Mwafaka wa Umeya wa Arusha wapatikana

Mwafaka wa Umeya wa Arusha wapatikana

Nashukuru muafaka umepatikana, ila kwa mtazamo wangu hii tendency tunayojijengea katika nchi zetu za Afrika sio nzuri..Yaani mtu anafanya makusudi kukwapua kura akijua tu mgogoro utatokea halafu mtunaenda meza ya majadiliano tunakubali kushare madaraka. Na hii sumu tusipo itoa itatumaliza wenyewe!
 
Acha ubabaishaji kwani kila kitu lazima uchangie? eti kama sikosei
Mimi nirifikiri wewe sasa unatupa habari za uhakika baada ya jamaa kuonekana kutokuwa na uhakika,kumbe na wewe unachojua ni kukosoa tu lakini hutoi way forward!!!
 
Hatimae ule utata wa meya ulio sababisha watu watatu kupteza maisha umepatiwa ufumbuzi baada ya mazungumzo yaliyokuwa yakifanywa na Waziri mkuu na Freeman Mbowe, kufikia mwafaka kuwa madiwa wakae wakubaliane ndipo leo walipo kaa madiwa wakafikia wamfaka kama ifatavyo...

Meya Gaundence Lyimo CCM
Naibu Meya Mallah CDM alipata kura 22 kati ya 25...2 zilisema hapana na 1 iliharibika
Kamati ya Uchumi na Elimu Bayo CDM
Kamati ya Fedha Lyimo TLP

Muda wote huo huiyu waziri mkuu alisubiri nini kufanya meeting? afute na hizo kesi zisizo kuwa na kichwa wala miguu.
 
Nguvu ya uma haikuwahi kushindwa, mapambano muda wote,kila sku,FREEDOM IS COMING
 
  • Thanks
Reactions: LAT
So tatizo ilikua ni kupata nafasi za uongozi tu
na sio mchakato wa uchaguzi kubakwa?

shame on mbowe,you can't stand for what is right!
Yaani hii itatumika kisiasa dhidi yenu kwamba "mna uchu wa madaraka"
hadi mjute,

Am watching

This is politics in it's purest sence. Sometimes compromising for a good course is a virtue and a sign of maturity.

Big up CDM
 
Kuna msemo usemao, FUNIKA KOMBE MWANA HARAMU APITE. Ktk hili mimi naona una maana zaidi. Speaker, you must think about this statment.
 
Shame on you ccm! Hivi mlishindwa kweli kukaa kwenye meza mpaka watu wakauawa kwa ajili ya uroho wenu wa madaraka? PM naye ni mbwiga na machozi yake ya kinafiki. Haiwezekani waziri mkuu kwenye kutoa maamuzi magumu anageuka kuwa bubu na kuegemea upande wa chama chake hata kama kunamakosa anafaa kuwajibishwa yeye na watendaji wake wengine waliohusika.
 
Kumbe kura hazikuibiwa na mshindi alikuwa halali! Sasa ilikuwaje? Mlikuwa mnatafuta umaarufu tu! CDM Mnashangaza!
 
Hatimae ule utata wa meya ulio sababisha watu watatu kupteza maisha umepatiwa ufumbuzi baada ya mazungumzo yaliyokuwa yakifanywa na Waziri mkuu na Freeman Mbowe, kufikia mwafaka kuwa madiwa wakae wakubaliane ndipo leo walipo kaa madiwa wakafikia wamfaka kama ifatavyo...

Meya Gaundence Lyimo CCM
Naibu Meya Mallah CDM alipata kura 22 kati ya 25...2 zilisema hapana na 1 iliharibika
Kamati ya Uchumi na Elimu Bayo CDM
Kamati ya Fedha Lyimo TLP

Kumbe majigambo yote ya nini? and what does that say about ccm and the government?
 
Mallah anatoka CDM kata ya Kimandolu na Bayo anatoka CDM kata ya Elerai
 
Kumbe kura hazikuibiwa na mshindi alikuwa halali! Sasa ilikuwaje? Mlikuwa mnatafuta umaarufu tu! CDM Mnashangaza!

FaizaFoxy - unaweza kujibu ni kwa nini Mizengo Pinda amekaa meza moja na Mbowe (waliye msafirisha usiku usiku chini ya ulinzi mkali wa police) na kuongea kuhusu u-mayor wa Arusha? Hivi unakumbuka kauli za ccm/serikali kwamba uchaguzi umeisha?

You don't need to be a brain surgen kujuwa kwamba serikali wafikia mwisho wa kufikiri kwa issue ya Arusha na hivyo wamelazimika kunywa kikombe cha CDM!
 
  • Thanks
Reactions: LAT
Asante sana kwa kutujuza mkubwa!Ila ukweli ni kuwa CC Magamba waliibaka Demokrasia,CDM walistahili kuchukua nafasi ya umeya.
 
Estomih Malla ni Diwani wa CHADEMA kata ya Kimandolu na Bayo pia anatoka CDM. Malla ndiye aliyetakiwa awe Meya wakamweka mamluki wao Lyimo.

Inaonekana una chuki mbaya na Lyimo.
Alichaguliwa kidemokrasia, tafadhali heshimu maamuzi wa wawakilishi wa Arusha.

Bora PM ametumia busara na kumwelewesha Mhe Mbowe nini maana ya siasa.
 
Shame on you ccm! Hivi mlishindwa kweli kukaa kwenye meza mpaka watu wakauawa kwa ajili ya uroho wenu wa madaraka? PM naye ni mbwiga na machozi yake ya kinafiki. Haiwezekani waziri mkuu kwenye kutoa maamuzi magumu anageuka kuwa bubu na kuegemea upande wa chama chake hata kama kunamakosa anafaa kuwajibishwa yeye na watendaji wake wengine waliohusika.

Unabwabwaja hali mradi jamvi la kuandika lipo.
Fungua macho, tumia akili Mungu aliyokupa ili uweze kutoa mchango wenye busara, si upuuzi ulioweka hapa.
WALIOSABABISHA MAUAJI ARUSHA NI CHADEMA ILI KUPATA MILEAGE YA KISIASA KWA KUTUMIA DAMU NA ROHO ZA WATU.
Mmelaaniwa nyie, One day you gonna pay .... Hatutawaacha kamwe katika hili.
 
Kumbe Lowassa bado anavision kuliko hawa Magamba wengine, nakumbuka alishauri CCM na CDM wakae meza moja wayamalize kiustaarabu, MAGAMBA wenzake wakamshambulia vibaya. Leo wamekula matapishi yao. Nafikiri sasa CCM wameanza kuona hali halisi ya mambo na kubaini propaganda zao zakizushi hazina nafasi tena katika Tanzania ya leo.
 
Sasa nimeelewa nini maana ya kuipa serikali muda maalum ili itekeleze matakwa ya wananchi.tusipo ibana h¨ªi serikali ya magamba mambo yataendelea kuwa magumu.hongera wote waliohusika kwenye muafaka.makamba anamatatizo ya akili ndo maana amelifikisha hili swala hapa lilipo wakati lilikua ni dogo sana.
 
Estomih Malla ni Diwani wa CHADEMA kata ya Kimandolu na Bayo pia anatoka CDM. Malla ndiye aliyetakiwa awe Meya wakamweka mamluki wao Lyimo.

Wengine hawatafurahia maoni yangu lakini Estomih Malla ndiye aliyetakiwa kuwa Mbunge wa Arusha, makao makuu wakaweka mamluki wao!
 
Back
Top Bottom