumie zaidi.mr.mbowe hapaswi kulaumiwa kwa hili kwani kuna watu walichukua maamuzi magumu kuliko yeye kama PM Raila odinga wa kenya na Morgan wa zimbabwe.ni ishara nzuri kwamba wakishindwa 2015 watashika njia hiyo hiyo badala ya kuingia msituni kama akina Outarra.ila hakutakuwa na serikali ya mseto!
 
uamuzi umefanywa na madiwani wenyewe wakimshirikisha dc arusha . Sihasa na comedy vyote ni aina za sanaa .
 
So tatizo ilikua ni kupata nafasi za uongozi tu
na sio mchakato wa uchaguzi kubakwa?

shame on mbowe,you can't stand for what is right!
Yaani hii itatumika kisiasa dhidi yenu kwamba "mna uchu wa madaraka"
hadi mjute,

Am watching

Watafanyaje mabadiliko bila kuingia kwenye ngazi za maamuzi? Huwezi kuleta demokrasia kama hupo nje ya maamuzi kijana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom