Kichwa Ngumu
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 1,726
- 314
aliyekuwepo ni nani? au ndio huyo huyo ambae amepata sasa?
Unabwabwaja hali mradi jamvi la kuandika lipo.
Fungua macho, tumia akili Mungu aliyokupa ili uweze kutoa mchango wenye busara, si upuuzi ulioweka hapa.
WALIOSABABISHA MAUAJI ARUSHA NI CHADEMA ILI KUPATA MILEAGE YA KISIASA KWA KUTUMIA DAMU NA ROHO ZA WATU.
Mmelaaniwa nyie, One day you gonna pay .... Hatutawaacha kamwe katika hili.
Kumbe huoni aliyepewa pipi ni nani, CCM wamechiwa umeya huku vitengo nyeti vya uchumi, Elimu na fedha vikienda upinzani kumbuka vilevile naibu meya anatoka CDM kwa hiyo ukiangalia vizuri ni kama baraza linaongozwa na CDM.chadema wamepewa pipi ya kijiti. wamefurahi
Hongera Mbowe kwa kumfundisha Pinda nini maana ya demokrasia maana Pinda alisema bungeni kuwa uchaguzi umemalizika lakini leo imebidi kula matapishi yake, kama hiyo ndiyo busara unayoisema ya Pinda kula maneno yake nakubaliana nawe lakini imemchukua muda mrefu sana kulijua hilo.Inaonekana una chuki mbaya na Lyimo.
Alichaguliwa kidemokrasia, tafadhali heshimu maamuzi wa wawakilishi wa Arusha.
Bora PM ametumia busara na kumwelewesha Mhe Mbowe nini maana ya siasa.
Na mimi nilikuwa nawaza kama hivi au?Kwa hiyo sasa chadema ni CCM C?.
Uchaguzi umekwisha sasa tunataka maendeleo kwa watu wa Arusha kama hukubaliani na matokeo ni zamu yenu sasa kwenda mahakamani tulisema tatizo ni muda tu Ha ha haa.Chadema bwana kwa hiyo mmejifariji?
Kwa hiyo sasa chadema ni CCM C?
Tokea lini na siasa nyie? Wachaga kazi yao ni kuiba tu.
Nashukuru muafaka umepatikana, ila kwa mtazamo wangu hii tendency tunayojijengea katika nchi zetu za Afrika sio nzuri..Yaani mtu anafanya makusudi kukwapua kura akijua tu mgogoro utatokea halafu mtunaenda meza ya majadiliano tunakubali kushare madaraka. Na hii sumu tusipo itoa itatumaliza wenyewe!
Nguvu ya uma haikuwahi kushindwa, mapambano muda wote,kila sku,FREEDOM IS COMING
Kuna msemo usemao, FUNIKA KOMBE MWANA HARAMU APITE. Ktk hili mimi naona una maana zaidi. Speaker, you must think about this statment.
Mkuu nadhani TLP wana diwani mmoja Michael Kivuyo aliyepewa unaibu meya wakati mgogoro ndo unashika kasi, baadaye akajiengua.
Pili nina maswali mawili ya msin gi sana ningependa kujua waziri mkuu na Mbowe wamejadili na kukubaliana nini;
1. Ni hatua gani zitachukuliwa dhidi ya polisi waliouwa raia wasiokuwa na hatia? Je, serikali itafanya nini kwa ajili ya familia za waliouwawa tar.5 jan??
2. Je Mary chatanda bado ataendlea kuwa mjumbe halali wa halmashauri ya manispaa ya Arusha??
Nawasilisha.
FaizaFoxy - unaweza kujibu ni kwa nini Mizengo Pinda amekaa meza moja na Mbowe (waliye msafirisha usiku usiku chini ya ulinzi mkali wa police) na kuongea kuhusu u-mayor wa Arusha? Hivi unakumbuka kauli za ccm/serikali kwamba uchaguzi umeisha?
You don't need to be a brain surgen kujuwa kwamba serikali wafikia mwisho wa kufikiri kwa issue ya Arusha na hivyo wamelazimika kunywa kikombe cha CDM!
Nashukuru muafaka umepatikana, ila kwa mtazamo wangu hii tendency tunayojijengea katika nchi zetu za Afrika sio nzuri..Yaani mtu anafanya makusudi kukwapua kura akijua tu mgogoro utatokea halafu mtunaenda meza ya majadiliano tunakubali kushare madaraka. Na hii sumu tusipo itoa itatumaliza wenyewe!
DudusMkuu heshima. I agree with you 100%. Wachambuzi mbali mbali wameanza kuhoji, kama sio kukejeli, kwamba hiyo ni demokrasia mpya Afrika. Eti mijitu inapoka haki wakati wa kupiga kura ikitegemea baadaye kukaa kwenye meza ya mazungumzo ili ku-share madaraka. Yametokea Kenya, Zimbabwe, Zanzibar, na leo Arusha.
Kimsingi siungi mkono ukosefu wa amani mahali, ila pia sikubaliani na "kurudisha" amani kwa mtindo huu mpya wa kukiuka sheria na hata Katiba ya nchi. Je, sheria zetu na Katiba zinatambua utaratibu huu "mpya"? Kidogo nailaumu CHADEMA, walichotakiwa kupigania na kusimamia ni "ukiukwaji wa taratibu" uliofanywa awali - yaani daima sheria ziheshimiwe hata kama kwa kufanya hivyo wangepoteza. Kisiasa, kama ambavyo baadhi wameshachangia, naona hii ina mrejesho mbaya kwa CHADEMA.